Thursday, November 26, 2015

MAGUFULI ATINGA OFISINI KWA MAJALIWA

jp1 
 Rais John Magufuli akitia saini  kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015  na kuzungumza nao kwa takribani saa moja (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jp3 
Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jp4 
Rais John Magufuli akiagana  na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali yajidhatiti kupambana na kemikali zenye madhara maeneo ya bandari

ke 
Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo akiwakaribisha wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali kushiriki katika mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam.
ke1 
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akifungua mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam.
ke3 
Wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam.
ke4 
Mwakilishi kutoka nchini Ujerumani Bibi. Stefane Deuser akichangia mada kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.
ke5 
Mratibu wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP) Bw.Patrick Mwesigye akizungumza leo jijini Dar es salaam kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.
Picha Zote Na Fatma Salum (MAELEZO)
1 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha la kushukuru baada ya kufanyika na  kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania salama salimini.
Msama amesema maandalizi yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,  linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya, ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine kutoka nje ya nchi.
Katika picha katikati ni Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Msama Promotion.
2 
Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
4
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.

Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD Akiwashukuru Wapiga Kura Wake Wananchi wa Jimbo la Chumbuni

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwataka kuwa wamoja na kujiandaa na maendekleo katika jimbo lake.
 Na kusema sasa makundi basi iliobaki ni Kazi Tu kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo na kusema yeye ni Mbunge wa Wananchi wa Chumbuni wote 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa hafla ya kuwashukuru 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar. 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.

MBUNGE WA UBUNGO SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU KUMCHAGUA NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mus’ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
 Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.
 Vijana wakiserebuka baada ya kuzungumza na mbunge wao Said Kubenea katika Soko la Mabibo.
 Mbunge Kubenea akizungumza na viongozi wa soko la Mabibo.
Hapa akiwahutubia wananchi katika soko la Mabibo.


WFP YAFAFANUA MAFANIKIO YAKE HAPA NCHINI

index 
Ofisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UN WFP – Tanzania),  Tala Loubieh (kulia), akifafanua jinsi Shirika hilo linavyofanya kazi hapa nchini tangu mwishoni  mwa Juni 2014  lilipobadili utamaduni wake wa zamani wa kugawa chakula moja kwa moja shuleni na kutumia  mtindo mpya   wa kustawisha mazao kwa kushirikiana na Shule, unaojulikana  kama “Home Grown School Meals Programme.” Kwa  kushirikiana na wilaya husika  kuratibu mpango huo wa kuwapatia  chakula wanafunzi shuleni kwa kununua chakula hicho kutoka kwa wakulima wadogo wadogo na jinsi  mkakati huu ulivyoweza  kuendeleza wakulima vijijini na kuimarisha uzalishaji wa wakulima  wadogo pia kuinua uchumi wao.
Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog

Askofu Mkuu wa Tabora Kuongoza ujumbe wa Tanzania kumuona Papa Francis Uganda.

6
Na Joseph Ishengoma, MAELEZO
Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka kesho (tarehe 27.11.2015) anatarajia kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda.
Baba Mtakatifu Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda kesho kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.
Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutembelea Bara la Afrika tangu alipoliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013.
Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) nchini Padre Raymond Saba amesema  Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo.
“Tulipata mwaliko kutoka Kenya na Uganda, lakini tumeangalia nafasi yetu na jinsi ya kushiriki katika ziara hii. Hatukuweza kutuma mwakilishi Kenya, lakini Askofu Ruzoka ataiwakilisha TEC Uganda,” amesema.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, jana mabasi mawili ya waumini wa dini ya Kikristo yaliondoka mjini Mwanza kuelekea Namugongo, Uganda ambapo Baba Mtakatifu atakapofanyia ibada.
Eneo la Namugongo ndipo Mfalme Kabaka Mwanga II alipowachoma na kuwaua mashahidi 22 wa Uganda waliofia dini katika karne ya 18.
“Natoa wito kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini, wafuatilie na kusikiliza kwa makini ujumbe wa Baba Mtakatifu aliouleta katika Barani Afrika kwa sababu unagusa moja kwa moja amani na ushirikiano miongoni mwa jamii,” amesema.
Kwa mujibu wa Padre Saba, Baba Mtakatifu hufanya ziara kufuatia mwaliko wa kanisa na serikali ya mahali husika au tukio la kimataifa linalohusiana na imani Katoliki.
Amesema, “Kanisa pekee yake haliwezi kufanikisha ziara ya Baba Mtakatifu. Ndio maana alipofika Kenya alipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na hata alipokuwa Marekani alipokelewa na Rais Baraka Obama ingawa sio rahisi kwa kiongozi wa Marekani kumpokea mgeni uwanja wa ndege.” 
Ziara ya Baba mtakatifu nchini Marekani ilipangwa kabla hajawa kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki. Ziara hiyo ilitokana na kongamano la kimataifa la familia lililofanyika mjini Filadelphia.
Papa Francis anatarajia kuhudhulia kongamano la vijana ulimwenguni nchini Poland mwaka 2016.

TAMASHA KUBWA LA BURUDANI LA INSTAGRAM PARTY KUFANYIKA JUMAMOSI VIWANJA VYA ESCAPE ONE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

  Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba.
 Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la burudani la Instagram party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
…………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’ litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini  Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa  Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu.
Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.
“Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.
Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo.
NHC YAZINDUA MAUZO YA NYUMBA KATIKA MRADI WA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM
NH9 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26, 2015 Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mauzo ya nyumba katika mradi mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam (kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah.
NH2 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya ramani ya mradi wa nyumba ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.
NH3 
Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza kwa umakini, Bw. Nehemia Kyando Mchechu.
NH4
NH1 
Mkutano ukiendelea.
NH5 
Waandishi wa habari wakitembelea  katika eneo la ujenzi huo.
NH6 
Ujenzi ukiendelea
NH7 
Ujenzi ukiendelea
NH8 
Waandshi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi huo.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
……………………………………………………………………………………..
Na Philemon Solomon Fullshangweblog
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 ambao unatarajiwa kugarimu kiasi cha zaidi ya  Sh 187, 927, 105,500 mpaka utakapomalizika .
Pia ikumbukwe kuwa mradi huu ni seemu ya mji mpya wa kisasa (Satellite City) unajengwa hapa ,mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fuko za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi  Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni mradi huu una jumla ya nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii.pia kutakuwepo na seemu ya maduka makubwa kwa ajili ya wakazi na maeneo ya jirani”Alisema Mchechu.

Serikali imejipanga kukuza na kuendeleza Stadi za Kazi nchini

za1
Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza stadi za kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza tija katika sekta zote nchini,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za2 
Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu faida za kuendeleza stadi za kazi ikiwemo kuongeza uzalishaji katika sekta zote nchini,kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za3 
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi na vyombo vya habari leo jijini Dar eS Salaam uliolenga kueleza mpango wa Serikali kuwawezesha wananchi kupitia mpango wa kuendeleza stadi za kazi unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2016/2017.
Picha Zote na Fatma Salum (MAELEZO)

Serikali kuendelea kushirikiana na Vijana katika kutatua changamoto zao

ol1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki.
Picha na Frank Shija,WHVUM.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na Vijana wa Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile (hawapo pichani) uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 6 – 14 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
ol3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bibi. Dorice Assenga (katikati) kwa niaba ya Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
ol4 
Baadhi ya vijana wa Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015.Kutoka kushoto ni Baraka Chedego, Paul Simango na Rwihula Daniel

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA ULINGO TANZANIA (UMOJA WA WANAWAKE WANASIASA).

has1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has4 
Baadhi ya Wanawake Wanaulingo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has5 
Balozi Getrude Mongela, akichangia moja ya kati ya mada zilizokuwa zikizungumziwa katika kikao hicho leo. Picha na OMR
has6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Wanaulingo alipokuwa akipokelewa alipowasili kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria kwenye Kikao maalum kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania kwa ajili ya kumpongeza . Picha na OMR
has7 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has8 has9 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has10 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya ‘Dua’ kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar na Katibu wa Ulingo Tanzania, Salama Aboud Talib, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has11 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya picha baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has12 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia jambo na Balozi Getrude Mongela baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has13 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has15 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has18 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR

Wahamiaji haramu wakamatwa Tabata Segerea

index 
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.
Ameongeza kuwa wahamiaji hao waliingia nchini ya usimamizi wa mwanamke mmoja anaeitwa Zainabu Umwiza (25) anaesemekana ni raia wa nchi ya Burundi ambae anajihusisha na biashara hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao ni kosa la jinai tayari kuwapeleka nchi nyingine na hivyo amemuomba ajisalimishe
“ Bi Zainabu Umwiza mwenye asili ya Burundi tunamwomba ajisalimishe maana yeye ni mfanyabiashara wa usafirishaji wa binaadamu  kutoka nchi za Afrika kwenda Ulaya” kamanda Kova alisisitiza.
Aidha kamanda Kova ameeleza kuwa polisi walifanya upekuzi katika nyumba ya mwanamke huyo ndipo walipowakuta wahamiaji hao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, usafirishaji wa binadamu kutoka Afrika kwenda bara la Ulaya unaofanywa na mwanamke huyo, ambao hufanyika kwa malipo ya Dolla 1000 kwa mtu mmoja.
Kamanda Kova ameongeza kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa kujua kwamba wana kibali chochote cha kuingia nchini waligunduliwa kuwa hawana na kueleza kuwa waliingia kupitia njia za panya na mbinu nyingine ambazo bado zinachunguzwa na kwamba wamewajulisha  idara ya Uhamiaji na watashirikiana nao katika upelelezi ili hatimaye sheria ichukue mkondo wake.
Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kundoa na kuzuia tatizo la wahamiaji haramu ambao wamekua tishio katika usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

NI MARUFUKU TAASISI ZA SERIKALI KUCHAPISHA KADI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

index

Zoezi la Usafi wa Mazingira Kuwa Endelevu Jijini Dar es Salaam

index
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Said Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) ofisini kwake  leo  alipokuwa akizungumzia zoezi la usafi na namna mkoa ulivyojipanga kutekeleza zoezi hilo siku ya 9 Disemba.
indexx
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juu ya usafi wa mazingira siku ya 9 Disemba.
indexxx
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) akimsikiliza Mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki (Kushoto) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji  wa  agizo la Mhe Rais la kufanya usafi wa mazingira katika maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara.                                
(Picha zote na Raymond Mushumbusi – Maelezo )
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki amesema zoezi la usafi wa mazingira litakalofanyika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, litakuwa ni endelevu kwa mkoa wa Dar es Salaam hata baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano. Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliagiza kuwa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu yatumike kwa kufanya usafi wa Mazingira kote nchini badala ya kufanya sherehe za gwaride la askari wa vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Akiongea na vyombo vya habari leo Mhe. Sadiki alianza kwa kumpongeza Mhe. Rais kwa uamuzi aliouchukua wa kubadilisha sherehe za uhuru kuwa ni siku ya kufanya kazi badala ya kwenda uwanjani na kuangalia gwaride na halaiki mbalimbali kama ilivyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.
“Mhe. Rais katurejesha kule tulipotoka ambako kauli mbiu ya sherehe za uhuru ilikuwa ni uhuru na kazi au uhuru ni kazi wakati watanzania walikuwa wakiungana na kufanya kazi kwa umoja na kushirikiana,” alisema, Mhe. Sadiki.
Aidha, Mhe Sadiki alisema, zoezi la usafi kwa  mkoa wa Dar es Salaam litaanza rasmi tarehe  1 Disemba mwaka huu na kumalizikia 9 Disemba mwaka huu  siku ya kilele cha  maadhimisho ya siku ya uhuru na kuongeza kuwa  zoezi hilo litakuwa  endelevu.
Mhe. Sadiki aliongeza kwa kusema kuwa, uongozi wa mkoa umewaomba wadau kujitokeza kwa kuchangia fedha au vifaa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo na amewataka watendaji kushawishi wananchi wa maeneo yao kutafuta vifaa badala ya kusubiri kuletewa na Halmashauri.
Pia, Mhe Sadiki amewahimiza watendaji wa mitaa na kata kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha maeneo wanayoyasimamia yanakuwa katika hali ya usafi muda wote ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko na pale  inakapobainika eneo fulani lipo katika mazingira ya uchafu  basi mtendaji wa eneo hilo atawajibishwa kwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kosa la kutotimiza wajibu wake.
Vilevile ametoa wito kwa wananchi kuzingatia usafi  kwa kuacha tabia za kutupa taka ovyo hasa wanapokuwa katika vyombo vya usafiri na kutokujisaidia katika mitaro au vichaka ili  kuepukana na uchafuzi wa mazingira kunakopelekea kutokea kwa magonjwa ya mlipuko .

LEAT WATOA MIZINGA 350 KWA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI

index
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwel
…………………………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE, MUFINDI
TIMU ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya kufugia  nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa vilivyoko katika mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.
Alisema kuwa malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.
Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili mathalani misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Juma alisema kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za usimamizi na uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma mkaa,ukataji miti uliokithiri na ujangiri  mambo ambayo inasababisha hasara kwa taifa.
Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo husababisha umaskini, kukauka kwa vyanzo vya maji kutoweka kwa uoto wa asili na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
“ Mradi huu utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko katika vikundi vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia jamii kwa kuzipatia vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo leat imetoa kwa kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto zote hizo endapo utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema

RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHIWA TUNZO

al1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Tunzo ya dhahabu iliyopewa  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka kwa  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council  katika Mji wa  Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20 kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
al2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiiangalia Tunzo ya dhahabu iliyopewa  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kukabidhiwa na  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council  katika Mji wa  Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20 kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Serikali yaweka mpango wa kutambua na kukuza watu wenye ujuzi wa chini na stadi za kazi.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA POLISI

ab1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto),  akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam.
ab2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa kufungua  mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa  Jeshi la Polisi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es Salaam.
ab3 
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
ab4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano Baraza hilo  uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chama cha Wakulima Tanzania (AFP) chapongeza hotuba ya Rais dk. John Pombe Magufuli

images 
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Chama cha Wakulima Tanzania (AFP) kimepongeza hotuba ya Rais wa awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11, Novemba 20 mwaka huu mjini Dodoma.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mahusiano wa Makundi Maalum wa AFP Bw. Peter Sarungi ameeleza kuwa hotuba hiyo imesimama katika mambo ya msingi na yenye kuleta mabadiliko ya kuijenga Tanzania mpya.
Aidha Sarungi aliongeza kwa kusema anaamini kupitia kauli mbiu ya hapa kazi tu uchumi wa nchi utakua na kuboresha huduma za afya,upatikanaji wa elimu kwa watu wote ,kupanda kwa thamani ya shilingi ya Tanzania,kuongeza heshima ya uchumi nje na ndani ya na kuwa na viongozi wawajibikaji.
“kwa kweli hotuba ya rais imegusa nyanja zote muhimu ikiwemo namna ya kukabiliana na kuondokana na rushwa,upatikanaji wa vituo vya afya bora,elimu na mimi naunga mkono jitihada hizi zenye tija ya kuleta mabadiliko ” alisema Sarungi.
Sarungi amekemea vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ikiwemo matumizi mabaya ya lugha za kejeli na kuzomea hali ambayo inaharibu utendaji wa kazi za Bunge na kuleta mgawanyiko baina yao .
“Kuna umuhimu wa kuziangalia upya kanuni za kudumu za bunge kwa kuongezwa vifungu vya kuzuia na kutoa adhabu kali kwa mtu yeyote ndani ya ukumbi wa bunge kutumia maneno ya vijembe, kejeli, misemo ya mafumbo na lugha za kuudhi ziwekewe msisitizo wa kuzikomesha ikiwemo kutoa adhabu kali ya kutandikwa viboko” alisema Sarungi.
Mwisho alitoa rai kwa wabunge kuzingatia mambo ya muhimu yaliyowapeleka bungeni ikiwemo kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi na kujenga umoja na upendo bila kujali itikadi za vyama vyao ili kujenga Tanzania mpya.

Muhimbili Yapokea Mashine ya kusaidia wagonjwa kupumua

MU1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua  endapo wamezidiwa baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.
MU2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo
MU3
Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa wagonjwa.
MU4 MU5
Meneja Mauzo barani Afrika, Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………………..
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator  ya kumsaidia mgonjwa kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000  sawa na Shilingi milioni 80.
Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland .
Akikabidhi mashine hiyo  mpya na  kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya miaka miwili.
Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi.
Akielezea  kuhusu mashine hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema  mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo  inaonyesha .

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index
MTU MMOJA MKAZI WA MWANJELWA WILAYANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADENI EZEKIA [25] ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA YA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUTUHUMIWA WIZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU HUKO MWANJELWA, WILAYA YA MBEYA MJINI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI MPAKA SASA HAIFAHAMIKI ALIIBA NINI NA SEHEMU GANI.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 14 MKAZI WA KITONGOJI CHA IHEWA, ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTINA S/O YUSTI, ALIUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO IHEWA KATA NA TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAO TANGU TAREHE 24.11.2015 MCHANA. MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI NA BIBI YAKE DAINES MPELWA NA SIKU HIYO YA TAREHE 24.11.2015 KWENDA SOKONI KUUZA MBOGA NA HAKURUDI/HAKUONEKANA HADI MWILI WAKE NJIANI TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA.
TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU ALIBAKWA NA KUZIBWA PUA HIVYO KUKOSA HEWA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJIANI UMBALI WA MITA 174 KUTOKA NYUMBANI KWAO HUKU UKIWA NA MICHUBUKO.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Airtel Tanzania yapiga ‘tafu’ Taswa SC

index 
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) Majuto Omary kwa ajili ya kutumika katika mechi zao.
……………………………………………………………………………………………
Kampuni ya Airtel Tanzania imeiipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo jana,  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira.
Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.
“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za
michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo.
Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao.
“Tumeomba kwa  kampuni nyingi, bado  hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.
Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. “ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu
inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.

COMPACT PLUS SUBSCRIBERS SCORE A FESTIVE EPL SEASON ON SUPERSPORT 3 – PLUS NEW SUPERSPORT 5 CHANNEL

‘Tis the season for giving and DStv is bringiimages 
ng football fans on Compact Plus tidings of great joy! The Barclays Premier League (English Premier League) currently in mid-season will return to SuperSport 3. Hence, Compact Plus subscribers will be delighted to know that from 01 December 2015, they will be able to access the bulk of the EPL action for the rest of the football season which ends in May 2016!
As part of MultiChoice Africa’s commitment to ensuring that DStv subscribers have a bumper Festive season this year, all active Compact Plus subscribers will get the EPL experience on SuperSport 3 while SuperSport 5 will be made available to provide coverage of the La Liga.
This move will ensure all the subscribers have a fantastic holiday season with a wide range of added entertainment for the whole family which includes the various holiday pop-up channels including the Nigerian Festivals, Hoolee, the Pope’s Kenya Visit alongside new channels like M-Net Family, Vuzu and Emmanuel TV!
“We understand that our subscribers are experiencing tough economic conditions at the moment and want to ensure we go the extra mile for our valued subscribers. The DStv festive season will give you 100% and more great family sport, kids programming, news and entertainment!,” said COUNTRY GM.
The Barclays Premier League is the sporting world’s most riveting soap opera, filled with larger than life characters who thrill, infuriate, spread joy and despair in equal measure.
From an unfortunate slip to losing grip of the title, to grabbing it via a stoppage time winner no other league in the football world comes close to delivering such amazing drama.
Featuring the cream of the Football Management crop who can always be depended upon for a newsworthy soundbite, to some of the beautiful games’ greatest players who regularly turn on the flair and style, the Premier League will keep fans across the globe on the edge of their seats, talking and tweeting non-stop from one match week to the next.
DStv Compact Plus subscribers will get to experience the unpredictability of the league that has been demonstrated this season. So far, this has been one of the most open football seasons in years with the likes of Leicester City competing with the big names for a top 4 slot, while champions Chelsea lag close to the drop zone.
This festive season will dish up its fair share of mouth-watering fixtures for subscribers to look forward to, including the following blockbusters:
• Arsenal v Man City – December 21, 2015
• Man Utd v Chelsea – December 28, 2015
• Everton v Tottenham – January 2, 2016
• Liverpool v Arsenal – January 13, 2016
• Man City v Everton – January 13, 2016
• Chelsea v Everton – January 16, 2016
• Liverpool v Man Utd – January 17, 2016
• Arsenal v Chelsea – January 24, 2016
So, can the reigning champ Chelsea survive relegation? Will Mourinho be fired? Who will make up the top 4 for Champions league qualification? Can Klopp revive Liverpool? Catch all this football drama on SuperSport 3 from 1 December 2015!
For more sports news and live match fixtures on SS3 and SS5, please visit www.supersport.com.

KAMPUNI YA MEGATRADE INVESTMENT LTD YAVIPIGA JEKI CHUKO KIKUU CHA USHIRIKA NA BIASHARA,MOSHI PAMOJA NA CHAMA CHA SOKA CHA MKOA WA KILIMANJARO

Meneja masoko wa Kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akimkabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni 1.5 ,katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro ,KRFA,Mohamed Musa kwa ajili ya kusadia ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa iliyoanza hivi karibuni.
Mweka hazina wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,Kusianga Kiata,akitizama hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha.
Baadhi ya wadau wa soka waliofika kushuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo jengo la Voda House.
Meneja Masoko kanda ya Kaskazini ,Edmund Rutaraka akimkabidhi Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Biashara ,Moshi,( MOCU),Profesa Faustine Bee hundi ya kiasi cha shilingi Mil 2 kusaidia maeneo mbalimbali yenye changamoto chuoni hapo.
Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi hundi kwa mkuu huyo wa chuo.
Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Bashara (MOCU) Profesa Faustine Bee akizungumza mara naada ya kukabidhiwa hundi hiyo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

BALOZI SEIF ALI IDI ATOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU HALI YA KISIASA ZANZIBAR

Makamu wa pili  wa rais wa Zanzibar Balozi Sindex 
Seif Ali Idi ameimabia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.
Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa   hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo  itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.
Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.
Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katIka visiwa hivyo.

WAKAZI WA MIKOA YA MANYARA,ARUSHA NA KILIMANJARO WAJITOKEZA UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .
Wanafunzi wa kozi ya awali ya Askari Polisi kutoka shule ya Polisi Tanania wakiwa katika manda,ano ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini.
Maanda,mano ya lipita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
Maandamano hayo yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi yakieekea katia viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kujinsia kanda ya kaskazini akimsikiliza Mwenyekiti wa Mwavuli wa Vikoba wa KIVINET ,Mama Mwingira wakati alipotembelea banda la KIVINET .

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukeketaji.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiiza maelezo kutoka TAWREF ambao pia wameshiriki katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Velonica Ollomi akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi,kulia kwake ni Afisa Kitengo cha elimu ya haki za binadamu na jinsia ,KWIECO ,Elizabeth Mushi.

SHIWATA kugawa nyumba 14 Mkuranga, yampongeza Dkt. Magufuli kumteua Majaliwa Waziri Mkuu

images 
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mkutano wa wanachama wake Jumamosi kutangaza majina ya wanachama watakaokabidhiwa nyumba 13 na misingi ya nyumba 14 katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam jana kuwa mkutano huoutakaofanyika Ilala, Bungoni Dar es Salaam kuanzia saa 4 pia watatangazwa viongozi watakaoshika nafasi za uongozi zilizo wazi.
Nafasi za uongozi zilizo wazi ni Makamu Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Marehemu Kepteni John Komba,Katibu ambayo ilikuwa inashikiliwana Selemani Pembe ambaye yupo India kikazi na Mweka Hazina ambaye Flowin Nyoni ambaye ni Mhadhiri wa Chuko Kikuu cha Dodoma.
Katika hatua nyingine SHIWATA imeupongeza uongozi wa Rais John Pombe Magufuli kumteua Mkufunzi wa Mpira wa Miguu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Alisema medani ya michezo inahitaji msukumo wa viongozi wanaojua michezo hivyo ni kipindi cha kujiandaa kuiletea sifa Tanzania kupitia michezo ya soka, ndondi, riadha,netiboli na mingine katika michezo ya Afrika Mashariki,Michezo ya Afrika, michezo ya madola na michezo ya dunia.
Taalib alisema ili kuonesha viongozi wetu wapya ni wapenda michezo hivi karibuni Rais Magufuli alikubali kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania kucheza kombe la dunia kati ya Stars na Algeria kwenye uwanja wa Taifa ambapo alimtuma Makamu wa Rais, Suluhu Samia Hassan kumwakilisha hiyo inaonesha Tanzania imepata viongozi wapenda michezo.
Alisema wasanii na wanamichezo watapiga hatua kubwa mbele kwenye uongozi wa Dkt. Magufuli kwani kuna kila dalili kuwa kazi zao zitathaminiwa na kupewa kipaumbele.
Taalib alisema mtandao wa SHIWATA ambao unajumuisha wanamichezo, wasanii, waigizaji, waandishi wa habari na wasanii wa kazi za mikono wamemkubali Dkt. Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo ya kufuatilia mambo hasa kuondoa kero za wanyonge ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawapati huduma muhimu za kijamii za elimu na afya.
Alisema wasanii wanaimani kubwa na Dkt. Magufuli kwani ni mchapakazi na mtu asiyependa wananchi wake wadhulumike wakiwemo wasanii ambao walizunguka nchi nzima kwenye kampeni zake na kujionea shida za wananchi zinazowakabili wakiomba mahitaji mbalimbali katika nchi yao yenye rasilimali lukuki.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 nchini inamiliki hekari 300 za kujenga nyumba za makazi wa bei nafuu ambako nyumba 120 zimekwisha jengwa katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na hekari 500 zilizotengwa kwa ajili ya kilimo zimelimwa na kupanda mazao mbalimbali katika kijiji cha Ngarambe Mkuranga.

No comments :

Post a Comment