Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (katikati), Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro, (wapili kushoto), Meenja wa Mpango wa
Uchagiaji wa Hiari wa PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, (kulia walosimama), wakishuhudia
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayinhu, (kushoto) na Kaimu MkurugeNzi Mkuu
wa NHIF, Michael Mhando, wakitia saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi
hizo mbili kushirikiana ambapo Wanachama wa PSPF wa Uchangiaji wa Hiari, watadhaminiwa
na Mfuko huo ili waweze kuingizwa kwenye utaratibu wa kupatia bima ya afya
kutoka NHIF. Makubaliano hayo yaklifikiwa leo Jumatano Novemba 18, 2015 makao
makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia
makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa
Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na
NHIF.
Makubaliano
hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa
PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M
Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10
wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla
hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa
PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadiz a serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi
Watanzania wote wanapata huduma za afya zilzio bora. “ Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais
inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa
huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema
Bw. Mayingu katika hotuba yake. Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael
Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea
katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye
uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa
maisha. wajasiriamali wadogo
ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika
shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam
Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando,
(wa pili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
Bw. Mayingu, (kushoto) na Bw. Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake
Bw. Mhando hotuba yake
Maafisa kutoka NHIF
Mwanachama wa PSPF, akisoma vipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Bw. Michael Mhando (kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro
Mwanachama wa mpango wa Uchagiaji wa
Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya, kutoka kwa mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omra Khalfan (kulia)
Mwanachama wa SPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin,akitoa maelezo wakati wa hafla hiyo
Meneja wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari,
PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (wa kwanza kulia),
na afisa wa PSPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika
wakwanza wa mpango wa Mfuko huo kuwapatia matibabu wanachama wake wa
mpango wa PSS
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi.Costantina
Martin, aliyesimama, akizungumza na maafisa wa NHIF, wakati wa hafla
hiyoMzee Mohammed Madenge, watatu kushoto), ambaye ni Mwanachama wa PSPF, wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neon la shukrani kwa niaba ya wenzake
















No comments :
Post a Comment