Friday, November 20, 2015

MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA WABUNGE KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TANO VIWANJA VYA IKULU NDOGO CHAMWINO MJINI DODOMA.


HA1
– Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya Wabunge wapya wa bunge la 11, walipokutana kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20, 2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mtoto Majaliwa mtoto wa Waziri Mkuu mpya kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA4
Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akimpongezwa na mkewe baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015.Picha na OMR
HA5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Peramiho, Mhe Jenister Mhagama, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi, Asham Abdallah Juma, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele , kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge Mchengerwa kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Viti maalum Kaskazini Unguja, Angela Malembeka, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
HA12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR

Arusha yawa mfano katika ukusanyaji kodi kieletroniki

images
Na Raymond Mushumbusi- Maelezo
Jiji la Arusha limekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na hatua kubwa iliyofikia  katika ukusanyaji kodi kwa halmashauri zake kupitia mfumo mpya wa ukusaanyaji kodi wa kieletroniki.
Hayo yamezungumzwa leo na na msemaji waOfisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Bi Rebecca Kwandu alipokuwa  akiongea na waandishi wa habari  juu ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali za serikali ulioanzishwa na TAMISEMI kwa lengo la kuboresha makusanyo ya mapato katika halmashauri zote nchini.
Bi Rebecca amesema jiji la Arusha limefanikiwa kuongeza mapato yake toka Tsh Billion 5 mwaka 2012/2013 hadi Tsh billion 10.7 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 214 huku mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo yameongezeka toka Tsh billion 1.2 mwaka 2013/2014 hadi Tsh Billion  4.8 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 400.
Aidha kwa mwaka 2015/2016 jumla ya Tsh Billion 8.2 zimetengw
a kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani sawa na asilimia 63 ya bajeti yote ya mapato ya ndani.
Naye Mwekahazina wa jiji la Arusha Bw. Kessy Mpakaya amesema mafanikio waliyoyapata ni kutokana na mabadiliko ya mfumo wa ukusanyaji kodi na tozo za serikali  kutoka mfumo wa kulipa kwa risiti mpaka mfumo wa kieletroniki ambao umewasaidia kuboresha ukusanyaji wa mapato ya jiji hilo.
“ Mfumo huu umetusaidi kutunza kumbukumbu za walipa kodi na makusanyo ya kodi kiujumla na pia fedha zilizokusanywa tumeziweka kwenye ununuzi wa vifaa, ujenzi wa barabara na miradi mbalimbali ya maendeleo” alisema Bw. Kessy.
Halmashauri nchini zinapaswa kufahamu kuwa teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo fikra za watumiaji wa mfumo na walipa kodi kubadilika.

ALEX MSAMA AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA TAMASHA LA KUSHUKURU DESEMBA 25, WAIMBAJI KUTOKA MAREKANI KUSHIRIKI

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi zake zilizopo Kinondoni Moroco wakati alipotoa mwelekeo wa maandalizi ya TAMASHA la Kushukuru linalotarajiwa kufanyika  Desemba 25  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kutoka  nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
Bw. Alex Msama amesema leongo la Tamasha hilo la Kushukuru ni kutoa shukura ni kwa mwenyezi mungu kutokana na kuijalia nchi yetu na kufanya uchaguzi uliokuwa haki na huru tukiwa salama kwa amani jambo ambalo tunapaswa kumshukuru mungu.
  Tumeshuhudia chaguzi katika nchi mbalimbali zinapitia Chanamoto nyingi zikiwemo Vurugu lakini nchini kwetu uchaguzi umepita salama na kutuletea kiongozi mchapakazi Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Msama ameongeza kwamba mbali ya waimbaji kutoka Tanzania kamati yake ya maandalizi iko  katika mazungumzo na waimbaji mbalimbali wa kimataifa kutoka nchini za nje. Kama vile Afrika Kusini, Marekani na Uingereza, Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa waimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Marekani kushirikishwa  katika matamasha ambayo Kampuni ya Msama Promotion imekuwa ikiyaandaa nchini Tanzania.
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la kushukuru, Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe.
3
Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari  kuhusu maadalizi yaliyokwishafanyika kwenye suala zima la ulinzi katika tamasha hilo.

Serikali yaboresha Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato

????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Na Georgina Misama Dar es Salaam
Serikali imeboresha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki katika mamlaka za serikali za mitaa.
Hayo yamesemwa na msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu leo jijini Dar es salaam.
Bi Rebecca amesema kuwa TAMISEMI imekuwa ikiendelea kwa nyakati tofauti kufanya maboresho mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kuzisaidia mamlaka hizo katika kuongeza mapato ya ndani na kuondokana na uteuzi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.
“Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI iliamua kuanzisha mfuko wa Local Governement Collection Information System (LGRCIS) baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa nyakati tofauti na zilionyesha kuwa hakukuwa na mfumo wowote wa kielektroniki kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Halmashauri” alifafanua Bi. Rebecca.
Mbali na hayo Msemaji huyo alisema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya kuanzishwa kwa mfumo wa LGRCIS ni pamoja na kupata taarifa za walipa kodi wa mamlaka za serikali za mitaa na kuhifadhiwa kwa usahihi katika kanzi data ya mfumo.
“ Kupata takwimu sahihi ya vyanzo vya mapato na kufanya usuluhishi kati ya kilichokusanywa na kilichotarajiwa kukusanywa, kuongeza mapato kwa kasi zaidi kwa kuwa na uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu, kuweka uwazi na uwajibikija katika makusanyo ya mapato,na kuhimarisha ulipaji miamala ya kodi na tozo itakayofanywa na walipakodi” aliongeza Bi Rebecca.
Pia alisema kuwa matarajio ya TAMISEMI ni kuwa mfumo wa LGRCIS utaleta mabadiliko makubwa katika Halmashaurina kuachana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu.
Hata hivyo teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo fikra za watumiaji wa mfumo wa walipakodi kubadili mazoea.

No comments :

Post a Comment