Sunday, October 4, 2015

MAMA SAMIA AFUNIKA TABORA, MAELFU WAFURIKA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofayika Octoba 4, 2015  kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Uyui katika jimbo la Tabora mjini.
Maelfu ya wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 4, 2015 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui, jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Nkenge lakini akashindwa katika kura za maoni, Mama Asupta Mshama, akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, Jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka akiomba kura katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia, uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, katika jimbo hilo mkoani Tabora.
Wasanii wa Bongo Movie, wakichangamsha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora.
Kiongozi wa wanakampeni wa Mama Ongea na Mwanao, wanaoundwa na kundi la Wasanii wa Bongo Movie, Steven Mengere maarufu kwa jina la Stev Nyerere, akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, katikajimbo la Tabora mjini mkoani Tabora. Kulia ni Msanii mwenzake wa Bongo Movie Wema Sepetu
Msanii maarfu kwa jina la Sina Nyonga, akionyesha umahiri wake wa kucheza sarakasi, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofayika  Octoba 4, 2015 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui jimbo la Tabora mjini.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Stara Thomas akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 4, 2015 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora.
Baadhi ya wasanii wakimuaga Mama Samia baada ya kumuombea kura Dk. Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 4, 2015 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui mkoani Tabora.
Vijana ambao ni Mashabiki wa CCM wakionyesha furaha zao wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika Octoba 4, 2015 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora.
Continue reading →

MAHAFALI YA KWANZA YA KIDATO CHA NNE KENYAMANYORI SEKONDARI MKOANI MARA YAFANA.

Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara George Ogutu akizungumza katika Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari Kenyamanyori iliyopo katika halmashauri hiyo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Ogutu alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ambayo yalifanyika jana Octoba 02,2015 katika Viunga vya Shule hiyo ambayo wakati inaanza kupokea wanafunzi wanaohitimu mwaka huu ilikuwa ni shule ya Kijiji cha Kenyamanyori na ilijengwa kwa nguvu za wakazi wa kijiji hicho ambao asilimia kubwa ni wakulima na wachache wakiwa ni wafugaji kwa msaada kidogo wa wafadhiri mbalimbali.
Wanafunzi 55 wanatarajia kuhitimu kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo.
 
Kwa sasa shule hiyo inapokea wanafunzi kutoka vijiji jirani kikiwemo kijiji cha Tagota ambacho kimeungana na kijiji cha Kenyamanyori na kuwa Kata moja ya Kenyamanyori. Awali vijiji hivyo vilikuwa katika Kata moja iliyojulikana kwa jina la Kata ya Turwa ambapo ilikuwa ikijumuisha vijiji vingine vitano kabla ya kugawanywa hivi karibuni.
 
Ogutu aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kujenga mahusiano mazuri na walimu jambo litakalosaidia kuongeza hamasa kwa waalimu katika ufundishaji. Pia aliwahimiza katika suala la kuendelea kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya shule hiyo.
Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara George Ogutu akizungumza katika Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari Kenyamanyori iliyopo katika halmashauri hiyo.
Mgeni Rasmi akiwa pamoja na Uongozi wa Shule ya Sekondari Kenyamanyori tayari kwa ajili ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa kwanza wa kidato cha nne katika shule hiyo.
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Kenyamanyori Sekondari akipokea Cheti cha Mwanafunzi mwenye nidhamu kutoka kwa mgeni rasmi
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne Kenyamanyori Sekondari akipokea Cheti kutoka kwa mgeni rasmi
Mwalimu wa taaluma akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa mgeni rasmi
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kenyamanyori Kabengo Zacharia akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kenyamanyori
Wazazi na Walezi wa Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kenyamanyori
Wazazi na Walezi wa Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kenyamanyori
Picha ya Pamoja katika Mgeni Rasmi na Wahitimu wa Kidato cha nne shule ya Sekondari Kenyamanyori iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara.
BINAGI MEDIA GROUP, INAWATAKIA KILA LA KHERI WAHITIMU WOTE KATIKA MTIHANI WAO WA MWISHO.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KATUMBA

 02
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia mkono wapenzi na wanachama wa CCM.
04
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Katumba wilayani Mlele ambako alimnadi mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Magufuli, wabunge na madiwani Oktoba 4, 2015
01
Baadhi ya wapenzi na wanachama wa CCM wakimshangilia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati  alipohutubia  mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Katumba wilayani Mlele ambako alimnadi mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Magufuli, wabunge na madiwani Oktoba 4, 2015.
((Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Kikwete na Rais Kenyatta Wazindua Barabara TAVETA

1
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakifunua vitambaa kuashiria kuanza ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Mwatate huko Taveta nchini Kenya Octoba 4, 205.Rais Kikwete leo ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Kenya.
5
6
Marais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Uhuru Kenyatta wa Kenya wakipeperusha Bendera za nchi zao kuzindua ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Mwatate huko Taveta nchini Kenya Octoba 4, 2015.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa eneo la TAVETA nchini Kenya ambapo alianza ziara yak e ya siku tatu kwa kuzindua ujenzi wa wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Mwatate huko Taveta.
4
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete eneo la TAVETA nchini Kenya muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
(Picha na Freddy Maro)

Rais Kikwete Azindua Jengo la Kuhifadhia Madawa la Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen Ijumaa Oktoba 3, 2015 . Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Seif S. Rashid na katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mhe Saidi Meck Sadick.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa  kwa  Mtendaji Mkuu wa CCBRT Bw. Erwin Telemans alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen. 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete viongozi mbalimbali  alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wadau alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa mabalozi wa nchi wafadhili  alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen.
Continue reading →

Wahitimu wa NBAA wameaswa kulinda, kutunza na kusimamia viapo vya taaluma yao.

07
Baadhi ya wahitimu wakijiaandaa kabla ya kuanza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
08
Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiongoza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
01
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiongea na wahitimu wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
02
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya kuongea na wahitimu wakati wa mahafali ya 37 wa Bodi hiyo pamoja na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
03
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa hotuba fupi kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
04
Baadhi ya wahitimu wa Bodi NBAA wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 972 walipata CPA na wahitimu 87 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
05
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akimpongeza mmoja wa wahitimu wa CPA aliyefanya vizuri kwenye mitihani yake wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
06
   09
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) na wahitimu CPA wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
..……………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wahitimu wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) ambao ni wataalamu wa masuala ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu wameaswa kulinda, kutunza na kusimamia viapo vyao wakati wakitekeleza majukumu yao ya kihasibu ipasavyo katika sehemu zao za kazi
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya NBAA yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
“Kiapo mlichoapa leo kiwe chachu ya ufanisi katika utendaji wenu wa kazi, kushuka kwa kiwango cha maadili katika utumishi kunatokana na kuota kwa mizizi katika suala la fedha”
Prof. Mwandosya aliendelea kusisitiza, “Mlinzi mkuu wa fedha katika sehemu yeyote ile ni Mhasibu, nanyi leo mnahitimu, mnapaswa kuwa waaminifu kwa familia zenu, taaluma yenu na kwa taifa mkiongozwa na kiapo mlichoapa, isiwe ni sehemu ya ajenda ya leo ya kutimiza wajibu, bali kiapo hicho kiwe cha kusisitiza maadili, uaminifu, uadilifu na uzalendo”.
Aidha, Prof. Mwandosya aliongeza kuwa Bodi ya NBAA na Watanzania wana wajibu wa kujenga fikra ya kizalendo kwa taifa lao na kujiamini katika masuala ya hesabu za fedha ili waweze kufikia viwango vya kimataifa kwa kuweka misingi imara kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ambapo mataifa mengine wavutiwe kuja kujifunza hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa taarifa ya Bodi hiyo kwa mgeni rasmi wakati wa maafali hayo alisema kuwa kituo hicho kimefanikiwa kinatoa mchango mkubwa nchi katika kukuza fani ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika mahafali hayo, idadi ya wahitimu imeongezeka mwaka huu na kufikia 972 waliopata CPA na wahitimu 87 kwa ngazi ya cheti cha utunzaji wa hesabu tofauti na hali ilivyokuwa mwaka jana 2014 ambapo kulikuwa na jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
Wakati huo huo, mmoja wa wahitimu hao Imelda Mzatulla alisema kuwa kiapo walichoapa kinawahamasisha kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa kanuni za maadili ya kiuhasibu na ukaguzi wa hesabu, kwa uaminifu, uadilifu na utaalamu kwa kuzingatia matarajio ya Serikali, muajiri, jamii na taifa kwa ujumla.
Kiapo hicho walichoapa wahitimu hao, pia kinawahimiza kuwa waendelee kushirikiana na kituo hicho cha NBAA kwa kuzingatia miongozo yote ya taaluma yao inayotolewa na Bodi hiyo nchini.

Hon. President of India presenting an Award for Best Medical Tourism facility to Apollo Health City, Hyderabad

Mr. Radhey Mohan (Vice president –
International Marketing, Apollo Health City, Hyderabad), Dr. Mahesh
Verma (Ministry of Tourism & Civil Aviation), Hon. Sh. Pranab
Mukherjee (Hon. president of India), Ms. Sangita Reddy (Joint Managing
Director, Apollo Hospitals Group) and Mr. Vinod Zutshi (Secretary –
Ministry of Tourism, Govt. of India).
Hon. President of India presenting an Award
for Best Medical Tourism facility to Apollo Health City, Hyderabad. This
is the third consecutive year that Apollo Health City, Hyderabad is
receiving this prestigious award.

WANAWAKE TOFATI ZENU ZA ITIKADI ZA VYAMA ZISIWAZUIE KUSHIRIKIANA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO – MAMA SALMA KIKWETE

X3Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre.
……………………………………………………………………….
Na Anna Nkinda- Maelezo, aliyekuwa Musoma
Wanawake wa mkoa wa Mara wameaswa kushirikiana kwa pamoja katika shughuli za maendeleo bila kuangalia tofauti ya itikadi zao za vyama kwa kufanya hivyo watajiletea  maendeleo yao kama wanawake.
Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa mkoa huo katika ukumbi wa mikutano wa Musoma Community Center (MCC) uliopo mjini Musoma.
Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema masuala yanayowahusu  wanawake hayana itikadi za vyama kwani maendeleo ni ya wote, katika mambo ya msingi waungane na kuwa kitu kimoja wasitenganishwe na watu.
Alisema ili wanawake waweze  kujiletea maendeleo ni lazima washikamane, wafanye kazi  kwa umoja na kutumia fursa zilizopo kwani  Serikali inasehemu yake ya kuwaleta maendeleo lakini maendeleo mengine yanahitaji jitihada zao binafsi.
“Sisi kama wanawake tunafanana kwa kila kitu tofauti iliyopo ni wajibu wa kila mmoja wetu katika jamii yake, shirikini kuchangia shughuli za maendeleo kama ujenzi wa barabara na shule kwa ajili ya watoto wetu na kuchangia huduma ya afya ili tuweze kupata huduma bora”.
Msiache kuzitumia fursa zilizopo wasimamieni  watoto wa kike wasome kwani wakiwa na elimu wataweza kujiajiri au kuajiriwa, wengine watakuwa viongozi wazuri miaka michache ijayo watawasaidia siku za baadaye”, alisisitiza Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwaaga wanawake hao na kuwashukuru kwa jinsi walivyokuwa wanamtia moyo katika kipindi chote cha miaka 10 ya utawala wa mme wake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jambo ambalo lilimpa ujasiri katika kufanya kazi zake za kuwasaidia wanawake na watoto wa Tanzania.
Mama Kikwete alisema, “Kazi yangu ninayoifanya kama mke wa Rais nimeitekeleza nilisema nitawasomesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu nimewasomesha, nimejenga shule ya watoto wa kike, nimewainua wanawake kiuchumi na nimesaidia kuimarisha afya ya mama na mtoto”, alisema Mama Kikwete.
Katika mkutano huo wanawake walipata fursa ya kuuliza  maswali mbalimbali na kuzitaja kero na changamoto zinazowakabili katika  maisha yao kama vile upatikanaji wa maji, uongozi, uchumi  na elimu.
Kwa upande wake Theresia Chacha ambaye ni mkazi wa Nyamagugu  wilaya ya Rorya alimshukuru Mama Kikwete kwa kumsomesha mtoto wake wa kike aitwaye Paschazia ambaye yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo Rufiji Mkoani Pwani.
“Mama Kikwete anasomesha watoto 15 kutoka mkoa wa Mara katika shule yake,  mwanangu ni mmoja wa watoto hao, anamgharamia  kila kitu hata nauli mama huyu  analipa mimi silipo chochote”.
Miaka yote hiyo sijawahi kumuona ndiyo namuona leo nakushukuru sana Mama, Mwenyezi Mungu akubariki naomba kiongozi ajaye aige mfano wako wa kuwasidia wanawake na watoto wa Tanzania”, Mama Chacha alishukuru.
Naye Anastazia Sangarya mkazi wa kata ya Mwisege ambae ni mjasiriamali alizitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na kupanda kwa ada ya ushiriki wa Maonyesho ya kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere maarufu kama sabasaba yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam kutoka shilingi 50,000 hadi 100,000.
Mama Anastazia alisema, “Sisi wanawake wajasiriamali tunaumizwa na ada kubwa ya ushiriki wa maonyesho ya sabasaba kwani tukishiriki licha ya kulipa kiingilio bado kuna gharama ya nauli na malazi”.
Kwa upande wa  mikopo tunayokopa benki riba yake ni kubwa na kama ikatokea umechelewa kurejesha kutokana na matatizo ya kifamilia benki haikuelewi tunakuomba mama yetu utusaidie kutatua changamoto hizi ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya wanawake wajasiriamali wa mkoa huu,”.
Mama Kikwete aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wanawake hao na kuwataka viongozi wao kuitisha mikutano ya mara kwa mara itakayosaidia kutatua kero zinazowakabili.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHUMBUNI USSI SALUM PONDEZA AMJADI, KATIKA MKUTANO WAKE WA KAMPENI VIWANJA VYA MABANDA YA NGOMBE CHUMBUNI UNGUJA.

 
Msoma Utenzi akisoma Utenzi maalum wakati wa Uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika Viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Zanzibar.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akiwa katika viwanja vya mkutano akishangilia na Picha ya Mgombea wake wa Ubunge kupitia CCM Ndg. Ussi Salum Pondeza AMJADI wakati wa mkutano huo
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Unguja.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwapungia mikono Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni wakati msoma utenzi akitaja majina ya Wagombea.
Continue reading →

SINA KINYONGO NA DK. MAGUFULI – PINDA

indexMhe. Mizengo Pinda
*Ataka watu watunze shahada zao
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mhe. Mizengo Pinda amesema yeye hana
kinyongo na uteuzi wa Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa
tiketi ya CCM kwa sababu anaamini kuwa Mungu alikwishamuandaa.
“Tulikuwa wengi kwenyhe kinyang’anyiro cha urais lakini Makamu wa Rais
ametolewa, Waziri Mkuu aliyepo ametolewa, Mawaziri Wakuu wastaafu
wametolewa, Majaji na mabalozi wametolewa, mawaziri wengine
wametolewa; hivi ni kwa nini useme kwamba wewe tu ndiye unayefaa
kuteuliwa? Ni kwamba Mungu alikwishamuandaa mmoja wetu,” alisema.
Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Oktoba 3, 2015) wakati akizungumza
kwa nyakati tofauti na wakazi wa jimbo la Mpanda Vijijini kwenye
mikutano minne ya hadhara iliyofanyika katika kata za Kasekese,
Kapalamsenga, Karema na Ikola.
“Magufuli ni muadilifu, ni mchapakazi, hana blah blah za kisiasa na
hapendi rushwa. Ni mtu anayetaka kuona matokeo na mwenye kujali watu
wanyonge. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu, ninamfahamu, ninaomba
mumpe kura ya ndiyo ifikapo terehe 25 Oktoba,” alisema Mhe. Pinda
wakati akimuombea kura Dk. Magufuli.
Akizungumzia mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mhe. Pinda alisema
Serikali ya CCM imefanya kazi nzuri kwa kufungua barabara za vijijini
akitoa mfano wa barabara ya Mpanda hadi Karema ambayo alisema
imeboreshwa tofauti na ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.
“Wakati huo ukitoka Mpanda kuja Karema ilimchukua mtu hadi siku tatu
wakati ni umbali wa km. 150 tu… leo hii mtu anatoka Karema hadi Mpanda
na kuunganisha mabasi ya Mwanza siku hiyo hiyo,” alisema.
Alisema katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015, Serikali ya awamu ya
tano imepanga kujenga reli mpya ya viwango vya kimataifa (standard
gauge) kutoka Kaliua kupitia Mpanda hadi Karema. Alisema anaamini reli
hiyo itakuwa ni kiungo cha kuleta maendeleo ya haraka kwenye ukanda
huo wa Magharibi.
Alisema Seikali itaendelea kuwaletea maendeleo wanandhi ikiwemo
kubotesha huduma za maji, umeme na mawasiliano ya simu.
Aliwataka wakazi wa jimbo hilo watunze shahada za kupigia kura na
wasikubali kurubuniwa na mtu yeyote iwe kwa fedha au kitu chochote.
“Usikubali kumpa mtu shahada yaka hata kama ni motto wako. Ninawasihi
mjitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura wala msisikilize vitisho vya
mtu yeyote kwamba hakutakuwa na amani,” alisema.
Mhe. Pinda alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la
Mpanda Vijijini, Bw. Selemani Moshy Kakoso pamoja na madiwani wa kata
zote nne.
Akiwa Karema, Mhe. Pinda alipokea kadi za wanachama waliorejea CCM
kutoka vyama vya CHADEMA NA ACT Wazalendo.

BONANZA LA MICHEZO MBALIMBALI KWA WANAWAKE WA JIMBO LA Tunguu-LAFANA

4
Mwenyekiti wa CCM Jimbo Tunguu Khatib Ramadhan Iddi akizungumza na washiriki wa CCM Bonanza lililofanyika Bungi Mkoa wa kusini.
1
Washiriki wa mchezo wa kukuna nazi wakishindana katika Bonanza la michezo ya Jimbo la Tunguu yaliyofanyika kiwanja cha Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
5
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali akimpa zawadi kepte wa tim ya Nage ya Bungi (B) Shida Saidi. (Kulia) mgombea Upunge wa Jimbo la Tunguu Khalifa Salim Suleiman.
2
Mshiriki wa mbio za Baskeli Zainab Juma akimaliza mbio hizo akishikilia nafasi ya nne.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Mchungaji Mtikila afariki katika ajali alfajiri leo OCTOBA 4, 2015

indexcMchungaji Christopher Mtikila
1Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Majira ya saa 10 alfajiri Octoba 4, 2015 kwa ajili ya gari Kijiji cha Msolwa Chalinze akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .

Dk Ali Mohammed Shein-kuiboresha sekta ya Uvuvi kwa kujenga kiwanda cha kusindika minofu ya samaki

indexZNa Masanja Mabula  -Pemba .
…………………………………….
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali MohammedShein ameahidi kuiboresha sekta ya Uvuvi kwa  kujenga kiwanda cha kusindika minofu ya samaki pamoja na kuwapatia mikopo  wavuvi .
Amesema kuwa  iwapo wananchi wa Zanzibar watamwamini  na kumchagua kuwa Rais wa Zanzibar kwa mara ya pili jambo la kwanza ni kuimarisha sekta ya uvuvi ambapo wavuvi watawezeshwa kwa kukopeshwa vifaa vya uvuvi ili waweze kufikia bahari kuu wa ajili ya uvuvi wa samaki .
Kauli hiyo ameitoa wakati akinadi sera za chama hicho pamoja  na kuomba kura kwa  wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika  kiwanja cha mpira Shehia ya Kiungoni Jimbo la Mgogoni Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba .
Dk Shein amesema kuwa anatambua kwamba wananchi wengi wa jimbo hilo wanajishughulisha na kazi ya uvuvi  , hivyo Serikali atakayoiongoza itasimamia uimarishwaji wa sekta ya Uvuvi lengo likiwa ni kutoa fursa za ajira kwa  vijana .
“Katika uongozi wa Serikali yangu utaimarisha sekta ya uvuvi kwa kujenga kiwanda cha kusindika minofuya samaki kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanajihusisha na kazi ya uvuvi nawaomba waniamini ”alifahamisha .
Akizungumzia sekta umeme, Dk Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi imeandaa  utaratibu wa kuwakopesha wananchi huduma hiyo  na  ambao umewawezesha wananchi wengi  kunufaika  na mkopo huo na  hivyo kuongeza kipato katika familia zao .
Amesema kuwa mafanikio hayo aliyaeleza mwaka 2010 wakati akiomba kura kwa wananchi na utekelezaji wake umefanikiwa kwa asilimia 85 jambo ambalo linampa imani ya kwamba anayoyasema atayatekeleza  katika  uongozi wake wa awamu ya pili iwapo atachaguliwa .
“ Katika kipindi cha miaka mitano tumefanya makubwa kwani huduma ya umeme tumekuwa tukiwakoposha  wananchi , na mpango huu umewanufaisha wananchi wengi haya yamo kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 ”alieleza .
Katika mkutano huo Mgombea huyo wa  Urais amepokea wanachama wapya 38 kutoka chama cha wananchi CUF na kutumia fursa hiyo kukemea tabia ya kunyanyaswa kwa wananchama hao baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi .
Amesema kuwa  Tanzania ilikubali  kuingia kwenye mfumo wa Vyama vya siasa ili kutoa fursa kwa kila mmoja kujiunga na chama cha siasa anachotaka , na kwamba kitendo cha kuwatisha kinakwenda kinyumena misingi ya demokrasia .
“Tanzania tuliridhia mfumo wa vyama vingi vya siasa , hivyo sio jambo la busara kutoa vitisho kwa wanachama wetu wanaohama vyama vya upinzani kwani unaenda kinyume na misingi ya demokrasia ”alisema Dk Shein . Naye Mjumbe  wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Mauwa Abeid Daftari amesema kuwa ahadi anazotoa  Dk Shein   zinatekelezeka na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga kwa kuhakikisha kwamba wanampigia kura nyingi katika uchaguzi  Mkuu baadaye mwezi  huu .
Mauwa amesema kuwa ni vyema  kupima sera za wagombea na kisha kufanya maamuzi sahihi wakati  wa uchaguzi oktoba 25 mwaka huu kwa kuwapigia kura wagombea wa CCM kuanzia urais wa Jamhuriya Muungano , Zanzibar ,wabunge , wawakilishi pamoja na madiwani .
“Ahadi za Dk Shein zinatekelezeka , nawaomba wananchi tusifanye kosa tufaneni  maamuzi sahihi kwa  kuhakikisha wanawapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ili waendelea kuwaletea maendeleo ya kweli ”alisisitiza Daftari .
Kwa upande  wake Balozi Amina Salim Ali amewataka vijana  kujiandaa kuboresha maisha yao  kwani Serikali imeandaa  mikakati  ya kuwafikisha katika uchumi wa maendeleo ya mafuta na gesi kutokana na mazingira yalioandaliwa na Serikali ya Mapinduzi kupitia Ilani yake ya uchaguzi .
Aidha Balozi Amina amesema kuwa waliohama CCM baada ya majina yao kukosa kupitishwa  ni walafi wa madaraka kwani wakati wanachukua fomu walikuwa wanafahamu kwamba anayehitajika ni mtu mmoja .
“Hata kama mtajitokeza  watu mia moja lakini anayehitajika ni mmoja tu , hivyo walioamua kuhama Chama wanasumbuliwa na ulafi wamaadaraka , hivyo kupitia CCM vijana wajiandae kunufaika na maendeleo ya uchumi wa mafuta na gesi ”alifahamisha Amina .
 Mapema Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete Kombo Hamad Yussuf amewataka wanaCCM kuwa wakweli na kuhakikisha kwamba mahudhurio yao kkwenye mikutano yaweze kuowana na idadi ya kura wakati wa uchaguzi ndani ya kisanduku

FREIGHT IN TIME (TZ) LTD, UPS’ AUTHORISED SERVICE CONTRACTOR IN TANZANIA HOLDS CUSTOMER EVENT

Mr Shamit Shah,Group Executive Director FiT
Mr Shamit Shah, Group Executive Director FiT.
Mr Dave(Centre) Freight in Time Financia Controller and guests
Mr Dave (Centre) Freight in Time Financial Controller and guests.
Mr Fred Mlay Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests
Mr. Fred Mlay, Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests.
victor maina, air and sea freight commercial manager
Victor Maina, Air and Sea Freight Commercial Manager exchanging views with the invited guests.
CEO sign industries M.P Esmail
CEO sign industries M.P Esmail giving a comment.
IMG_9978
Invited guests mingle during the event.
IMG_9889
Freight In Time (TZ) LTD (‘FiT’), the Authorized Service Contractor of UPS (NYSE: UPS), a global leader in logistics,opened its doors tovalued customers at a special event today at The Southern Sun Hotel in Dar es Salaam. The event highlighted FiT’s appreciation to local customers and in turn provided customers with an opportunity to meet FiT’s management and ask questions first hand.
FiTopened in Tanzania in 1997 and provides customers with a broad range of services with flexible pick-up and delivery times.  Since 2005, the company became the authorized service contractor in Tanzania ofUPS and has served its customers with the highest level of service backed by UPS’s world class network and technology, its focus on service quality, and a deep-rooted culture of precision and innovation..UPS is a recognized leader with expertise in international air freight forwarding, regional supply chain management and intra-Africa logistics. Customers can combine package and freight services for greater supply chain efficiency and cost-effectiveness.
Shamit Shah, Group Executive Directorof FiT commented, “FiT and UPS’partnership in Tanzania has gone from strength to strength over the last 10 years and we wanted to give something back to our loyal customers. The event is a testimony of our commitment to providing our customers with an efficient, reliable service. Providing a platform for discussion and interaction, the event also offered an opportunity to demonstrate our appreciation of their loyalty.”
“Our customers are at the heart of what we do, we will continue to support our clients to develop their businesses, through our global network and innovative services facilities”, he added.
FiTemploys 72 local citizens and operates at airports in Dar, Zanzibar, Kilimanjaro, Mbeya and Mwanza. UPS Border point offices include Namanga, Holili,HoroHoro, Tunduma, Kasumulu and Sirare, whilst also serving seaports in Dar Es Salaam and Mombasa.
UPS, a global leader in logistics with 435,000 employees worldwide, has been in the region since 1988, with its regional headquarters based in the UAE. The India Sub-Continent, Middle East and Africa region is the largest UPS region with more than 70 active countries. Through access to a worldwide network serving over 220 countries and territories, UPS is invested to the success of a daily delivery average of more than 18 million packages and documents.

MSIWAKEKETE WATOTO WENU – MAMA SALMA KIKWETE

imagesNa Anna Nkinda – Maelezo, aliyekuwa Tarime
…………………………………………………..
Wakazi wa wilaya ya Tarime wametakiwa kuachana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa mila za ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mwito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua uboreshaji wa Hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo mkoani Mara.
Mama Kikwete alisema ukeketaji unaleta matatizo  makubwa ikiwa ni pamoja na kupata matatizo wakati wa kujifungua, mtoto wa kike kupata maumivu makali wakati wa ukeketaji na pia kitendo hicho husababisha kutoka damu nyingi na matokeo yake ni kifo.
“Wazazi na walezi acheni mila hizi ambazo hazina faida kwa wakati huu na ni ukiukwaji wa haki za binadamu bali wasomesheni watoto wenu wa kike ili waweze kuwa walezi bora wa familia zao na jamii kwa ujumla”, alisisitiza.
Aliendelea kusema kuwa katika jamii baadhi ya wanawake wanadhalilishwa, kunyanyasika kijinsia na kupata mateso ya aina mbalimbali kama vile kupigwa, kunyimwa haki ya kumiliki mali na kutokuwa na maamuzi ya matumizi ya mali ya familia hata kama wao ndiyo wazalishaji.
Alisema, “Tabia hizi hazikubaliki kabisa katika Dunia ya leo.Mwanamke anayo haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu pia anayo haki ya kufanya maamuzi  ya pamoja kwa kile alichozalisha kwani mwanamke ni binadamu na siyo chombo cha kuzalisha mali. Binadamu wote ni sawa”.
Kwa upande wa  watumishi wa kada ya afya aliwahimiza kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia kwamba miundombinu ya Hospitali hiyo imeboreshwa  lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya hususani akina mama , watoto na wazee.
Mama Kikwete aliwaomba viongozi, kina baba na wadau mbalimbali  waliohudhuria uzinduzi huo  kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza  na hatimaye kuokoa kabisa vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika wilaya hiyo pia wahakikishe kina mama na watoto wanapata huduma bora za afya.
“Akina mama wajawazito wahudhurie kliniki muda wote wa ujauzio pia hakikisheni wanajifungulia katika vituo vya afya na hospitali. Wapelekeni watoto kliniki hadi watakapotimiza umri wa miaka mitano ili wapate kinga wanazostahili”,  aliwasihi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Dkt. Calvin Mwasha alisema wazo la uboreshaji wa Hospitali hiyo liliasisiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Glorius Luoga alipofanya ziara Hospitalini hapo mwanzoni mwa mwaka huu na kubaini kuna matatizo ya uchakavu mkubwa wa majengo.
Uchakavu wa miundombinu ya maji safi na taka, ubovu wa mfumo wa umeme, uchakavu wa vitanda na matandiko,uchakavu na uhaba wa vifaa tiba na vitendea kazi, uhaba wa madawa, ukosefu wa jengo la utawala na upungufu wa watumishi mbalimbali.
“Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya wilaya ya Tarime wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wakati, wachimbaji madini wakubwa (ACACIA North Mara Gold Mine) na wadogo, Taasisi za Umma na binafsi, watumishi wa Umma na wananchi walifanikiwa kuchanga shilingi milioni 345, mashuka 80 na vitanda tisa”, alisema Dkt. Mwasha.
Aliyataja maboresho yaliyofanyika kuwa ni majengo ya wagonjwa wa nje, akina mama na watoto, maabara, upasuaji ambapo mwanzo kulikuwa  na chumba kimoja cha upasuaji baada ya maboresho kuna vyumba vinne na jengo la upimaji virusi kwa hiari (VCT).
Wodi za wazazi, magonjwa ya akina mama na upasuaji, akina baba, TB wanaume na wanawake, majengo ya jiko ambalo kwa sasa litatumika kama jengo la kuhudumia wateja wa mifuko ya bima ya afya (CHF na NHIF) na jengo la ufuaji.Ujenzi ambao bado kuanza ni Jengo la utawala na sehemu ya kupumzikia  wagonjwa.
Dkt. Mwasha alisema kuna  vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 263 ambavyo vimeagizwa kutoka China kupitia kwa mwenyekiti wa maboresho Peter Zacharia. Kutokana na mahusiano yake mazuri na wafanyabiashara wa huko vifaa hivyo ambavyo bado  havijalipiwa vimeshafika wilayani Tarime.
Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine ya standard stabilizer moja, oxygen concentrator moja, vitanda 130, baiskeli za kubebea wagonjwa 20, mashine ya kupimia full blood picture moja, BP Machine Digital 50 na nguo za kuvaa wagonjwa.
Hospitali ya wilaya ya Tarime ilijengwa mwaka 1956 tangu kipindi hicho inahudumia wananchi wa wilaya  hiyo, Serengeti na Rorwa.

Happy birthday Hellen

New Picture (2)Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko wa kampuni ya Frontline Porter Novelli (FPN) Bi Hellen Kiwia akifurahia zawadi ya Champagne aliyopewa na wafanyakazi wenzie katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo hii, Happy birthday Hellen, live long.

Mama Samia Suluhu Asimikwa Umalkia Wilayani Maswa, Wamwita ngole

New Picture (1)
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
………………………………………………………………………………….
Na Thehabari.com
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan leo amepewa heshima ya kusimikwa kuwa malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na kupewa jina jipya la Ng’walu Majura.
Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo leo na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Magharibi kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Mama Suluhu ambaye amepewa jina jipya la heshima hiyo la Ng’walu Majura alivishwa mavazi maalum ya kimila ya heshima ‘Ngole’ yaani malkia na kukabidhiwa mkuki maalum, ungo na usinge pamoja na kupewa zawadi anuai za vyakula vya kimila kwa kabila la Wasukuma eneo hilo.
Wakimpa heshima hiyo akinamama wa UWT walisema Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo kwa kuwa ni mwanamke aliyekuja kuibua mambo mazuri kwa ushindi wa CCM na Tanzania kwa wanawake. Akinamama hao waliahidi kumuunga mkono ili kuhakikisha anashinda na kuwatoa kimasomaso Wanawakea wa Tanzania.
Kwa upande wake Mama Samia Suluhu amewashukuru akinamama hao kwa heshima na zawadi mbalimbali walizompa na kuwaahidi kupigania maslahi yao zaidi endapo chama chake kitafanikiwa kuunda Serikali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Alisema licha ya kupigania maendeleo ya taifa zima yeye kama mwanamama ana ajenda maalum za kuwapigania akinamama kuanzia huduma za kijamii hadi uwezeshwaji kwao ili kuleta usawa na maendeleo kwa jamii hiyo.
Alisema amepokea kilio cha maji Maswa na kwa kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa maji atahakikisha Maji yanapatikana kupitia miradi anuai inayotekelezwa eneo hilo na kwa kuanzia watachimba visima 10 maeneo mbalimbali ya Maswa ili kuwapatia maji wakazi wa maeneo hayo.
Mapema majira ya asubuhi Mama Samia Suluhu alifanya mkutano wa kampeni katika Jimbo la Meatu akiinadi ilani ya CCM kwa wananchi, ambapo aliwaomba kuichagua CCM kwani imepanga kufanya mengi kwa wanaMeatu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, ujenzi wa malambo na majosho kwa ajili ya kuhudumia mifugo yao.
Alisema ili kuondoa migogoro kwa wafugaji na wakulima safari hii Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kupima ardhi yote ya vijiji na Wilaya na kisha kuainisha mipaka ya wakulima na wafugaji na kuwamilikisha jamii hizo kumaliza migogoro.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MAMA SALMA KIKWETE AKIONGEA NA WANACHAMA WA UWT WA MKOA WA MARA.

X1Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono viongozi na wanachama wa UWT wa Mkoa wa Mara wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre kwa ajili ya mkutano wa ndani na wanachama hao-Octoba 3, 2015.
X3Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre.
X2Umati wa wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiongea nao Mjini Musoma.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

MO ATUA SINGIDA KUSHIRIKI MKUTANO WA KAMPENI ZA URAIS

IMG_4146
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_4126
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
IMG_4130
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.
IMG_4131
Watoto wakimpokea kwa shangwe aliyekuwa Mbunge wao jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Singida mjini kwa ajili ya kuhudhuria kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli pamoja na kumuombea kura kwa wana Singida.
IMG_4137
Pichani juu na chini ni Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na watoto waliojitokeza kumpokea uwanjani hapo.
IMG_4150
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiagana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Dkt. Magufuli, January Makamba kabla ya kuelekea kwenye viwanja vya Peoples Singida mjini ulipofanyika mkutano wa kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli. Kulia ni Msaidizi wa MO, Duda Jumanne.
IMG_4157
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akipata picha ya ukumbusho na wanaSingida wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MADEREVA DAR ES SALAAM

unnamed unnamedvRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Madereva katika Hotel ya Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam Octoba 3, 2015 .

MAMA SAMIA AMALIZA ZIARA SIMIYU

Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 3, 2015 katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma,
kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM,
Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 3, 2015
katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa
chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai.
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma,
kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM,
Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 3, 2015
katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa
chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma,
kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM,
Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Octoba 3, 2015
katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa
chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
Octoba 3, 2015 katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa
chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
Octoba 3, 2015 katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa
chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai.

JUSSA MWANASIASA MWENYE KUONA MBALI

Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema: “Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi…”. Pia Waswahili wanasema: “Akili ni nywele”
Mshitakiwa Karama aliipinga hoja ya Waziri Majivuno kwa kusema: “….Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima…”
Nimekuwa nikiyatafakari mafungu hayo matatu ya maneno ili kuona kama yana uhalisia wowote katika maisha yetu ya leo.
 
Pichani Ndugu  Saidi Mwamende akimuliza swali   Mhe: Jussa,  (Hayupo Pichani)
 
Hivi majuzi swahibu yangu Said Mwamende alinipigia simu na mara tu baada ya kuijbu, nilihisi sauti yake imejaa furaha, ndipo nikamwuliza ”umepandishwa cheo?” Akanijibu: “Hapana, bali nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania zinavyokwenda na nikakumbuka ule mkutano wa Mheshimiwa Ismail Jussa alioufanya na Wanadiaspora hapa Washington. Yale aliyoyasema ndiyo yanayoendelea kutokea hivi sasa”. Nikakurupuka kuchakura maktaba yangu kuitafuta rekodi ya mkutano ule ili nijikumbushe aliyoyasema Mheshimiwa Jussa. Baada ya kuiangalia tena, nikaona sehemu ambayo Swahibu yangu Said Mwamende alimwuliza Mheshimiwa Jussa swali ambalo lilihitaji mwono na mtazamo wa kina wa kisiasa: “Je, UKAWA, tuseme, kwa upande wa chama chako wewe atakuwepo Mheshimiwa Lipumba, na tuseme kwa upande wa CHADEMA Mzee wetu Mbowe. Watu hawa tayari wameshagombea Urais. Je hamuoni kwa CCM kwa sasa hivi kuna hombwe la aina fulani? Kuna Mheshimiwa Lowassa inawezekana kwamba hatogombea CCM kutokana na labda hawatomtaka. Mnafikiriaje UKAWA kama mtamchukua yule Lowassa ili mumuweke pale agombee?” Kwa ulimi wa fasaha kuliko wa Karama wa Kusadikika, Mheshimiwa Jussa alilijibu swali la Bwana Mwamende ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania katika Jiji la Washington na Vitongoji vyake (DMV), kwa kusema: “Katika siasa, wiki moja inaweza kuwa muda mrefu sana”. Aliendelea kwa kusema kuwa siyo Lowassa tu, anaweza kupitishwa Loawassa akaachwa mtu mwengine mwenye ugomvi na Lowassa vilele. Kwa sababu CCM hivi sasa siyo chama tena kinachowaunganishwa na itikadi. Kinachowaunganisha ni Escrow na kwamba kila mmoja atapata mgao wake kiasi gani”.
 Mhe: Ismail Jussa  akijibu swali la  Saidi Mwamende  (Hayupo pichani)
 
Katika mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu jijjini Washington, Bwana Ismail Jussa, aliwathibitishia Wanadiaspora wa Tanzania nchini Marekani pamoja na ulimwengu kwa ujumla kuwa Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima, lakini nadharia hiyo wakati wake umepita na hautorejea tena. Kwani katika kujibu swali la Katibu wa Jumuiya ya Watanzania kwaishio jijini Washington na vitongoji vyake Bwana Said Mwamende, Mheshimiwa Jussa alisema ni mapema mno kulitolea kauli swala hilo, ispokuwa “nitasema moja ambalo litatosheleza swali lako”

‘Moja’ hilo la Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mji Mkongwe, Zanzibar ambaye nywele zake bado ni nyeusi, linathibitisha kuwa nafasi hiyo aliyonayo kupitia ridhaa ya wananchi wa Jimbo lake hakuipata kwa sudfa tu, bali alistahiki na anaistahiki. Bali ni Mwanasiasa aliyekomaa na mwenye kuona mbali. “Nilisema mapema kwamba nazungumza na Mwenyekiti Mbowe, nazungumza na Mwenyekiti Lipumba na nazungumza na Mwenyekiti Mbatia. Sioni kwamba kwa wote hao kuna fikra ya ung’ang’anizi kwamba lazima niwe mimi”. Alisema Bwana Jussa kwa kujiamni, na kusisitiza “Hilo silioni kwa sasa hivi”. Upana wa wigo wa mawasiliano yake hayo unadhihirisha ukomavu wa akili yake, na kwamba fikra zake hazikufungika ndani ya vichochoro vya Mji Mkongwe, bali zimevuka Bahari ya Hindi na kuangaza Tanzania yote na hata nje ya mipaka yake. Mheshimiwa Jussa hakuwa anastawisha Baraza tu au ‘kumwondosha njiani’ Bwana Mwamende, bali alikuwa anazungumzia uhalisia wa mambo yanavyopaswa kuwa. Aidha hakuwa akitumia ulaghai wa kisiasa pale aliposema: “Na ninachojua ni kwamba viongozi wetu wanaangalia hata nje ya vyama katika kupata mgombea ambaye ataweza kuwakilisha vyema misimamo na ajenda ambayo UKAWA inaisimamia”. Bwana Jussa ambaye kitaaluma ni msoni wa Sheria, alidhihirisha wazi kipaji chake cha kuweza kushtukia na kufichua mbinu sa kisiasa zilizojificha. Aidha si mtu anayekhofu kuelezea maoni yake binafsi kwa manufaa ya umma. Haya yanaonekana alipoendelea kunena: “Nikwambie kitu kimoja, hili ni mawazo yangu binafsi: ‘Mimi nahisi CCM wana khofu na hilo unalolisema kama Chama. Na ndiyo maana tulikuwa tunajua sote kwamba CCM ilikwisha tangaza kwamba Mkutano wao Mkuu wa kumpata mgombea ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi wa April. Lakini juzi tulimsikia Nape Nnauye akisema kuwa kutokana na sababu ya kura ya maoni, na Bunge la Bajeti linofuata baadaye, itakuwa vinaingiliana. Kwa hivyo bora uakhirishwe mpaka baada ya Bunge la Bajeti’..” Kigogo huyo wa Chama Cha Wananchi CUF, aliitafsiri kauli hiyo ya CCM kama ni mbinu ya kuvuta wakati na kwenda karibu na uchaguzi wakidhani wataweza kuliepuka jambo hilo. “Kwa hiyo, tafsiri yangu ni kwamba wanataka kwenda zaidi, ili wakidhani wataweza kuliepusha hilo” Alichambua bwana Jussa ambaye kadiri nywele zake zinavyopotea, ndivyo akili zake zinavyozidi kukomaa.
Pichani Makamu Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Mwakilishi wa sasa wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa.
 
Tangu ujanani mwake, Mheshimiwa Ismail Jussa alikuwa akipenda kukaa na watu wazima akijua kuwa huko ndiko kwenye hazina za hekima na maarifa. Mwenendo wake huo, ndio uliopanua muono wake na kuweza kuichambua CCM na kuielezea kuwa ni Chama kilichopoteza mwelekeo, itikadi na misingi kiliyoasisiwa chini yake, na kwamba kilichobaki ni makundi makundi ndani yake yenye kupigania maslahi binafsi.
 
“Kwa jinsi ninavyoona, ile CCM ya Nyerere ambayo mpo pale kwa sababu ya Ujamaa na Azimio la Arusha haipo tena. Kilichobakia ni kwamba ni vipi kila mtu na kundi lake na rafiki zake watafanikiwa kupata nafasi wakavuruge nchi”
 
Jussa si mtu wa papara wala pupa, bali mtu ni mwenye subira, na alimtaka Bwana Mwamende kujiunga naye katika mbuga ya subira na kuupa nafasi wakati ufanye kazi yake.
 
“Kwa hiyo ninachosema, hayo tuyaachie wakati wake ukifika. Kama atatoka miongoni mwa hao, kama atatoka nje ya hao, au kama atatoka miongoni mwa viongozi wa UKAWA tuuachie wakati utasema”.
 
Aidha kwa mara nyengine alisisitza imani yake juu ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA juu ya msimamo wao wa kuwa na mgombea mmoja:
 
Nataka nikuhakikishie kuwa kwa upande wa UKAWA si hoja kwamba awe Lipumba, Slaa, Mbowe au Mbatia. Si hoja kabisa kwa sasa hivi. Hoja ni nani ataweza kubeba bendera ya UKAWA”
Mheshimiwa Jussa alimalizia jibu lake kwa kusema “Nadhani tutafika vizuri”.
 
Kauli hiyo ilikuwa inatabiria “Safari ya Matumaini” ya Mheshimiwa Edward Lowassa iliyogeuka na kuwa “Safari ya Uhakika”.
 
Naam, akili si nywele, na wala mvi si dalili ya hekima. Bali elimu ndiyo mwangaza, khaswa pale inapotiliwa nguvu na tabia ya kukaa na watu wenye busara. Maneno aliyoyasema Mheshimiwa Jussa tarehe 28 Februari 2015 nchini Marekani, ndiyo ambayo leo hii yanatuongozea siasa za Tanzania.

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM ZILIZOFANYIKA UWANJA WA KIUNGONI KOJANI PEMBA.

8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM,Wananchi wapenda amani waliohudhuria katika  mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM za kuomba kura wagombea nafazi za Uongozi katika Chama hicho,uliofanyika Octoba 3, 2015  uwanja wa Mpira Kijiji cha Kiungoni Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,
6
Baadhi ya wanachama wa CCM,Wananchi wapenda amani waliohudhuria katika  mkutano wa hadhara uliofanyika  Octoba 3, 2015 uwanja wa Mpira Kijiji cha Kiungoni Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  wakati alipozungumza nao.
5
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC Balozi Ali Abeid Amani Karume allipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kojani Wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kijiji cha Kiungoni  wakati wa  mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika Octoba 3, 2015  uwanja wa Mpira Kijijini hapo, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
9
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC pia Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kojani Wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kijiji cha Kiungoni  wakati wa  mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika  Octoba 3, 2015  uwanja wa Mpira Kijijini hapo, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
4
Baadhi ya Viongozi walioungana na mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM wakiwa katika uwanja wa Mkutano wa hadhara uliofanyika Octoba 3, 2015  katika jimbo la Kojani kijiji cha Kiungoni Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba  ikiwa ni mfululizo wa kampeni za CCM zinazoendelea.
1
Vijana waliojitoa katika Chama cha CUF na kuingia CCM wakinyoosha mikono juu kuonesha ishara ya kuunga mkono chama cha Mapinduzi kwa uwezo wake wa kuelezea sera zake kwa Wanachama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kiungoni jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Pemba leo,yake mbali mbali inayofanyika Unguja na Pemba,
2
Wananchi wa Kojani wakiteremka katika lori wakati walipoingia katika uwanja wa Mpira Kiungoni Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba palipofanyika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM.
3
Wapenzi na wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kojani kijiji cha Kiungoni Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba  ikiwa ni mfululizo wa kampeni za CCM zinazoendelea,
  7
Baadhi ya wanachama wa CCM,Wananchi wapenda amani waliohudhuria katika  mkutano wa hadhara uliofanyika leo uwanja wa Mpira Kijiji cha Kiungoni Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  wakati alipozungumza nao.
{Picha na Ikulu.]

RAIS Kikwete-kuongoza maelfu kuombea amani Jumapili Oktoba 4,Makhabane, Mahlangu watua kukoleza utamu

 Msanii wa nyimbo za Injili raia wa Uingereza, Ifheanyi Kelechi (katikati) ,
akiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini
Dar es Salaam, tayari kutumbuiza katika Tamasha la Amani linalofanyika leo
Uwanja wa Taifa Dar. Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions wanaoratibu
tamasha hilo, Alex Msama. Kushoto ni Mratibu, Hudson Kamoga.
(Picha na Francis Dande)
 ………………………………………………..
 
NA MWANDISHI WETU
 
RAIS Jakaya Kikwete kesho Jumapili Oktoba 4 anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya watanzania katika Tamasha
la kuombea amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, linalofanyika katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam
chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema maandalizi yote
yamekamilika ikiwemo kuwasili kwa waimbaji wa kimataifa Sipho Makhabane na
Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na Ifeanyi Kelechi kutoka nchini Uingereza.
Alisema waimbaji hao nguli wa muziki wa injili Afrika, wamekuja kuungana na wengine
mahiri wa hapa nchini kupamba Tamsha hilo la kihistoria litakalohudhuriwa na
viongozi wa kiroho wa ndani na nje ya nchi wakiwamo wachungaji zaidi ya 200 na
maaskofu 50.
Continue reading →

NHC YAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZA MOROCCO SQUARE,Waziri Kiruki aipongeza NHC kwa ufanisi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
(Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Wageni waalikwa.
 Wageni waalikwa.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Burudani ya muziki.
Burudani ikiendelea.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
………………………………………………………………………………………
Na Francis Dande
 
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela
Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa
kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya  makazi na biashara.
Waziri Kairuki aliyasema
hayo juzi  jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizindua  mauzo ya nyumba  za biashara
na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square,  Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.
Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na
wenzake kwa  kazi nzuri wanayoifanya kwa
kiasi kikubwa katika kuleta  uhai na
taswira nzuri ya  shirika hilo.
Alisema kuwa serikali inatambua kuwa  makazi
ni jambo  muhimu kwa maendeleo ya
taifa, ndiyo  maana imekuwa ikichukua
hatua  mbalimbali ili kuwezersha
sekta  ya nyumba kuwa endelevu na
yenye  tija kwa wananchi  na uchumi wa nchi.
Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza
sekta hii ni kuwa  na Sheria ya Mikopo ya
nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya  mwaka
2008,  iliyoanzishwa  kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya  nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa
nyumba  na taasisi za fedha  kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta
hii muhimu.
Aidha , alisema tangu kuwapo kwa  sheria
hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya  zaidi ya benki 50 zilizopo nchini
zikitoa  mikopo ya nyumba kwa  Watanzania, 16  kati ya
hizo zikiwa zimesaini makubaliano na
na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza
kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.
Naibu waziri huyo alisema kuwa  kutokana na
kuwepo kwa  changamoto  ya riba kubwa
ya  mikopo ya nyumbva inayotozwa  na benki mbalimbali ambayo ni kati ya
asilimia 18  na 25, serikali
itaendelea  kushirikiana na wadau
mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya
kuewezesha  benki  kupunguza riba  katika
mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua  nyumba.
Aliwahimiza Watanzania
kutumia  fursa zilizopo za mikopo
ya Benki kununua  nyumba zinazojengwa na
NHC, ikiwamo kujitokeza  kwa wingi
kununua nyumba hizo za  za mradi wa  Morocco Square ambao una nyumba za ofisi
hoteli, makzi na maduka makubwa.

MAHAFALI YA SITA YA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

PS1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Dr Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali
……………………………………………………………………
Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya wanataaluma waliosajiliwa. Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha  Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).
Aidha Bodi imepongezwa kwa kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.
 Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi kwa kuongeza  masomo ya maadili, ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni  mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika matumizi ya rasilimali fedha. “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa na Bodi.
Alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali, msingi na taaluma.
PS4
Mgeni Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja
PS5
Sehemu ya wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
PS3
Dk Hamis Mwinimvua akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi
PS2
Dk Hamis Mwinimvua katikati aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho  na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA YA LUPA ENEO LA NJIA PANDA ISANGA JIJINI MBEYA

Kipande cha barabara ya njia Panda Isanga karibu na Hotel ya Lifti Valey jijini Mbeya (LUPA WAY )ambacho kimejengwa upya kwa kuongezewa njia kimeleta sura mpya jijini hapa  lakini kimeleta pia changamoto kwa madereva hasa kwa nyakati za usiku  kwani hakuna taa hivyo nivema watumiaji wa barabara hii wakachukua tahadhari kwa kuto endesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zisizo za lazima …JAMIIMOJABLOG

Flaviana Matata ndani ya The Mboni Show

flaviana matata akihojiwa na thembonishow-10
Mwanamitindo wakimataifa Flaviana Matata ambaye anafanyia shughuli zake nchini Marekani , leo alikuwa kwenye kipindi cha Runinga cha The Mboni Show kama mgeni mwalikwa akiiwakilisha PSPF akiwa mmoja wa Balozi wa PSPF akiwakilisha DIASPORA.
Akiwa kwenye kipindi hicho sambamba na mwanadada Mboni Masimba alizungumzia masuala mbalimbali ikiwepo maisha ,familia sambamba na kazi zake kama balozi wa PSPF ndani na nje ya nchi.
PSPF ni wadhamini wa kuu wa The Mboni Show .
flaviana matata akihojiwa na thembonishow flaviana matata akihojiwa na thembonishow-9 flaviana matata akihojiwa na thembonishow-6
flaviana matata akihojiwa na thembonishow-18
mara baada ya show hadhira iliyokuwepo ilijiandikisha katika mpango wa kuchangia kwa hiari wa mfuko huu wa PSPF , Ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na mfungo huo ambao zaidi ya kupata mafao pia unaweza kukuwezesha kununua nyumba /viwanja / mkopo kwa wajasiriamali /wa elimu na mengi mengineyo.
flaviana matata akihojiwa na thembonishow-16ONJA RED CARPET

VYAMA VITANO VIMEKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Na Mwandishi Wetu
………………………………
Viongozi wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015
Tamko hili ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.
2. Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.
3. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea.
4.Viongozi wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na sio madhabahu.
5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6. Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.
7. Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.

DK. JOHN POMBE MAGUFULI:UKINUNULIWA IPO SIKU UTAUZWA, AJIRA NYINGI KWA VIJANA KUTENGENEZWA

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini Singida wakati akiomba kura za ndiyo kwa wananchi hao waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo mkubwa.
Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi kuwa makini kutokana na watu waliojipanga kununua shahada zao za kupigia kura na kusema wakatalieni wakija kununua shahada zenu za kupigia kura kwani mtu akija kununua shahada yako maana yake ni kwamba ananunua uhuru na haki yako na iko siku akitaka atakuuza ili kurudisha gharama zake.
Dk Magufuli ameongeza kuwa Serikali yake ina lengo la kutengeneza ajira za vijana waliomaliza vyuo vikuu  kwa kuwasaidia kiushauri na kuanzisha makampuni na serikali itawakopesha mitaji ili waweze kuendesha kampuni zao na kujiinua kiuchumi lakini pia kukuza uchumi wa wananchi masikini na taifa kwa ujumla.
Vijana  na wanawake wa vijijini pia watanufaika na mpango huo wa serikali kwa kuwakopesha mitaji ambapo kila Kijiji , Mtaa na Kata  watapewa mkopo wa  shilingi milioni 50,000,000. kwa ajili ya  kuwakopesha mitaji vijana na wanawake pale walipo.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani  nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu ukishirikisha wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SINGIDA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa wa Peoples mjini Singida leo na kusisitiza suala zima la watanzania kutoichezea Amani tuliyonayo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji akimpigia debe na kumuombea kura Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Singida mjini Ndugu Juma Sima  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mohammed Dewji katika mkutano huo. 
????????????????????????????????????
Vijana wa bodaboda wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa katika mkutano huo
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi na mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Ndugu Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakati akimuombea kura Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali wakiwa wamekaa meza kuu wakati mkutano huo ukiendelea.
????????????????????????????????????
Meneja wa kampeni za CCM na mgombea ubunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga Ndugu Januari Makamba akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida akihutubia umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo na kumuombea kura Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wananchi wakifuatilia hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Umakini wa kusikiliza sera wakati wa hotuba hiyo iliyotolewa na Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Picha mbalimbali zikionyesha umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wagombea udiwani wa Singida mjini wakinyanyua mikono yao juu wakati wakiomba kura kwa wananchi kwenye mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaombea kura  mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Bw. Juma Sima na wagombea wa viti maalum mkoa wa Singida kutoka kulia Bi. Asha na Martha Mlata kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananfunzi wa chuo cha Uhasibu mkoani Singida kutoka Team Magufuli wakimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Msafara wa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Tarafa ya Ilongelo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakifurahia kumuona Dk. John Pombe Magufuli wakati alipowasili Kiomboi. 
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mjini Kiomboi ambako alifanya mkutano wa kampeni.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi Ndugu Mwigulu Nchemba katika mkutano uliofanyika mjini Kiomboi.
????????????????????????????????????
Msafara wa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ukivuka mto Sibiti wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambao daraja lake limeharibika na haliwezi kupitika kwa sasa jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wananchi, Dk. Magufuli ameagiza Meneja wa Tanroad mkoani Singida kuanza mara moja ukarabati wa daraja hilo ili wananchi waanze kulitumia.
????????????????????????????????????
Daraja la Sibiti lililoharibika.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wa Sibiti  wakimkaribissha Dk. John Pombe Magufuli kwa ndelemo na vifijo wakati alipopita katika kijiji hicho.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wa Nduguti wakiwa katika mkutano uliofanyika kijijini hapo huku wakiwa juu ya mawe na miti.
????????????????????????????????????
Ni Full mzuka tu mbele ya Dk. John Pombe Magufuli
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nduguti.
????????????????????????????????????
Mamia ya wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika tarafa ya Ilongelo jimbo la Singida Magharibi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni tarafa ya Ilongelo Singida vijijini.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Singida Magharibi Ndugu Lazaro Nyalandu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilongelo Singida Vijijini.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples.
????????????????????????????????????
Msanii Msami na kundi lake wakifanya vitu vyao jukwaani.
????????????????????????????????????
Mh. Temba kulia na Chege wakionyesha burudani saafi katika mkutano huo.

No comments :

Post a Comment