Friday, October 30, 2015

DKT. MAGUFULI ASHINDA URAIS WA TANZANIA 2015, JK AMPONGEZA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015

WAFUASI wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, wakishangilia baada ya mgombea kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli, kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, Jaji mstaafu, Damian Lubuva, amemtangaza leo Oktoba 29, 2015, Dkt John Pombe Magufuli kwa kupata asilimia 58.16 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake mkubwa mgombea wa UKAWA, Mh, Edward Lowassa, amepata asilimia 39.97 ya kura zote.






No comments :

Post a Comment