Siku ya mahafali. Mfumo wa hifadhi ya jamii unaonufaisha
wigo mdogo wa nguvukazi kwa sehemu kubwa ya gharama ya sekta isiyokuwa rasmi na
ambao hawana kazi ambapo idadi kubwa wakiwa vijana waliaomaliza elimu ya shule ya
msingi, sekondari na vyuo vikuu nchini
Wiki
iliyopita tuligusia baadhi ya mambo yanayosababisha kuwagusa sana wachangiaji
wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii hasa pale wanapokuwa wanapoteza
uanachama na kinga yao ya hifadhi ya jamii pale wanaondoka au kuhamia mfuko
mwingine wa pensheni ya hifadhi ya jamii wakiwa ndani ya nchi na akivuka mpaka
na kwenda nchi nyingine.
Lakini
kuna mifano kutoka katika nchi fulani za kiafrika ambazo zimefanikiwa
kutekelezwa katika bara hili la Afrika kwa kutumia kanuni zinazokubalika hapa
ulimwenguni, mfano mzuri ni pale kama nchi jirani zetu za Zimbabwe na Malawi
jambo kama hili la kuhamisha kinga ya hifadhi ya jamii mtu akivuka mpaka na kwenda
nchi nyingine pale wanapoondoka au kuhamia mfuko mwingine wa hifadhi ya jamii
hufanyika bila usumbufu na hivyo bila kupoteza uanachama na kinga yake ya
hifadhi ya jamii.
Jambo
la tatu ni kwamba, mfumo wa pensheni wa hifadhi ya jamii umekuwa ni eneo ambalo
imekuwa na ufahamu mdogo wa kujaribu kuelezea mfumo kamili juu ya sera za jamii
ambazo zinaweza kuungana na kuhusiana na sera za kiuchumi za nchi husika. Kwa
mantiki hii hivyo kuna haja kubwa ya kuweka msukumo mkubwa kati ya sera za
kijamii na sera za kiuchumi ili kufanya kazi kwa pamoja lengo likiwa ni kuleta mabadiliko
ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Lengo
la sera za kijamii na hata kwenye malengo ya milenia kwa nchi ya Tanzania hasa
katika eneo la mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii iwe ni kupunguza na
kuondoa umasikini na ubaguzi, na kusaidia lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuwa na msingi mkubwa wa kodi kwa ajili ya
mapato ya serikali.
Hata
hivyo bado mfumo huu unachangia sana kuleta tofauti kubwa za kijamii, na hata
kati ya wanachama wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu mafao yanayotolewa na jinsi
ya kukokotoa pensheni unafuata wastani wa mishahara mizuri mitatu ya mwisho ya
mfanyakazi ya mwezi, na idadi kubwa ya wafanyakazi ni wa kima cha chini na
anapofikia kustaafu hupata pensheni ya chini zaidi na zaidi ukilinganisha na
mfanyakazi aliyekuwa akipata mshahara wa kima juu zaidi yake kwa mwezi. Na hii
inaonesha au kudhihirisha wazi ya kuwa michango ya wafanyakazi wa kima cha
chini ambao ndio wengi zaidi inasaidia kuwalipia pensheni kubwa wafanyakazi wa
kima cha juu zaidi.
Lakini
pamoja na hayo, picha inaonekana wazi ya kuwa kuna ongezeko kubwa la sekta
isiyokuwa rasmi na mfumo wa watu wengi kutokuwa na kazi, wakati huo huo sekta
iliyo rasmi ikiwa kwa ujumla inadidimia kila siku kukicha, na hata ushahidi
unaonesha ya kuwa karibu idadi kubwa ya wafanyakazi ambao ni wanachama wa
mifuko hii ya hifadhi ya jamii wanazidi kuondoa michango yao na kukimbilia
kujiunga na sekta isiyo rasmi.
Kushikiria
kwa makini kwa ajili ya kuboresha mabadiliko ya manufaa ya mifuko ya pensheni
ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya mfumo unaonufaisha wigo mdogo wa nguvukazi kwa
sehemu kubwa ya gharama ya sekta isiyokuwa rasmi na ambao hawana kazi ambapo
idadi kubwa wakiwa vijana waliaomaliza elimu ya shule ya msingi, sekondari na
vyuo vikuu nchini kwa kweli hili ni jambo lisilokuwa la usawa na kutovumilika
ambapo moja kwa moja linaonesha kumwelekeza na kuisukuma serikali kuwa angalifu
pamoja na wadau wengine wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini juu ya idadi kubwa
ya watu kuwa na kinga ndogo ya hifadhi ya jamii. Hivi karibuni, ingawa ni
Afrika na sehemu zingine katika ulimwengu unaoendelea, ubunifu na njia za
kusadiana pamoja zimekuwa zikichukuliwa na kufanyiwa kazi kwa ajili ya kupanua
kinga ya hifadhi ya jamii kwenye sekta isiyo rasmi.
Mwisho,
sababu kwa nini mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii hapa nchini mara kwa
mara imekosa uaminifu na shukrani kutoka kwa wanachama na wadau wengine, hii
inaonesha wazi ya kuwa kumekosekana na viwango vinavyotakiwa taasisi hii ya
sekta ya hifadhi ya jamii na serikali kuvitumia katika uendeshaji na utendaji wa
kila siku kama vile viwango vya huduma bora kwa wateja
Inapendekezwa
ya kuwa, kwa ajili ya kushawishi kuleta maendeleo nchini kuna haja kubwa
kupanga viwango vinavyotakiwa katika ngazi ya nchi na hata katika ngazi ya Afrika
Mashariki kwa kutumia mfumo wa haki za binadamu, kwa kutumia mwongozo wa
viwango vya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutumia viwango vya Kimataifa huenda
vikasaidia sana kukubalika kwa mfumo wa pensheni wa hifadhi ya jamii katika
nchi zetu za Afrika Mashariki
Christian
Gaya ni mwanzilishi wa kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa
masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa barua pepe: gayagmc@yahoo.com na kwa habari zaidi za
kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni simu namba +255 655 13 13 41
No comments :
Post a Comment