Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha.
Mwasilishaji wa mada Hossana Mpango akizungumza na washiriki (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo.
Washiriki wa warsha ya siku moja ya
ujasiriamali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF).
Na Mwandishi wetu
SERIKALI imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kisera kuwezesha kukua kwa viwanda vidogo na vya kati nchini.
Kauli hiyo imo katika
utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF)
kuhusu ukuaji wa sekta hiyo katika muktadha wa upatikanaji wa fedha.
Akiwasilisha utafiti huo
mmoja wa watafiti Hossana Mpango alisema kwamba kwenye utafiti wao
wamebaini mgongano mkubwa wa kisera na utendaji, unaosababisha kukwama
kwa maendeleo ya sekta hiyo.
Alisema ingawa kuna tatizo
kubwa la ajira ambalo limefanya watu wengi kukimbilia kujiajiri
wenyewe, kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo hasa sera na uwapo wa
mlolongo wa taasisi zinazopishana mamlaka na huku wakiwa ndio wanatoa
leseni.
Alizitaja taasisi hizo
zinazopishana mamlaka kama Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) mamlaka ya kodi (TRA) halmashauri mbalimbali
nakadhalika.
Alisema mabadiliko ya
kisera yatawezesha kutengeneza muundo unaojali ukuaji wa sekta hiyo hasa
kwa kuangalia kodi zinazolipwa ambazo kwa sasa ni za aina moja bila
kuangalia uwekezaji unaohusika.
Sekta hiyo ya wajasirimali
wadogo na wa kati yenye watu milioni 3 kwa mujibu wa utafiti wa mwaka
2012 inakabiliwa na tatizo la kutokua kutokana na vikwazo mbalimbali
vikiwemo pia kukosekana kwa mafunzo ya ujasirimali na uwezo wa kupata
fedha za mtaji.
"Ni dhahiri upatikanaji wa
fedha kutoka nje ili kuendeleza mtaji ni tatizo. Lakini tatizo hili
linakuwagumu zaidi kutokana na riba kubwa, uchelewefu wa kupata mikopo,
rushwa katika utoaji na ukosefu wa nidhamu ya fedha kwa wakopaji”
alisema Hossana.
Alisema pamoja na mambo
hayo kuna matatizo mengine makubwa yanayokwamisha ukuaji wa sekta hiyo.
Matatizo hayo mengine ni gharama kubwa zinaootokana na haja ya kukidhi
masharti ya uendeshaji wa viwanda hivyo vidogo na vya kati, tozo
zinazojirudia, ukosefu wa soko na elimu ndogo ya wajasirimali.
Alisema mabadiliko ya
kisera yatasaidia kuimarisha sheria na kuweka sawa mwelekeo wa sekta
hiyo kwa kuzingatia kwamba inahitaji mchango mkubwa wa nje ili kukua.
Alisema mathalani ingawa
kuna SACCOS, taasisi hizo zinashindwa kwenda kukopa kutokana na riba
kubwa na kuwapo kwa mfumo wa kodi na makato mengine yakiwemo ya tozo
usiokuwa na tija.
Alisema suluhu nyingine
inayostahili kufanywa ni kwa taasisi za kifedha kufuata tabia njema za
kimataifa za utoaji wa mikopo unaozingatia pamoja na mambo mengine
ukubwa wa mikopo na malipo kwa kuangalia manufaa ya kiuchumi.
"Ili viwanda hivi vya
chini na kati kukua masuala ya kifedha na yasiyo ya kifedha ni lazima
yaangaliwe na kushughulikiwa..." alisema.
Matatizo mengine ni pamoja
na sekta hiyo kukosa msaada huku taasisi mbalimbali zinazohitaji
kushirikiana zikifanya vitu kila mmoja na wake.
Taasisi hizo ni SIDO, TRA, WDF, YDF, BRELA na pia miundombinu inayokera katika maeneo hasa ya vijijini.
Pia ili kukuza sekta hiyo
ni vyema serikali ikatengeneza miundombinu inayojkidhi haja ya ukuaji wa
sekta hiyo kama maghala, masoko, barabara, maji, umeme kwa lengo la
kupunguza gharama za kufanya biashara.
Pia utafiti huo ulishauri
kwamba serikali ni lazima kutenga fungu ambalo litatumiwa na taasisi
kama SIDO, NEEC na hata maofisa biashara wa wilaya kwa ajili ya mafunzo
ya ujasirimali na uendeshaji wa biashara.
Mapema Mkuu wa idara ya
utafiti na machapisho wa ESRF Profesa Fortunata Makene, aliwataka
washiriki wa warsha hiyo kutoa michango katika kuboresha uelewa ili
serikali iweze kutatua kizungumkuti cha ukuaji wa sekta hiyo.
SUPERSPORT KWENDA LAIVU ALL AFRICAN GAMES
Meneja Mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa
Kusini mwa Afrika, Graeme Murray akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa habari kutoka nchi za Afrika (hawapo pichani) katika hoteli ya
OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.
Na Modewjiblog, Mauritius
WAKATI leo
michezo ya 11 ya All African games chaneli ya SuperSport imetangaza
rasmi kwamba watashika usukuni wa kurusha matangazo ya michezo hiyo
kupitia SuperSport 9 Michezo hiyo imeanza juzi.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika mkusanyiko mkubwa wa MultiChoice uliohusisha
waandishi wa habari, masupastaa na chaneli wanazofanya kazi nazo katika
hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.
Akiwa mtu kati Naicker
alisema kwa kujiamini kwamba urushaji wa matangazo hayo ni sehemu ya
uuzaji wa sura ya michezo ya Afrika katika mabara mengine.
Akiwa katika mazungumzo
hayo ambayo yalioongozwa na mmoja wa watu wanaotoa burudani kubwa ya
utangazaji ndani ya SuperSport, Carol Tshabalala alisema hali hiyo
inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta nzima ya burudani
na michezo na kampuni ya MultiChoice.
Mkuu wa masoko wa
SuperSuport, Motheo Matsau akifurahia jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari katika visiwa vya Mauritius.
Katika mazungumzo hayo
ambapo pia alikuwapo Mkuu wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau,
Meneja mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray
na mgeni maalum Anthony Baffoe, mchezaji wa zamani wa kimataifa na
Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Naicker alisema ubora wa chaneli yake
unatokana na kuweza kunoa vipaji vya watangazaji wake kufikia kiwango
cha juu kabisa cha ubora.
Kama mwekezaji mkubwa wa masuala ya michezo katika bara la Afrika, SuperSport imepata matokeo ya kuridhisha na yenye tija.
“Mwaka 2006 tulipeleka
kundi dogo la watu 26 Abudja kutangaza mpira lakini leo hii tunaringia
kuwa na asilimia 100 ya watangazaji wenyeji wakifanyakazi zao katika
nchi za Nigeria na Ghana,”alisema Murray.
Baffoe naye aliongeza
kwamba mchango wa SuperSport umeongeza zaidi ya utangazaji na kuwezesha
kuongezeka kwa kiwango cha uprofesheni katika ligi mbalimbali barani
Afrika.
Mchezaji wa zamani wa
kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Anthony Baffoe akifafanua
jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
“SuperSport iliweka msingi
wa utoaji leseni kwa klabu, kuwaelimisha watawala, kuweka viwango vya
msingi katika viwanja, kusaidia kuanzishwa kwa umoja wa wachezaji,
kuwafanya wachezaji kuwa wadau muhimu katika ligi na kuwaruhusu
wajipange kwa maisha nje ya soka,” alisema.
Murray alielezea jinsi
watangazaji walivyoweza kujishirikisha katika ligi za wenyeji kama mfano
bora namna ambavyo Supersport imesaidia michezo katika bara hili
“Tulianza kushirikiana na
Ligi Kuu ya Nigeria mwaka 2006 na imeendelea kukua mwaka hadi mwaka,”
alisema. “Tuliweza kuingia katika Super Eagles’ League ya Nigeria na
ligi ya kikapu ya Nigeria, ligi zote mbili zinafanya vyema kuliko hapo
awali.Tumekuwa washirika wa Ligi Kuu ya Kenya kuanzia mwaka 2008 na Ligi
Kuu ya Ghana toka mwaka 2012. Inatakiwa kukumbukwa kwamba kabla ya
kuingia kwetu Kenya hakuna hata mechi moja ya ligi iliweza kutangazwa
katika runinga na sasa ligi inazidi kukua.”
Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Aidha SuperSport katika
siku za karibuni imekamilisha mkataba na waendeshaji wa Ligii kuu ya
Zambia kuendelea kuonekanakana katika Supersport kwa miaka mitano ijayo.
Aidha chaneli ya SuperSport inajipanga kuanzisha jarida nchini Zambia litakalouza soko la Zambia kwa mataifa ya Afrika.
Mkuu wa masoko wa
SuperSport, Motheo Matsau pia ameongeza kwamba kunahitajika kuuza kwa
michezo bara la Afrika na kwa yakini kama maendeleo yaliyopo
hayataonekana kwa dunia , itakuwa hakuna maana, kinachojalisha ni kwa
kadamnasi ya kimataifa kujua kwamba Afrika ina vipaji bora kabisa katika
michezo.
Alisema kupitia matangazo
ya chaneli hiyo kunaonesha kwamba mauzo yanaleta faida kama ulivyo
mchezo wenyewe na hilo ndilo linafanya Super Sport kuwa chaneli bora
zaidi duniani.
Wakati mtu akitoka katika
mafunzo ya utangazaji ya chaneli hii anajua michezo na ajui namna
ambavyo masuala ya utangazaji yanavyofanyakazi. Watu hawa wanakuwa
mabalozi wetu na vyanzo muhimu sana vya habari.Tunatia SuperSport uhai
kwa kuwakutanisha watu hawa.”
Naicker katika mazungumzo
hayo alisisitiza kuendelea kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya
SuperSport na wadau wa michezo wa bara la Afrika.
“Sisi si kwamba tunalipa
fedha kwa ajili ya kupata kibali cha kutangaza au kupiga picha za video
tukio la burudani hii, lazima kuwepo na utoaji wa elimu, mchakato
unaostahili kukabiliwa na pande zote mbili.
Tunapaswa kujua muda gani
unastahili kuchezwa na mambo gani ambayo hayastahili kuyatangaza.
Tumetengeneza kijarida cha utangazaji ili kila mmoja aweze kusoma
kuwasaidia wengine katika mchakato wa namna matangazo yanavyorushwa na
ushawishi wake lojistiki, usahihi wa muda na upangaji fixtures.
Tunataka ujenga ushirikiano wenye ufanisi kwa muda mrefu,” alisema.
Naicker pia alitumia nafasi hiyo kuelezea furaha yao ya kupata zabuni ya kutangaza michezo ya olimpiki ya mwaka 2016.
Carol Tshabalala wa Supersport akiendesha mkutano na waandishi wa habari.
“Tutakuwa chaneli nyingi za michezo hiyo, kiwango cha chini kabisa zikiwa ni chaneli 6 kwenye SuperSport bouquet,” alisema.
“Tutarusha kila tukio
ambalo mwafrika ana nafasi ya kutwaa medali. Tumetengeneza makundi ya
watangazaji na timu zao kufuatilia timu za Kiafrika katika tukio hilo
kubwa. Aidha tayari tumeshaanza mazungumzo na mamlaka kubwa za michezo
katika nchi za bara la Arika kujua watu ambao wanaweza kutwaa medali ili
kuanza kuandaa stori zao kuelekea michezo ya Olimpiki.”
“Tunajivunai si tu kuwa watangazaji wazuri wa michezo katika bara la Afrika, bali duniani,” anasema Naicker.
Kwa kuwatumia masupastaa
wa Afrika kama akina Sammy Kuffour kuelezea masuala ya kiufundi na
utaalamu wa ndani unachokiona, kusaidia kunyanyua michezo kutoka katika
ngazi za awali chini kabisa kwa kuwa na miradi maalumu, SuperSport
inaongoza katika kuelezea mafanikio ya Afrika katika michezo kwa mataifa
mengine duniani.
Mwandishi wa habari hizi
na wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika wapo nchini Mauritius katika
moja ya maonesho makubwa ya watoa burudani kwa njia ya televisheni na
video ya MultiChoise wanaotumia mtandao wa DSTV na GoTv.
Carol Tshabalala wa SuperSport.
Mgombea Mwenza Urais CCM Ahaidi Neema kwa Wajasiliamali Dar es salaam
Mgombea mwenza wa kiti cha urais
Bi. Samia Suluhu akiwapungia mkono wanaCCM na wananchi wengine
waliohudhuria mkutano wake wa kampeni alipowasili uwanja wa Yombo Buza,
Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Temeke, Abass Mtemvu jijini Dar es Salaam akizungumza katika
mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu leo katika uwanja wa Yombo Buza,
Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha burudani ya kughani kwa semi cha FATAKI kikiburudisha wanaCCM na wananchi waliohudhuria
mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu leo katika uwanja wa Yombo Buza,
Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais MamaSalma Kikwete akimkabidhi Ndugu Hassan Kaunje ilani ya Uchaguzi ya
Chama Cha Mapinduzi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hizo tarehe 3.9.2015.
Mjumbe
wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimtambilisha rasmi
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Manispaa ya Lindi Ndugu
Hassan Suleiman Kaunje kwa wanachama wa CCM na wananchi wakati akizindua rasmi
kampeni hizo kwenye uwanja wa Fisi huko Lindi tarehe 3.9.2015.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Manispaa Mama Salma
Kikwete akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF na Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Mitandi Ndugu Laibu Kaisi aliyeamua kurejea Chama Cha
Mapinduzi wakati wa sherehe za uzinduzi rami za kampeni za Chama hicho katika
Manispaa hiyo.
Baadhi
ya vijana wakimshangilia kwa vifijo Ndugu Hassan Kaunje, Mgombea Ubunge kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uzinduzi
rasmi wa kampeni hizo katika Wilaya ya Lindi Mjini tarehe 3.9.2015.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha
Mapinduzi, (CCM) wa Wilaya ya Lindi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiongozana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini Ndugu Hassan Suleiman
Kaunje wakiwapungia mikino mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi
rasmi wa kampeni kwenye Jimbo kwenye uwanja wa Fisi uliopo Manispaa ya Lindi
tarehe 3,9.2015.
Baadhi
ya vijana wakimshangilia kwa vifijo Ndugu Hassan Kaunje, Mgombea Ubunge kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uzinduzi
rasmi wa kampeni hizo katika Wilaya ya Lindi Mjini tarehe 3.9.2015.
Mwenyekiti
wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya CCM
Bwana Abdallah Majura Bulembo wakiingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam ambapo alifungua mkutano wa Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Mkoa
na Wilaya leo Septemba 3, 2015. Katika tukio linguine, Rais pia alikutana na
ujumbe wa bunge la Burundi ukiongozwa na Spika wa bunge hilo Mhe. Paschal Nyabenda
na naibu Spika Agaton Rwassa Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na spika wa Bunge la Burundi Mhe.Paschal
Nyabenda(kushoto) na Naibu Spika wa Bunge la Burundi Mhe.Agathon Rwasa muda
mfupi baada kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salam leo mchana.Spika huyo
na ujumbe wake walimtembelea Rais Kikwete leo.
LOWASSA, MBOWE WAANZA KUPASUA ANGA KWA CHOPA, MPANDA "KWATAPIKA" , WAELEKEA KIGOMA
Kwa mara ya kwanza tangu mgombea wa
kiti cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CHADEMA,
akiwakilisha vyama vya UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akifuatana na
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wameanza kuruka kwa chopa
"kushambulia' mikoa ya Magharibi ambapo leo Septemba 3, 2015, wametua
Mpanda, mkoani Katavi na kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye
shule ya msingi Shule ya Msingi Kashaulili
CHOPA, ilioyowachukua Mh. Lowassa, na Mwenyekiti Mbowe, ikiruka baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni
Mmoja wa wananchi akibebwa baada ya kuzirai
kutokana na msongamano katika mkutano wa kampeni za mgombea urais, Edward
Lowassa, kwenye Uwanja wa Kashauriri Mjini
Mpanda mkoani Katavi
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha
EFM, Samira Sadiq (kushoto), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani),
kabla ya kumkaribisha Meneja wa Mawasiliano wa redio hiyo kuzungumza na
waandishi wa habari kuhusu tamasha la muziki mnene bar kwa bar
litakaloanza kesho kutwa Jumamosi, Agosti 5, 2015 Mkuranga mkoani Pwani.
Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart,
Haidari Chamshama na katikati ni Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio,
Denis Ssebo. Kampuni ya simu ya Smart wamedhamini tamasha hilo.
Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama.
Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), na Meneja
Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama,
wakiwaonesha moja ya jezi zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya
tamasha hilo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.
No comments :
Post a Comment