MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU (CCM) YUSUF MANJI AZINDUA KAMPENI ZAKE DAR ES SALAAM
Kiongozi
wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia (kulia),
akimtambulisha Yusuf Manji katika uzinduzi huo.
Mgombea
nafasi ya udiwani Kata ya Mbagala Kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Yusuf Manji (kushoto), akihutubia wananchi na makada wa chama
hicho katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika eneo la Kichemuchemu
Kaskazini Dar es Salaam leo jioni.
Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia, akihutubia katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Mchumi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Urio akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Kada wa CCM, Godbertha Kinyondo akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
Makada wa CCM wakiserebuka
Vijana wa hamasa wa CCM wakiwa kazini.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Michango mbalimbali ikitolewa.
Umati ukimsikiliza Yusuf Manji.
Mkazi wa eneo hilo, Sharifa Ali akimueleza Manji kuhusu kero ya kutokuwa na soko.
Dogo
akihubia kwenye uzinduzi huo. Dogo huyo alisema wana CCM wanapaswa
kumchagua Magufuli kuwa Rais, Mbunge Mangungu na Diwani Manji.
Chipukizi wakifanya vitu vyao.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Yusuf Manji (kulia) akifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WA AFRIKA KUSINI SIPHO MWAKABANE KUSHIRIKI TAMASHA LA KUOMBEA AMANI OKTOBA 4 MWAKA HUU.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusina na Msanii wa Afrika Kusini,Sipho Mwakabane ambaye atatumbuiza katika tamasha Oktoba 4 mwaka huu. Pia amesema kuwa msanii huyo wa nyimbo za Injili wa kimataifa. Na kulia ni Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga.

Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salam amesema kuwa watanzania wote bila kujali kabila, rangi na dini zote wajitokeze katika tamasha hilo la kuombea amani ambapo viingilio ni sawa na bure kabisa watu wazima kwa nafasi ya VIP wataingia kwa shilingi elfu tano (5000), kawaida elfu tatu (3000) na watoto ni shilingi elfu moja(1000)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama leo jijini Dar es Salaam.
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama leo jijini Dar es Salaam.
……………
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Afrika kusini, Sipho Mwakabane kuwa atashiriki tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu.
Ameyasema hayo wakati akizungumzakwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Afrika kusini, Sipho Mwakabane kuwa atashiriki tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu.
na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama.
Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani
katika nchi yetu.
hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagia maombi hayo aidha
Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu,
tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania
kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo
ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu
ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu
ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
Alisema baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo
litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba
11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora),
Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).
litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba
11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora),
Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).
Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Nchini -lafana
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa
Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati)
akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi
katika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa
Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika
jijini Dar es Salaam leo (jana).wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi wa
Mfuko huo Bi Matilda Nyallu.
Picha na Benjamin Sawe
Wafanyakazi wa Mfuko waMfuko wa
Pensheni wa PSPF wakiwa katika Banda la Mfuko huo wakatikatika Kongamano
la Wajasiriamali Wanawake nchinikabla yauzinduzi wa Kampuni ya Voice of
Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam
leo (jana), wa kwanza kulia ni Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari
kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP
Media, Reginald Mengi akizindua Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures
Tanzania (VoWET) katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini
lililofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa VoWET nchini Bi.
Mahida Waziri.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP
Media, Reginald Mengi akimlisha keki Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida
Waziri katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini mara baada ya
uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania.
Nyalandu kuzindua kampeni zake SINGIDA
…………………………..
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, leo anazindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya kutetea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini.
Nyalandu, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka 15 sasa, anawania tena nafasi hiyo wakati akiwa na rekodi yenye kujivunia kutokana na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Eliah Digha, alisema uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika Kata ya Mtinko jimboni humo.
Alisema Nyalandu alichelewa kuzindua kampeni hizo kutokana na kuwa na majukumu mazito ya kichama na kiserikali na kwamba, wananchi walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa siku hii ya leo.
Digha, ambaye pia ni mgombea udiwani katika Kata ya Msange, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uzinduzi huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni Nyalandu kupanda jukwaani na kuzungumza na wapigakura wake.
“Tunazindua kampeni zetu rasmi leo katika Kata ya Mtinko na baada ya hapo ni nginjanginja mpaka uchaguzi…hatutakuwa na muda wa kusimama hivyo, wapinzani wajiandae kwani hakutakuwa na mapumziko wala mtu kuomba poo. Wametaka kujaribu muziki wa Nyalandu sasa ndio wamewekewa hivyo kama hawajajipanga itakula kwao,” alisema Digha.
Alisema uzinduzi huo utapambwa na vikundi mbalimbali vya burudani kutoka mkoani Singida na kwamba, shughuli nzima itaanza saa nne asubuhi.
Kwa upande wake, Nyalandu alisema atatumia mkutano huo kueleza mafanikio yote yaliyopatikana na mikakati yake mipya ya kuendelea kulivusha jimbo hilo kimaendeleo.
Amesema katika kipindi cha uongozi wake, kwa kushirikiana na wananchi wake wamefanya mambo makubwa kwenye sekta zote muhimu ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii ikiwemo kuwawezesha vijana na akinamama kuanzisha miradi ya ujasiriamali.
Nyalandu, ambaye ni miongoni mwa makada 32 wanaounda timu ya ushindi ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amesema hana shaka na ushindi mwaka huu.
Amesema wagombea wa CCM kuanzia wa urais, wabunge na madiwani wataibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na historia ya utendaji kazi itaendelea kuwainua.
“Dk. Magufuli ana historia ambayo haina utata kuanzia kwenye utendaji kazi hadi uadilifu wake hivyo si wa kufananisha na wagombea wengine kwenye nafasi ya urais. Nyalandu anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge akiwa na historia ya kujivunia mbele ya wapigakura wa Singida Kaskazini…vivyo hivyo kwa madiwani wa CCM ambao wanagombea kwa ajili ya kuwatumia watu na si kwa maslahi binafsi kama walivyo wapinzani,” alisema Nyalandu.
Aidha, ametua fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo na kusikiliza mikakati yake mipya kwa ajili ya maendeleo ya Singida Kaskazini.

![]() |
| Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki(EABC)Lilian Awinja akizungumza katika mkutano huo. |
![]() |
| Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini kwaajili kuuhabarisha umma. |
CHIKU ; Heri ya Monica Mbega alileta maendeleo jimbo la Iringa mjini kuliko mchungaji Msigwa
……………………………..
MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia
ACT Wazalendo Bi Chiku Abwao(pichani) amesema heri ya miaka mitano ya
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mobica Mbega ( CCM) kuliko miaka mitano
ya Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)hivyo ametawa mwaka huu wananchi
kumchagua yeye
Akizungumza katika mkutano wake
wa kampeni za Ubunge jana kata ya Kihesa alisema iwapo atakuwa mbunge
wao atahakikisha anakuwa mbunge wa mfano wa kuwaletea maendeleo sahihi.
Kwani alisema kuwa
historia ya jimbo hilo mwaka 1995 walichagua NCCR mageuzi ambapo Bw
Mfalamagoha Kibasa kuwa mbunge ila baada ya kushindwa kutekeleza ahadi
zake mwaka 2000 walimchagua Monica Mbega ( CCM) ambae kipindi cha kwanza
alifanya Kazi vizuri na mwaka 2005 wananchi walimchagua tena ila
hakuweza kufanya Kazi ndipo walipomchagua Mchungaji Peter Msigwa(
Chadema) ambae hajafanya Kazi yoyote.
Hivyo alisema kwa
sasa imani yake juu ya wanaume kuwa wabunge katika jimbo hilo
haipo tena kwani hawana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi na
kudai kuwa iwapo mbunge aliyemaliza muda wake mchungaji Msigwa
angetekeleza ahadi zake vema leo asingesimama kugombea ubunge bali
angemuunga mkono mbunge huyo ili aendelee kwa kipindi cha pili
ila kwa kuwa hakuna jipya alilolifanya hana imani nae na hivyo ni
wakati wa wananchi wa jimbo hilo kuwapima wagombea wengine
waliojitokeza nje ya mbunge huyo .
Alisema ahadi za
mbunge aliyemaliza muda wake zilikuwa zaidi ya 14 ikiwemo ya
kuwawezesha wananchi waliojiunga katika vikundi kupatiwa mitaji ya
kuanzisha biashara kwa wakati huo alisema yeye si mbunge wa
kutoa pesa bali atawawezesha kiuchumi kwa kuwapa nyavu (mitaji) ila
baada ya kuwa mbunge alianza kuwasema vibaya wananchi kwa kudai
yeye si mbunge wa kutoa pesa (ATM)pia aliahidi ujenzi wa soko la
kisasa Kihesa na kumweka mwanasheria katika ofisi yake ila hadi
sasa hakuna alichofanya na akikumbushwa hukimbilia kujenga chuki na
kila mtu .
Bi Abwao ambae
amepata kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa na mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chadema alisema kuwa hali ya
chadema na UKAWA kwa sasa imepoteza mwelekeo na chadema kugeuka ni
chama cha kutetea mafisadi tofauti na iliyokuwa awali kuwa chama
cha kupinga ufisadi .
Hivyo alisema sababu
ya kukihama chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo ni kutafuta
chama cha upinzani makini ambacho atawatumikia wananchi bila ya
kuwajengea maswali kama ilivyo hivi sasa kwa mgombea wa Chadema
Iringa mjini mhungaji Msigwa ambae alikuwa mbele kupinga ufisadi na
hata kusema wanaomuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa
ambae ni mgombea wa Chadema kwa sasa wakapimwe akili zao .
Alisema Chadema kwa
sasa imekuwa ni chama cha kupiga dili akiwemo aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo Mchungaji Msigwa ambae leo kati ya maswali magumu ambayo
anahojiwa na wapiga kura wake ni juu ya kauli yake dhidi ya wale
wanaomuunga mkono LOwasa kutakiwa kupimwa akili zao.
Akielezea kuhusu
sera zake kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini iwapo watamchagua
kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anautumia vema mfuko wa
jimbo kwa kuwasaidia wazee ,vijana na wanawake kuwa na vikundi vya
kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali miaka mitano iliyopita kwa
mfuko huo kushindwa kufanya kazi yoyote.
Pia kuhakikisha
anaibana serikali ili vijana kupewa mikopo nafuu na kuzuia posho
kwa watumishi wa umma ambazo zimekuwa zikikwamisha maendeleo katika
jimbo hilo .
Dk Shein Aendelea na Kampeni Zake na Kusema Ataendeleza Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Kuleta Maendeleo Zaidi kwa Wazanzibar katika Wananchi Wake na Elimu Bure Zanzibar.
Mgombea
Urais wa Zanzibar Kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana
na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Mpira Konde
Kisiwani Pemba kuendelea na Kampeni Kisiwani Pemba.
Mgombea
Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika
katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais
wa Zanzibar Dk Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira
Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama
wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili
katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa
Kampeni zake kisiwani Pemba.
Taswira
ya wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia CCM katika
viwanja vya mpira Konde Pemba kama inavyooneka Mwanachama huyu wa CCM
akishangilia akiwa na picha ya Mgombea Urais wa CCM Dk Shein.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad
akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo
Zanzibar katika kipindi chake Dk Shein cha miaka mitano na kuwataka
kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar
katika sekta mbalimbali za Jamii

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.

Katibu
wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu
akiwahutubia Wananchi wa Konde katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea
Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika katika uwanja wa mpira Konde
Kisiwani Pemba.
HAPPY BIRTHDAY KAMANDA RAS MAKUNJA
Siku kama ya leo 19 September ndio
siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule
ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja aka mkuu
wa viumbe wa ajabu “Anunnaki Alien” alizaliwa mjini Dar-es-Salaam,
akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja),
Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja mtunzi na mwimbaji mahili wa muziki wa dansi leo ndio Happy Birthday !!!!! yake
pia unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni at
MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA KONDE KASKAZINI PEMBA
Naibu katibu Mkuu wa CCM
ZanzibarVuai Ali Vuai akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la
Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika Mkutano wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka
huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
Picha zote na Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Konde
Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika Mkutano wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka
huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein akiteta jambo na Naibu katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali
Vuai wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwezi Octoba mwaka huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa
mpira wa Konde,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine katika mkutano
wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka
huu,mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mpira wa Konde,
Kikundi cha Kwaya kitwacho
DK.Salmin cha Konde Wialaya ya Micheweni wakitoa burudani wakati
wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwanadi wagombe wa
Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kwa wananchi,mkutano uliofanyika katika
uwanja wa mpira wa Konde,[
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini
Pemba Bw.Mberwa Hamadi Mberwa wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi
Mkuu uliofanyika leo katika viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na
kuwanadi wagombea ngazi mbali mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na
Udiwani.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi
CCM akiwa na Picha la Mgombea Urais wa Ranzibar Dk.Ali Mohamed Shein
wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika
viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na kuwanadi wagombea ngazi mbali
mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na Udiwani,
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
CCM wakionesha picha za Mgombea Urais wa Ranzibar Dk.Ali Mohamed Shein
wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika
viwanja vya Mpira Konde Mjini,sambamba na kuwanadi wagombea ngazi mbali
mbali ikiwemo Ubunge,Uwakilishi na Udiwani,
Wajumbe wa jumuiya ya wanawake wa
Mkoa wa kaskazini Pemba wakiwa katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi
Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika
uwanja wa Mpira Konde Mjini na kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
TPB YAKADIDHI JENGO LA KITUO CHA AFYA PEMBA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud
(Wanne kushoto waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania,
TPB, Profesa Litice Rutashobya, (watatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu
wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na
wanakijiji, mbele ya jengo la Kituo Cha Afya, Ungi, Shehia ya Msuka
Mashariki, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya TPB kukabidhi jengo hilo
kwenye hafla iliyofanyika Sptemba 17, 2015. Kituo hicho kimekamilishwa
ujenzi wake na TPB.
Waziri
Abloud, akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa kituo hicho.
Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Letice
Rutashobya, (katikati mwenye miwani) na Meneja Mkuu anayeshughulikia
masuala ya shirika wa TPB, Noves A. Moses
Waziri
Aboud, (wapili kulia), Profesa Letice Rutashibya, (wapili kushoto),
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mbunge wa
jimbo la Konde, Khatib Suleiman Haji, wakibadilishana mawazo mara baada
ya ufunguzi wa jengo hilo la Kituo cha Afya
DR. JOHN POMBE MAGUFULI AHANI MSIBA WA MWALIMU WAKE MAREHEMU COLNER PASTOR KIJIJI CHA NYAKATUNTU BIHARAMULO
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Colner PaStor mwalimu
aliyemfundisha katika shule ya msingi ya Chato, Dk. Magufuli alionekana
mwenye huzuni kutokana na kifo cha mwalimu wake huyo wakati alipohani
msiba huo katika kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo mkoani
Kagera.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-BIHARAMULO)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimfariji mama Paskazia Mufuruki mjane wa Marehemu mwalimu Colner
Pastor wakati alipohani msiba huo katika kijiji cha Nyakatuntu wilayani
Biharamulo loe
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Father Erasto Nakule mara baada ya kuwasili nyumbani
kwa marehemu Colner Pastor.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Father Anthony mara wakati alipohani msiba wa Marehemu
mwalimu wake Colner Pastor.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akishiriki katika sara ya kumuombea marehemu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
CCM Ndugu Abdallah Bulembo akishiriki kuweka shada la maua katika kaburi
la marehemu mwalimu Colner Pastor.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akitoa heshima zake katika kaburi la aliyekuwa mwalimu wake marehemu
Colner Pastor.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa CCM
Biharamulo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia
hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli wakati akihutubia mjini
Biharamulo.
Amona Mpanju kwa mbali akihutubia katika mkutano huo
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika mjini Biharamulo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo mjini
Biharamulo.
Wananchi wakipunga mikono yao juu
kutokana na kufurahishwa na hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe
Magufuli.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Biharamlo Ndugu Oscar Mkasawakati.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea ubunge jimbo la Biharamulo na wahgembea wa viti maalum
mkoa wa Kagera.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wana
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
wakati wa mapokezi ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia
wananchi katika kijiji cha
WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.
………………………………….
Wanafunzi wanaosoma masomo ya
Sayansi kote nchini wameshauriwa kuongeza bidii katika kujifunza masomo
hayo ili kuendana na juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwawezesha
wanafunzi hao kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli Manyele kwenye sherehe
ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri
katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2013 na 2014.
“Kama wachunguzi wa Serikali
ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na Biolojia tumeona
ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo ya
Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.
Amesema Zoezi la kuwapongeza na
kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na
Biolojia limeanzishwa kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali
za Viwandani na Majumbani.
Aidha, amesema Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha vipaji vyao vya
masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua kuwa Katika sherehe
hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule mbalimbali za
Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo Fedha, Vyeti
na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa upande wa
wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.
Kwa upande wa Wanafunzi
waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza, Marian,
Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko
jijini Mwanza.
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa
tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007
chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na
tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia
na Bioloji.
WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU KUFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)
………………………………….
WIZARA ya Afya na Ustawi wa
Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia
matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe za
hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na matumizi ya madawa ya
kulevya.
Akizungumza katika hafla ya
utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya kemia na biolojia
kwa mwaka 2013-2014 iliyofanyika leo Ijumaa (Septemba 18, 2015), Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Donan Mmbando alisema
hatua hiyo ni mkakati wa serikali wa kudhibiti matumizi ya dawa za
kulevya nchini.
Dkt Mmbando alisema Wizara
kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa mchango
mkubwa wa uchunguzi wa kimaabara kuweza kutambua dawa za kulevya na pia
kuwatambua waathirika wa dawa hizo.
“Serikali inatambua umuhimu na
unyeti wa kazi zinazofanywa na wakala wa maabara na mkemia mkuu wa
serikali katika kulinda afya na usalama wa watu na mazingira pamoja na
kuleta uelewano katika jamii” alisema Dkt Mmbando.
Aidha alisema serikali
itaendelea kuitegemea Taasisi hususani katika utaalamu kwa utatuzi wa
masuala yanayohusiana na kulinda afya na usalama wa jamii, hivyo
itahakikisha inaiwezesha taasisi hiyo katika mahitaji ya rasilimalli
watu na fedha.
Aidha Dkt Mmbando aliwapongeza
walimu na wanafunzi wote waliofanya vyema katika mitihani yao na
kuwakumbusha juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo
yanaweza kufuta ndoto ya kuwa nguvu kazi ya taifa.
Watakao Hujumu Miundombinu ya DART Kulipa faini ya laki tatu.
Mkurugenzi wa Mifumo Junn Mlingi
kutoka Taasisi ya Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport)
akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa
Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na waandishi wa habari
walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo katika
kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads
wakipanda gari la Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jana jijini Dar es
Salaam katika ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi wa DART kabla ya
kuanza kutumika .
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads
wakikagua kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara ambacho
ujenzi wake umekamilika kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Afisa wa Tanroads
akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara
katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa
miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads
wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka
walipokuwa wakifanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana
jijini Dar es Salaam.
………………………………………
Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam
(DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa
Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa
miundo mbinu ya mradi huo.
Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.
“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.
Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.
Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden Dragon kutoka Japan.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA KUPOKEA MISAADA YA VIFAA MBALIMBALI KUSAIDIA SHULE MPYA YA MSINGI KAKUNI MKOANI KATAVI.
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI
nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu
Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta mpakato zilizotolewa na
kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni iliyo
katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo jijini Dar es salaam. Shule
hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia wazo la Wazo la Waziri Mkuu,
Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya kisasa katika kijiji hicho
na inajengwa kupitia michango na misaada ya wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI
nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu
Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na
kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni iliyo
katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya
NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa
Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezi vilivyotolewa na NMB
kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa
Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma
Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare
uliotolewa na kikundi hicho kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi
Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi .
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini
Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni
hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya msingi Kakuni mkoani Katavi,
ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki
ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani
ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi
wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. MILIONI 330 KWA SHULE ALIYOSOMA
HUAWEI na NMB zimetoa msaada huo
ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya
kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo
alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika
shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya
makabidhiano ya msaada huo yaliyofanyika leo mchana (Ijumaa, Septemba
18, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meneja
Uhusiano wa kampuni ya HUAWEI, Bw. Jin Liguo alisema kampuni yake
inaamini msaada huo utasaidia kupunguza tofauti za kiteknolojia zilizopo
kwenye sekta ya elimu.
“Kampuni ya HUAWEI iko Tanzania
tangu 2001 na imedhamiria kufanya kazi na wanajamii kila inapoona
imepata fursa ya kufanya hivyo, na hasa katika elimu ambako pia
tumelenga kupunguza tofauti za kiteknolojia zinazojitokeza kwenye sekta
hiyo,” alisema Bw. Liguo.
Kampuni hiyo imetoa kompyuta za mezani 50, HUAWEI Tablets 100, Laptop tano, Printers mbili, Scanner mbili, Projector mbili, Projector Screens mbili, Power System seti moja na Audio System seti moja vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 150,000 (sawa na sh. milioni 300).
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa
Fedha wa Benki ya NMB, Bw. Waziri Barnabas alisema benki hiyo imelenga
kukuza michezo shuleni na ndiyo maana imeamua kutoa msaada wa vifaa vya
michezo kwa shule hiyo ya Kakuni.
Benki ya NMB imetoa kompyuta nne;
jezi za michezo jozi 192 (soka 72, wavu 40, kikapu 40 na pete 40);
mipira 40 (soka 10, wavu 10, kikapu 10 na pete 10). Pia imepanga
kuchangia ununuzi wa madawati yenye thamani ya sh. milioni 10 ambayo
alisema yapo tayari ila yanasubiri ujenzi wa kituo cha walimu ukamilike.
Vifaa hivyo vina thamani ya sh. Milioni 30.
Akizungumza katika hafla hiyo
fupi, Waziri Mkuu Pinda aliwashukuru wawaklishi wa HUAWEI na Benki ya
NMB kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza
ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.
“Wazo la ujenzi wa shule mpya ya
msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye
shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa
hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi
shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya
na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema
Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha leo mbele ya waandishi wa
habari.
“Niliwaza pia kufanya ukarabati
lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani wanafunzi waliopo ni
wengi kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao
800. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” aliongeza.
Waziri Mkuu alisema alipeleka
maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65
kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha
akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati
huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla
katika kuisimamia ndoto aliyokuwa nayo.
Alisema aliishirikisha Halmashauri
kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia
taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh.
bilioni 1.3/-.
Alisema alipeleka barua kuomba
michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi
mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 785 na dola
za Marekani 267,834 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi
amebakiza kiasi cha sh. milioni 40 na dola za Marekani 117,495.
“Katika kuanza zoezi la kukusanya
fedha Aprili 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi
yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh.
milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi
– Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza
gharama,” alisema.
Hadi sasa majengo yaliyokamilika
ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili
(wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja,
ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na majengo mawili ya vyoo yenye matundu
48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua za mwisho.
Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania
watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado
anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba 18 za walimu,
bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi,
kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource
Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote,
mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba
mbili za walinzi na uzio wa shule.
Alitaja vitu vingine ambavyo bado
vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti
vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya
awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo –
shule ya msingi na shule ya awali. Vyote hivi alisema vitagharimu sh.
bilioni 2.18.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, SEPTEMBA 18, 2015
FDL KUTIMUA VUMBI KESHO
Kundi A, Polisi Dar watakuwa
wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii
Mkuu ya Dodoma watapambana na Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri
mjini humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza
na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na
Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha
Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu
Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha
Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya
Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC
watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na
Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume
mkoani Mara.
VPL KUENDELEA WIKIENDI HII
Jumamosi mabingwa watetezi wa
kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United
watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports katika dimba la Kambarage
mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano
wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons
watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini
humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe
Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa
michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa
Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa
Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu
mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto
Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
MAJAMBAZI WANNE WAUAWA KWA RISASI ARUSHA-Wakutwa na AK 47 mbili, SMG moja, bastola tatu na Radio “call” mbili za Polisi
Wakutwa na AK 47 mbili, SMG moja, bastola tatu na Radio “call” mbili za Polisi.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
…………………………………..
Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa na askari Polisi wakati wa mapambano ya majibizano ya risasi usiku wa tarehe 17.09.2015 saa 3:30 maeneo ya Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na halmashauri ya Jiji la Arusha.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisini
kwake leo asubuhi. Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Sabas
alisema Jeshi hilo lilipokea taarifa za Kiintelejensia juu ya kuwepo kwa
kundi la majambazi lililotaka kufanya uvamizi na uporaji ndani ya jiji
la Arusha.
“Tulipata taarifa toka tarehe 19.08.2015 mwezi mmoja nyuma juu ya uwepo wa kundi la majambazi toka nchini Kenya ambao wangeshirikiana na wengine wa hapa nchini kwa nia ya kufanya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo taasisi za fedha”. Alisema Kamanda sabas.

“Baada ya taarifa hizo tukaendelea
na ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtu aitwaye Sixtus Alfredy Ngowi
(51) Mtanzania, Mkazi wa Ngulelo jijini hapa ambapo baada ya mahojiano
alikiri kwamba huwa anashirikiana na majambazi wenzake toka nchini Kenya
katika kufanya matukio mbalimbali ya kiuhalifu hapa nchini”. Alifafanua
Kamanda Sabas.
Baadhi ya matukio ambayo
ameyafanya ni pamoja na tukio la uporaji wa fedha zaidi ya dola
2,000,000 lilitokea jijini Dar es salaam mwaka 2005 kwenye Kampuni ya
Security Group 4 na kisha kufikishwa Mahakamani.
Mbali na tukio hilo pia mwaka 2002 alihusika na tukio la uvamizi wa Benki ya NBC tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro. Mwaka 2014 jambazi huyo amewahi kushtakiwa nchini Kenya kwa matukio ya uhalifu katika Mahakama ya Mlimani Law Court iliyopo jijini Nairobi lakini baadae aliachiwa huru.

Alizidi kukiri kuhusika katika
matukio ya ujambazi huku akishirikiana na wenzake katika matukio ya
unyang’anyi wa kutumia silaha katika jiji la Arusha ambalo lilikuwa
linawalenga wafanyabiashara wakubwa wa Madini ya Tanzanite na Hoteli za
Kitalii. Miongoni mwa tukio walilolifanya ni kumjeruhi mfanyabiashara wa
madini aitwaye Mathius Manga ambaye alipigwa kwa risasi kwenye ubavu wa
kulia.
Kamanda Sabas alisema kwamba mara baada ya kuridhishwa na mahojiano baadae jambazi huyo alikubali kushirikiana na Polisi ili aweze kufanikisha juu ya upatikanaji wa wenzake ambao siku ya jana walipanga kuvamia katika duka la kubadilishia fedha liitwalo Sanya lililopo jijini Arusha.
Walipokuwa wanaelekea kwenye eneo la tukio akiwa anaongozana na askari Polisi kwa nia ya kufanikisha kuwapata majamabzi wengine, mara tu baada ya kufika kabla hawajawakamata majambazi hao ambao walikuwa kwenye gari aina ya Noah rangi ya silver yenye namba za usajili T. 981 AVK walishtuka na kuanza kulishambulia gari lililokuwa na askari Polisi na kumjeruhi mwenzao Sixtus Alfedy Ngowi ambaye alifariki muda mfupi wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Mara baada ya kuona hivyo, Polisi
nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi watatu huku wengine
wakifanikiwa kukimbia. Katika upekuzi kila mmoja alikutwa na bastola
pamoja na risasi. Pia walikuta mabegi matatu meusi ambapo ndani yake
kulikuwa na bunduki mbili aina ya AK 47 zenye namba 83 LG 3953 56-1 na
nyingine yenye maandishi ya kirusi pamoja na SMG moja yenye namba 56-1
28038394.
Bastola ambazo zilikutwa toka kwa majambazi hao zilikuwa na namba CZ 75 Compact Luger-9mm namba A. 269206, CZ 85 B Luger 9mm namba 051967 na Chines Pistol namba 967741. Pia zilipatikana magazine nne tupu za SMG, risasi 85 za SMG/AK 47 na risasi 28 za bastola.
Mbali na silaha hizo pia walikutwa na Radio “Call” mbili aina ya Kenwood zilizokuwa hewani na wimbi la Polisi Arusha, bullet proof moja, vifaa vya kusafishia bunduki, mifuko mitatu ya kubebea pesa na vifaa vingine.
Majambazi hao ambao kwa sasa miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Mount Meru walikutwa pia na vitambulisho mbalimbali vya Jamhuri ya Kenya pamoja na simu tano aina ya Nokia, Tecno na Samsung. Kamanda Sabas alisema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliofanikiwa kukimbia na kubaini mtandao mzima wa kundi hilo.
Kamanda Sabas alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushirikiana na Jeshi hilo juu ya utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuonya yoyote ambaye atajiingiza katika matukio ya kufanya uhalifu Jeshi hilo litamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA HUDUMA ZA “DUTY FREE SHOP” MAGEREZA MKOANI ARUSHA
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil (wa pili kushoto) , akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Huduma za Magereza Duty free shop Mkoani
Arusha leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha (wa
kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir
Minja (wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Smart LTD, Bw.
Mohamed Panjwani.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil (kulia), akisoma jiwe la Msingi
kwenye hafla ya uzinduzi wa Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha
(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi wakati wa
kumkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Huduma za Duty free
shop ya Magereza Mkoani Arusha.
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
Magereza mbalimbali yaliyopo Mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Mbaraka Abdulwakil(hayupo pichani).
Bidhaa za majumbani zinazopatikana katika Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha waliosimama
mara tu baada ya kuzindua Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani
Arusha(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir
Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, SACP. Hamis
Nkubasi(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, SACP.
Venant Kayombo(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Mart LTD,
Bw. Mohamed Panjwani.
………………………………………………………..
Na Lucas Mboje, Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil amepongeza kasi ya Utendaji kazi
wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja pamoja na
Uongozi wote wa Jeshi hilo kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango
wa Serikali ya Awamu ya Nne wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na
zenye manufaa Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao
ya kazi hususani huduma za “Duty free shops”.
Mhe. Mbarak Abdulwakil ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa “Duty free shop”ya Magereza Mkoani Arusha iliyofanyika leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Binafsi wa Mkoa wa Arusha walihudhuria hafla hiyo.
“Nampongeza kwa dhati Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kwa jitihada hizi ambapo matunda yake yanaonekana na amethibitisha kwamba azma ya kusambaza huduma hii nchi nzima ipo pale pale na jitihada zinaonekana”. Alisema Abdulwakil.
Ameongeza kuwa lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama unatekelezwa ipasavyo kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
Aidha, Mhe. Abdulwakil amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha Maafisa, askari pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar Mart LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.
Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za “Duty Free Shop” na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenda kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.
Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya “Duty Free Shops” tisa(09) ikiwemo Gereza Kuu Ukonga na Keko – Dar es Salaam, Gereza Isanga – Dodoma, Gereza Kuu Karanga – Moshi, Gereza Butimba – Mwanza, Gereza Ruanda – Mbeya, Gereza Lilungu – Mtwara, Gereza Uyui – Tabora, Chuo KPF – Morogoro na duka la tisa(09) ni Gereza Kuu Arusha.

MANJI AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA VIONGOZI WA BIASHARA AFRIKA
……………………………………………………..
NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji
amenyakua tuzo ya kielelezo cha viongozi wa biashara wa Afrika kwa
mwaka 2015.
Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, aliwapiku
wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo bilionea namba moja Afrika,
Aliko Dangote.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi Quality Group,
ilisema tuzo hiyo ilimshtua ‘bosi’ wao kwani hakutarajia na kwamba
itasaidia kuvutia wawekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii
nchini.

Tuzo hizo zilitolewa Septemba 16 mwaka huu.
Taarifa hiyo iliongeza Manji ni chachu kwa vijana kufanya vizuri
kwenye sekta zao na itasaidia nchi kusonga mbele katika kujikwamua na
umasikini.
Tanzania inaendelea kujukulikana kimataifa na itasawaidia watanzania
kwa ujumla kufanya kazi ama biashara katika nchi nyingine bila ya
vikwazo visivyo na msingi kupitia tuzo hiyo.
Baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Emirates Group,
Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege ya
Emirates inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na
nyingine kubwa.
Wengine ni Mwenyekiti wa Emmar Properties, Mohammed Alabbar pia
bilionea kutoka India, Ratan Tata anayemiliki kampuni kubwa ya
Emeritus of Tata Sons Ltd.
Pia bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri, Mukesh Ambani ambaye
ni mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni Yingluck
Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Manji, pia kampuni yake ya
Quality Group imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa
uhakika kwa bara la Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”

MKUU WA WILAYA YA MAGHARIB B AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UCHAGUZI MKUU UJAO
MKUU WA WILAYA YA MAGHARIBI ( B),
AYOUB MOHD MAHAMOUD AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA
NAMNA WALIVYOJIPANGA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA HARAKATI
ZINAZOEENDELEA ZA KUELEKEKEA UCHAGUZI MKUU NCHNI. MAZUNGUMZO HAYO
YALIFANYIKA OFISINI KWAKE MWERA ZANZIBAR.
Na Rahma Khamis na Takdir Ali Maelezo Zanzibar
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B
Unguja Ayoub Mohd Mahamoud amewataka wanasiasa, viongozi wa dini na
taasisi za kiraia kuzungumza na kuhimiza amani wakati huu wa kampeni
ili Zanzibar iendelee kuwa nchi yenye utulivu.
Hayo ameyaeleza Ofisini kwake
Mwera wakati akizunumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni za
Uchaguzi zinavyoendelea baada ya wananchi wengi kuhamasika na
kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo.
Amesema katika kuendeleza amani
Serekali inaendelea na jitihada za kuweka walinzi katika mikutano ya
kampeni na kujaribu kutenganisha mikutano maeneo mbalimbali ili
wasikutane.
Akizugumzia suala la amani Ayoub
amefahamisha kuwa sio suala linaloihusu Serekali pekee bali ni la
kila mwananchi hivyo amewanasihi waendelee kuienzi kwani kutoweka
kwa amani iliyopo haitakuwa kazi rahisi kuirejesha.
Kwa upande wa wanasiasa Mkuu wa
Wilaya amesema wanachohitaji ni uongozi hivyo hawanabudi kuwa
waangalifu katika kaulizao ili zisijenge hamasa kwa vijana wao kuvunja
amani iliyopo.
“Kuna baadhi ya watu wanadhani
kuwa wakati huu wa kampeni Serekali itakua haishughulikii nawambia
Serekali ipo haijenda likizo hivyo atakaekwenda kinyume hatutomuachia”.
Amesema changamoto zinazoikabili
Wilaya yamagharibi ni kuwa na mikutano mingi katika kwa wakati mmoja
jambo ambalo linaweza kupelekea kutokea kwa ugomvi hasa wakati
wanachama wanaporudi mikutanoni kutokana na hamasa wanazokuwa kuwa
nazo.
Aidha amewanasihi wananchi
wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa kuanza kufanya fujo na kuvunja
amani ya nchi kwa wale wenye vyama na wasio na vyama kwani hakuna
mbadala wa amani .
“Jitihada za Serekali kuhamasisha
amani zinaonekana kuzaa matunda hivyo tuendelee kuhamasishana na
kunasihiana kwani siku 30 za kampeni zilizobaki zisipelekee amani
kutoweka kw siku nyingi zinazokuja.” Alsisitiza Mkuu wa Wilaya.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA BAADHI YA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI
(Picha zote na OMR)
viingilio Tamasha la Amani hadharani
………………………………….
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia
kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
imetangaza kiingilio kwa VIP ni shilingi 5000 kwa watakaohudhuria katika
tamasha hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions, Alex Msama viti vya kawaida watalipa shilingi 3000.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze
kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na
tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za
Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
Alisema baada ya kumalizika
jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba
8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13
(Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga)
na Oktoba 18 (Mwanza).
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA) yadhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri
……………………….
MAMLAKA ya
Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA), imetoa Sh. 10, 486,000 kwa ajili ya
kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri zaidi katika miaka
10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Tuzo hizo
zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA zinatarajiwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani
City, Dar es Salaam, ambapo pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais
Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa sekta ya michezo katika
uongozi wake.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja
Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo, alisema
wameamua kusaidiana na TASWA kwa sababu Rais Kikwete ni mdau mkubwa wa
michezo na pia wa masuala ya utalii.
‘’Dk. Kikwete
ni mdau mkubwa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa kipindi
chote ambacho amekuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
hatimaye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ametembelea hifadhi hii
mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa letu
waliomtangulia.
‘’Pia amekuwa
mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
katika kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya Ngorongoro
katika mataifa mbalimbali duniani alikokwenda kwa ziara za kikazi.
‘’Jambo hili
limeleta watalii wengi nchini kutoka mataifa mbalimbali dunini. Vile
vile ziara zake za mapumziko hifadhini wakati wa sikukuu mbalimbali
zimewahamasisha sana Watanzania walio wengi kutembelea hifadhi hii
kutoka kote nchini na hata nchi jirani,’’ alisema Akyoo.
Pia alisema
waandishi wa habari ni wadau wakubwa na muhimu katika harakati za utalii
na ndiyo sababu wameamua kuisaidia TASWA ifanikishe shughuli yake.
Kwa upande
wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru mamlaka ya hifadhi
hiyo na kusema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuomba wadau wengine
waungane nao kufanikisha jambo hilo.
‘’Kama
tulivyosema bajeti yetu ni Sh milioni 130, juzi (Jumatano) tulipata watu
wa GSM Foundation waliotupa Sh. Milioni 50, tunaomba na wengine
tushirikiane nao katika hili,’’ alisema Mhando.
Alisema TASWA
imeamua kuandaa hafla ya wanamichezo kumuaga Rais na pia kumpa tuzo kwa
vile wakati wa uongozi wake amefanya mambo makubwa katika sekta ya
michezo.
Kwa mujibu wa
Mhando, wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na TASWA
kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.
Wanachama SHIWATA kunufaika na viwanja bure
…………………………
MAKUNDI ya wasanii, wanamichezo na waabdishi wa habari
wanaendelea kumiminika kulipia nyumba za bei nafuu baada ya Mtandao wa
Wasanii Tanzania (SHIWATA) kutoa viwanja bure katika kijiji cha Wasanii
Mkuranga.
“Tumeanzisha ofa maalum kwa
wanachama wetu kupata kiwanja bure kama atakuwa amelipia benki sh.
200,000 za kumjengea msingi wa nyumba yake katika kijiji chetu Mwanzega
Mkuranga ambako mpaka sasa kati ya hekari 300 tulizonazo za makazi ni
hekari kumi tu zimejengwa nyumba 120,.” alisema Taalib.
Alisema katika misingi hiyo
wanaotaka kumaliza nyumba zao gharama yake jumla itakuwa sh. 850,000 kwa
nyumba ya chumba kimoja, sh. 3,800.000 kwa nyumba ya vyumba viwili na
sh. 6,400,000 kwa nyumba vya vyumba vitatu na sebule.
Mwenyekiti Taalib alisema bado
nafasi iko wazi kwa wasanii wanaotaka kuwekeza kwa kujenga shule,
hospitali, kumbi za starehe na viwanja vya nmichezo wanakaribishwa.
Alisema makundi ya wasanii ambao
bado hawajajiunga na mtandao huo watapewa ofa ya kulipa sh. 70,000 kwa
mtu mmoja katika vikundi na mmoja mmoja atajiunga kwa sh. 120,000 ambapo
atapewa pia katiba ya mtandao huo.
Alisema wanachama wanaotaka
kutembelea kijijini kumeandaliwa usafiri wa kila Jumamosi kwa nauli ya
kwenda na kurudi ya sh. 10,000 kwenda kujionea maendelea ya kijiji cha
Mwanzega, Mkuranga.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
WATU TISA WAFUASI WA CCM NA CHADEMA WAJERUHIWA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA MAENEO YA MBATA BUCHANI JIJINI MBEYA.
WATU WAWILI RAIA WA KIGENI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MBATA – BUCHANI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CCM BW. SHAMBWE SHITAMBALA AKIWA NA WAFUASI WAKE, WAPENZI WA CHAMA HICHO ALIKUWA AKIFANYA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA ENEO HILO KWA MUJIBU WA RATIBA YAKE.
MGOMBEA HUYO AKIWA KATIKA MKUTANO HUO, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW. JOSEPH MBILINYI ALIKUWA AKIPITA ENEO HILO AKIWA NA MSAFARA WAKE KUELEKEA MAENEO YA NSOHO KWENYE MKUTANO WA KAMPENI. KUTOKANA NA KITENDO HICHO WAFUASI WA CCM AMBAO WALIONEKANA KUWA WENGI HADI ENEO LA BARABARA HIVYO KUPELEKEA MSAFARA WA BW. MBILINYI KUTOWEZA KUPITA ENEO HILO HALI ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU ZILIZOPELEKEA KUJERUHIWA KWA WATU NA UHARIBIFU WA MALI.
KUTOKANA NA VURUGU HIZO, WAFUASI TISA WA VYAMA HIVYO VYA SIASA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. ROBERT KERENGE (58) KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA 2. SALUM MWANSASU (35) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 3. ATUPELE BROWN (39) MKAZI WA GHANA [CCM] 4. ROSE NELSON (30) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 5. SAKINA SALUM (25) MKAZI WA GHANA [CCM] 6. MALANYINGI MATUKUTA (31) MKAZI WA FOREST [CCM] 7. AGABO MWAKATOBE (44) MKAZI WA GHANA [CHADEMA] 8. JAILOS MWAIJANDE (23) MKAZI WA ITIJI [CHADEMA] NA 9. GABRIEL MWAIJANDE, DEREVA WA MGOMBEA UBUNGE [CHADEMA].
AIDHA KATIKA VURUGU HIZO GARI LA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW.JODEPH MBILINYI AINA YA TOYOTA LAND CRUISER YENYE NAMBA ZA USAJILI T.161 CPP LILIHARIBIWA KIOO CHA MBELE, TAA MOJA YA NYUMA UPANDE WA KUSHOTO NA KIOO CHA UPANDE WA DEREVA KWA KUPIGWA MAWE. PIA PIKIPIKI ZENYE NAMBA ZA USAJILI T.332 CHV AINA YA T-BETTER NA T.383 CSE AINA YA SKYMARK ZILIHARIBIWA KWA KUVUNJWA SIDE MIRROR ZA UPANDE WA KUSHOTO NA ZIPO KITUO CHA POLISI KATI.
KWA MUJIBU WA RATIBA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA KWA TAREHE 17.09.2015, ILIKUWA IKIONYESHA CHADEMA SAA 10:00 ASUBUHI HADI SAA 15:00 ALASIRI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA NSOHO NA SAA 15:00 ALASIRI HADI 18:00 JIONI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA MAENDELEO WAKATI CCM KWA MUJIBU WA RATIBA WALITAKIWA KUFANYA KAMPENI KATA YA ITENDE SAA 08:00 ASUBUHI HADI SAA 13:00 MCHANA NA SAA 13:00 MCHANA HADI SAA 18:00 JIONI MTAA WA MBATA, KATA YA GHANA AMBAPO NIPO TUKIO HILI LILIPOTOKEA.
UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUPELEKA JALADA LA UCHUNGUZI KWA MWANASHERIA WA SERIKALI ILI WALIOHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO WAFIKISHWE MAHAKAMANI.

KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA IDARA NYINGINE, LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI MSUMBIJI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ARQUEMIDES JOAO MAHANJANE (40) NA 2. HENRIQUES BENDITO ASSUBA (36) WOTE WAKAZI WA MAPUTO WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI VIPANDE 2 VINAVYODHANIWA KUWA NI PEMBE ZA FARU ZENYE UZITO WA KILO 5 ½, VIPANDE 4 VYA MAWE YADHANIWAYO KUWA NI MADINI YENYE UZITO WA KILO 1 ½ NA MZANI 01 [PORTABLE ELECTRONIC SCALE].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KASUMULU MPAKANI, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA WAKIWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI ABL 860 MC AINA YA TOYOTA HILLUX VIGO D/CABIN WAKITOKEA NCHINI MALAWI KUINGIA NCHINI. NYARA HIZO PAMOJA NA VITU HIVYO VILIKUWA VIMEFICHA CHINI YA CHASES YA GARI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA MAENEO YA MIPAKANI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.

Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAKABIDHIWA PIKIPIKI TANO KWA AJILI YA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO KUAKABILIANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WATOTO.
MWAKILISHI WA SHIRIKA LA
KUHUDUMIA WATOTO ZANZIBAR (SAVE THE CHILDREN), BI MALI LISSON
AKIMKABIDHI FUNGUO, ZA PIKIPIKI TANO, NAIBU WAZIRI WA AFYA MAHMOUD
THABIT KOMBO KWA AJILI YA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO KWA MKONO WA
WILAYA KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA WIZARA YA AFYA MNAZIMMOJA MJINI
ZANZIBAR.
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAHMOUD
THABIT KOMBO AKITIA SAINI BAADA YA KUPOKEA PIKIPIKI TANO KWA AJILI YA
KUWARAHISISHIA KAZI WAKUU WA VITENGO VYA HUDUMA YA MKONO KWA MKONO WA
WILAYA.
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAHMOUD
THABIT KOMBA AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI NA WAKUU WA VITENGO VYA MKONO
KWA MKONO WALIOKABIDHIWA PIKIPIKI HIZO.
PIKIPIKI WALIZO KABIDHIWA WAKUU WA
VITENGO VYA MKONO KWA MKONO KWA AJILI YA KUWASAIDIA SHUGHULI ZA
KUFUATILIA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA KWA WATOTO.
PICHA ZOTE NA MIZA OTHMAN –MAELEZO ZANZIBAR.
Dk Mauwa Daftari -wakinamama tushikamane kuhakikisha tunamuunga Mkono Samiya Suluhu Hassan
……………………………………..
MJUMBE wa Kamati Kuu ya
Halmashauri kuu ya Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Dk Mauwa Abeid
Daftari amewataka wanawake kuondoa tofauti zao za kisiasa bali
washirikiane na wawe kitu kimoja kwa kuhakikisha wanamuunga Mkono
Mgombea mwenza wa Chama hicho Samiya Suluhu Hassan .
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi Dk Mauwa amewataka wanawake kuweka kando tofauti zao na
wadumishe ushirikiano kwa kumuunga Mkono Mgombea mwenza kwa kuwa ni
suluhisho la changamoto zinazowakabili akinamama .
Amefahamisha kwamba ukombozi wa
mwanamke umewadia na kueleza kuwa hayo yatatimia iwapo wanawake
watashikamana kwani kilio cha kundi hilo cha siku nyingi kimepata wa
kukinyamazisha kwani Samiya ndiyo ukombozi wa mwanamke.
“Mwaka huu ndiyo wa ukombozi kwa
akinamama , napenda kuwaomba tushikamane kuhakikisha tunamuunga Mkono
Samiya Suluhu Hassan kwani anafahamu changamoto zinatukubili ili
kufanikisha hilo lazima tuondoe tofauti zetu za kisiasa ”alisisitiza .
Aidha ameeleza kwamba kumchagua
Samiya kuwa makamu wa Rais ni mikakati ya kufikia usawa katika vyombo
vya maamuzi ikiwemo Bunge na Baraza la Wawakilishi (hamsini kwa hamsini)
hivyo ni vyema wanawake kokote nchini kulitambua hilo .
“Ni wakati wa wanawake kufikia
nusu kwa nusu katika vyombo vya maamuzi , na hili limeanza kuchomoza
kwani tumekuwa tukihitaji kwa muda mrefu hatimaye limetimia ”alieleza Dk
Mauwa .
Naye Mjumbe wa Halmashauri ya
Chama Hicho Asiya Sharif amesema kuwa kitendo cha CCM kumpendekeza
Samiya Saluhu Hassan ni hatua za kuutokomeza mfumo dume ambao
unaendelea kuwakandamiza wanawake kwa muda mrefu .
Amesema kuwa wanawake wamekuwa
wakikosa haki zao za msingi ikiwemo kutoshiriki vyema katika vikao vya
maamuzi kutokana na kuwepo na mfumo dume hali ambayo kwa sasa imeanza
kupatiwa ufumbuzi wake .
“Tujiandaeni kuutokomeza mfumo
dume ili tuweze kushiriki ipasavyo kwenye vyombo vya maamuzi , kwani
kuna haki nyingi zimekosekana kutokana na baadhi ya wanaume kuwazuia
akinamama kushiriki katika kufanya maamuzi ”alifahamisha .
Kwa upande wake Khadija SKibano
amesema ukombozi wa mwanawake umefika na kuelezea haja kwa wananchi wa
Tanzania kushikamana pamoja na kumtetea mwanamke na kuongeza kwamba bado
wananchi ni watumwa wa siasa .
“Bado wananchi tunasumbuliwa na
mapenzi ya chama , lakini kusema kweli mwaka huu ni lazima tushikamane
pamoja na tuachane na ushabiki wa vyama vyetu kwani ukombozi wa mwanamke
umewaidia ”alieleza Khaadija .
Hivyo wameshauri wanawake
kuwashawishi waume zao pamoja na ndugu na jamaa zao kila mmoja
kuhakikisha kwamba wanaunga mkono juhudi za ukombozi wa akinamama .

No comments :
Post a Comment