
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja
vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa
Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN
MICHUZI.


Umati
wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye
viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa
wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni
za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Wafuasi
wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa
wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni
za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.

Wafuasi
wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati
alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam,
kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti
29, 2015.
Sehemu
ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua
habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya
Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji
hilo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe
akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika
mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani
ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua,
leo Agosti 29, 2015.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa
Zanzibar katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman
Mbowe.
Viongozi
wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya
maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, leo Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe
(kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali
mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu
wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar
aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika
kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.


Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji
la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es
salaam leo Agosti 29, 2015.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati
wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo
Agosti 29, 2015.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo Agosti 29, 2015.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.
MAELFU ya wananchi waliohudhuria
mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri
kupitia CHADEMA, anayewakilisha vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananci
UKAWA, Mh. Edward Lowassa, pale Jangwani jijini Dar es Salaam leo
Jumamosi Agosti 29, 2015
NA
K-VIS MEDIA
MGOMBEA
kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CHADEMA, akiwakilisha
vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Mh. Edward Lowassa, amesema
akichaguliwa kuwa rais, vipaumbele vyake ni Elimu, Miundombinu, Kilimo na Afya.
Akizundua
kampeni hizo leo Jumamosi Agosti 29, 2015, kwenye mkutano uliovunja rekodi
kutokana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu pale Jangwani jijini Dar es
Salaam, Mh Lowassa amesema, kipaumbele chake cha kwanza ni Elimu, Elimu, Elimu,
akifafanua kuwa maendeleo yoyote pale Duniani yanakuwepo endapo wananchi wake
wamepata elimu bora.
“Serikali
ya UKAWA, itatoa elimu bure kuanzia ile ya msingi, sekondari na vyuo vikuu.” Alifafanua.
Pia alisema, UKAWA, itazingatia suala la Kilimo kwa kuwa ndio eneo litakalotoa
ajira nyingi kwa watanzania na kilimo chenyewe kitakuwa kile cha kisasa cha
kutumia mashine na umwagiliaji.
Pia
UKAWA itaangazia suala la mawasiliano ya barabara na reli, ambapo kwa kuanzia
itahakikisha reli ya kati inajengwa upya kuanzia Dar es Salaam, Kigoma hadi
Mwanza.
Hali
kadhalika UKAWA itaangazia pia suala la afya ambapo hospitali za kisasa na
zenye vifaa vitakavyotoa huduma iliyo bora zitajengwa maeneo ya vijijini na sio
mijini tu, “ Tunataka watanzania watibiwe hapa hapa nchini kwa kupata huduma za
afya zilizo bora hadi vijijini na sio watu wachache tu wenye uwezo kwenda
kutibiwa nje na wanhyonge wanabaki kupoteza maisha.” Alifafanua.
Hata
hivyo katika hotuba hiyo ambayo ilikuwa fupi, amesema mengi yanapatikana kwenye
tovuti ya CHADEMA, ambapo ilani kwa ukamilifu wake inapatikana humo.









































No comments :
Post a Comment