Saturday, August 29, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:NITAUNDA MAHAKAMA MAALUM ZA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UFISADI NA UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA


01
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Njombe katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba wa CCM mjini  humo, Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo huku akiahidi kuboresha mambo mbalimbali katika serikali yake ikiwemo Elimu, Kilimo, Viwanda.
Ameongeza kwamba watu wengi watajiuliza na kusema hizi ni siasa fedha atapata wapi? ” Mimi si mwanasiasa ila ni mtendaji zaidi na ninajua mianya inayopoteza fedha za serikali  nipeni kazi nikazibe mianya hiyo” Amesema wakuu wa idara mbalimbali za serikali wajiandae na kujiweka sawa kabla hajaapishwa kwani hatavumilia uzembe kazini, Wizi na Ufisadi huku akiahidi kuanzisha mahakama maalum itakayoshughulikia kesi za ufisadi na ubadhirifu wa mali za serikalini ili watuhumiwa wahukumiwe haraka.
Uchaguzi mkuu wa jamhuri ya muungano ya Tanzania  wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini Kote. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-NJOMBE)
1
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo.
2
Umati uliohudhuria katika mkutano huo.
3
Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akimnadi Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
4
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa pamoja na wananchi waliohudhuria katika mkutano wake wa kampeni mjini Njombe leo.
5
Wananchi wakipunga mikono yao juu kama ishara ya kumkubali Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
7
Mgombea ubunge wa jimbo la Njombe Kusini: Edward Mwalongo akijinadi mbele ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
8
Mabasi maalum yaliyopambwa picha za Dr. John {ombe Magufuli.
9
Mlemavu huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja alikuwa ni miongozi mwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
10
Mgombea ubunge wa jimbo la Kyela mkoani Mbeya Dr. Harrison Mwakyembe akimnadi Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Njombe katika uwanja wa Nanenane.
11
Shilole akikamu jukwaani kaazi kwelikweli.
12 13
Kada wa CCM aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la Katiba akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Njombe leo.
14
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mh. Temba akifanya vitu vyake jukwaani.
15
Chege naye amekonga nyoyo za wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
16
Mama Martina Jonas wa Njombe akiwa na watoto wake ambao ni watumishi wa CCM  kulia Edward Mpogolo na kushoto Rodrick Mpogolo wakati alipohudhuria katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Njombe
17
Vijana waendesha Bodaboda wakipiga vuvuzela wakimshangilia  Dr. John Pombe Magufuli.
18
Wana CCM wakishangilia.
19
Msafara wa Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Nanenane.
20
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wakati akiwa njiani kuelekeamjini Njombe kwa ajili mkutano wa kampeni.
21
Akina mama wakimpokea kwa matawi ya miti huku wakicheza ngoma.
22
Wananchi wakimpokea kwa mabando yenye kumsifu Dr. John Pombe Magufuli.
23
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe.
24
Vikongwe hawa ambao majina yao hayakufahamika wanaonekana wakijadili jambo wakati wa mkutano wa kampeni wa Dr. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe.
25
Wananchi hawa wakifurahia hotuba ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe mkoani Njombe.
26
Hawa wakifuatilia mkutano huo.
27
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akilimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula.
29
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa mwananchi katika kata ya Tandala mkoani Njombe 
30
 Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju akisalimia wakazi wa Iwawa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika stendi ya Mabehewani Makete.
31
Huu ni ujumbe wa wananchi wa Makete walioutoa kwa jia ya mabango kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Iwawa Makete.
32
Wananchi wakishangilia huku wakiwa wameshikilia vipeperushi vyenye picha ya Dr. John Pombe Magufuli.
33
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa CCM na mjumbe wa kamati kuu Mh. Pindi Chana katikati ni Mgombea ubunge wa jimbo la Makete Bw. Norman Sigala.

Mgombea Mwenza MAMA SAMIA ATINGA SINGIDA LEO

 Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akiwahutubia wananchi katika mkutano huo leo
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, alipohutubia katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo.
 Baadhi ya viongozi na wananchi wakijimwayamwaya kwa furaha  wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimiabaadhi ya viongozi, baada ya kuwasili  katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo.
 Wananchi waliojawa na furaha wakimkimbilia kumlaki, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika viwanja vya Kyengege, Iramba mkoani Singida leo
 “Baba hakimbii nyumba” Kijana akiwa na bango linalowasema wanaaokimbia  kutoka CCM kwenda upinzani kutokana na kutochaguliwa katika nafasi za uongozi, kijana huyo alipokuwa kwenye mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, uliofanyika leo Iramba mkoani Singida.
 Mgombea Ubunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba akiselebuka na baadhi ya viongozi na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika eneo la Kyengege, Iramba mkoani Singida, leo.
 Mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibu, Mwigulu Nchemba akiomba kura, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika leo katika jimbo hilo.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa mgombea Mwenza huyo, uliofanyika leo katika jimbo hilo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kushoto ni Mgombea wa Ubunge jimbo la Mkalamo, Allan Kiula
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mkalamo, Allan Kiula, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni, wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo, kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Singida. Picha na Bashir Nkoromo).

KARUMA MWENYEKITI MPYA WA TWFA

Canada
Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini (TWFA)  umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Nafasi ya katibu msaidizi imekwenda kwa mwandishi wa habari za michezo Someo Ng’itu, na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFWA imekwenda kwa Debora Mkemwa na Theresia Mng’ongo.
Mgeni rasmi katika uchaguzo huo alikuwa ni katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambapo na uchaguzi ulisimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya uangalizi wa Jeremia Wambura kutoka kamati ya Uchaguzi ya TFF.
TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya mpira wa miguu ya wanawake nchini.

SHUKURANI ZA CCM KWA KUJITOEKEZA KWA WINGI SANA KWENYE MIKUTANO

unnamed

BANK OF AFRIKA TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 210 KUSAIDIA MATIBABU YA WOTOTO WANAOZALIWA NA MIGUU ILIYOPINDA

  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani
kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya
CCBRT
…………………………………………..
NA  FRANCIS DANDE
 
RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana
aliongoza  matembezi ya hisani ya
kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani
kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya
watoto waliopinda miguu.
Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika – Tanzania, lengo kuu
lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia
watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni
ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja
iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa
watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu
nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa
ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika –
Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria
kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli
zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu
wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili
jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa
jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata
matibabu,” alisema Mwanaidi .
Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza:
“ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa
Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi
chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya
watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na
matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu
wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”

Rose Mhando athibitisha Tamasha la kuombea Amani katika kuelekea uchaguzi mkuu

12Na Mwandishi Wetu
…………………………………..
MWIMBAJI wa muziki wa injili Rose Mhando  amethibitisha rasmi kushiriki katika Tamasha kubwa la kihistoria la kuiombea Amani nchi kuelekea uchaguzi mkuu linarotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kabla ya kwenda mikoani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa maandalizi  ya tamasha hilo Alex Msama, alisema Mhando tayari amethibitisha kuimba siku hiyo, ambako tayari ameshaanza maandalizi ikiwa pamoja na nyimbo mpya ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha amani.
Msama alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo la kihistoria yanaendelea vizuri  ikiwa pamoja na waimbaji kujiandaa vizuri watakuwepo waimbaji kutoka nchi zaidi ya tano kuungana na watanzania katika tukio hilo ambalo litashirikisha matukio mbalimbali.
Aidha Msama alisema kuwa mbali ya kuliombea taifa amani kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema kuwa waimbaji wengine wanaendelea kuthibitisha  ambapo pia mbali ya kuimba mmojammoja wataimba wimbo wa pamoja  ambao umeandaliwa, hivyo Msama aliwaomba watanzania kujitokeza katika tukio hilo muhimu la kitaifa.
Naye  Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Beno John Chelele alisema tamasha hilo ni la muhimu  hasa katika kipindi hiki cha uhaguzi ambao umekuwa wa tofauti na chaguzi zilizowahi kufanyika miaka ya nyuma.
“Kila Mtanzania  ashiriki  tuliombee taifa letu kokote litakakopita tamasha hili ni la muhimu hasa katika wakati huu wa uchaguzi ambao ni wa aina yake,” alisema Beno.
Tamasha hilo litanzia mkoa wa Dar es Salaam Oktoba 4, Morogoro Oktoba 7, Iringa 9,Mbeya Oktoba 11, Dodoma Oktoba 14, Shinyanga Oktoba 16 na kumaliziwa na Mwanza Oktoba 18.

MABALOZI WAZUNGUMZA NA Dk.Ali Mohamed Shein.

????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.
[Picha na Ikulu.]
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo.

UZINDUZI WA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA OKTOBA 4, 2015 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu  utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Benno Chilele (kushoto), akizungumza katika tamasha hilo. Kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa Tamasha la Krismas na Pasaka, Alex Msama. 
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

BUNGE LA WATOTO OYSTERBAY SHULE YA MSINGI MKOANI MANYARA WAFANIKIWA KUWARUDISHA WATOTO WA MITAANI SHULE

Abdallah Waziri – ambaye ni mmoja wa watoto wa mitaani aliyerudishwa shule kwenye kikao cha leo.
Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake katika kikao  cha bunge katika shule ya oysterbay mkoani manyara
Mbunge Nasri Selemani akifuatilia hoja kwa makini.wakati kikao cha bunge la watoto likiendelea katika shule ya oysterbay mkoani manyara 
 Mbunge Nasri Selemani ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa nyumbani na sasa kwa jitihada za bunge amerudishwa shuleni,,akichangia hoja.
Mtangazaji wa Kipindi cha Tafakari Time Benedicta Mrema akizungumza na Abdallah Waziri na kumkabidhi mchango wa shilingi 57,800 aliochangiwa kwa ajili ya kumuwezesha mahitaji ya shule.
Raisi wa Bunge la watoto Oysterbay, Manyara – Sarah David akitoa hotuba ya ufunguzi wa bunge la watoto katika shule ya oysterbay mkoani manyara
Wabumbe wa Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Wajumbe a Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Waliosimama, Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
Mtandao wa  Marafiki wa Elimu Babati (BADENET) ulianzishwa mwaka 2012 chini ya uongozi wa Asia Mtibua, mtandao huu ulianzishwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za elimu pamoja na kuanzisha kituo cha kupashana habari.
Moja ya mafanikio ya BADENET ni kuanzishwa kwa Bunge la Watoto katika shule ya msingi Osterbay mkoani Manyara. Bunge hili lilianzishwa kwa lengo la kuwaleta pamoja watoto waliopo shuleni na ambao wapo nje ya shule ili waweze kujadili masuala ya elimu ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuweza kusikilizwa wao kama watoto. Bunge hili la watoto linajumuisha wajumbe 43 (26 wasichana na 17 wavulana) na hukutana mara 1 kwa kila mwezi. Mpaka sasa jumla ya watoto wa mitaani 19 wamerudishwa shuleni na wanasoma, wapo wanaoingia asubuhi na wengine mchana.
Leo hii Bunge la watoto Oysterbay mkoani Manyara limekutana kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili  watoto wa mitaani “Chokoraa” ili kuzungumza namna ambavyo watawawezesha  watoto hao kupata fursa ya elimu kama watoto wengine waliopo shuleni. Katika kikao cha leo bunge limefanikiwa kumrudisha shuleni mtoto Abdala Waziri ambapo alichangiwa na wabunge, marafiki wa elimu na walimu jumla ya shilingi 57,800 ili zimuwezeshe kununua mahitaji muhimu ya shule.
Mkakati wa bunge la watoto katika shule ya msingi Osterbay ni kuhakikisha kuwa kila mbunge anamrudisha shuleni mtoto yoyote ambaye yuko mtaani na kuhakikisha wanafurahia fursa ya kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.
Timu ya Tafakari Time, kipindi kinachorushwa kila siku ya alhamisi kupitia ITV ilishiriki kikao cha leo kwa lengo la kujifunza uendeshwaji wa shughuli za bunge hili la watoto.

Ofisi ya Madini Mtwara kutoa leseni za madini ndani ya siku moja

1
Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe akielezea hatua za Wizara katika kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) mjini Mtwara. Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wachimbaji wa madini kuhusu huduma hiyo pamoja na kuwasajili.
2
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
3
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando akifungua mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini kutoka katika mkoa wa Mtwara.
4
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini kutoka Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA), Festo Balegele akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
5
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
6
Mtaalam kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtwara, Juma Namuna akielezea umuhimu wa wachimbaji wa madini kujiunga na mfuko huo ili kunufaika kwa kupata mikopo.
7
Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha akielezea faida za kujiunga na huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao katika mafunzo hayo.
8
Mchimbaji mdogo wa madini ya chumvi, Hussen Abdalah akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
9
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa nne kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na wachimbaji wa madini kutoka Lindi walioshiriki mafunzo ya huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyofanyika mjini Lindi.
…………………………………………..
Na Greyson Mwase, Mtwara
Ofisi ya Madini, Kanda ya Kusini yenye ofisi zake mjini Mtwara imeanza kutoa huduma za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini ndani ya siku moja tofauti na ilivyokuwa awali.
Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando katika mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini mkoani Mtwara.
Mhando alisema kuwa awali maombi yalikuwa yakichukua muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mtandao na kuongeza kuwa ofisi yake imeboresha mtandao na kuanza kutoa leseni ndani ya siku moja.
Alisema ofisi yake ina uwezo wa kushughulikia ombi moja la leseni ndani ya nusu saa iwapo mwombaji atakuwa amekamilisha vigezo vyote vinavyotakiwa.
Alieleza kuwa tangu huduma ya mtandao iboreshwe ofisi ya madini imekuwa na uwezo wa kushughulikia maombi 20 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa inachukua muda mrefu.
Akielezea mikakati ya ofisi yake katika utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao, Mhando alisema ofisi imejipanga kwa zoezi la kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanaingizwa katika mfumo huu na kunufaika na huduma hiyo
Aliongeza kuwa ili kuwafikia wachimbaji wa madini ya chumvi ambao idadi yako kubwa ni wazee, ofisi yake imeweka utaratibu wa kuwatembelea kwenye maeneo yao ya kazi, kuwapa elimu pamoja na kuwasajili kwenye mfumo huu.
Akielezea faida za mfumo mpya wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao Mhando alisema kuwa mfumo utawawezesha wamiliki wa leseni za madini kupata taarifa za leseni zao wakati wowote pamoja na kufanya malipo ya leseni zao kwa njia ya mtandao yaani M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa
“Mfumo huu utapunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wachimbaji na kuondoa dhana ya kwamba kuna upendeleo kwenye utoaji wa leseni za madini.” Alisema Mhando.

Rais Kikwete azindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao

w1
Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.
w2
Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya  baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.w5 w6
w3
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao.(picha na Freddy Maro)

SEHEMU YA HOTUBA YA MWAKYEMBE

MAGUFULI AMJULIA HALI NA KUMPA POLE MEYA WA JIJI LA MBEYA MH ATHANAS KAPINGA BAADA YA KUPATA AJALI

 
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas
Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za
maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi
(ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo.
 Mmoja wa Wauguzi walioko kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU),akimpa maelezo mafupi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli alipokwenda kumjulia hali n kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wauguzi walioko katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa Mbeya,mara baada ya kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas
Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za
maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mke wa Meya Mama Kapinga mara baada ya kutoka
kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas
Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za
maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
 
 PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA

DK, FAUSTINE NDUGULILE AKIHUTUBIA MKUTANO VIJIBWENI

  Mgombea Ubunge Jimbo la Kigamboni  kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) DK.Faustine Ndugulile akihutubia Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mzimu Kata Vijibweni Kigamboni Dar es Sallam (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA).
 Wananchi wakifurahia alipokuwa akipanda jukwaani Mgombe ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM DK.Faustine Ndugulile
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke na Mjumbe Halmashauri kuu Mkoa, Yahaya Sikunjema  (kulia) akimkabidhi Ilani ya Chama hicho Mgombea nafasi ya Udiwani kupitia Chama hicho   Zacharia Mkundi  katika mkutano wa kampeni ulio fanyika Kata ya Vijibweni Dar es Sallam
 

Rais Kikwete akutana Alpha Konare Mjumbe wa AU Sudan ya Kusini

SU1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Mhe.Alpha Oumar Konare ambaye ni msuluhishi wa Umoja wa Afrika(AU) katika mgogoro wa Sudan ya Kusini ikulu jijini Dar es Salaam jana.Mbali na majadiliano yaliyohusu vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa changa la Sudan ya Kusini Bwana Konare ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Mali(1992-2002) na mwenyekiti mstaafu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika alimweleza Rais Kikwete umuhimu wa kutumia Kiswahili katika mikutano ya Umoja wa Afrika.(picha na Freddy Maro)
SU2

Rais Kikwete amjulia hali Bwana Charles Kizigha

KIZ1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mwandishi wa habari Mkongwe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Sunday News Bwana Charles Kizigha nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam jana jioni.Aliyesimama kulia ni mtoto wa mwandishi huyo wa habari Mhe.Angela Kizigha ambaye ni Mbunge wa Afrika Mashariki.Rais Kikwete alimtembelea Bwana Kizigha nyumbani kwake baada ya kupata taarifa kuwa ni mgonjwa(picha na Freddy Maro) 

KIZ2 KIZ4

WAANDISHI HABARI WA ZANZIBAR WAPATIWA MBINU BORA ZA KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI MKUU.

 X2
Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka akifafanua kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuripoti uchaguzi Mkuu.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
X4
Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi, alipotembelea katika mafunzo hayo huko ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Weles Mjini Zanzibar.
X1
Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan (aliesimama)akifahamisha kitu katika mafunzo ya siku tano yalimaliza jana Agosti 28 yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
X3
Badhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu wakisikiliza nasaha zilizotolewa na Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka (hayupo pichani) katika mfunzo yaliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
05
Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble (wakatikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wasimamizi wa mafunzo hayo (kulia) aliekaa ni Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan na kushoto ni Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali mpya ya Abdalla Mzee

3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wananchi jana wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali mpya ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba akiwa katika ziara ya Moahuo kufungua miradi ya maendeleo.
,[Picha na Ikulu.]
2
Waziri wa Afya Rashid Suleiman akisalimiana na Wananchi wakati wa Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee pia kumkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake katikasherehe hiyo jana,
4
Balozi Mdogo wa China nchini Tanzania anayeishi Zanzibar Xie Yunliang akitoa salamu zake kwa wananchi na Viongozi wakati wa sherehe za  uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee inayojengwa na Kampuni kutoka China Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoweka jiwe la msingi  katika ziara ya  kufungua miradi ya maendeleo.
1
Baadhi ya wananchi wa Mji na Vitoji vya Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba wakiwa katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la Msingi wa ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani inayojengwa na kampuni kutoka China jiwe hilo lililowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana.

Wanawake Wamlilia Maji Mgombea Mwenza wa CCM

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.
Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.
Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara.
Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
……………………………………………
Na Joachim Mushi, Longido
WANAWAKE wa Wilayani Longido wamemsimamisha mgombea Mwenza wa urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu njiani akielekea jukaani kuhutubia wananchi wakimlilia kuwatatulia kero ya maji katika Kata ya Longido ambapo kila familia imekuwa ikipata huduma hiyo mara moja kwa wiki hali ambayo wamesema haikidhi mahitaji.
Bi. Samia alilazimika kusimama eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika wakichota maji kwa zamu huku kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi mara moja kwa kila wiki kiwango ambacho akinamama wengi walisema akikidhi mahitaji kwa familia zao.
Mgombea huyo wa CCM aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama mwanamke anajua shida ya maji inavyowatesa akinamama katika familia ikiwa huduma hiyo inapokuwa tatizo katika upatikanaji wake, hivyo atalisimamia suala hilo. Alisema Serikali ya CCM itakapoingia madarakani imetenga shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kupeleka maji eneo la Longido mradi ambao utamaliza kero ya maji eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa kuwawezesha wafugaji wa eneo hilo wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa ya mifugo kwa wafugaji ili kuwaendeleza.
“…Kazi hii tutaifanya ndani ya kipindi kifupi mara tu baada ya kufanikiwa kurudi madarakani, Serikali inayomaliza muda wake imefanya mengi na sisi tutaendeleza na kuboresha zaidi. Alisema wanajua kilio cha mahakama katika wilaya ya Longido hivyo mara baada ya kuingia madarakani wataijenga.
Alisema akiwa njiani katika mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo wa ukame katika vijiji lakini anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye atakufa na njaa endapo hali hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya CCM katika ghala la chakula ina akiba ya kutosha.
Mgombea huyo mwenza wa CCM pia alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo Monduli aliwaomba wanaMonduli kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya chama hicho ambayo pia imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Longido na Longido hadi Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba wanaMonduli kumchagua mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Bi. Namelok Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na historia nzuri ya utendaji kama alivyokuwa babayake marehemu, Edward Moringe Sokoine. Aliwaomba pia kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu.

MAMA SAMIA AHUTUBIA LEO MBULU NA BABATI

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Mgombea ubunge jimbo la Mbulu Vijijini, kwa tiketi ya CCM, Fraten Maasai, akiomba kura baada ya kutambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan  katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Umati wa wananchi waliohudhuria  mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, leo  kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiingia kwenye  mkutano wake wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Kijana akionysha bango la kumfagilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano wa kampeni za CCM za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Mgombe mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akimsalimia kijana Augustine Male, mwenye ulemavu, ambaye alihudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza huyo, leo Mbulu Mjini.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Karatu, kwa tiketi ya CCM, Wilbard Lorri, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji cha Mbulumbulu katika jimbo hilo.
Mwananchi akiwa na mabango ya kuwafagilia mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Mbulu mjini.
Wananchi katika Kijiji cha Mbulumbulu, wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kufanya mkutano wa kampeni katika eneo hilo leo
Kina mama wakimzawadia mavazi, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha.
Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika eneo la Karatu mjini, Mama Samia ambapo alilazimika kuwasalimia, wakati akiwa njiani kwenda  Mbulu leo
 
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwasalimia wananchi waliosubiri msafara wake kkwenye makutano ya mkoa wa Arusha na Manyara, wakati akitoka Arusha kuingia Manyara
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Magugu, wilayani Bbati mkoani Manyara leo.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE APINGWA KUPITA BILA KUPINGWA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU

 Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipinga kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili wake, Paulo Kalomo.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga, akionesha fomu namba 10 ambazo alikabidhi kwa Msimamizi wa Uchaguzi. 
 Wakili wake, Paulo Kalomo, akizungumza katika mkutano huo kuhusu sheria inavyoelekeza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga amepinga vikali kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma.
Mkinga alitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi na kueleleza kuwa sababu zilizotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kuwa hakupeleka fomu namba 10 hazikuwa na ukweli wowote.
“Nilipofika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa nilisaini na kukabidhi tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 (fomu namba 10) na baada ya kusaini nilimkabidhi msimamizi wa uchaguzi pamoja na fomu namba 8B,picha, stakabadhi ya malipo ya dhamana ambapo vilihakikiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gervas Lupembe” alisema Mkinga.
Mkinga alisema katika jambo lisilo la kawaida msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo hilo hakubandika kwenye ubao wa matangazo tamko hilo na alipomfuata msimamizi huyo kumuulizia msaidizi wake Lupembe alikiri kupokea na kuziwasilisha kwa kiongozi wake ili kutia saini ambaye naye alikiri kuzipokea lakini wakati ana bandika tamko hilo la Mgombea wa CCM fomu hiyo hakuiona.
Alisema katika pingamizi alilowekewa dai mojawapo ni kutokuwepo  tamko hilo kwenye fomu zake hali inayoonesha wazi kuwa kulikuwa na mchezo mchafu uliofanyika ili kumpitisha Filikunjombe bila kupingwa.
Mkinga alisema kuwa kuwaondoa wagombea kwa sababu zisizo za msingi ni kuiminya demokrasia na kuirudisha nchi nyuma kwani kunaweza kusababisha kukosa viongozi wazuri na kubakia na viongozi wasiofaa na wasiotaka kushindanishwa kwa kuwapa nafasi wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Mgombea huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alimuomba msimami wa uchaguzi wa jimbo hilo kutupiliambali pingamizi lililotolewa dhidi yake na mgombea mwenzake ambapo anasubiri majibu baada ya kuandika barua ya malalamiko.

WHO YATOA DAWA ZA MILIONI 42.2 ILI KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU NCHINI.

Inline imageKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Donan Mmbando (katikati) akipokea msaada wa dawa za kuthibiti maambukizi ya kipindupindu kutoka kwa mwakilishi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Rufaro Chatora(kulia). Kushoto ni Mganga Mkuu kutoka Wizara hiyo Dkt. Margaret Mhando.
Picha na Ally Daud
 …………………………………………………
 
 
Na Ally daud-Maelezo
 
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imepokea msaada wa  dawa  za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini kutoka Shirika la Afya Duniani zenye thamani ya shilingi milioni 42.2.
Msaada huo umepokelewa leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Donan Mmbando.
Akizungumza mada baada ya kupata msaada huo amesema dawa hizo ambazo ni katoni 1000 za water guard,  lita 100 za Cresol Saponated  zitasaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Naye  mwakilishi  wa Shirika la Afya Duniani(WHO)  nchini Tanzania Dkt.. Rufaro Chatora amesema kuwa ni wajibu wao kusaidia kupamabana na maambukizi ya ugonjwa huo ili kuhakikisha unatokomea nchini.
Ameongeza kuwa ni jukumu la wananchi la kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kudhibiti hali ya usafi kuanzia mwili , chakula na mazingira yanayowazunguka kwa ujumla.
Dkt. Chatora amesema  kuwa ni vema wananchi wakapigwa  marufuku kuuza vyakula sehemu za kampeni ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Aidha , Mwakilishi huyo wa WHO amesema kuwa Shirika lake litatoa msaada wa shilingi milioni 159.8 kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuzuia ugonjwa wa KipindupinduNchini .

TWIGA KUFUNGA DIMBA NA IVORY COAST

tanzaniteTimu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
Twiga Stars iliyoweka kambi kisiwani Zanzibar kwa takribani mwezi mmoja sasa, itacheza mchezo wake pili Septemba 9, dhidi ya Nigeria kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Congo-Brazzavile Septemba 12, 2105.
Jumla ya timu nane za Wanawake kutoka Barania Afrika zinashirki fainali hizo ambazo ni Nchi za Afrika Kusini, Cameroon, Ghana, Misri (wamejitoa) kundi B, na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast, Nigeria na Tanzania kutoka kundi A.
Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya nusu fainali.

A Fraudster Suspect in Dar ES SALAAM Court

SONY DSCA fraudster suspect, PhiliphMbithiMutiso (28), Kenyan National, resident of Namanga in Kenya at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar Es Salaam on 28th August 2015 faced with three charges under the Economic and Organised Crime Control Act of 2002, including fraudulently operating of a communication network and illegally receiving and terminating International Telecommunications Traffic, using unlicensed equipment thus causing a loss amounting to Tshs 757,200,000/- to the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) and the United Republic of Tanzania. The suspect who unlawfully operated the international gate-way in Arusha Region and Namanga appeared before the Principal Resident Magistrate HurumaShahidi was remanded till 10th September 2015 when the case comes up for another mention. Several fraudster suspects have been intercepted and booked interfering with the national communication network system, since the establishment of the Telecommunications Traffic Monitoring System (TTMS).(Photo by SemuMwakyanjala, TCRA)

Wadau wa Maendeleo ya Viwanda Watangaza vyema Fursa za Uwekezaji nchini

 DSC09586
Naibu katibu mtendaji kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango anayesimamia klasta ya Miundombinu na huduma, mhandisi Happiness Mgalula akitoa hotuba katika mkutano uliowahusisha ujumbe wa wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka Tanzania  na ujumbe wa  wawekezaji kutoka nchini China.
DSC09565
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasikiliza kinachoendelea ndani ya mkutano wa wadau wa maendeleo ya viwanda.
DSC09592
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasoma kwa makini baadhi ya nyaraka katika mkutano huo.
DSC09687
Picha ya pamoja kati ya wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka Tanzania na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China.
…………………………………………………..
Na Adili Mhina.
Wadau wa maendeleo ya viwanda nchini wametumia vyema fursa ya kutangaza na kuwashawishi wawekezaji wa kigeni kutoka nchini China kuwekeza katika maeneo muhimu yatakayohimiza maendeleo ya viwanda na kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.
Hayo yametokea katika mkutano wa siku mbili mfululizo kati ya wadu wa maendeleo ya viwanda kutoka serikalini, sekta binafsi nchini pamoja na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China uliomalizika jana. Mkutano huo ulioandaliwa na kituo cha kimataifa cha kupunguza umaskini cha nchini China, Mfuko wa maendeleo wa China-Afrika kwa kushirikiana na kituo cha uwekezaji Tanzania na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ulibeba ujumbe usemao, “punguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda”.
Katika hotuba yake kwa niaba ya katibu mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya mipango, naibu katibu mtendaji anayesimamia klasta ya miundo mbinu na huduma mhandisi Hapness Mgalula alisema Mkutano huo umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania ipo katika maandalizi ya kuandaa  mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) ambao umebeba dhima ya kuendeleza uchumi wa viwanda.  “mkutano huu sio kwamba tu umekuja wakati muafaka lakini pia ni muhimu kwa sababu miongoni mwa yatakayojadiliwa hapa yatatumika katika kuboresha huo mpango”, alisema Mgalula.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), bi Juliet Kairuki  aliueleza ujumbe kutoka China kuwa kuwa Tanzania kuna maeneo mbali mbali ya uwekezaji ambayo yanaweza kuleta tija kubwa kwa Taifa pamoja na wawekezaji.  Alisisitiza zaidi kwa wawekezaji hao kuwekeza katika kujenga viwanda nchini ili kuondokana na usafirishaji bidhaa ghafi kwenda nchi za nje. Miongoni mwa maeneo aliyoyawekea msisitizo katika uwekezaji wa ujenzi wa viwanda ni pamoja na;  ubanguaji wa korosho, usindikaji wa mbegu za mafuta, utengenezaji wa nguo, ngozi, utengenezaji wa nyama bora na maziwa.
Alisisitiza kuwa pamoja na kuwa  uwekezaji wa ujenzi wa viwanda katika maeneo hayo utasaidia kukuza ajira kwa wanachi  vilevile utasaidia kuongeza thamani ya bidhaa zinazotoka nchini kwenda kuuzwa nchi za nje. “kwa sasa bidhaa nyingi zinauzwa zikiwa ghafi na hii inafanya kuuza bidhaa bei ya chini wakati kama tukifanikiwa kujenga viwanda na kuuza bidhaa za viwandani thamani ya mazao yetu itaongezeka na italeta faida upande wa serikali na vilevile kwa muwekezaji,”.
Nae mkurugenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Palangyo aliwahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji hivyo yeyote anayekuja kuwekeza ajue kuwa yupo katika eneo salama na lenye tija kibiashara. Alieleza kuwa Tanzania ina faida nyingi za kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa amani na utulivu wa taifa toka kipindi cha uhuru, uwepo wa maliasili za kutosha kama vile madini na gesi asilia, upatikanaji wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo,  kuwepo kwa bahari inayotumika kupitisha bidhaa mbalimbali hususani kwenye nchi zisizo na bahari, na zingine nyingi.
Kwa upande wa Zanziabar Mkurugenzi wa uwekezaji  kutoka mamlaka ya uwekezaji vitega uchumi Zanzibar  (ZIP) Nasriya Nassor alieleza wadau kuwa Zanzibar ina fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za utalii, uvuvi, kilimo pamoja na maeneo mengine kama huduma za kifedha, usafirishaji, nishati pamoja na huduma mbalimbali za jamii.
Wawekezaji hao kutoka nchini China walionesha kuridhishwa na uwepo wa fursa mbalimbali zilizopo nchini na kueleza kuwa katika kutimiza azma ya kupunguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda Tanzania, China ina jukumu kubwa hususani katika kutoa mawazo, uzoefu, elimu, fursa na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

DR. JOHN POMBE MAGUFULI ATIKISA JIJI LA MBEYA

1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mbeya katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nzovwe jijini Mbeya huku akiwaambia wananchi hao kwamba anawaomba kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu kuwatumikia watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama, ukabila, Dini wala ukanda.
Akisisitiza kauli yake Dr. Magufuli amesema nipeni kazi kwani mimi sio mwanasiasa bali ni mtendaji, mkweli na Mchapakazi yaani “Hapa Kazi Tu”(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MBEYA)
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano huo
3
Mwigulu Nchemba akimpigia debe Mh. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
4
Mgombea ubunge jimbo la Kyela Mh. Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia katika mkutano huo.
5
Kada wa CCM Bw. Richard Kasesela akimpigia Debe Dr. John Pombe Magufuli.
6
Maelfu ya wananchi wakipunga mkono kama ishara ya kumkubali Dr. John Pombe Magufuli.
7
Msami msanii wa muziki wa kizazi kipya akitumbuiza katika mkutano huo.
8
Msanii Matonya akifanya vitu vyake jukwaani.
9
Msanii Sheta akikamua.
10
Shilole naye amekamua vya kutosha katika mkutano huo.
11 12 13
Baadhi ya wana CCM wakiwa wameshikilia mabango yenye picha za Dr. John Pombe Magufuli.
15
Wanamuziki wa bendi ya TOT wakifanya vitu vyao jukwaani.
16
Jamaa huyu naye akitoa burudani ili mradi CCM Mbele kwa mbele.
17
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipuga mkono kwa wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwnanja wa Nzovwe tayari kwa mkutano wake wa kampeni.
19
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi mara baada ya kuwahutubia mjini Mbeya leo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akitembea kwa miguu na wananchi mara baada ya kushuka kwenye gari lake wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa mkutano mjini Mbeya.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea udiwani wa Mbeya mjini.
26
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM  Ndugu William Lukuvi kushoto , Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro katikati na Mwigulu Nchemba.
27

Baadhi ya wana CCM wakifuatilia mkutano huo.
magu
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya mjini Bw. Sambwee Shitambala kwenye mkutano wa kampeni iliofanyika kwenye viwanja vya Nzovwe jijini Mbeya.

Balozi wa Misri amuaga Rais Kikwete Ikulu

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuagana na Balozi wa Misri anayemaliza muda wake Mhe.Hossam Moharram ikulu jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy Maro)
unnamedn

NHC YATILIANA SAINI YA MAKUBALIANO YA MIKOPO YA NYUMBA NA BENKI NNE ZA HAPA NCHINI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel, Dar-es-Salaam leo asubuhi. Leo NHC imetiliana rasmi  saini na benki na taasisi za Diamond Trust Bank Tanzania Limited, Equity Bank Tanzania Limited, First National Bank Tanzania Limited, International Commercial Bank Tanzania Limited.  
Tayari NHC inafanya kazi na benki kumi na mbili ambazo ni Azania Bank, Bank of Africa, Bank ABC, Commercial Bank of Africa, CRDB Bank, Dar es Salaam Community Bank, Exim Bank, KCB Bank, National Bank of Commerce, NIC Bank, National Microfinance Bank na Stanbic Bank.
PICHA ZOTE ZA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel, Dar-es-Salaam leo asubuhi. Leo NHC imetiliana rasmi  saini na benki na taasisi za Diamond Trust Bank Tanzania Limited, Equity Bank Tanzania Limited, First National Bank Tanzania Limited, International Commercial Bank Tanzania Limited.  
Tayari NHC inafanya kazi na benki kumi na mbili ambazo ni Azania Bank, Bank of Africa, Bank ABC, Commercial Bank of Africa, CRDB Bank, Dar es Salaam Community Bank, Exim Bank, KCB Bank, National Bank of Commerce, NIC Bank, National Microfinance Bank na Stanbic Bank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya NHC na mabenki manne iliyofanyika Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel, Dar-es-Salaam leo asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Felix Maagi pamoja na Mwakilishi wa benki ya Diamond Trust Bank Tanzania Limited wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Felix Maagi akipena mkono na Mwakilishi wa benki ya Diamond Trust Bank Tanzania Limited mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano.hayo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa , Felix Maagi pamoja na Meneja Mkuu wa Mikopo wa Equity Bank wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania,Felix Maagi akipena mkono na Meneja Mkuu wa Mikopo wa Equity Bank mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi pamoja na Mkuu Huduma za Wateja wa Benki ya First National Bank Tanzania Limited, Francois Bank wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania,Felix Maagi akipena mkono na Mkuu Huduma za Wateja wa Benki ya First National Bank Tanzania Limited, Francois Bank mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi pamoja na Mwakilishi wa International Commercial Bank Tanzania Limited wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akipena mkono na Mwakilishi wa International Commercial Bank Tanzania Limited mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki nne zilizoingia mkataba na NHC.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki nne zilizoingia mkataba na NHC.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania,Felix Maagi akijadiliana jambo na Mkuu Huduma za Wateja wa Benki ya First National Bank Tanzania Limited, Francois Bank kabla ya kutiliana saini ya makubaliano hayo.

Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifuatilia utiaji saini huo uliofanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
indexW
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE
• MTU MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI.
• MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA B AADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUCHANA BENDERA YA CHAMA NA KUBANDUA BANGO LA MGOMBEA.
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA DAWA YA KULEVYA [BHANGI].
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ATHUMANI ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA ENEO MLIMA NYOKA NJE KIDOGO NA JIJI LA MBEYA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA ITEWE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
UCHUGUZI UNAFANYIKA KUPATA UKWELI WA SABABU ZILIZOPELEKEA MAUAJI HAYO, KWANI ZIPO TAARIFA ZINAZODAI KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WATATU NI BODABODA NA WALIKUWA WAKISINDIKIZA LORI LILILOKUWA LIMEBEBA SHABA BILA KUWASILIANA NA ASKARI WALIOKUWA DORIA ENEO HILO AMBALO UWA NA MATUKIO YA UHALIFU YA MARA KWA MARA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. ASKARI POLISI WALIOKUWA KWENYE ENEO LA TUKIO PAMOJA NA WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO WANAHOJIWA KUPATA UKWELI. UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBINISYE MWANDOBO (65) MKAZI WA KISEGESE ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISSION ITETE KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISEGESE, KATA YA KISEGESE, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/KANUNI/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMANI JOHN @ MWAKASEGE KWA KOSA LA KUHARIBU MALI [KUCHANA PICHA] YA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO ILOMBA, KATA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA ALIONEKANA AKIWA AMEBEBA MABANGO YA PICHA ZA MGOMBEA WA URAIS HUKU YAKIWA YAMECHANWA VIPANDE VIPANDE NA NDIPO JITIHADA ZA KUMKAMATA ZILIFANYIKA NA KUMFIKISHA KATIKA KITUO KIDOGO CHA POLISI ILOMBA.
AIDHA KATIKA TUKIO JINGINE, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FADI MWASHIMAHA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI [KUCHANA BENDERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI].
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA NA VIJANA WENGINE WALIITOA BENDERA HIYO ILIYOKUWA JUU YA MTI NA KISHA KUICHANA KWA MADAI KUWA MTI HUO ULIOKUWA UMEFUNGWA BENDERA HIYO NI MALI YAO.
WATUHUMIWA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO HII KUTOKANA NA MAKOSA HAYO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NSAJIGWA BROWN (23) MKAZI WA ITUNGE 2. AHOBOKILE RUBEN (21) MKAZI WA ITUNGE NA 3. AYUBU CHURA (25) MKAZI WA BONDENI – WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 25.
WATUHUMIWA YA WALIKAMATWA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO ENEO LA BONDENI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments :

Post a Comment