Edwald Lowasa Waziri mkuu wa
Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiwasili katika
makao makuu ya ofisi za CHADEMA tayari kwa kuchukua fomu za kugombea
urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia chama hichi leo jijini
Dar es salaam.
Edwald Lowasa Waziri mkuu wa
Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiwapungia
mkikono wananchi kwenye makao makuu ya CHADEMA.
Edwald Lowasa Waziri mkuu wa
Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiingia katika
ofisi za makao makuu ya chama hicho kwa ajili ya kuchukua fomu za
kugombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho.
WAZIRI Mkuu wa zamani Edward
Lowassa, amechukua fomu kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kimpitishe kugombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Katika Makao Makuu ya chama
chake hicho kipya leo Edward Lowassa alipokewa na maelfu ya watu
waliovalia sare za chama huku wakiimba wana imani naye.
Edward Lowassa aliwasili makao makuu mchana moja kwa moja akaenda ofisi za Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa.
Huku akisindikizwa na
Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria wa chama Tundu Lissu na Naibu
Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Edward Lowassa aliingia katika
ofisi hizo katika jukwaa maalumu la kupokea fomu.
Lissu ndiye alikuwa mzungumzaji
wa kwanza kwa kuwahakikishia wanachama hawakubahatisha kumpokea Lowassa
kwa sababu walifanya utafiti wa kina.
“Kamati Kuu imejiridhisha kwa
kushirikiana na viongozi wote wa juu akiwemo Katibu Mkuu na manaibu wake
wote wawili, Mwenyekiti na makamu wote wawili, wajumbe wa Kamati Kuu na
Mkutano Mkuu, kuwa Edward Lowassa ndiye kiongozi tunayemtaka hivyo
Jumapili iliyopita tuliitisha Kamati Kuu ya dharura kumpitisha,” alisema
Lissu.
Baada ya kukabidhiwa fomu
aliyolipiwa na wanachama waliochangishana fedha hadi kufikia Sh milioni
moja, Edward Lowassa alisimama kuwasalimia waliohudhuria kwa kuwaahidi
kufanya kazi kwa juhudi ili kuiondoa Tanzania katika hali mbaya ya
kiuchumi.
“Nashukuru kwa kunipa heshima
kubwa namna hii, sina maneno ya kuwashukuru zaidi ya kuahidi kufanya
kazi kwa bidii ili iwe malipo ya mlichonifanyia.
“Shukurani yangu itakuja baada
ya kushinda uchaguzi, lakini ushindi hauji bila umoja. Chadema inaweza
kuleta mabadiliko kupitia ukawa.
Baada ya kumaliza kuzungumza
alisimama Mbowe kutoa neno la shukurani kwa Edward Lowassa kwa kusema
Chadema kitaendelea kuwa chama makini kinachosimamia maamuzi yake.
Vilevile alizungumzia ratiba ya
vikao vya kujadili fomu ya mgombea ambaye mpaka sasa ni Edward Lowassa
pekee, “Vikao vitaanza Agosti mbili kujadili namna tutakavyoingia katika
uchaguzi mkuu.
“Baraza Kuu litaketi Agosti
tatu kujadili fomu ya mgombea na kujadili ilani ya uchaguzi, Mkutano
Mkuu utafanyika Agosti nne kupitisha jina la mgombea na mgombea mwenza.
“Vikao vya kamati Kuu
vitaendelea tarehe tano, sita hadi saba kuidhinisha wagombea wa ubunge
kwa kushirikiana na Ukawa. Kazi ya kujadili wagombea si ndogo nawaomba
waandishi wa habari muwe wavumilivu msipige ramli,” alisema Mbowe.
Baada ya kumalizika hafla hiyo Edward Lowassa alitoka nje kwa ajili ya picha ya pamoja kuwaonyesha wanachama fomu yake.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa
Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo
imefanyika leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja
kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani,
wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30,
2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja
kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani,
wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30,
2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe
kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26
ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani
leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la
kabila la Masai na Kiongozi wa Mila ya Laibuwanani, Kisota Lengitambi,
wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwela Msingi la Ujenzi wa Barabara
ya Kia-Mererani. leo julai 30, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada
ya kumvisha vazi hilo. Picha na OMR
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa
kumbukumbu baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-
Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John
Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na
OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai
wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la
Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha
na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi,
Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji
wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani
Manyara. Picha na OMR
Serikali yatakiwa kuanzisha kitengo cha Idara ya Mikopo Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
……………………………………………………………………………..
Na Maryam Kidikona Miza Kona –Maelezo Zanzibar
Serikali imetakiwa kuanzisha
kitengo cha Idara ya Mikopo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ili
kuwaondosha usumbufu wananchi wanapotakata kurejesha fedha za mikopo
ZAIDI YA MECHI 900 ‘LIVE ‘KUTIMUA VUMBI NDANI YA SUPERSPORT
Meneja Uhusiano wa DSTV, Barbara
kambogi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
jijini Dar es Salaam leo julai 30, 2015 kuhusu moto wa la Liga utawashwa
ndani ya Super Sport 3(SS3) Afisa masoko wa Multichoice Tanzania,
Furaha Samaly (kushoto) na kulia ni Meneja uendeshaji wa DST,Ronald
Shelukindo.
………………..
Mechi zenye ubora wa HD pamoja na michuano ya Ligi kuu ya Uingereza (EPL),Ligi ya Hispania (La liga),Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA),Ligi ndogo za Ulaya (Europa),Mechi za FIFA za kirafiki za
kimataifa na Klabu bingwa ya Dunia ,Kombe la Ujerumani ,Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) na Kombe la FA.
kimataifa na Klabu bingwa ya Dunia ,Kombe la Ujerumani ,Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) na Kombe la FA.
Wateja wa DStv wakae tayari kwenye msimu wa mabingwa ulimwenguni ambapo Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine huku Manchester United wakihitaji kurudisha kiti chao cha ubingwa
Uingereza.
Katika msimu huu zaidi ya mechi 900 za kimataifa zitaonyeshwa
kimataifa na wateja wa DSTV Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi 450 live
huku wateja wa Dstv premium watazawadiwa mechi zote.
Babra amesema wateja wa Dstv vituko vya michuano yote ya
ligi kuu Uingereza vitaletwa kupitia Suparspot (SS5) kinochopaatikana katika
kifurushi cha Premium na SS5 itakuwa ndio nyumba ya soka la Afrika kwa Ligi kuu
ya Uingereza.
Uingereza.
Katika msimu huu zaidi ya mechi 900 za kimataifa zitaonyeshwa
kimataifa na wateja wa DSTV Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi 450 live
huku wateja wa Dstv premium watazawadiwa mechi zote.
Babra amesema wateja wa Dstv vituko vya michuano yote ya
ligi kuu Uingereza vitaletwa kupitia Suparspot (SS5) kinochopaatikana katika
kifurushi cha Premium na SS5 itakuwa ndio nyumba ya soka la Afrika kwa Ligi kuu
ya Uingereza.
Afisa masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samaly akifafanua jambo.
Meneja uendeshaji wa DST,Ronald
Shelukindo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu chanmeli mpya
ya michezo katika kingamuzi cha Multchoice.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa katika uzinduzi wa channel katika hafla hiyo.
NGOMA AFRICA BAND WAFUNIKA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TÜBINGEN 2015
Bendi maarufu ya muziki wa
dansi barani ulaya Ngoma Africa band maaruka kama FFU-Ughaibuni au
viumbe wa ajabu Anunnaki Alien’s inayoongozwa na kamanda Ras
Makunja,bendi hiyo yenye makao yake kule ujuerumani ,juzi iliuhakikishia
ulimwengu tena kwamba muziki wao ni moto wa kuotea mbali! bendi hiyo
ilifanikiwa kwa mara nyingine kuyafunika maonyesho ya kimataifa ya
International African Festival-Tübingen 2015,yaliofanyika katika viwanja
vya Fest Platz,jijini Tübingen,Ujerumani.
Bendi hiyo ilipanda jukwaani
majira ya saa 4.00 usiku huku uwanja huo ukiwa umezungukwa na ulinzi
mkali ! kamanda Ras Makunja akikiongoza jukwaani kikosi chake
kilichoshamili vijana wa kazi akina Afande Mo Benda (Soloist) Sajent
JoJo Sousa(Drumer) Kopro. Aj Nbongo (Bass) kijana Liga (Rhthym guitar)
madansa Jessica Ouyah na Sarah Fina kikosi hiko kilifanya show la kukata
na shoka.siku ya jumamosi 26 Julai 2015.
wapitie hapa www.facebook.com/ ngomaafricaband wasikilize na www.reverbnation.com/
TANZANIA YAFANYA KUFURU MBIO ZA NYIKA SARPCCO.
Wanariadha wa mbio za nyika katika michezo ya majeshi ya
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) wakiendelea na mbio hizo
jana katika mji wa Mbabane Swaziland ambapo wanariadha wa Polisi
Tanzania walifanikiwa kushika nafasi tatu za mwanzo.(Picha na Frank
Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Wanariadha wa mbio za nyika kutoka Polisi Tanzania
wakipongezana baada ya kumaliza kukimbia mbio hizo jana katika mji wa
Mbabane Swaziland ambapo michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini
mwa Afrika(SARPCCO) inaendelea. Tanzania walifanikiwa kushika nafasi
tatu za mwanzo katika mbio hizo.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la
Polisi-Swaziland)
………………………………………………………………………….
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland.
Wanariadha
wa Polisi Tanzania walioshiriki katika mbio za nyika katika michezo ya
majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini (SARPCCO) wamefanya kufuru kwa
kuzoa medali zote baada ya kushika nafasi tatu za juu.
Wanariadha
waliofanya vizuri na nafasi zao katika mabano ni pamoja na Basili John
(1), Fabian Nelson(2) na Josephat Joshua(3) ambapo mshindi wa
kwanza aliweza kutumia muda wa dakika 29:26:00.
Wanariadha
wengine kutoka Tanzania walioshiriki mbio hizo ni pamoja na Osward
Revelian, Wilbado Peter, Silvester Naal na Fabiola Willium kwa upande wa
wanawake na hivyo kusababisha ushindi wa jumla kwa kupata medali ya
dhahabu.
Kwa matokeo
hayo timu ya Tanzania inayoshiriki michezo hiyo imefanikiwa kufikisha
medali sita za dhahabu, nne za fedha na mbili za shaba na hivyo
kujihakikishia nafasi nzuri katika ushindi wa jumla wakati michezo hiyo
itakapofikia ukingoni Agosti pili mwaka huu.
Akizungumzia
matokeo hayo Kocha wa Wanariadha hao Rogart Steven alisema wanariadha
hao walijiandaa vyema na kujituma licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa
kutoka kwa wanariadha wa Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.
Katika
Michezo ya Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Wanariadha kumi na mbili
pekee ambao wameonyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo ukilinganisha
na mataifa mengine ambayo yameleta idadi kubwa ya wanamichezo..
EU increases humanitarian aid for Burundi refugees
The European Commission is releasing
€4.5 million in humanitarian assistance to help the increasing number
of refugees from Burundi that have fled to neighbouring countries. More
than 175 000 people, the majority of them women and children, are
estimated to have already left the country. “We cannot overlook the
deteriorating humanitarian situation affecting Burundi.
Refugee numbers are up in the
last three monthswhich is a serious cause of concern in an already
fragile region. This additional EU humanitarian funding will help
neighbouring countries accommodate refugees and meet their most urgent
needs.
It is a strong signal of the
EU’s solidarity with the most vulnerable people caught in a difficult
situation beyond their control,” said EU Commissioner for Humanitarian
Aid and Crisis Management Christos Stylianides, underlining “the
generous hospitality of the countries in the region who have welcomed
their Burundian neighbours.” This funding increase brings the total
humanitarian aid for the Great Lakes region for 2015 to €56.5 million.
The aid released mainly for
Burundi refugees amounts to €9 million since the end of April, when
their numbers started growing. Certain refugee camps have become
overpopulated and health risks have continuously worsened.
Serikali yasaini Mkataba wa kukusanya zaidi ya Sh. milioni 12 kupitia mapato ya ndani kwa mawaka 2015/16
Baadhi
ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA wakati wa hafla ya
kusaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya mapato ya ndani kwa mwaka wa
fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.
(Habari Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
……………………………………..
Serikaki imesainiana Mkataba wa
Makubaliano ya kukusanya Sh. Milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.
Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA.
“Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia malengo tuliyojiwekea katika kukusanya mapato ya ndani katika mwaka huu wa fedha” alisema Waziri wa Saada.
Waziri huyo aliwaasa watendaji wa TRA kuwawekea wafanya kazi mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa na wanapokwenda kinyume na makubaliano ya kazi watawajibishwa kwa mujibu wa sheri, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Bernard Mchomvu alimhakikishia Waziri wa Fedha kuwa watafikia lengo walilokubaliana kukusanya na hata kuzidi kiwango hicho ambacho kimeainishwa katika bajeti ya Serikali.
Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA.
“Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia malengo tuliyojiwekea katika kukusanya mapato ya ndani katika mwaka huu wa fedha” alisema Waziri wa Saada.
Waziri huyo aliwaasa watendaji wa TRA kuwawekea wafanya kazi mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa na wanapokwenda kinyume na makubaliano ya kazi watawajibishwa kwa mujibu wa sheri, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Bernard Mchomvu alimhakikishia Waziri wa Fedha kuwa watafikia lengo walilokubaliana kukusanya na hata kuzidi kiwango hicho ambacho kimeainishwa katika bajeti ya Serikali.
WATIA NIA JIMBO LA MALINDI CCM WAJIELEZEA WASFU WAO KWA WANANCHI.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana
wasio na Ajira Tanzania (TUEPO), Ussi Said Suleiman ambae pia ni mtia
nia kugombea Uwakilishi Jimbo la Malindi kwa tiketi ya CCM akinadi sera
zake kwa wananchi wa Tawi la Mkunazini. Zoezi hilo limefanyika Skuli ya
Maandalizi Kidutani Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Daktari Bingwa wa binaam Abdalla
Juma Sadala (Mabodi) ambaye ni mtia nia kugombea Ubunge wa jimbo la
Malindi kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na
wanachama wa chama hicho katika mkutano wa wagombea uliofanyika Skuli ya
Maandalizi Kidutani Mjini Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Malindi
wakiwasikiliza kwa makini wagombea wa nafasi za Uwakilishi, Ubunge na
Udiwani wakijieleza kwao ili wawachague.
Wagombe Uwakilishi, Ubunge na Udiwani Mwenyekiti wa Mkutano huo (hayupo pichani) wakati akitoa maelezo kwao.
ZANZIBAR YAANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELECTRONIKI KUSAMBAZIA DAWA NA KUPATA TARIFA ZA MADAWA VITUONI.
Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib
Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi
wa madawa jinsi unavyofanyakazi zake kwa haraka, katika hafla ya
uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini
Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la John Snow
Incorporated (JSI) nchini, Deo Kimera akitoa nasaha zake kwa Viongozi
na Maafisa wa Afya waliopata elimu juu ya matumizi ya mfumo mpya wa
Ugavi wa madawa wa kielektroniki walioshiriki katika hafla ya uzinduzi
wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mshauri Mwandamizi kutoka Shirika
la Misaada la Marekani USAID Kelly Hamblin akitoa shukran zake kwa
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano yao ya
kufanikisha Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa nchini,
katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel
Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid
Seif Suleiman akitoa shukrani zake kwa Shirika la John Snow Incorporated
(JSI) kutokana na juhudi zao za kuwawezesha maafisa wa Afya wa Zanzibar
kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa kwa njia ya
kielektroniki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park
Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mfamasia kutoka Bohari Kuu
Zanzibar Bi. Khadija Ali Shehe akielezea changamoto walizokumbana nazo
wakati wa kutumuia mfumo wa Karatasi katika Usambazaji wa Madawa
vituoni kabla ya kuzinduliwa Mfumo mpya wa kielectroniki hii leo.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya
Gombani Pemba Abdalla Mbaruk Saleh akitoa ushuhuda wa namna Mfumo mpya
wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa unavyofanya kazi zake kwa haraka na
ufanisi, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt
Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna katikati akizindua Mfumo mpya wa
Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa
Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Kulia kwake ni Msimamizi wa taaluma
kutoka Shirika la John Snow Incorporated (JSI) Anselm Namala ,na
kushoto ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman. Hafla ya uzinduzi wa
mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna kushoto akihutubia mara baada ya
uzinduzi wa Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa
kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Hafla ya
uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini
Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Shirika la Umoja wa Mataifa kukabiliana na biashara, YA matumizi za dawa za kulevya ZANZIBAR
Continue reading →
JESHI LA POLISI LANOLEWA JUU YA HAKI ZA BINADAMU KIPINDI CHA UCHAGUZI
Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Semina ya Siku mbili
kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu nchini ili kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika
kulinda haki za binadamu kipindi cha uchaguzi. Semina hiyo imefanyika
huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.
…………………………………………………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Jeshi la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza.
Kufanya hivyo kutalipelekea Jeshi
hilo kuepuka lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya
Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani.
Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu
Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa
Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki
za Binadamu nchini huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.
Amesema Jeshi hilo linawajibu wa
kuhakikisha Sheria za nchi zinafuatwa lakini jambo la msingi ni
kuzielewa Sheria hizo kabla ya kuzitekeleza.
Jaji Mihayo amesema inashangaza
kuona kuwa Tanzania inaelekea katika kipindi cha uchaguzi Mkuu wakati
Maafisa na Makamanda hawazielewi vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi
unaokuja.
Hivyo amewaomba Maafisa
Wawaelimishe Makamanda wenzao juu ya Sheria na kanuni za uchaguzi ili
wakati utakapofika watende haki na Wajibu wao bila ya upendeleo.
“Polisi kazi yenu nikuhakikisha
Sheria zinafuatwa lakini zitafutwa vipi wakati wenyewe hamzijui..Jambo
la msingu ni kuzisoma na kuzielewa kwanza ndio mufanye juhudi za
kutekelezwa” alisema Mihayo.
Amefahamisha kuwa Jeshi hilo
linapaswa kufuata Sheria za nchi bila kufuata matakwa ya Watawala na
kwamba Watawala hao watabadilika kulingana na uchaguzi lakini Wananchi
wataendelea kuwepo.
“Jeshi la Pilisi linawajibika kwa
Wananchi na si Viongozi wa Serikali hivyo nakuombeni mzijue Sheria na
muwe wakwanza kuzitekeleza” Alishauri Jaji Mihayo.
Kwa upande wake Kamishna wa Jeshi
la Polisi Zanzibar Hamdan Makame ameshukuru Mtandao wa Watetezi wa haki
za Binadamu kwa kuendesha Semina hiyo katika kipindi muafaka cha
harakati za uchaguzi mkuu.
Amesema kila mtu ni mlinzi wa haki
za binadamu katika kila sehemu anayofanyia kazi nakwamba jambo muhimu
ni kuhakikisha Haki zinalindwa hasa ikizingatiwa kuwa suala la haki za
binadamu ni lakimataifa.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Harusi Mpatani
ameliomba Jeshi hilo kuhakikisha linawalinda Wananchi wote ikiwemo
Watetezi wa haki za binadamu.
Semina hiyo ya siku mbili
iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ni
mwendelezo wa kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika kulinda haki za
binadamu ili kuufanya uchaguzi unaokuja uwe huru,haki na Salama.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA ECG NA AL KAN KUTOKA MISRI, IKULU DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Wafanyabiashara wa ECG na Al Kan kutoka nchini Misri, wakati walipofika
Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015 kwa
mazungumzo.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na Wafanyabiashara wa ECG AL Kan kutoka nchini Misri, baada ya
kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA SUMATRA, TRA, TABOA, RC-DSM NA WAZIRI WA FEDHA IKULU KWA MAZUNGUMZO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi
ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA,
SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati
walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi
Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.
“MESI WA SIMBA ATUA COASTAL UNION”
Kulia ni winga mpya wa Coastal
Union Ibrahim Twaha ” Messi” akisaini mkataba wa miaka miwili wa
kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim El Siagi kushoto ni
Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai.
Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahi.
……………………………………
NA MWANDISHI WETU,TANGA
TIMU ya Coastal Union ya Tanga
imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili kujiimarisha vilivyo katika
safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia
timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa
Simba,Ibrahim Twaha “Messi”
Utiliaji saini wa mkataba huo
ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa na kushuhudiwa
na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja wa
timu hiyo,Akida Machai.
Akiuzngumza mara baada ya
kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi
alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa
aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .
Alisema kuwa winga huyo ana vitu
adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa
katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika
msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
“Niseme tu safari hii
tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani
hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El Siagi.
Kwa upande wake,Ibrahim Twaha
“Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa mafanikio timu
hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania
Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Sasa ni kama nimerudi nyumbani
kwa sababu awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja
kubwa kurudi tena Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la
kuipa mafanikio “Alisema Messi.
Awali akizungumza,Meneja wa
Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiri
kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na kurudisha
makali yao ya miaka ya nyuma.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Siku za hivi karibuni kumeibuka
baadhi ya watu ambao wamekuwa kwa makusudi na kwa malengo maalum
wakitunga na kujiandikia taarifa, za uongo, kujenga hofu na au kupotosha
na kisha kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa malengo
mahsusi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.
Watu hao katika nyakati tofauti
wamekuwa wakitengeneza uzushi na uongo huo na kuusambaza kwenye mitandao
pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo lisilo wazi.
Baadhi ya uzushi na uongo
uliotungwa na kusambazwa na watu au kikundi hicho ni pamoja na hii ya
leo inayoeleza mambo mbalimbali juu ya Ndugu Edward Lowasa na ambayo
watunzi wake wameandika kuwa imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.
Ifahamike kuwa uzushi huo na
mwingine uliofanywa na watu au kikundi hicho umekusudia kujenga msukumo
ambao haupo ili kuujengea umma hofu ya huruma dhidi yao ili kusukuma na
kushinikiza agenda zao.
Jambo hilo ni uzushi mtupu kwa
sababu kwanza Ndugu Nape na wajumbe wote wa Sekretarieti hawapo jijini
Dar es Salaam badala yake wapo mikoani kushiriki katika zoezi la kura ya
maoni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea Udiwani na Ubunge zoezi ambalo
litakamilika Agosti Mosi, 2015.
CCM inasisitiza kuwa habari hizo
si za kweli, zimeandikwa na watu kwa malengo binafsi ya kugombanisha,
kujenga chuki na uhasama baina ya Ndugu Nape, Chama, Wajumbe wa
Sekretarieti na wananchi kwa ujumla bila sababu.
Viongozi, wana-CCM na wananchi
kwa ujumla hawana budi kupuuza uzushi wowote ule unaotolewa na
kusambazwa na watu au vikundi vya hovyo vinavyotumiwa na watu kwa
maslahi binafsi, badala yake CCM itakuwa inatoa taarifa sahihi kwa
wakati ili kutoruhusu uwepo au kuibuka kwa ombwe la mawasiliano baina ya
umma na Chama.
Imetolewa na:-
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
Lumumba, Dar es Salaam.
29/07/2015
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na
viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe.
Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa
chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima
ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo
tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za
Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
PICHA NA IKULU
Jaji Mutungi Ajiandikisha Katika Daftari la Kudumu La Wapigakura
Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi
akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha mapema Leo
katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida
Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi fomu ambazo zimebeba taarifa zake
kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge
Jijini Dar es salaam
Alama za vidole zikichukuliwa na
Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha
taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho.
Jaji Mutungi akipiga picha kwa ajili ya kitambulisho
Mhe.Jaji Francis Mutungi akipokea kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw.Ernest Moses Selelya.
………………………………………………………….
Zikiwa zimebakia siku chache tu
kuisha kwa siku zilizotengwa na Serikali kwa wananchi kujiandikisha
katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR katika Jiji la
Dar es salaan,
Picha no 2479. Mhe. Jaji Francis
S.K. Mutungi akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha
mapema Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
Picha no.2464 Mwandikishaji
Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi fomu ambazo
zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha
Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAITAKA TUME KUONGEZA VIFAA ILI KUFANIKISHA ZOEZI
Mwenezi
wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis ‘Gadafi’ akizungumza na
waandishi wa habari kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………..
Chama Cha Mapinduzi
mkoa wa Dar es Salaam kimeitaka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi
waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.
mkoa wa Dar es Salaam kimeitaka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi
waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu
wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi alisema anawashukuru waandishi kwa
ushirikiano waliounesha kwenye mkutano
wa kumtambulisha mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.
wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi alisema anawashukuru waandishi kwa
ushirikiano waliounesha kwenye mkutano
wa kumtambulisha mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.
Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza
kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani
na Ubunge .
kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani
na Ubunge .
Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na
shauku ya kutaka kujua maoni ya CCM juu ya kuondoka kwa Edward Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa
aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi
CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.
shauku ya kutaka kujua maoni ya CCM juu ya kuondoka kwa Edward Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa
aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi
CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.
MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MIRATHI YA MWANDISHI WA HABARI
Mahmoud Ahmad Arusha
Mahakama ya mwanzo ya
Maromboso imetupilia mbali kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na mke wa
aliyekuwa ofisa mwandamizi wa jumuiya ya Afrika Mashariki,Phil Kleruu
aitwaye Hilda Kleruu kwa madai kwamba siyo mwaminifu na hivyo amekosa
sifa ya kuwa msimamizi wa mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini
marehemu ,Betty Luzuka.
Kesi hiyo ya mirathi
iliyovuta hisia za watu mbalimbali jijini Arusha ilifunguliwa katika
mahakama ya mwanzo ya Maromboso yenye nambari 222 ya mwaka 2013
iliitaka mahakama hiyo ipitie hukumu yake iliyotolewa Septemba 27 mwaka
2013 na hakimu Prince Gideon iliyompa ushindi kaka wa
marehemu,Ssarongo Luzuka.
Hilda, alifunguliwa kesi na kaka wa
marehemu, Ssarongo Luzuka akimtuhumu kujimilikisha mali za marehemu bila
kufuata utaratibu wa kifamilia na kimahakama mara baada ya marehemu
kuaga dunia Agosti mwaka 2013 katika hospitali ya Shreee Hindu ya jijini
Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akitoa hukumu ya pingamizi mbele ya
mahakama juzi hakimu aliyekuwa akisiliza pingamizi hiyo,Moka Mashaga
alisema kuwa kitendo cha mdaiwa kuchukua fedha kwenye akiba ya marehemu
kabla na baada ya kifo chake kimethibitisha kwamba hakuwa mwaminifu kuwa
msimamizi wa mirathi.
Katika hukumu ya kesi
hiyo iliyosomwa kwa muda wa saa 1;30 mahakama hapo hakimu huyo alisema
kwamba mpingaji(Hilda) amepoteza sifa ya kuwa msimamizi wa mirathi kwa
kuwa alitaka kuuza mali za marehemu kabla hata shauri lililowasilishwa
mahakamani hapo kusikilizwa.
“Ushahidi wa mdaiwa ni hafifu na
umetupwa ,mahakama inakubaliana na ushahidi wa wadai kwani umeonyesha
walikuwa karibu na marehemu na alipougua waliweza kutuma fedha za
matibabu na hata kumhudumia”alisema Hakimu Moka
Hatahivyo,Hakimu huyo alienda mbali
zaidi na kusema kuwa wosia uliowasilishwa na upande wa mdaiwa una dosari
kwa kuwa haukuwa na mhuri na kuongeza kwamba kitendo cha wakili wa
upande wa mdaiwa,Wilferd Mirambo kutofika mahakamani hapo kuthibitisha
wosia huo kimethibitisha wosia huo una dosari na wakili huyo hakutaka
kujiingiza katika makosa.
“Mahakama inaheshimu wosia lakini
uwe umefuata sheria wakili Mirambo pamoja na kuitwa mahakamani lakini
hakuweza kufika kuthibitisha wosia huo,mahakama inathibitisha kwamba
kitendo cha kutofika mahakamani kinathibitisha kwamba hakutaka
kujiingiza kwenye makosa”alisisitiza Hakimu huyo
Akimalizia kusoma hukumu hiyo hakimu
Moka alisema kwamba kaka wa marehemu Sarongo Luzuka pamoja na dada wa
marehemu Jullie Luzuka wataendelea kuwa wasimamizi wa mirathi ya
marehemu kwa kufuata sheria za mirathi na baada ya siku 30 watapaswa
kuleta orodha ya mali za marehemu mahakamani hapo ili ziweze kugawanywa
kwa mujibu wa sheria.
NGOMA AFRICA BAND WAFUNIKA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TÜBINGEN 2015
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa
band maaruka kama FFU-Ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki Alien’s
inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye makao yake kule
ujuerumani ,juzi iliuhakikishia ulimwengu tena kuwa mziki wao ni moto wa
kuotea mbali! bendi hiyo ilifanikiwa kwa mara nyingine kuyafunika
maonyesho ya kimataifa ya International African Festival-Tübingen
2015,yaliofanyika katika viwanja vya Fest Platz,jijini
Tübingen,Ujerumani.
Bendi hiyo ilipanda jukwaani majira ya saa 4.00 usiku huku
uwanja huo ukiwa umezungukwa na ulinzi mkali ! kamanda Ras Makunja
akikiongoza jukwaani kikosi chake kilichoshamili vijana wa kazi akina
Afande Mo Benda (Soloist) Sajent JoJo Sousa(Drumer) Kopro. Aj Nbongo
(Bass) kijana Liga (Rhthym guitar) madansa Jessica Ouyah na Sarah Fina
kikosi hiko kilifanya show la kukata na shoka.siku ya jumamosi 26 Julai
2015.
wapitie at www.facebook.com/ngomaafricaband wasikilize at www.reverbnation.com/ngomaafricaband
Trilioni nane zatumika kuboresha umeme ndani ya miaka 10
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
…………………………………
Zaidi ya Dola billioni nne za
Kimarekani ikiwa sawa na Trilioni nane kwa shilingi ya Kitanzania
zimewekezwa katika sekta ya umeme kwenye Miradi yote ya uzalishaji,
usambazaji na usafirishaji wa umeme nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la ugavi la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi
Felchesmi Mramba wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika kipindi cha
miaka 10 (2005-2015), Serikali imeongeza uwezo wa mitambo ya kuzalisha
umeme katika Gridi ya Taifa kutoka MW 891 hadi kufika MW 1,501.24 sawa
na ongezeko la asilimia 68.5.
“Baadhi ya miradi iliyokamilika
ni pamojaj na mtambo wa kuzalisha umeme MW 100 uliopo Ubungo, na Ujenzi
wa mtambo wa kufua umeme MW 45 uliopo Tegeta jijini Dar es salaam.
Miradi mingine ni mtambo wa kuanzisha umeme MW 60 Mwanza, na mradi wa
umeme wa Somanga Fungu MW 7.5 Mkoani Lindi” amesema Mkurugenzi huyo.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mramba,
kukamilika kwa Miradi hiyo kumewezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika
nchini na kufanikisha kuondoa mgawo wa umeme hususani kuanzia mwaka 2012
na hivyo kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za
kiuchumi na kijamii.
Mtendaji huyo Mkuu wa TANESCO
ameeleza kuwa kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa
umeme kwenye Gridi ya Taifa na nje ya Gridi ya Taifa ikiwemo utekelezaji
wa Mradi wa Kinyerezi 1 (MW 150) kwa kutumia Gesi asilia, mradi wa
kupeleka umeme katika miji ya Mpanda, Ngara, na Biharamulo.
Aidha Mkurugenzi huyo ametoa ufafanuzi kuhusu kubadilisha mfumo umeme wa LUKU utakaofanyika tarehe 1/8/2015.
“Zoezi la kubadilisha mfumo wa
LUKU litachukua muda wa saa 24 kuanzia usiku wa manane wa Agosti Mosi,
2015 hadi usiku wa manane wa tarehe 2/8/2015 sio siku saba kama
ilivyoenezwa katika mitandao ya kijamii,” amesema.
Lengo la zoezi hili ni kuongeza
kasi na kuwawezesha watu wengi kuunganishwa na mfumo mpya wa LUKU
utakaohudumia idadi kubwa zaidi ya watu tofauti na hali ilivyo sasa.
JUMUIYA YA ULAYA YAKABIDHI MIUNDOMBINU YA USALAMA BARABARANI KWA SHULE ZA MSINGI KASULU NA ILALA
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya
Ulaya EU Bw. Fabrizio Moroni akizungumza wakati kukabidhi miundombinu
ya Usalama Barabarani kwa shule za msingi za Ilala na Kasulu
iliyofadhiliwa na Jumuiya hiyo katika kusaidia masuala ya Usalama
barabarani kwa wanafunzi wa jiji la Dar es salaam katika hafla
iliyofanyika shuleni hapo.
Kamanda Abel Swai kutoka Kikosi
cha Usalama barabarani Makao makuu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha
Elimu ya usalama barabarani akizungumza jambo wakati wa makabidhiano
hayo.
Wanafunzi wakikabidhiwa mabegi katika hafla hiyo.
Bw. Ramadhan Kayupayupa kutoka Amend akiwaongoza wanafunzi kuimba wimbo wa usarama barabarani wakati wa hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Bw. Tom Bishop
kutoka AMEND,Kamanda Abel Swai kutoka Kikosi cha Usalama barabarani
Makao makuu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha Elimu ya usalama
barabarani na Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya EU Bw. Fabrizio Moroni
wakiwa katika hafla hiyo.
Bw. Khamis Mlangala Afisa Elimu ya Watu wazima na Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Ilala akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Viongozi hao kutoka Jumuiya ya Ulaya, Kikosi cha Usalama Barabarani na Manispaa ya Ilala wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo.
Paisha Yazinduliwa rasmi jijini Dar Es Salaam
Mgeni
rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment,
Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform
mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya
serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu
za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu
za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure
kabisa.
Meneja
bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya
kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana
katika hoteli ya serena.
Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi .
No comments :
Post a Comment