Friday, June 5, 2015

NSSF yatoa bilioni 55.6 kwa wajasiriamali 7000


IMGL7668
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano wa tano wa wadau wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii wa  NSSF kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Juni 2, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Tibenda, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ,Dr. Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Abubakari Rajab. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu).

Na Queen Lema na Christian Gaya ARUSHA

MFUKO wa hifadhi ya taifa ya jamii(NSSF)umefanikiwa kutoa kiasi cha Bilioni 55.6 kwa wajasiriamali mbalimbali ambapo pia fedha hizo  zimeweza kuwanufaisha wajasiriamali 7000 kutoka sehemu mbalimbali nchini.


hata hivyo riba hiyo ilikuwa kati ya asilimia 9.3 hadi kufikia 10.7 ambapo kwa taasisi nyingine za kifedha hufikia riba ya asilimia 15 mpaka 30 hali ambayo nayo inachangia sana kuwadidimiza wajasiriamiali ambao wanategemea mikopo.

Akiongea katika mkutano mkuu wa tano wa mwaka ambao uliwajumuisha wadau na wanachama wa NSSF mkurugenzi mtendaji Dakt Ramadhani Dau alisema kuwa mikopo hiyo kwa wajasiriamali ilitolewa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita na mpaka sasa wameshaweza kuwanufaisha wajasirimali wengi hapa nchini.

Dkt Dau alifafanua kuwa kilichofanya mfuko huo kuweza kutoa mikopo kwa wajasiriamali ni baada ya kuona kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wajasimali na kutokana na changamoto hizo zimesababisha washindwe kufikia malengo yao mbalimbali.

Alidai kuwa kwa sasa changamoto mojawapo ambayo inawakabili wajasiriamali hao ni pamoja na ukosefu na upatikaji wa mitaji, kutokuwa na dhamana, kutozwa riba kubwa,  ukosefu wa elimu za biashara pamoja na nidhamu na kudhubuti kuanza kufanya biashara hali ambayo kama wajasiriamali wa sasa wataweza kutatuliwa hayo basi wataweza kufikia malengo makubwa

Awali akiongea kwa niaba ya serikali Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa mfuko huo wa NSSF umeweza kuwabeba wajasiriamali sana ingawaje pia mifuko ya hifadhi ya jamii inahusika sana kuweza kulibeba taifa la Tanzania hasa kwenye sekta muhimu hususani sekta ya ujasiriamali

“Kazi iliyofanywa na NSSF tangia mwaka 1997 mpaka 2012  mpaka sasa ni kubwa sana na ya tija ambapo imekuwa ni mchango mkubwa sana kwa uchumi wa taifa letu. nampokengeza sana Dakt Ramadhani Dau kwani kwa kipindi chake NSSF imepata maendeleo makubwa sana na mpaka sasa NSSF wamepata tuzo ya kimataifa ISO kwa kutoa huduma bora kwa wanachama wake”.alisema Pinda

Pinda alifafanua kuwa kwa pamoja na kuwa NSSF imeweza kuwasaidia wajasiriamali kwa kiwango cha juu lakini bado kuna changamoto kuwa sekta ya ujasiriamali ni sekta ya watu ambao wapo ovyo sana jambo ambalo halina ukweli kabisa.

“napenda kuwasihi hata watumishi wa umma kuwa wasiridhike na kisha kuona ujasirimali ni watu wa chini jiwekezeni hata huku acheni kunata na kama watu wote tutakuwa wajasiriamali ni wazi kuwa wakati tutakapostaafu hatutaweza kupata shida”aliongeza

No comments :

Post a Comment