Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.
Ofisa
wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi
msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera
kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa yamvua na kuharibikiwa na mali
zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.
OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya
Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za
masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi
Zanzibar.
Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za
masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa
uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa
makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe
chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake
kwa kusaidia Jamii.
uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa
makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe
chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake
kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali
wananchi wakati wa maafa na kutowa
shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika
katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali
wananchi wakati wa maafa na kutowa
shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika
katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
SHUGHULI MBALIMBALI ZA WAZIRI MKUU ARUSHA NA DODOMA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid
baada ya kuhudhuria sala na heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa
Ukonga, Egin Mwaiposa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3,
2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na Wakufunzi na watalaam wa mashine za kuandikisha wapiga
kura za BVR wakati alipotembelea Kituo cha mafunzo ya BVR kwenye Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Juni 2, 2015.
Taswa FC kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Baobab ya Bagamoyo.
Mchezaji wa timu ya soka wa
waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa fc), Martin Peter (jezi ya
kijani kulia) akipambana na mmoja wa wachezaji wa timu ya makipa, Ivo
Mapunda.
kikosi cha baobab
……………………………………………………
Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa
habari za michezo nchini (Taswa FC) Ijumaa hii itacheza mchezo maalum wa
kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Baobab
ya Bagamoyo.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa
10.00 jioni kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Baobab na tmgeni
rasmi atakuwa mkurgugenzi wa shule hiyo, Hlafan Swai.
Mbali ya Swai, viongozi wengine wa shule hiyo watahudhuria mechi hiyo maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto
Omary amesema kuwa awali walipanga kucheza mechi mbili, ya wanaume
(mpira wa miguu) na wanawake (netiboli), hata hivyo wachezaji wa Taswa
Queens hawakuweza kuanza mazoezi na hivyo kulazimika kufuta mechi hiyo.
Majuto alisema kuwa wamepokea
maombi kutoka uongozi wa shule hiyo na hasa baada ya kutoa mwanafunzi
bora kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne, Nyakaho Marungu. Alisema
kuwa wamehamasika kupata mwaliko huo ambapo mechi hiyo itakuwa kama
sehemu ya sherehe ya kufunga shule.
Baadhi ya wachezaji wa Taswa FC
wakataokuwepo katika mechi hiyo ni Ali Mkogwe, Wilbert Molandi, Salum
Jaba, Deogratius “Super Deo” Maganga, Julius Kihampa, Sweetbert
Lukonge, Elius Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi
Seif, Jose, Martin Peter, Athuman Jabir, Muhidi Sufiani na Jabir
Johnson.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya
wafanyakazi wa shule hiyo ni John Kanakamfumu, Herry Morris (kocha wa
timu ya wanafunzi), Renatus Kavishe, David Ntungi, Hadji Juma, Madata
Lubigisa, Athuman Tippo na wengineo.
“Huu ni mchezo wa kudumisha
ushirikiano wetu kwani sisi ni waandishi wa habari za michezo na pia ni
wazazi, hivyo tunaweza kuwapeleka watoto wetu kusoma kaika shule hiyo
bora, hivyo nawaomba wachezaji wote wafike kwa wingi ili kuona mechi
hiyo ya aina yake,” alisema Majuto.
KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika Equality for Growth (EfG), JaneMagigita
akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi
wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa
Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la
siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar
es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa
tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth
(EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.
……………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe
amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani
wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.
Akizunguza
Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake
wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha
wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na
uendeshaji wa biashara zao.
Alisema
kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi
duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo
kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya
kisera.
“Wafanyabishara
wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa
kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania,”
alisema Wangwe.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth
(EfG), Jane Magigita, alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha
wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala
muhimu yanayowahusu katika biashara zao.
Alisema
kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani
Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo
‘Sauti ya Mwanamke Sokoni’.
Alisema
kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea
uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha
shughuli biashara za shughuli za soko.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com simu namba 0712-727062)
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF lazindua jezi mpya za timu za Taifa pamoja na tovuti mpya
Jamal Malinzi, akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo.
Muonekano wa jezi mpya ya nyumbani.
Muonekano wa jezi mpya ya ugenini.
……………………………………………………
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa
zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua
inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya
uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee
uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni
rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa
jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi
zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF ,
Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za
Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi
mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali
mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi
kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli
hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba
1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu
duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite
hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya
kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum
kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao
uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
Leo hii ndugu mgeni rasmi
tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa
niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa
wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya
michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa
iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa
timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti
194.
Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana
ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa
mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania wenzetu
watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni
wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi
tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika
orodha hii na wametangulia mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi
miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa
fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na makusanyo
mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila
mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi
na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya juhudi za
TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa
shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali
ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz).
Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na
FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza
mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.
Kupitia tovuti hii wadau wa mpira
watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala mbali mbali
yahusuyo mpira wa miguu.
Tovuti hii itakuwa pia na sehemu
ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu na matukio
mbali mbali katika historia ya mpira wetu.
Tunaomba wadau wenye kumbu kumbu
mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya zamani na
kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.
Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi shughuli ya leo
tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa. Jezi hizi
zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine ya nyumbani.Tunawapongeza
watanzania wote walioshiriki katika kubuni jezi na mwisho tuliunganisha
ubunifu tofauti na kupata jezi itakayozinduliwa leo.
Ubunifu huu tayari umetafutiwa
hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii kwa kuwakamata na
kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote watakaodiriki
kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu unafanyika kumpata
msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini kwa ajili ya
wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa umechangia maendeleo
ya mpira wa miguu.
TFF inawashukuru na kuwapongeza
sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro
Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu ya Taifa na kutuwezesha kubuni na
kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru sana.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba
nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu ya mpira wa vijana.kwa
kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF tumejipanga vilivyo
kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali za vijana za Afrika
umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
Mechi za ufaulu zitafanyika kati
kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda kikosi cha awali cha vijana chini
ya umri wa miaka 15 kujiandaa na michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na
michuano ya copa coca cola ya mwaka jana.
Tunapenda tuchukue fursa hii
kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu ya
Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,kupata uenyeji
wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF limeipatia
Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17
mwaka 2019.
Tunaomba Serikali itushike mkono
katika hili ili tuweze kuandaa mashindano mazuri.Lakini haitakuwa vyema
Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini tukatolewa hatua ya
makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF tutazindua mashindano ya
taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.
Wachezaji bora wa mashindano haya
ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya kushiriki fainali
za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka 2109.
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru Mh Dr Fennela
Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na michezo kwa
ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika shughuli nyingine
za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
Jamal Malinzi
Dar es salaam
03/juni/2015
WASIFU WA KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA, MAREHEMU ONEL ELIAS MALISA
Marehemu
alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi, Mkoa wa
Kilimanjaro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kidia mwaka
1951 – 1954 na baadae Shule ya Msingi Kidia Juu (Kidia Upper Primary
School) mwaka1955 – 1958. Alihitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne
mwaka 1974 katika Shule ya Sekondari Mawenzi akiwa mtahiniwa wa
kujitegemea (Private Candate). Aidha, alisoma Cheti cha Sheria Chuo
Kikuu cha D’Salaam mwaka 1975 – 1976 na baadaye Shahada ya Kwanza ya
Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1977 – 1980.
Marehemu ajiunga na Jeshi la
Magereza mwaka 1964 baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari
Magereza Chuo Ukonga, D’Salaam yaliyofanyika kuanzia Januari – Julai,
1964. Ndani ya utumishi, alipata fursa ya kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi
Daraja la Pili (Advance Course) Chuo Ukonga, D’Salaam kuanzia Aprili –
Julai, 1967 na Mafunzo ya Uongozi wa Juu (Gazetted Course) kuanzia
Februari – Mei, 1974.
Kutokana na utendaji wake wa kazi, marehemu aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
• Afisa Magereza Daraja la Tatu mwaka 1964
• Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka 1967
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu mwaka 1971
• Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka 1975
• Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
• Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka 1978
• Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka 1982
• Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza mwaka 1984
• Kamishna wa Magereza mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 – 2002
• Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka 1967
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu mwaka 1971
• Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka 1975
• Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
• Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka 1978
• Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka 1982
• Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza mwaka 1984
• Kamishna wa Magereza mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 – 2002
Aliwahi kufanya kazi katika vituo
mbalimbali vikiwemo Gereza Butimba – Mwanza, Isanga – Dodoma, Wami
Vijana – Morogoro, Chuo cha Usalama Moshi, Gereza Songwe – Mbeya, Chuo
Ukonga – D’Salaam na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, D’Salaam.
Aidha, marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Magereza kama ifuatavyo:-
• Mkufunzi Mkuu Chuo Ukonga mwaka 1975
• Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga mwaka 1981
• Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
• Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1984
• Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.
• Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga mwaka 1981
• Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
• Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1984
• Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.
Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake. Baadhi ya mambo aliyoyafanya ni kama ifuatavyo:-
• Alianzisha na kuimarisha mahusiano baina ya Jeshi la Magereza na Magereza ya nchi nyingine Afrika na duniani.
• Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
• Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
• Kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani aliweza kushauri na kusimamia kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-
• Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
• Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
• Kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani aliweza kushauri na kusimamia kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-
– Sheria ya Bodi ya Parole
– Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community Service)
– Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community Service)
Nishani alizotunukiwa akiwa kazini ni:-
• Nishani ya mstari wa nyuma
• Nishani ya Utumishi mrefu
• Nishani ya Utumishi uliotukuka
• Nishani ya Utumishi mrefu
• Nishani ya Utumishi uliotukuka
Hata baada ya kustaafu kazi,
marehemu aliendelea kutoa mchango wake kwa kushauri mambo kadhaa pamoja
na kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya Jeshi na Taifa. Kutokana na
mchango wake huo alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya
Muungano Daraja la Nne na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 26 Aprili, 2015.
Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa uliotufika.
Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa uliotufika.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA
Programu ya kukuza ajira zenye staha kwa vijana kuzinduliwa juni 5, 2015
Mratibu wa Programu ya kukuza
Ajira zenye Staha Dar es Salaam, kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo
ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha mada kuhusu
utekelezaji wa program hiyo jana jijini Dar es Salaam. Programu hii
inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission
Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
Mshauri wa maswala ya Sera na
Miradi ya Maendeleo wa Tanzania Youth Vision Association Bw. Elly
Ahimidiwe Imbyandumi akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa
kutathmini utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha katika
jiji la Dar es Salaam (YEID jana katika ukumbi wa Kituo cha Vijana cha
Don Bosco cha jijini Dar es Salaam.Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa
asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind
Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
Afisa Vijana kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akielezea jambo
wakati wa mkutano wa asasi za Vijana kujadili utekelezaji wa Programu ya
Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga
kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii
inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission
Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
asasi za vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa
mkutano wa asasi za Vijana uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ili
kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar
es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo vijana ili waweze
kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za
kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania
(OMT) na Youth For Africa (YOA).
Washiriki wa mkutano wa asasi za
Vijana ILI kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha
jijini Dar es Salaam (YEID) wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Frank Shija, WHVUM
KINANA KUANZA ZIARA KESHO KUELEKEA KAGERA, GEITA ,MWANZA
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape Nnuye akizungumza na
waandishi wa habari ambapo alizungumzia ratiba ya ziara ya Katibu Mkuu
wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana katika mikoa mitatu ,Kagera,Geita
na Mwanza itakayoanza tarehe 4 June.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha picha ya muonekano wa basi
maalum litakalotumika kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa kuelekea
mkoani Kagera.
………………………………………………………………………………..
NA HAFIDH KIDO, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana anaanza ziara ya siku 28 leo katika mikoa mitatu ya Kagera, Geita
na Mwanza kukamilisha mikoa yote 30 nchi nzima.
Ziara hizo zenye malengo ya kukagua utekelezwaji wa ilani
ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama zimekuwa na mafanikio
kwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi hasa wa mikoani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema
wataondoka jijini leo kwa basi maalumu ambapo watasimama njiani katika
mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia
wananchi.
“Ziara rasmi itaanza June 4 katika Wilaya ya Nyakanazi
mkoani Kagera, lakini kesho (leo) tutakunywa chai Morogoro chakula cha
mchana tutakula Dodoma halafu tutasalimia wananchi katika Mikoa ya
njiani kama Singida, Nzega na tumepanga kulala Kahama mkoani Shinyanga,
tukiamka ziara ndio itaanza rasmi,” alisema Nape.
Aliongeza kuwa katika ziara hiyo watatembelea majimbo yote
ya uchaguzi hivyo amewataka wana-CCM na wananchi wengine kujitokeza kwa
wingi kumsikiliza Katibu Mkuu katika ziara hiyo ya kihistoria.
“Hii ni ziara ya kihistoria kwa sababu ya mambo matatu,
kwanza tutatembelea visiwa vyote vya Ukerewe mabavyo ni nadra
kutembelewa na viongozi, pili huu ni mwaka wa uchaguzi kuna masuala
mengi yanahitaji ufafanuzi,” alisema.
Akitaaja ratiba ya ziara hiyo Nape alifafanua kuwa,
“Kuanzia Juni 5 mpaka Juni 15 tutakuwa Mkoa wa Kagera, Juni 16 mpaka 21
tutakuwa Mkoa wa Geita na Juni 22 mapaka Julai 2 tutakuwa Mwanza
kuhitimisha ziara ya nchi nzima kwa mkutano mkubwa wa kihistoria.”
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu faida za
ziara hizi Nape alisema kuna masuala mengi ya kimaendeleo yalisimama
lakini alipopita Katibu Mkuu Kinana ufumbuzi umepaikana, akitolea mfano
mashamba yaliyobinafsishwa bila kufuata utaratibu alisema Rais Jakaya
Kikwete, amefuta hati nyingi za mashamba ya wawekezaji na kurudishwa kwa
wananchi.
“Kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na zahanati zimeshajengwa
lakini hakuna vibali, nimepata taarifa kuwa vibali vimeshapatikana na
huduma zinaendelea, kulikuwa na matatizo ya ardhi za wananchi
kuchukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Tanga, Arusha, Babati na
maeneo mengine lakini kila kitu kipo sawa sasa na wananchi wanamshukuru
Kinana,” alisema.
Aliongeza kuwa, “Nisisitize kuwa tumesema tutaondoka na
basi maalumu kwa sababu kama kuna mwingine atafanya hivyo atakuwa
ametuiga, mkumbuke hili wazo la kuondoka na basi ni la Katibu Mkuu.”
Ikiwa ziara hizi zitamalizika salama Julai 2 mwaka huu,
Kinana atakuwa Katibu Mkuu pekee wa CCM tangu kuanzishwa kwake Februari
5, 1977 kuzunguka nchi nzima kuangalia uhai wa chama na kusikiliza na
kutatua kero za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.
Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!
Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira |
Wayege wakicheza ngoma |
Habari na picha kwa hisani ya
Mkala Fundikira wa TBN central zone
Filamu ya MPANGO MBAYA kuzinduliwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
MPANGO MBAYA
ni filamu iliyochezwa na washiriki 10 waliofanikiwa kuingia katika
Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) msimu wa kwanza 2014
na kushirikisha baadhi ya waigizaji mahiri kutoka katika kiwanda cha
Filamu Tanzania.
Filamu ya Mpango Mbaya
ni filamu ambayo imetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu huku
ikikidhi viwango vya kimataifa na ni filamu ambayo ina ubora wa hali ya
juu kuanzia ubora wa picha, Sauti, rangi mpangilio wa matukio na
upigwaji picha wake na ubora wa washiriki wa filamu hiyo
Filamu
hii itazinduliwa mnamo tarehe 12 Juni 2015 Katika Ukumbi wa Mlimani
City na pia Filamu hii itaendelea kuonyeshwa kwa siku mbili mfululizo
katika ukumbi huohuo.
Picha chini ni baadhi ya taswira za washiriki wa filamu hiyo
TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA
Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama
ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda,
Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina
na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili
kulia).
Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na
Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi
baada kukabidhi mradi wa kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha
Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa
msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo
Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha
Magoza, Kata ya Kiparang’anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla
ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji
kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano
hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya
kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka sehemu
na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho
Akina
mama wakazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda,Mkuranga,
wakiwa wamebeba ndoo za maji waliyoteka katika Kisima cha maji
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji
hicho kwa gharama ya sh. mil. 56. Hafla ya TBL kukabidhi kisima hicho
cha maji ilifanyika mwishoni mwa wiki.
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA(TANAPA) KUPITIA UJIRANI MWEMA WAKABIDHI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA ASHIRA WILAYA YA MOSHI
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi huo. |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo. |
RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini. |
Tanki la Maji la mradi wa ujirani mwema uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA). |
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini. |
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ashira katika wilaya ya Moshi . |
Kaimu Mkurugenzi mkuu TANAPA,Ibrahim Musa akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi , |
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji uliofadhiliwa na TANAPA kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi. |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini, |
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AZINDUA DUKA JIPYA LA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO.
Duka jipya la kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi,Tigo lafunguliwa mjini Moshi. |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya simu za mkononi ya Tigo lililozinduliwa mjini Moshi. |
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akifuatilia kwa makini shughuli za uzinduzi wa duka la Tigo katika mji wa Moshi. |
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo,wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo mjini Moshi. |
Meneja huduma kwa wateja kanda ya Kaskazini,Gwamaka Mwakilembe akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea vitengo mbalimbali ndani ya duka hilo. |
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa kazini. |
Uuzaji wa simu za aina mbalimbali pia ulikuwa ukifanyika katika duka hilo. |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama ,akifurahia jambo mara baada ya kutembelea ndani ya duka hilo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tigo. |
UTAFITI WA KISIASA ULIOFANYWA NDANI YA MANISPAA YA IRINGA WAMBEBA FRANK KIBIKI
frank kibiki akiongea na wananchi stand kuu ya mabas iringa.
wananchi wakimsikiza frank kibiki alipokuwa maeneo ya stand kuu
…………………………………….
na fredy mgunda,iringa
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Highland Zone
Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya
Mwanahabari , Frank Kibiki aliyetangaza
nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza
huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya
Mwanahabari , Frank Kibiki aliyetangaza
nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza
huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa
wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa
mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki
inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa
vijana, wanawake, walemavu na wazee.
wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa
mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki
inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa
vijana, wanawake, walemavu na wazee.
Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SHZER, Patson William alisema utafiti huo umefanywa
katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza
kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza
kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9,
Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve
2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve
2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea
kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa
kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji
wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya
kazi.
kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa
kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji
wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya
kazi.
Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo
watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni,
Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga,
Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga,
Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta
majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge
anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia
vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge
anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia
vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana
kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka
2010.
kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka
2010.
Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na
wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo,
litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo,
litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya
kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema
vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema
kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema
vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema
Profesa Sospeter Muhongo atangaza nia rasmi , MJINI Musoma
……………………………………………
WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.
Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa
takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila
kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita
kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni
Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.
“Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.
“Ukiacha takwimu ambayo kwa Dunia ya sasa ni lazima, nchi yetu lazima ijiamini, kuongeza ushindani, kuongeza upendo, bila kusahau rushwa ambayo kwa uhakika inapaswa kupigwa vita kwa vitendo ili nchi yetu isonge mbele,” alisema Muhongo.
Kuhusu uchumi, Profesa Muhongo alisema kwamba ni aibu Tanzania kupitwa kiuchumi na Mataifa waliyokuwa nayo sawa, akitolea mfano wan chi za Brazil, China, India na Kenya ambao wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye elimu na utafiti.
Alisema nchi ikiwa na watafiti, wananchi wao hawataishi kwa mashaka, huku akisema endapo atapitishwa kuwania nafasi hiyo na kuwa rais wa Tanzania, atahakikisha kwamba anakuza uchumi wan chi kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 10 na 15 kwa kipindi cha miaka mitano hadi 10 ya urais wake.
“Nimeweza kufanya kazi ya gesi na mafuta kwa miaka kadhaa kwenye nchi mbalimbali, hivyo hakika kama chaguo ni wataalamu, basi mimi nastahili kwa sababu sioni mwingine mwenye uwezo wa kutangaza kuondoa kero za Watanzania na jinsi atakavyoziondoa.
“Ndio unaweza kusema utaondoa umasikini kwa wananchi au kuongeza mishahara, lakini ili hilo liweze kufanikiwa kwa vitendo, ni lazima pia katika kipindi cha uongozi wako uweze kukuza uchumi wako kwa kiasi kikubwa, bila hivyo hakuna kitu,” alisema Muhongo.
Aidha Profesa Muhongo alisema kwamba Duniani kote nchi zimepiga hatua kwa kuwekeza kwenye wataalamu na viwanda, hivyo Tanzania inapaswa kuangalia namna ya kuwekeza kwenye sekta hizo, bila kusahau sekta ya elimu yenye umuhimu mkubwa.
Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alisema kwamba akiwa Waziri wa Nishati na Madini, ndio mtu ambaye alifanikiwa kwa vitendo kutekeleza ilani ya CCM kwa kuhakikisha kwamba vijiji vingi vinapata umeme kwa kuongeza bajeti na kusimamia kwa vitendo wakala wa umeme vijijini (REA).
Alisema kusudio la kuhakikisha kwamba wananchi wake wanaendelea kupata umeme kwa bei nafuu ni kati ya mambo anayoona yanafaa kuongezewa chapuo na usimamizi wa aina yake, hivyo mwenye uwezo wa kulitatua hilo ni yeye.
SERIKALI YAMALIZA MGOGORO NA WAFANYABIASHARA.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya
Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea kutoa ushirikiano,
utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali kwa maslahi na
maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya
wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki
(EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru Waziri wa Fedha kwa
ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka hiyo hasa katika
kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la ukusanyaji Kodi
nchini.
3- Mwenyekiti wa Jumuiya ya
wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza Waziri wa Fedha Mh. Saada
Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa serikali katika utatuzi wa
changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili
kwa pamoja waweze kufikia malengo ya taifa ya kuwa na uchumi imara
kupitia ukusanyaji wa Kodi.
4- Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu akipongeza kazi iliyofanywa
Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFDs) na
kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya
Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya
muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi
ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto
kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na
Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Mzee Benard Mchovu.
…………………………………………………………..
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi ,kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za ulipaji kodi.
Hayo ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi ,kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za ulipaji kodi.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda AISIFU mifuko ya hifadhi za jamii
NA Mahmoud Ahmad,ARUSHA.
………………………………………………
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda
amesifu juhudi za mifuko ya hifadhi ya jamii nchini inayomilikiwa na
serikali kwa kazi nzuri iliyofanya ikiwemo ujenzi wa vyuo vikuu
mbalimbali kikiwemo cha Dodoma,Nelson Mandela pamoja na jengo la Bunge
la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu Pinda alitoa pongezi
hizo alipokua akifungua mkutano wa tano wa wanachama wa mfuko wa jamii
wa NSSF unaoendelea mkoani Arusha na kushirikisha viongozi wa mifuko
mingine ya ndani ya nchi na ile ya nje ya nchi.
Alisema pasipo kuwepo kwa mifuko
hiyo mambo mbalimbali ya maendeleo yakiwemo ya ujenzi huo kamwe
yasingefanyika kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali jambo ambalo
lilisababisha serikali kuitumia mifuko hiyo kwa makubaliano ya kulipa
deni litakalotokana na shughuli hizo za maendeleo.
Alisema mbali na mchango huo wa
ujenzi wa miundo mbinu pia mifuko hiyo imeweza kuchangia pato la taifa
kwa kiasi cha asilimia 11 tofauti na sekta zingine ambazo bado zina
michango midogo katika pato la taifa mbali na ile ya utalii na madini.
Pia alisema hadi hivi sasa
mifuko hiyo ina mtaji wa kiasi cha shilingi trilioni tano na milioni
miambili na arobaini na mbili mtaji ambao unampa uhakika wa kuendelea
kuwepo kwa mifuko hiyo na kamwe haiwezi kutetereka kwa namna yoyote hata
kutokana na misukosuko mbalimbali inayoonekana.
Aliahidi serikali kurejesha
madeni yote yanayodaiwa na mifuko hiyo kutokana na kazi mbalimbali za
maendeleo zilizofanywa nayo ili kuwezesha mifuko hiyo kuendelea kukua na
kutoa michango yake katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.
Naye mkurugenzi mkuu wa NSSF
Ramadhan Dau alisema mwaka huu shirika lake limekaa na kutathimini
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania na kuja na kauli
mbiu ya Hifadhi ya jamii na ujasiriamali yenye mikakati mbalimbali ya
kuiondoa jamii dhidi ya changamoto hizo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa
ni ukosefu wa mikopo toka taasisi mbalimbali za kifedha kutokana na na
kukosekana kwa mali za kuweka kama dhamana ambapo tayari shirika lake
limeanza kutoa mikop yenye masharti na riba naafuu ya kiasi cha shilingi
bilioni 55.6 ambapo watu 7000 mpaka sasa wameshanufaika.
Alitaja changamoto nyingine kuwa
ni ukosefu wa ujuzi na nidhamu ya biashara kwa wajasiriamali kutokana
na ukosefu wa elimu ambapo shirika lake tayari limeanza mazungumzo na
taasisi za serikali ikiwemo Veta,Sido na nyinginezo ili kuweza kutoa
mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao.
Pia alitaja changamoto nyingine
kuwa ni ukosefu wa uthubutu na woga kwa wajasiriamali katika kuanzisha
biashara na kujiajiri ambapo katika mkutano huo wamewaalika watu
mbalimbali ambao watatoa ushuhuda wao wa maisha yao ya kujiajiri kama
chachu ya wajasiriamali kujiamini na kutuhubutu kufanya biashara.
Aliwataja watu waliowaalika kuwa
ni pamoja na mfanyabiashara Patrick Mfugale anayemiliki kampuni za
Pickkork,mfanyabiashara Salim Salum Bakhresa na mfanyabiashara maarufu
afrika raia wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote.
Pia alitaja mafanikio mbalimbali
yaliyofikiwa na shirika lake hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya
wanachama,ujenzi wa majengo mbalimbali ya kitega uchumi ambapo pia
aliweza kutaja matarajio yao mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali ya
Apollo katika mji ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Pia alitaja mradi mwingine
wanaotaraji kuufanya ni ule wa ujenzi wa kituo cha michezo,ujenzi wa
mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 1000 utakaochangia katika gridi ya
taifa utakaofanyika katika mji wa Kibaha mkoani Pwani pamoja na ujenzi
wa viwanda vya bidhaa zitakazotumia rasilimali mbalimbali zitokanazo na
wanyama na mimea.
BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA UKONGA EUGEN MWAIPOSA
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo
nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati
bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea
bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na
matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu)
akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge
kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen
Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary
Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi
wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati
baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi.
Eugen Mwaiposa.
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye
hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga
Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake
mjini Dodoma.
Kubomoka kwa tuta la Kijiji cha Jombwe Mkoa wa Kusini Pemba kunatokana na mabadiliko ya tabia nchi
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
imesema sababu ya kubomoka kwa tuta Kijiji cha Jombwe Mkoa wa Kusini
Pemba ni kupanda kwa kina cha maji kinachotokana na athari za mabadiliko
ya tabia ya Nchi na baadhi ya Wananachi walivunja mawe yaliyokuweko
kwenye tuta hilo.
Hayo yameelezwa huko Baraza la
Wawakilishi Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabibu Fereji wakati
alipokuwa akijibu suala la Mh. Saleh Nasouro Juma (Jimbo la Wawi).
Alisema kuwa tuta hilo lipo Mkoa
wa Kusini Pemba Kijiji cha Jombwe na Sipwese Wananchi waliweza
kulitumia tuta hilo ni kama njia ya kwenda Muambe pia wanafunzi
walilitumia kwa ajili ya kwendea Skuli hiyo mnamo mwaka 2010 tuta hilo
lilianza kubomoka na kurahisisha njia ya maji ya chumvi kupita na
kuelekea Kijiji cha Sipwese hadi Chuo cha Mafunzo Kengeja.
Alifahamisha kuwa tuta hilo zaidi
ya urefu wa mita 100 mbali ya kuwani kizuizi cha maji ya chumvi
yanayoingia katika maeneo hayo kwani tuta hilo limetumika zaidi kama
kivuko katika maeneo hayo.
Aidha alisema uingiaji wa maji
ulianza mwaka 2002 wakati tuta hilo lilijengwa mwaka 2004 kutokana na
kutumiwa vibaya halikuweza kuchukuwa muda mrecu likabomoka.
Hata hivyo Serikali kwa sasa
haijasaidia kujenga tuta hilo bali Mpango huo ndio utakao toa dira ya
kushughulikia maeneo yalioingia maji ya chumvi ambayo yapo (145) Uguja
na Pemba.
Sambamba na hayo Waziri huyo
amesema juhudi za kupunguza maji ya chumvi kuelekea maeneo hayo Serikali
ikishirikiana na wananchi kupitia Ushirika wa (Green Peace and
Enveronmetal Conservation- GPEC) imeweza kupanda miti ikiwemo
Mikoko,Mikandaa yenye urefu wa heka tatu za miti hiyo zimepandwa eneo
hilo na imeweza kuendelea kustawi vizuuri kuhifadhi mazingira .
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI LEO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
wajumbe wa Kamati ya uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania, wakati
walipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Juni 02,2015.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi Maalum
Asema :Jitahidini kuepusha migogoro-Dkt. Bilal awaasa wafugaji .
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewataka
wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya
kuchukua sheria mkononi ili kuhakikisha usalama wao na watu wanaopakana
nao unakuwepo wakati wote. Mheshimiwa Makamu wa Rais amezungumza hayo
leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka Chama cha
Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwernyekiti wao Ally Hamis Lumiye.
Makamu wa Rais
alisema, si busara kwa wafugaji kujichukulia sheria mkononi na kwamba
matatizo yanayowakabili wafugaji ni muhimu yakatatuliwa kwa kufuata
sheria za nchi. “Jitahidini kuepusha migogoro hasa ile inayosababisha
watu kupoteza maisha. Tusichukue sheria mkononi, sote lazima tuwe watii
wa sheria,” Makamu wa Rais alisema.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama cha Wafugaji Tanzania,
Mwenyekiti wa Chama hicho Ally Hamis Lumiye alisema, chama cha wafugaji
kwa sasa kinakabiliwa na changamopto kubwa hasa baada ya kuwepo
mgawanyiko unaolenga kukimomonyoa chama hicho hasa kufuatia kujitokeza
baadhi ya wafugaji kuamua kupora madaraka ya chama hicho na hivyo
akaitaka serikali kuungana nao katika kuzima nguvu za waporaji hao.
“Mheshimiwa
Makamu wa Rais leo hii tumekuja kwako kwa jambo moja nyeti. Wapo baadhi
yetu wasiotaka kuona wafugaji tunajikomboa kwa kuwa na umoja kama huu.
Wamefikia hatua ya kupora chama hiki na jitihada zetu za kutaka
kuwadhibiti zinaonekana kuwa ngumu kufuatia baadhi ya viongozi wa
serikali kuwatambua waporaji hao,” alisema mwenyekiti huyo.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa jambo la uporaji wa chama kamwe haliwezi
kuachwa kimya kwa kuwa wafugaji na chama chao kimesajiliwa hivyo
wafuate sheria hizo hizo ili kupata haki yao kama inaonekana kutokuwepo.
Pili alisisitiza kuwa atalifanyia kazi suala hilo kupitia nafasi
ziliozpo chini yake na kulipatia ufuimbuzi wa haraka.
“Mimi nami ni
mfugaji, chama hiki ni muhimu kwa maslahi ya wafugaji. Kwa kuwa tuna
katiba inayokiongoza na kwamba tunazo sheria ambazo zilifuatwa hadi
kukipatia chama hiki usajili, basi hakuna haja ya kusikitika sana.
Tutumie taratibu hizi hizi ili kuondokana na hao wanaotaka kupora
mamlaka ya chama hiki,” alisema na kuongeza:
“Ni muhimu
kiwepo chama imara kwa maslahi ya wafugaji wote. Chama hiki kinaweza
kuwasaidia sana katika kukabiliana na changamoto mlizonazo maana kwa
kuwa wamoja ni nguvu.”
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC,
Clement Kiondo, wakati alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu wa
Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015 kwa mazungumzo. Picha
na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji
la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani kutoka Kituo
cha kuelelea watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo
Kigamboni, kinachosimamiwa na TBC. Mshana alifika na ujumbe wake Ofisini
kwa Makamu Ikulu jijini Dar esSalaam, leo kwa ajili ya mazungumzo na
kumkabidhi zawadi hizo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Saa ya ukutani kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani
baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Khanga zenye Nembo ya TBC na zinazotangaza Utalii wa
ndani kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC,
Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao
yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni
2, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Tisheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani
baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement
Mshana, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbi na baadhi ya
wafanyakazi wa Kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu,
kilichopo Kigamboni baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
BIlal, akiagana na wajumbe walioongozana na Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, Omar Rajab (kushoto) na Maico
Rugendo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es
Salaam, leo. Picha na OMR
Rais Dk.Shein aondoka Nchini leo
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa
Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo
wakati wakiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani.[Picha na
Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiagana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati
akiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani pamoja na Ujumbe wa
Viongozi mbali mbali.[Picha na Ikulu.]
No comments :
Post a Comment