Na Julius Mtatiro
Kwa ufupi
Dk Mwinyi alianza safari yake ya elimu ya Msingi
jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1972 – 1976, Shule ya Msingi
Oysterbay. Kati ya mwaka 1984–1985 wazazi wake walimhamishia Misri na
akasoma katika Shule ya Msingi “Manor House Junior” ambako alihitimu
elimu ya msingi. Shule hii ilikuwa na hadhi ya “Middle School za
Tanzania” kwa wakati huo. Mwinyi alipelekwa Misri kwa sababu baba yake,
Ali Hassan Mwinyi, alikuwa balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo.
Historia yake
Dk Hussein Mwinyi alizaliwa Desemba 23, 1966 huko
Unguja, Zanzibar (Desemba mwaka huu atatimiza miaka 49). Dk Mwinyi ni
mtoto wa Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania) na mama Sitti Mwinyi. Kwa sasa Dk Mwinyi ni Mbunge
wa Kwahani Zanzibar na ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dk Mwinyi alianza safari yake ya elimu ya Msingi
jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1972 – 1976, Shule ya Msingi
Oysterbay. Kati ya mwaka 1984–1985 wazazi wake walimhamishia Misri na
akasoma katika Shule ya Msingi “Manor House Junior” ambako alihitimu
elimu ya msingi. Shule hii ilikuwa na hadhi ya “Middle School za
Tanzania” kwa wakati huo. Mwinyi alipelekwa Misri kwa sababu baba yake,
Ali Hassan Mwinyi, alikuwa balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo.
Aliporejea Tanzania, alipelekwa Shule ya Sekondari
Azania na kuendelea na masomo ya kidato cha I – IV mwaka 1982 – 1984.
Alipohitimu kidato cha nne alipelekwa Shule ya Sekondari Tambaza kusoma
kidato cha tano peke yake mwaka 1984 -1985.
Dk Mwinyi tangu zamani ni mtu wa kupenda kusaidia
watu, aliomba na kuchaguliwa kusomea utabibu wa binadamu. Alianza masomo
ya udaktari nchini Uturuki mwaka 1985 kwenye Shule ya Utabibu ya Chuo
Kikuu cha Marmara na kuhitimu Shahada ya Utabibu wa Binadamu mwaka 1992.
Kwa sababu hakumaliza kidato cha VI, alipokuwa
huko ughaibuni alipitia masomo ya mwaka mmoja ya kujiandaa na udahili wa
Chuo Kikuu “Pre University Studies”. Chuo cha Marmara kinapokea hata
wanafunzi wa kidato cha nne kuanza kusomea shahada ya utabibu lakini
lazima wapitie mwaka mmoja wa maandalizi kama alivyofanya Mwinyi.
Alipohitimu shahada ya kwanza alirejea Tanzania na
kufanya kazi kwa mwaka mmoja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mwaka
1993, Mwinyi aliendelea na masomo ya juu ya utabibu kwa kuunganisha,
safari hii akipelekwa Uingereza katika Hospitali ya Hammersmith ambako
alihitimu shahada ya uzamili ya utabibu mwaka 1994 na kuunganisha
shahada ya uzamivu ya udaktari hapohapo Hammersmith na kuhitimu mwaka
1997.
Alirejea nchini kwa mara nyingine na kufanya kazi
katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuki (HKMU)
kwa miaka miwili hadi mwaka 1999.
Mwaka 2000, Dk Mwinyi alizidisha nguvu yake ndani
ya CCM kwa kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), akashinda na
mwaka 2007 aligombea tena NEC na kushinda na tangu wakati uo aliteuliwa
kuingia kwenye Kamati Kuu ya CCM hadi leo hii.
Dk Mwinyi amemuoa Mariam Herman na wana watoto wanne; Ibrahim, Jamila, Tariq na Sitti.
Mbio za ubunge
Dk Mwinyi alijitosa kwenye siasa mwaka 1999
akiliwania Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani (Bara) na kushinda. Alipokuwa
mbunge, Rais Benjamin Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii, alikaa katika wadhifa huo hadi mwaka 2005.
No comments :
Post a Comment