Friday, May 1, 2015

Serikali yadhamiria kukamilisha Miradi ya Kitaifa ya Kimkakati

 

01
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
02
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
03 04
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya  uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
07
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
08
Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
09
Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiongea na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila (Kulia) mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima. Anayewasikiliza ni Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy.
010
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiongea na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
011
viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 uliokuwa ukifanywa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
……………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli
Serikali imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miradi ya kitaifa ya kimkakati iliyoibuliwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo unaofikia kikomo mwaka ujao wa fedha wa serikali.
Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nagu alisema kuwa mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kutandika reli za uzito wa ratili 56.12 kwa yadi kwa umbali wa km 9 kati ya stesheni za Lumbe, Mto Ugalla na Katumba; kukamilisha malipo ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo ambapo mabehewa yameshaanza kupokelewa Novemba 2014; kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli iliyoharibiwa na mafuriko katika maeneo ya Ruvu – njia panda ya Mruazi.
Waziri Nagu aliongeza kuwa kwa upande wa Barabara hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa kilometa 502.6 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kilomita 560, na ukarabati wa kilomita 78.8 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kukarabati kilomita 131.5. Kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madaraja ambapo daraja la Kigamboni limefikia asilimia 75, Sibiti asilimia 22, Kilombero asilimia 26, Mbutu asilimia 99, Lukuledi II asilimia 25 na Kavuu asilimia 36.
Katika sekta ya Uchukuzi, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa shehena iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 14.3 Machi 2015 dhidi ya lengo la tani milioni 13.0 kwa mwaka 2014/15; kuongezeka kwa ufanisi wa bandari katika kupakua magari kwa kila shifti moja ya saa 8 kufikia magari 886 kwa shifti kufikia Machi 2015 ikilinganishwa na lengo la magari 600 kwa shifti katika mwaka 2014/15; kupungua kwa muda wa meli kupakia na kupakua mizigo bandarini kutoka lengo la wastani wa siku 5 mwaka 2013/14 hadi wastani wa siku 3.7 kufikia Machi 2015; kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa malipo kwa njia ya mtandao mwezi Julai, 2014; na kuanza  kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa masaa 24 kwa siku zote za juma. Aidha, kwa upande wa bandari ya Bagamoyo, hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ujenzi wa bandari; na kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kupata wawekezaji katika bandari za Mtwara na Mwambani -Tanga.
“Katika sekta ya nishati, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542) Machi 2015, na ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) umefikia asilimia 86.9 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 2015. Kwa upande wa usambazaji wa umeme vijijini, wateja wapya 2,602 wameunganishiwa umeme katika mikoa ya Simiyu, Singida, Kagera, Tanga, Ruvuma, na Iringa,” alisema Dkt. Nagu.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, shughuli nyingine zilizotekelezwa nia katika sekta ya nishati, ni pamoja na kukamilika kwa usimikaji wa mitambo 4 ya kufua umeme yenye uwezo wa jumla ya MW 150, kuendelea na ujenzi  wa vituo vya kupoza na njia za kusafirisha umeme, na kuendelea na ujenzi wa  karakana, majengo ya utawala, na barabara za ndani katika mradi wa Kinyerezi I; kukamilisha ulipaji fidia kwa eneo la Makambako katika mradi wa usafirishaji umeme wa Makambako – Songea;  na kuanza ujenzi wa nguzo za njia ya umeme katika mradi wa msongo wa kV 400 wa Iringa – Shinyanga.
Akiwasilisha kazi zilizotekelezwa katika sekta  ya Maji, Dkt. Nagu alisema kuwa  ulazaji wa mabomba katika mradi wa maji Ruvu Chini kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam kazi ambayo imekamilika kwa kilomita 52.43 kati ya kilomita 55.93 za mradi sawa na asilimia 93.8; kwa upande wa mradi wa maji Ruvu Juu: mkandarasi amekamilisha utafiti wa udongo na uchunguzi wa awali wa mahali yatakapojengwa matanki Kibamba na Kimara; na kwa upande wa mradi wa Bwawa la Kidunda,  wananchi wamelipwa fidia ya shilingi bilioni 7 kupisha ujenzi wa barabara na eneo litakapojengwa bwawa.
“Kwa upande wa miradi ya maji vijijini, jumla ya miradi 123 ya maji ilijengwa na kukamilika. Idadi hii imenufaisha wananchi wapatao 463,750 na kuongezeka kwa ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma katika mikataba kutoka siku 265 hadi siku 90. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo bwawa la Iguluba (Iringa) na Wegero (Mara) yamekamilika. Vile vile, ujenzi wa bwawa la Kawa (Rukwa) umefikia asilimia 95, bwawa la Sasajila (Dodoma) asilimia 66.09 na Mwanjoro (Shinyanga) asilimia 45.4,” aliongeza Waziri Nagu.
Katika sekta ya kilimo, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kupatikana kwa hati za mashamba mawili ya Bagamoyo na Mkulazi; maghala 30 yamekarabatiwa na kupatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbozi na Momba.  Vile vile, skimu 30 za umwagiliaji zimepatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbarali, Kyela na Iringa; na mafunzo juu ya kubaini na kudhibiti visumbufu, matumizi bora ya maji, utunzaji na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji na kutumia mwongozo wa uendeshaji skimu za umwagiliaji yametolewa.  Aidha, ujenzi wa maghala 2 katika Wilaya ya Mlele umekamilika.
Vile vile katika sekta ya viwanda, Waziri Nagu alizitaja kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Itoni – Mkiu – Liganga na Mchuchuma kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha mitambo kufika maeneo ya Mchuchuma na Liganga; na kuanza uthamini wa mali za wananchi watakaohama eneo la Mchuchuma. Vile vile, fidia shilingi bilioni 53 imelipwa katika eneo la kujenga kituo cha Biashara na Huduma Kurasini; na fidia ya shilingi bilioni 7 imelipwa katika eneo la uwekezaji Bagamoyo na Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Mechants Holding International kwa ajili ya kujenga bandari na eneo la viwanda. Aidha, katika kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua viluwiluwi wa mbu, Kibaha, kazi ya ufungaji wa mitambo na ujenzi wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2015.
Akizungumzia upande wa maendeleo ya rasilimali watu, Dkt. Nagu alisema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na kuendelea kugharamia wanafunzi 159 wanaoendelea na mafunzo katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya nchi ambapo wanafunzi 124 wanagharamiwa na Serikali na wanafunzi 35 wanagharamiwa na nchi wahisani; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, ufundi na ustawi wa jamii.
Kwa upande wa utafutaji wa rasilimali fedha, Waziri Nagu alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inatumia kanzidata bora inayohifadhi taarifa inayoweza kuthaminisha bidhaa na hivyo kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Vilevile, alisema kuwa tozo kwa ajili ya uwekezaji katika elimu umeanza Julai 2013 ikiwa asilimia 2.5 ya mapato ghafi ya kampuni za simu.
“Katika sekta ya fedha, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuongezea Benki ya Maendeleo ya Kilimo mtaji wa shilingi bilioni 60; kuendelea kuongeza mtaji wa Benki ya Rasilimali kufikia shilingi bilioni 212 ambapo mtaji kutoka Serikalini ni shilingi bilioni 152.2 na shilingi bilioni 59.8 zimetokana na malimbikizo ya faida; na  mali za Benki ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 26.5 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 34.8 mwaka 2014,” alisema Dk. Nagu.
Kuhusu eneo la huduma za utalii, Dkt. Nagu aliongeza kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na usanifu wa ujenzi wa Utalii House awamu ya pili na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji mapato (utalii, uwindaji na upigaji picha). Aidha, idadi ya watalii kutoka nje iliongezeka kutoka watalii 1,090,905 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014. Vile vile mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.81 mwaka 2013 hadi dola za Marekani bilioni 1.98 mwaka 2014.
“Kwa upande wa Biashara, hatua iliyofikiwa ni kurekebisha sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa  elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo; kuanzishwa kwa kampuni ijulikanayo kama Tanzania Mechantile Exchange plc kusimamia na kuendesha soko la mazao ya bidhaa na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya mipakani, Kikanda na Kimataifa,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Dkt. Nagu maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/16 yamezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16). Aidha, Mpango huu umezingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini – MKUKUTA II (2010/11 – 2014/15), Malengo ya Milenia, Mwongozo wa Mpango na Bajeti  kwa mwaka 2014/15; Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2014/15 yaliyojadiliwa na Bunge Novemba, 2014; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010 – 2015); na sera na mikakati ya kisekta.

WARSHA YA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI DAWA ZANZIBAR (eLMIS) KWA WAKURUGENZI NA MAAFISA WA WIZARA YA AFYA.

1
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akitoa maelezo na kuwakaribisha washiriki wa warsha ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Shangani mjini Zanzibar.
2
Mfamasia mkuu Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu mfumo huo mpya wa kielectroniki ulivyoanza kufanyakazi Zanzibar.
3
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif ambae alikuwa Mwenyekiti wa warsha hiyo akitoa muongozo kwa washiriki .
4
Mkurugenzi Usimamizi wa Mifumo ya kielectroniki kutoka Shirika la John Snow Incoparated (JSI) akizungumzia uimarishaji wa mfumo na mafanikio yake kwa washiriki wa warsha hiyo.
5
Meneja wa Zoni ya Unguja ya mfumo mpya wa usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki Biubwa Khamis (aliesimama) akitoa uzoefu wa usambazaji wa  mfumo zamani na huu wa sasa katika warsha hiyo.
6
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya siku moja ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

MJASIRIAMALI WA VYAKULA VYA MIFUGO AJISHINDIA PIKIPIKI YA STARTIMES

Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugajipia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopoBamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja waStarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5,  Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya
kuibuka mshindi wa droo hiyo ya  tatu
ya kujishindia
pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati
akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya
P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia
kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
  
Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia
pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis
Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama,
jijini Dar es Salaam  akionyesha nyaraka
za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa
katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano
ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga
na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia
shilingi 10,000/- na kuendelea.

KIFO CHA MBITA: CCM YATOA SALAAM ZA RAMBIRAMBI

indexSALAAM ZA RAMBIRAMBI ZILIZOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU ABUDLRAHAMAN KINANA WAKATI WA KUAGA MWILI WA BRIG. GEN. HASHIM MBITA (Mst)
TAREHE 29 APRILI, 2015 – LUGALO DAR ES SALAAM
………………………………………………………………….
Ndugu Rais, Amiri Jeshi Mkuu na Ndugu Waombolezaji,
Maisha ni safari na kila safari huwa na mwisho wake,  Tuko hapa kwa kuwa safari ya Brig. Gen. Hashim Mbita duniani imefika ukingoni.  Tumekusanyika hapa siyo kuhuzunika bali kujivunia safari ya mafanikio makubwa ya Mwanamapinduzi, Mpiganaji, Mwanadiplomasia, Mwanahabari, Mwanasiasa na Mzalendo wa mfano.
Mwanasayansi mashuhuri Albert Enstain aliwahi kusema kuwa, thamani ya mtu itapimwa kwa mchango wake kwa jamii siyo kwa kile alichokipata kutoka kwa jamii yenyewe.  Hakuna ubishi, Brig. Gen Mbita alitoa mchango mkubwa kwa Watanzania na Waafrika.  Aliipenda na kulitumikia Taifa lake.  Alishiriki kikamilifu kulijenga na kuliimarisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika miaka ya awali na aliongoza Chama cha TANU kwa ufanisi.  Lakini mchango na umahiri wake ulidhihirika katika kuiongoza Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika.
Kwa kumbukumbu zilizopo kila kazi na jukumu alilopewa Brig. Gen. Mbita iwe Jeshini, Serikalini, katika Chama, katika kuongoza Ukombozi na baadaye kuandika historia ya Ukombozi, aliteuliwa kwa makusudi maalum na kwa malengo maalum.  Alipelekwa Uingereza kutoka Ikulu kwa lengo la kusaidia kulijenga Jeshi la Wananchi Tanzania liwe la kizalendo baada ya maasi ya mwaka 1964. Kwa kuamini kuwa Chama imara ndicho kinachotoa uongozi bora kwa Taifa, Brig. Gen. Mbita aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa TANU ili kuleta ufanisi na nidhamu katika Chama.
Kuna msemo maarufu jeshini usemao Kamanda aliye jasiri anaweza kuwa na bahati. Lakini hakuna Kamanda anayeweza kuwa na bahati bila ya kuwa jasiri. Ujasiri aliokuwa nao Brig. Gen. Mbita ndiyo iliyokuwa sababu ya kuteuliwa kwake kuiiongoza Kamati ya Ukombozi wa Afrika.  Alishiriki kuvijenga vikosi vya Frelimo (Msumbiji), ZANU-PF (Zimbabwe), SWAPO (Namibia), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola), MOLINACO (Comoro), PAIGC (Guinea Bissau, Cape Verde)  na vyama vingine.  Aliviandaa vikosi hivi kupambana na majeshi makubwa yenye silaha nzito na za kisasa na yenye nguvu nyingi.  Lakini mwaka 1994, Brig. Gen Mbita alihitimisha kazi ya Ukombozi wa Afrika kwa ushindi mkubwa.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua na kuthamini mchango na kazi kubwa iliyofanywa na Brig. Gen. Mbita katika kukiendeleza na kukiimarisha Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi. Katika maisha yake kazini na hata baada ya kustaafu aliendelea kutoa ushauri, maoni na wakati mwingine kutoa uzoefu wake ndani ya Chama. Tutauenzi mchango wake, tutajifunza utendaji wake, tutajitahidi kuiga mwenendo wake na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na ardhi na mwenye kutupa na kutuondolea uhai, ili amuonee huruma mja wake huyu.  Brig. Gen. Mbita atabaki kuwa na nafasi muhimu katika historia ya mapambano dhidi ya ukoloni, ubeberu, ubaguzi wa rangi na uonevu.
Alikuwa kiongozi mwenye msimamo na mwenye kuelewa mambo mengi lakini msikivu. Inawezekana Watanzania wengi hatukumjua kwa kuwa hakushughulika kujulikana. Alikuwa jasiri na vile vile alikuwa na wingi wa unyenyekevu. Ujasiri wake ulidhihirika katika kufanikisha majukumu aliyokabidhiwa lakini unyenyekevu ulimzuia kujinadi.  Alitanguliza utumishi na kujiepusha na utukufu. Nafasi alizoshika zilikuwa za juu na zenye kuheshimika.  Kama angependa angeweza kupata umaarufu mkubwa katika nafasi aliyokuwa nayo lakini hiyo haikuwa hulka yake.  Maisha na Utumishi wake ni darasa kamili kwetu sote.
Tunawashukuru viongozi waliokuja kuwakilisha vyama mbalimbali kuungana na Watanzania kumuenzi Brig. Gen. Hashim Mbita.  Wanafalsafa wanatuambia ushindi wa kumbukumbu za wale tutakaowakumbuka zitadumu katika mioyo ya watu na katika historia ya Taifa walilolitumikia. Sihitaji kuwashawishi Ndugu waombolezaji wenzangu kukiri kuwa Brig. Gen Mbita atabaki kwenye mioyo yetu na kuendelea kukumbukwa na wananchi wengi wa Bara la Afrika alioshirikiana nao kuwarudishia Uhuru wao na heshima yao.
Kwa kumalizia, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole kwa Mama Mjane, Watoto, Ndugu na Jamaa, Marafiki na kwa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Mwenyezi Mungu amfungulie milango ya Pepo.
Imetolewa na:
Idara ya Itikadi na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi

WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR

th6Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) nchini Tanzania Dkt.Albina Chuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala la wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam. Kongamano hilo la siku 2 linajadili namna Bora ya uendeshaji wa Taasisi za Takwimu na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za masuala ya Takwimu Barani Afrika. th2Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo. th3 Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam. th4Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.th1 th5Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.

Mmoja afariki bandari kuu ya Mkoani Pemba

index 
Na Masanja Mabula Pemba
KIJANA mmoja Ali Omar (23) ambae ni mpagazi kwenye bandari kuu ya Mkoani Pemba, amefariki dunia, baada ya kuzidiwa na maji wakati akiogelea kwenda gatini, muda mfupi baada ya kujirusha kutoka kwenye meli ya M.v Maendelo.
Tukio hilo lilitokea juzi baina ya majira ya saa saa 2:00 na 2:15 asubuhi, mara baada ya kijana huyo kujikuta meli hiyo inataka kumchukua Unguja pale alipojisahau kwamba tayari meli imeshaondoka bandarini.
Taarifa kutuka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo zinasema kuwa,  imekua ni kawaida kwa wabebaji wa mizigo mara meli inapowachukua masafa mafupi, huamua kujirusha na kuogelea hadi kwenye gati.
Walieleza kuwa hapo juzi, kijana huyo kabla ya kukumbwa na mauti, nae alijirusha umbali wa kati ya mita 75 na 100 na alianza vizuri kuogelea ingawa akiwa amebakisha mita 20 kufika kwenye gati alianza kuzidiwa na maji.
Mmoja kati ya mashuhuda hao Ali Said Ali, alisema awali walidhani kijana huyo anafanya utani kwa kuzama kwake na kuzamuka, lakini mara ya pili baada ya kuzama na kuchukua dakika moja na kuona viatu vikielea, waliamua kumfuata na kumpata akiwa ameshakunywa maji.
“Vijana wenzake ambao wanajua masuala la kupiga mbizi, walimfuata na kumleta juu, akiwa anatweta na katika harakati za kumtapisha maji wakamuona anaanza kulegewa na mwili.
Nae Juma Mohamed Kombo alisema kutokana na hali yake kuona inazidi kuwa mbaya, walimfikisha hospital ya Abdalla Mzee ambayo kwa sasa iko karibu na bandarini, ingawa walisema alikufa papo hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba Juma Yussf Ali, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema sababu ya kifo cha marehemu huyo baada ya kupata taarifa za kidaktari, ni kukosa kupumua kikawadia.
Alisema kijana huyo alijitahidi sana kuogelea mara baada ya kujirusha kutoka kwenye meli hiyo, ingawa baadae alizidiwa sana na maji na juhudu za kumuokoa zilifanyika, ingawa baadae alikumbwa na umauti.
“Sisi tulivyopata taarifa kutoka kwa watendaji wetu, ni kwamba umbali aliojirusha kijana huyo hadi kwenye gati ni kati ya mita 50 na 100, ingawa yeye alizidiwa na maji karibu na gati’’,alisema.
Hatahivyo aliwataka wapagazi hao kwenye bandari hiyo ya Mkoani kuwa makini wakati wanapokuwa kwenye shaghuli zao za ubebaji wa mizigo na kuwataka wanapochukuliwa na meli waache kujitupa.
Hili ni tukio la kwanza kuwahi kutokea kwa mpagazi kujirusha kwenye meli baada ya kuchukuliwa masafa mafupi na kisha kufariki dunia kutokana na kuzidiwa na maji.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC, JIJINI HARARE, ZIMBABWE.

R1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa. Picha na OMR
R2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. Picha na OMR
R3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal. Picha na OMR R4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015. Picha na OMR R5 R6Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.
Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika. Picha na OMR 

KLABU YA MICHEZO YA RIADHA YA DAR ES SALAAM ‘DAR RUNNING CLUB’ YAANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA MARATHON 02 MAY 2015

images 
Klabu ya michezo ya riadha ya Dar Es Salaam “Dar Running Club” (DRC) imeandaa mashindano ya mbio yajulikananyo kama “Mayday marathon” yatakayofanyika tarehe 02 Mei 2015 yatakayoanza na kumalizika katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay (Police Officers Mess).
Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Inspekta Generali wa Police Ernest Jumbe Mangu (IGP).
Akizungumza na waandishi wa habari Mlezi wa Klabu ya DRC Mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni bwana Camillus Wambura) amesema DRC ni klabu ambayo ilianzishwa rasmi kutokana na makundi mawili tofauti yenye malengo sawa kimichezo, yaani Kinondoni police jogging club kutoka Polisi mkoa wa Kinondoni na Dar Es Salaam Athletic Club yenye washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya Dar Es Salaam wakaamua kuungana na kuwa DRC.
DRC ina madhumuni makubwa ya kuendeleza michezo ya riadha nchini mpaka nje ya nchi na kuhimiza afya njema kimwili na kiakili, lakini pamoja na hayo muungano huu wa klabu unasaidia sana kuimarisha mahusiano kati ya Polisi na raia, hii inasaidia sana katika usalama na kukuza na kuendeleza dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jamii. Aliongezea….
Naye Captain wa DRC bi (Stella Mandago, na mratibu wa mashindano haya amesema kuwa Mashindano haya yanatarajia kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi pia, mashindano haya yatakuwa na washiriki watakao shiriki katika mbio za kilometa ishirini na moja nukta moja (21.1km) na kilomita kumi (10.0Km) yakiwa na lengo la kukuza na kuendeleza michezo ya riadha Tanzania na nje ya nchi ili kuwawezesha wanamichezo kufikia hatua za kimataifa na kuhimiza maisha yenye afya pia kudumisha mahusiano baina aya police na jamii.
Klabu ya michezo ya Riadha “Dar Runing Club” inachukua fursa hii kukukaribisha kushiriki mbio hizi zinazotarajiwa kuanza majira ya saa kumi na mbili asubuhi 12:00 katika viwanja tajwa hapo juu, aliongezea…..
Kutakuwa na zawadi kwa washindi kumi wa kwanza kwa wanawake na wanaume kama ifuatavyo kwa nusu marathoni ya km 21
Mshindi wa kwanza TZS 1,100,000
Mshindi wa pili TZS 800,000
Mshindi wa tatu TZS 600,000
Mshindi wa nne TZS 350,000
Mshindi wa tano TZS 300,000
Mshindi wa sita TZS 250,000
Mshindi wa saba TZS 200,000
Mshindi wa nane TZS 1500,000
Mshindi wa tisa of TZS 100,000
Mshindi wa kumi of TZS 50,000
Kutakuwa pia na washindi wa 3 kwa mbio za Km 10 kama ifuatavyo
Mshindi wa Kwanza TZS 500,000
Mshindi wa PIli TZS 300,000
Mshindi wa tatu TZS 200,000

PINDA AKUTANA NA DANGOTE

da1 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. Watatu kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) da2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake jijini Dar es salaam April 30, 2015. Kushoto kwake ni balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) da3Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kushoto) na  balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu (kulia) baada ya mazungumzo yao  ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

wakimbizi kutoka Nchini Burundi waliokimbia mwaka 1972 wapewa uraia

KT1Waliokuwa wakimbizi kutoka Nchini Burundi waliokimbia mwaka 1972 wakaingia nchi na kupelekwa makazi ya Ulyankulu Mkoani Tabora na wengine kuhamishiwa Makazi ya Mishamo Mwaka 1978 hatimaye wamepatiwa uraia wa Tanzania.na hapo ni baadhi yao wakiwa wako kwenye mstari kusubiria kukabidhiwa vyeti vyao vya uraia wa Tanzani katika zoezi lililokuwa likiendelea kwenye makazi hayo. KT2Mkuu wa Makazi ya wakimbizi Mishamo Fred Nisajire akiangalia moja na rejesta iliyo na majina ya wakimbizi waliopewa uraia akihakiki kujiridhisha kama kweli anayepewa cheti cha uraia ni Yule aliyeandikiwa jina halisi ndani ya orodha husika ,Pembeni ni maafisa wa uhamiaji na wale wafanyakazi wa Shirika  la Kimataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR )Wakiwasanjari kusaidiana mchakato unakamilika kama uliyvyopangwa. KT3Mmoja wa waliokuwa wakimbizi akiwa amebeba mwanaye kifuani kama anavyoonekana akielekea eneo la kupokelea cheti chake cha uraia na kuwa raia mpya wa Tanzania, hivyo kusahau yaliyopita na kuanza ukurasa mpya wa maisha katika nchi ya Tanzania.kama unavyomwona akiwa na furaha tele machoni kwa tabasamu lake. KT4Baada ya kukamilisha zoezi la ugawaji na upokeaji wav yeti vya uraia hawakuweza kumsahau mungu wao walikwenda kanisani na kukusanyika kumwomba mungu aweze kuwasaidi katika maisha mapya ya uraiani na kuepukana na taabu na adha za ukimbizi. Hapo wapo kanisani moja ya kanisa lililoko eneo la kijiji cha Lugufu Makazi hayo ya Mishamo.
 (Picha zote na Kibada Ernest Kibada. Makazi ya Mishamo Mkoani Katavi)

Ujumbe wa Bodi ya TRA wakutana na Dr. Shein

tr1 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA Benard S.Mchonvu wakati alipoongoza ujumbe wa Bodi hiyo leo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais,[Picha na Ikulu.] tr2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Bodi TRA ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo asubuhi ukiongoza na Mwenyekiti wake Benard S.Mchonvu (wa tatu kushoto) ,[Picha na Ikulu.] tr2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na ujumbe wa Bodi TRA baada ya mazungumzo yaliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar  leo asubuhi (kushoto)  Mwenyekiti wake Benard S.Mchonvu ( katikati) Rished Bad TRA Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]

NMB YAKABIDHI HUNDI YA SH. BILIONI 1.5 KUCHANGIA MADAWATI

unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Kaimu Mtendaji  Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols  mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 1.5 ukiwa ni mchango wa Benki ya NMB kwa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili zisaidie kutatua tatizo la madawati kwa shle za msingi nchini. Kiasi hicho cha fedha kitatolewa kwa miaka mitano. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea hundi ya mfano (dummy cheque) yenye thamani ya sh. bilioni 1.5 kutoka benki ya NMB zikiwa ni mchango wa taasisi hiyo kwenye kampeni ya uchangiaji madawati kitaifa.
Akizungumza na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam jana jioni (Jumatano, Aprili 29, 2015), kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols alisema wameamua kutoa mchango ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa madawati linalozikabili shule za msingi na za sekondari hapa nchini.
“Tunaelewa kwamba shule nyingi hapa nchini zinakabiliwa na uhaba wa madawati … tunaamini kuwa elimu bora inachangiwa pia na mazingira mazuri ya kusomea ikiwa ni pamoja na kukaa kwenye madawati wanapoandika. Kama sehemu ya mchango wetu kwa jamii (CSR), tumeamua kutenga sh. bilioni 1.5 ili zisaidie kupungua tatizo hilo,” alisema.
Akipokea mchango huo, Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo ulioambatana na Bw. Borghols kwa kuamua kusaidia juhudi za Serikali kutatua tatizo hilo. Alisema mchango huo ni mkubwa na anaamini kwamba utawachochea wadau wengine kuchangia juhudi za Serikali kutatua tatizo la madawati nchini.
“Nimecheki na watu wangu kwa kweli mahitaji ni makubwa lakini naamini mchango wenu utasaidia kupunguza tatizo la madawati kwa kiasi fulani. Tunawashukuru kwa uamuzi wenu wa kuchangia suala hili la kitaifa,” alisema.
Hadi sasa Serikali inahitaji kununua madawati 1,016,476 kwa ajili ya shule za msingi na za sekondari. Kati ya hayo, madawati 892,772 yanahitajika kwa ajili ya shule za msingi na madawati 123,704 yanahitajika kwa ajili ya shule za sekondari.
Madawati hayo yote yataigharimu Serikali kiasi cha sh. bilioni 91.4/- kwa gharama ya sh. 90,000/- kwa kila dawati.
Hata hivyo, Serikali iliamua kutenga fedha za chenji ya RADA ili zitumike kununua madawati na vitabu. Fedha hizo, zilisaidia kununua madawati 168,163 kwa bei ya sh. 90,000/- kwa dawati moja.

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 100 KWA SACCOS YA WALIMU WILAYANI RUANGWA MKOANI LINDI

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Mashariki, Yessaya
Mwakifulefule akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa,
Nicholous Kombe,  mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi millioni 100 ikiwa ni mkopo uliotolewa na mfuko huo kwa
wanachama wa SACCOS ya waalimu wilayani Ruangwa..Hafla hiyo ilifanyika
Wiyani Ruangwa hivi karibuni.

Wanachamawa  Walimu Saccos wa Wilaya  ya Ruangwa mkoani
Lindi wakifurahia   mkopo wenye thamaniya shilingi Milioni 100 uliotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa wanachama wa Saccos hiyo. Anaeshuhudia wa pili kulia ni Meneja wa LAPF,  Kanda ya Mashariki,
Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Wilayani Ruangwa hivi
karibuni.

 
Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe: William Lukuvi katika ziara yake Mkoni Mwanza.

1
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana Bw Baraka Konisaga (Kulia),ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakimkaribisha Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi muda mfupi kabla ya Mheshimiwa Lukuvi kupoekea ripoti ya awali ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza
2
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw Baraka Konisaga akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi wakati wa kupokea taarifa ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza ambayo imekuwa kero kwa wananchi wa jiji hilo katika
ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo
3
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akijadiliana jambo na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya
Kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza kufuatia tume iliyoundwa na Mheshimiwa Waziri mwezi uliyopita.
5
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na watendaji wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) mara baada ya kupokea ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wataalamu wa kujitolea wakikaribishwa nchini

1
Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Shota Yanagisawa (aliyesimama) akijitambulisha kwa Kaimu Katibu Mkuu – Utumishi Bw. HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kukaribishwa nchini iliyofanyika Utumishi mapema leo.
2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akiwakaribisha wataalamu wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kuja kujitambulisha Utumishi.
3
Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani wakishukuru baada ya kukaribishwa.
4
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akiagana na Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha iliyofanyika Utumishi.

Fight of the Century’ to air ONLY on DStv in Sub-Saharan Africa

New Picture (4)29 April 2015: MultiChoice Africa would like to inform the general public and all television broadcasters that ONLY SuperSport International has rights to air the ‘Fight of the Century’ bout taking place this weekend between Floyd Mayweather and Manny Pacquiao in Sub-Saharan Africa.
From this Saturday, 2nd of May, DStv will air the super-fight on SS6 and SS6 HD to enable all DStv Premium viewers to watch the action in High Definition. The build-up to the live event will begin at 8pm and headed by former boxer, Brian Mitchell, with a professional record of 45-1-3 and a panel that includes Phillip Ndou, who fought Mayweather in 2003, and legendary referee Stan Christodoulou. Viewers will also be treated to breaking news, extensive behind-the-scenes coverage, documentaries, one-on-ones with Mayweather and Pacquiao, plus past fight highlights involving the pair.
The rights also include live streaming, which is available to Premium subscribers on the SuperSport app. The build-up will culminate in The Fight of the Century which will air from the early hours of Sunday on May 3rd.
No other television station/event organiser or entity shall screen this boxing match on any other programme or channel in a public place or free-to-air, live or repeated, without the authorisation of MultiChoice since this will be in violation of the directives governing the distribution of programmes and television channels. It furthermore interferes with and infringes upon the programme and channel distribution rights and arrangements of third parties.
SuperSport’s knock-out build-up programming to ‘The Fight of the Century’ includes:
• Studio analysis headed by former boxer, Brian Mitchell and a panel that includes Phillip Ndou and legendary referee Stan Christodoulou on SS6 from 10pm CAT on Saturday.
• Updates on the biggest fight in boxing history plus “Big Fight Special” on SuperSport Blitz at 7am, 1pm and 7pm CAT daily.
• Wall-to-wall big-fight programming on Friday, 1st May on SS6 from 6am to 5.30pm CAT.
• SS6 will cross live to the MGM Grand Garden Arena in Las Vegas at midnight on Friday for the pre-fight weigh-in.
• After the weigh-in, Pacquiao’s six-knockdown defeat of Chris Algieri will be broadcast on SS6 to remind fans of his power and excitement.
• SS6 will cross to Las Vegas for the tournament at 3am CAT on Sunday morning. The undercard features WBC super-bantamweight champion Leo Santa Cruz against Jose Cayetano, plus WBO featherweight champion Vasyl Lomachenko against Gamalier Rodriguez.
• In the unfathomable possibility of missing the live fight action, DStv subscribers can catch the repeat the fight on SS6 at 7am CAT on Sunday and again on SS5 from 9pm CAT. Repeats will continue throughout the week.
• The bulk of the programming will also be available on the Video on Demand service.
PLEASE NOTE: SuperSport advises fight fans to set their alarm clocks for 4:30am CAT as the big Las Vegas bouts typically start at any time between 5:15am and 6am CAT.
For more information about this much-anticipated #MayPac bout, please visit www.dstv.com.

CHAWAKAMA yafanya ziara Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA, hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo
2
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA) wakisikiliza kwa makini walipofanya ziara katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam.
3
Mkurugenzi Msaidizi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wanne kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

NHC yang’ara maonesho ya Mei Mosi jijini Mwanza

 

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.

 Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.

Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

Anti poaching efforts lower elephant poaching in Ruaha

TANZANIA NATIONAL PARKS
images
On 23rd April, 2015, the ITV News network of UK ran an article with a title “Exposed: Tanzania’s elephant killing fields”. The article cited a decrease of elephants in Ruaha National Park from 8,500 in 2014 to just over 4,200 now. The article further pointed out that the main reason for the decline is “poaching and claimed that these findings are part of the Great Elephant Census, an ambitious two year project to conduct an aerial survey of elephant numbers and distribution across Africa”.
Tanzania National Parks would like to categorically deny the above accusations and is hereby giving clarification on the same for the interest of the general public:
• Tanzania National Parks is not informed of the release of any official census results indicating the decrease of elephants in Ruaha National Park.
• The practice of conducting census in the protected areas including National Parks is done on the basis of ecosystems as animals do migrate from one area to the other. Therefore, it is expected that any official release of the census results should have included the whole ecosystem of Ruaha-Rungwa and not Ruaha alone.
• Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) is an authority mandated to conduct wildlife census in all protected areas in Tanzania. Therefore as of now they have not released any official results regarding the census.
• As pointed out in our regular news releases, there have been significant improvement in efforts to fight poaching in Ruaha National Park that has resulted to a significant decline of elephant poaching incidences inside the park from 82 in 2012/2013 to only 36 in 2013/2014 and only 12 incidences between July 2014 and March 2015. These efforts will eventually lead to further decline and/or halting of elephant poaching in all National Parks.
In view of the above, Tanzania National Parks would like to assure the public that once the official results of the census are out, the public will be officially informed.
Issued by Corporate Communication Department
Tanzania National Parks
30th April, 2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com

No comments :

Post a Comment