![]() |
| Hali halisi ya magari ilivyo katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo mchana mwendo wa saa saba --- picha taarifa via WhatsApp |
![]() |
| Dar es Salaam --- taarifa-picha via WhatsApp |
![]() |
| picha-habari via WhatsApp |
Inaripotiwa kuwa Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia vilupuzi vya machozi katika kituo cha mabasi cha Ubungo ili kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kutokana na mgomo wa madereva.
Mgomo huo wa madereva wa mabasi na malori umeanza rasmi leo asubuhi nchi nzima na kuathiri kabisa sekta ya usafirishaji, ambapo Jijini Dar es Salaam mgomo huo pia umehusisha "daladala".
Shuhuda mmoja anaripotiwa na blog ya Malunde1 kuwa katika neo la Ubungo bajaj na pikipiki nazo zinalazimishwa kugoma na dereva akibisha anapigwa na usafiri wake kuharibiwa.
![]() |
| Dar es Salaam --- habari-picha via WhatsApp |
"Yaani Subby moro road hakuna daladala yeyote inayotembea wanafunzi na wafanyakazi wamerudi manyumbani wasio na usafiri binafsi."
"Yaani sasa hivi inasikika milio ya risasi na mabomu sijui kinachoendelea."
"Ubungo hapafai abiria kuna mabomu ya machozi abiria wanapiga mawe magari ya polisi na bodaboda au bajaji akijaribu kuchukua abiria anapigwa na chombo kuharibiwa."
"...Arusha hawajagoma."
![]() |
| Dar es Salaam --- habari-picha via WhatsApp |
| Hali katika kituo cha mabasi Tabora --- Blogu ya Fundikira |
| Tabora --- Blogu ya Fundikira |
| Tabora --- Blogu ya Fundikira |
- Inasemekana kuwa sababu zao za kugoma ni kutokana na masharti mapya na magumu yaliyowekwa na mamlaka husika ambayo ni Dereva akitaka kuongeza muda wa leseni yake atatakiwa alipe aende kozi ya udereva kwa muda wa Tsh 560,000 (laki tano na sitini).
| Mbunge Aden Rage (mwenye T-shirt nyekundu) akifanya mawasiliano kabla ya kuogea na baadhi ya askari na abiria waliokuwa wamekusanyika katika kituo cha mabasi Tabora. |
| Rage akiwa kituo cha Polisi na wananchi |
![]() |
| Mwanza |
![]() |
| Mwanza |
![]() |
| Mwanza |
![]() |
| Mwanza |
| Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha
daladala cha Darajani-Ubungu huku kukiwa hakuna daladala yoyote
inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala
jijini Dar. --- Pamoja Blog |
| Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya kubebea mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuh |






.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments :
Post a Comment