Thursday, April 30, 2015

NHC YANG'ARA MAONESHO YA MEI MOSI JIJINI MWANZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.
Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.
 Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.
Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jana.

 

KAIMU KATIBU MKUU UTUMISHI HAB MKWIZU AWAPOKEA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN

KIM KARDASHIAN NA VAZI LAKE MTAANI

Mwanadada anayetamba nchini Marekani kutokana na kutosihiwa vituko, Kim Kardashian akiwa ameongozana na mtoto wa dada yake Kourtney, Mason mwenye umri wa miaka 5 wakitoka kufanya manunuzi. 

Kim ( 34 ) anayetamba na kipindi cha luninga cha Keeping Up With The Kardashians ambaye pia ni mke wa mwanamuziki Kanye West alionekana akiwa amevaa jeans na sweta ambalo kimuonekano ni kama limechakaa, lakini ndio staili hiyo. 

Bongo watu wangesema sweta yake imechakaa hadi kuchanika. Mume wake, Kanye West hupendelea mara kwa mara kuvaa mavazi ya aina hii.


WANANCHI WA KIJIJI CHA LUGAGALA, JIMBO LA PERAMISHO WASIFU UTENDAJI WA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH AMOS MAKALLA

Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero kupitia Chama Tawala (CCM), Mh. Amos Makalla akipokea zawadi ya mbuzi na gunia la Mahindi kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Lugagala kilichopo Jimbo la Peramiho Songea. Naibu Waziri aliwahakikishia wananchi hao kwamba Serikali itajitahidi kukamilisha mradi huo ili kuwaondolea adha ya maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lugagala mara baada ya kutoka kukagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji. Wananchi hao walifika kumsikiliza na kumueleza kilio chao cha tatizo la maji katika kijiji hicho.

MBUNGE WA MVOMERO MH AMOS MAKALLA KUONGOZA WANANCHI WA JIMBO LAKE KUMUONA WAZIRI MKUU ILI KUTATUA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akimpa pole na fedha za matibabu mmoja wa wakulima aliyejeruhiwa kwa kuvunjwa Mkono. 

Mbunge wa Mvomero Mh, Amos Makalla ameridhia pendekezo la wananchi kumuona Waziri Mkuu Mh, Mizengo Pinda kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watatu walipoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wafugaji kulishia Mazao ya wakulima katika mashamba yaliopo bonde la mgongola.
 

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama waliitisha mkutano wa hadhara kijiji cha Kugugu kuongea na wakulima wanaolima katika bonde la Mgongola, ambapo pamoja na mambo mengine wananchi walimuomba Mbunge wao kuundwe Kamati ya kumuona Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusiana na mipaka ya bonde la Mgongola ambalo limekuwa mahakamani kwa zaidi ya miaka 15 na machafuko ya mara kwa mara yametokana na bonde hili kwa wafugaji wa kijiji cha Kambala kulishia mifugo Mazao ya wakulima na kupelekea uvunjifu wa Amani wa mara kwa mara.
 

Akiongea kwa niaba ya wananchi, mkazi wa Kigugu ndugu Salihina Mpenda alisema kuwa "kesi ya bonde la Mngongola imekuwa muda mrefu na serikali haichukui hatua huku watu wanaendelea kufa kila kukicha, na imefika wakati jitihada zako Mbunge ulizozifanya kuwaleta mawaziri 4, barua ulizomuandikia Waziri mkuu na Waziri wa ardhi sisi wananchi tunakupongeza ila inapaswa tukuongezee nguvu tukamuone Waziri mkuu" alisema mkulima huyo.
 

Akijibu hoja hiyo, Mbunge na Naibu Waziri aliridhia ombi lao la kuundwa Kamati ya wakulima ya kumuona Waziri mkuu na akawataka wachague watu kumi na yeye kama Mbunge atagharamia gharama zote.
 

Aidha kwa upande mwingine mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga amewahakikishia hali ya usalama ndani ya bonde la Mgongola ni shwari wakulima waendelee na shughuli zao kwani na Ulinzi wa Askari wa doria umeimarishwa.
Maelfu ya wananchi wakimpongeza Mbunge wao Amos Makalla kukubali kufadhili Kamati ya kwenda kumuona Waziri mkuu.
Mamia ya wananchi akimpokea mbunge wao aongee na wakulima bonde la Mgongolwa.

KITUO CHA TELEVISHENI CHA ITV CHASHINDA KWA MARA NYINGINE TUZO YA UBORA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

SERIKALI YADHAMIRIA KUKAMILISHA MIRADI YA KITAIFA YA KIMKAKATI

Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Sehemu ya Wabunge waliohudhuria uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima wakimsikiliza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.

WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI

Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahalo
Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.
Dk bana akizungumza katika mdahalo
                                    Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
                           Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
IMG_4917
Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
                                                  Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.

LA LIGA, REAL MADRID YAIFUNGA ALMERIA 3-1

Real Madrid imeendelea kuwafukuza kwa kasi vinara wa ligi kuu nchini Hispania maarufu La Liga wapinzani wao wakuu FC Barcelona, baada ya usiku wa kuamkia leo kuwatandika Almeria mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu. 

Mabao ya Madrid yaliwekwa kimiani na James Rodríguez, Mauro Dos Santos ambaye alijifunga na bao la tatu likafungwa Alvaro Arbelo.

HAKUNA WA KUIZUIA CHELSEA KUTWAA UBINGWA, WAITUNGUA LEICESTER 3-1

DK SHEIN ALIPOZINDUA MBIO ZA MWENGE SONGEA

NIC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU KWA WATOTO WENYE UONI HAFIFU KITUO CHA ALBINO BUHANGIJA SHINYANGA

Shirika la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona mbali(Telescope Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye msimamizi mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali (katikati),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34 vilivyotolewa na Shirika la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)
Mtaalam wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson akiwaelekeza watoto hao namna ya kutumia Darubini Kiona mbali.
Watoto wakifanya majaribio kuhusu matumizi ya darubini kiona mbali.
Mtaalam wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson na Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange wakiwaelekeza watoto hao namna ya kutumia Darubini kiona mbali.

BALOZI KAMALA ABAINISHA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI ZINAZIPATIKANA TANZANIA

BENKI YA POSTA YAJIVUNIA UTENDAJI BORA KWA MWAKA 2014 ULIYOIPA FAIDA NONO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia ,Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo leo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

BRIGEDIA JENERALI ( MSTAAFU ) HASHIM MBITA AZIKWA LEO KWENYE MAKABURI YA KISUTU, JIJINI DAR

Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Hamis Makuka.
Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita, ambaye amezikwa kwa heshima zote za kijeshi na kwa taratibu ya dini ya Kiislam kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo

No comments :

Post a Comment