Thursday, April 9, 2015

MTUHUMIWA WA TUKIO LA BOMO LA BOSTON ATIWA HATIANI KWA MAKOSA 30

Mwanaume anayetuhumiwa kuhusika na tukio la mabomo katika mbio za marathoni za Boston mwaka 2013, amekutwa na hatia ya mashtaka yote 30 yanayomkabili ambayo yanaweza kumfanya akabiliwe na adhabu ya kifo.

Jopo la wazee wa mahakama ya Massachusetts, wataamua iwapo mtuhumiwa huyo Dzhokhar Tsarnaev, atapatiwa adhabu ya aina gani.

Watu watatu walikufa na wengine zaidi ya 260 wamejeruhiwa wakati mabomu yalipolipuka katika eneo la kumalizia mbio za marathoni Aprili 2013.

MWANAUME MMOJA KATI YA 10 HUDUNDWA NA MWANAMKE NCHINI KENYA

CHUO KIKUU CHA CAPE TOWN KUONDOA SANAMU LA MKOLONI CECIL RHODES

CRISTIANO RONALDO AFIKISHA MAGOLI LA 300 AKIWA NA KLABU YA REAL MADRID

RADIO ZA JAMII ZASHUKURU KWA KUPOKEA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA NJIA YA SAUTI

LIVERPOOL KUCHEZA NUSU FAINALI KOMBE LA FA NA ASTON VILLA APRIL 19' 2015

Wachezaji wa timu ya Liverpool wakipongezana baada ya kuifunga Blackburn bao 1-0 na kufanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya nusu fainali ya kombe la FA.
Mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho akikimbia kwa furaha mara baada ya kuifungia timu yake bao 1-0 katika dakika ya 70 ya mchezo wa robo fainali wa kombe la FA dhidi ya Blackburn, mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Ewood Park.
Kwa matokeo hayo, Liverpool watacheza nusu fainali na Aston Villa, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Wembley jumapili ya tarehe 19 April 2015.

RWANDA YAADHIMISHA MIAKA 21 YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI

Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura wakiwasha mishumaa maalumu kuwakumbuka raia waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Mratibu Mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Mratibu Mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akipata maelezo juu ya mwenendo wa mashauri toka ICTR mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa pichani. 
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akipata maelezo juu ya mwenendo wa mashauri toka ICTR mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa pichani.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. 
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.

YANGA YAIFUNDISHA SOKA COASTAL UNION, YAIFUNGA 8-0, TAMBWE APIGA 'HAT TRICK'

Kiungo wa Yanga, Salum Telela, akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 8-0. (Picha na Francis Dande).
Simon Msuva akishangilia bao aliloifungia timu yake.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.
Haruna Niyonzima akiruka kihunzi cha, Hamoud Abdulhalim.
Amis Tambwe akiwatoka wachezaji wa Coastal Union.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAONGEZEKA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AYAPOKEA MATEMBEZI YA VIJANA YA KUMUENZI MZEE ABEID AMANI KARUME

g1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja leo kupokea matembezi ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi katika kumuenzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,[Picha na Ikulu.] g2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja leo kupokea matembezi ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi katika kumuenzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,[Picha na Ikulu.] g3
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika matembezi ya kumuenzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakiingia katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo ambapo yatapokelewa na rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] g4
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakibeba Picha la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika matembezi ya kumuenzi kiongozi huyo yaliyoanzia Mwera na kumalizia katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo ambapo yatapokelewa na rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] g5

KATIBU MKUU WA SEKRETARIETI YA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC AKUTANA NA BALOZI KAMALA

BALOZI SEIF AKUTANA NA BALOZI MDOGO MPYA WA INDIA, AWATAKA WAWEKEZAJI ZAIDI TOKA INDIA KUWEKEZA VISIWANI ZANZIBAR

Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. 
Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar.

                                          Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameyashauri Makampuni na Taasisi za uwekezaji kutoka Nchini India kuwekeza miradi yao katika Visiwa vya Unguja na Pemba ili kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kukaribisha wawekezaji mbali mbali kuwekeza hapa Nchini .

Alisema India bado ina nafasi pana kwa Makampuni yake kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi hasa katika Sekta ya Viwanda kama ilivyowahi kutumia fursa hiyo hapa Zanzibar katika miaka ya 80.

Akizungumza na Balozi Mdogo Mpya wa India hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Sekta ya Viwanda ni eneo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza Umaskini.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa na malengo la kuimarisha sekta hiyo kwa azma ya kulisaidia kundi kubwa la Vijana wasio na ajira ambalo limekuwa likiongezeka kila mwaka baada ya kumaliza masomo yao.

“ Ipo haja kwa wawekezaji wa Sekta ya Viwanda kutoka Nchini India kurejea tena Zanzibar kuwekeza miradi yao ya viwanda ili kusaidia uchumi wa Taifa pamoja na kupnguza wimbi la vijana wasio na ajira “. Alisema Balozi Seif.

MWAKILISHI MKAZI WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI, AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM LEO

DK KAMANI AWAPATIA MISAADA WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO KIJIJI CHA LAMADI

VITA YA UGAIDI KENYA YAFUNGA KAMPUNI 13 ZA KUHAMISHA FEDHA

Serikali ya Kenya imeagiza kufungwa kwa kampuni 13 za kuhamisha fedha ili kuzuia vikundi vya wapiganaji wa Kiislam kutotumia kutuma fedha za kufanya mashambulio ya kigaidi.

Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph Nkaissery pia amesema Kenya imefunga akaunti za benki 86 za watu binafsi pamoja na mali zao kushikiliwa.

Hatua hizo zinaaminika kuilenga kampuni ya mabasi na hoteli inayodaiwa kuwa na uhusiano na kampuni ya nchini Somalia.

REPARATIONS FOR THE 7TH EAC-EABC MEDIA SUMMIT IN HIGH GEAR


Dar is set to host the Premier EAC Media Event on 14-15 May 2015



East African Community Headquarters, Arusha, 8 April, 2015: The EAC Secretariat together with the East African Business Council (EABC) and CEOs of Media Houses are finalizing preparations for the 7th EAC-EABC Media Summit, which is to be held from 14 to 15 May 2015, at the Hyatt Kilimanjaro Hotel Dar es Salaam, Tanzania.



The 7th EAC-EABC Media Summit will bring together over 250 Media owners, CEOs, Publishers, Editors, prominent Media personalities and practitioners on a round table discussions under the theme: The Role of the Media in Deeping Democracy in the Region, with sub-themes on Democracy in the EAC: Achievements and Challenges; The Role of Media in Electoral Processes, and Regional Security, Business Environment and Media: Towards a Common Goal.



We see the Summit as a vehicle to increase the visibility of EAC’s flagship in the integration process and EAC-EABC joint activities through the media is commendable,” comments Mr. Kajubi Mukajanga, Chair of the Regional Preparatory Committee of the 7th Media Summit and also the Executive Secretary of Media Council of Tanzania (MCT). “This will also be a time to network with and update the Media industry on the latest developments in the East African regional integration process,” he said.



The Head of Corporate Communications and Public Affairs at the EAC Headquarters Owora Richard Othieno notes that the Media Summit is designed to, among others; advance the relationship between the EAC/EABC and the media, who have long been recognized as strategic partners for the Community in achieving its key objective of deepening and widening regional integration and development process.



Launching the EAC Media Scholarship Fund sponsored by EAC-KfW-AKU, and announcing and recognizing Winners of the EAC Media Award Competition 2013/14 are expected at the Media Summit over a Gala Dinner.

ZAKHEM FC /FFU SC, KUSAKA BINGWA WA JUMLA MICHUANO YA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM

Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na kupata timu tatu zitakazouwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya mabingwa ya mikoa ya TFF,kesho Alhamis Aprili 09/2015,katika uwanja wa Karume jijini kutakuwa na mchezo wa fainali ya kumpata Bingwa wa jumla wa michuano ya ligi ya mkoa.

Timu zitakazoumana katika fainali hiyo ni ZAKHEM FC dhidi ya FFU SC,ambazo zitashuka dimbani majira ya saa kumi jioni zikishuhudiwa na umati wa mashabiki waliokuwa wakiyafuatilia mashindano hayo tangu yalipoanza kutimua vumbi.

Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,timu zilizofanikiwa kuuwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya maabingwa ni pamoja na ZAKHEM FC,FFU SC na CHANGANYIKENI SC.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,ameipongeza kamati hiyo ya mashindano kwa kusimamia vizuri uendeshaji wa ligi tangu ilipoanza.
Imetolewa na DRFA,
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano DRFA
Omary Katanga/+255766358585/+255784500028.

KUZIONA TWIGA, SHE-POLOPOLO TSH.2,000/=

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (She-Polopolo) kiingilio cha juu sh.5,000 kwa VIP na sh. 2,000 kwa majukwaa yaliobakia, mechi hiyo itachezwa ijumaa jioni saa 10 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Twiga Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage imeendelea kujifua katika hosteli za TFF zilizopo Karume, kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kuwnaia kufuzu kwa Michezo ya Afrika nchini Congo- Brazzavile mwezi Septemba mwaka huu.

Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki tatu zilizopita jijini Lusaka nchini Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Zambia, hivyo katika mchezo wa ijumaa kuhitaji ushindi wa aina yoyote tu ili kuweza kufuzu kwa fainali hizo.

TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi siku ya ijumaa jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuja kuwapa sapoti Twiga Stars watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Taifa.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (She-Polopolo) inatarajiwa kuwasili usiku wa saa 7.25 kuamkia alhmisi kwa shirika la Ndege la Ethiopia wakiwa na msafara wa wachezaji 18 na viongozi saba na watafikia katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani Kariakoo.

Msafara wa Zambia (She-Polopolo) unaongozwa na mkuu wa msafara Lenny Khuwa, kocha mkuu Albert Kachinga, kocha msaidizi Kape Saili, kocha wa magolikipa Yona Phiri, daktari wa timu James Nyimbili, mchua misuli Conerlia Chazura, na meneja wa timu ni Besa Chibwe.

Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili ni Rachel Nachula, Annie Kibanji, Chiko Nkhoma, Osala Kaleo, Joana Benai, Meya Banda (Nahodha), Misozi CR Chisamu, Jane Nshika Chalwe, Milika Limwanya, Mary Wilombe, Grace Chanda, Barbra Banda, Memory Mwaseba, Hazel Natasha Nali, Martha Tembo, Mary Mwakapila na Ireen Lungu.

Kesho jioni She-Polopolo wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa, uwanja ambao ndio utakaotumika kw amchezo huo.

Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Uganda wanatarajiwa kuwasili leo mchana ambao ni Ms Anna Akoyi , Ms Nakkito Nkumbi , Ms Jane Mutonyi, na Ms Nabikko Ssemambo, Kamishina wa mchezo Ms Nomsa Jacobeth Mhalangu kutoka nchini Afrika Kusini anatarajiwa kuwasili leo jioni.

TFF YAMPONGEZA TENGA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.

Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.

Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA ILIYO ENDESHWA NA MJASIRIAMALI BI. MARY DAVID JIJINI DAR

Mjasiriamali na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja wa wajasiliamali ambaye pia ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake wa jinsi alivyo nufaika na mafunzo kama haya na mpaka sasa anajitegemea na Kupata kipatochake na kuwasaidia wengine.
Wa kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada ambaye amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi wake umuhimu wa mikutano kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata elimu Bora ya Kilimo.
Bwana Daniel Ambaye ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake katika maswala ya kilimo.
Mwendeshaji msaidizi wa Semina Hiyo Bwana Saidi akitoa mafunzo ya juu ya kuanzisha kilimo kwa kutumia Green House pamoja na faida zake

No comments :

Post a Comment