Ngabwe Mlulu
 |
| RAIS
mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, (kulia), akiwa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akijibu maswali
baada ya kutoa "somo" kwenye muhadhara ulioitishwa na wizara ya Mambo
ya Nje, ambapo msemaji mkuu alikuwa Rais huyo mstaafu, na mada kuu
ilikuwa "Demokrasia ya Uchumi, na takwa jipya la uchumi wa kimataifa.
Rais Mkapa, alihadharisha juu ya taifa kuingia "kichwakichwa" kwenye
mikataba ya kiuchumi na badala yake wizara ya Mambo ya Nje, inapaswa
kuwa mshirika mkubwa katika kufukia mikataba mbalimbali ambayo nchi
inaingia na mataifa ya kigeni hususan yaliyoendelea |
 |
| Mkapa, aksilakiwa na waziri Membe, wakati akielekea ukumbini |
 |
| Mkapa (katikati), waziri Membe, (kushoto) na balozi Rajab Gamaha |
 |
| Waziri Membe, akitoa hotuba ya kumkaribisha Rais mstaafu Mkapa, ili atoe mada yake kwa waliohudhuria muhadhara huo |
 |
| Baadhi
ya wafanyakazi wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
na wanachuo kutoka chuo cha Diplomasia, wakimsikiliza Rais Mkapa |
Posted by Ngabwe Mlulu on 07:34
 |
| Askofu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, (kushoto),
akisaidiwa na mlinzi wake, kupanda ngazi kjuingia kituo kikuu cha polisi
kati jijini Dar es Salaam mapema leo saa moja asubuhi, Aprili 9, 2015.
Gwajima aliyefika kuitikia wito wa polisi kjumalizia mahojiano dhidi
yake kufuatia kile kinachoelezwa kuwa ni kutoa maneno makali dhidi ya
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarpo Kadinali
Pengo, mwishoni mwa mwezi uliopita. Taarifa kutoka kituo kikuu cha kati
cha polisi zilizoifikia K-VIS Blog, zinasema, Gwajima alitoka kwenye
kituo hicho majira ya saa 6 mchana, na kuwaambia waandishi wa habari
kuwa, ameachiwa kwa dhamana yenye masharti kwamba, anatakiwa kuwasilisha
nyaraka zinazoonyesha muundo wa uongozi wa kanisa, kueleza umiliki wa
helikopta ya kanisa, hati za kanisa, na idadi ya makanisa aliyonayo,
majina ya bodi ya wadhamini wa kanisa, idadi ya nyumba zinazomilikiwa na
kanisa, na maelezo juu ya mpiga picha wa video wa kanisa |

No comments :
Post a Comment