Mwanachama wa mfuko wa PSPF na familia yake wakifurahia
mafao ya pensheni anayoyapata pamoja na vivutio vingine vinavyotolewa na mfuko
huo kwa wanachama wake
Christian Gaya Majira Machi 31, 2015
Hifadhi ya jamii bado inaonekana kuwa kama mkakati
mojawapo muhimu unaoweza kuchagia kupunguza umasikini na kuleta maendeleo
endelevu nchini.
Lakini kwa Tanzania ambapo
uchumi wa sekta isiyokuwa rasmi inazidi......
kuongezeka kuwa kubwa zaidi na sehemu
ambayo hata mipango ya miundo mbinu na mikakati ya kuzuia majanga ni mibovu,
hivyo kuonekana kuwa na njia ndefu kufikia huko. Umaskini unaongezeka zaidi
maeneo ya sehemu za vijijini, kwa matukio ya umaskini wa vijijini ni mkubwa
zaidi kuliko umasikini wa mjini.
Ubaguzi wa jinsia nao
unaongezeka. Ukiachana mbali na umaskini, watu ambao wanaishi na wako katika
maisha hatarishi ni jambo muhimu sana hasa unapozungumzia mambo yanahusiana na
hifadhi ya jamii. Maisha hatarishi ni maisha yapoanza kushuka kuwa chini ya
mstari wa umasikini
Mafao
taslimu yanayotolewa kwa ajili ya mfanyakazi ambaye hajiwezi kwa muda fulani
inatakiwa iwe ya kutosha lakini siyo ya juu sana ambayo yanaweza kufanya watu
baada ya kupona wasione haja ya kurudi kazini tena haraka iwezekanavyo baada ya
kurudia hali yake ya kawaida aliyokuwa nayo kabla ya kuumia
Viwango
vya uchagiaji kwa ajili ya mifuko ya hifadhi ya jamii vinatakiwa siyo tu visiwe
kama mzigo kwa wafanyakazi na waajiri lakini ni pamoja na kuhamisha hisa kwa
ajili ya vizazi vijavyo, au kutumia ruzuku za mapato ya makusanya ya serikali
kwa ajili ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watu wachache wanaopatiwa huduma ya
hifadhi ya jamii
Pamoja na mambo yote
yaliyoongelewa hapo juu, kwa watu wanaoishi chini ya msitari wa umaskini, idadi
kubwa ya watu wako katika hali hatarishi ya kuwa maskini au wanaelekea kwenye
kukutana na umasikini mkubwa na kutisha. Hata ingawa kuna hitaji kubwa, kinga
ya hifadhi ya jamii Tanzania ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watanzania
wote.
Kwa Tanzania hakuna hifadhi
ya jamii inayowalinda wananchi wote yaani inayochangiwa kutokana na makusanyo
ya kodi ya mapato ya wananchi wenyewe. Hakuna hata jitihada au mikakati ambayo
inalenga kusaidia masikini nchini ili angalau hata kuboresha utawala bora na
shughuli za sekta za umma, kuwasaidia hata kuwafundisha jinsi ya kutengeneza na
kutumia rasilimali zao za asili, kutengeneza na kuwaundia kazi za kufanya, na
jinsi ya kujiundia fursa za kujitengezea mapato, hata jinsi ya kufufua au
kuboresha mifumo ya kinga za hifadhi ya jamii zile za asili kama vile za
kifamilia, za kiukoo, na hifadhi za jamii zingine zisizo rasmi na hata
kuboresha na hata jinsi kuwafundisha njia za kufikia huduma muhimu za jamii.
Lakini pamoja na hayo kuna baadhi ya mipango ya hifadhi ya jamii inayoendeshwa
na serikali, na vile vile na hata na taasisi zisizo za kiserikali na sekta
binafsi.
Kwa sasa, mipango ya
hifadhi za jamii zilizo rasmi zaidi hushughulikia makundi ya watumishi wa
serikali, askari polisi, jeshi la wananchi, na kwa wale wanaofanya kazi kwenye
taasisi za umma na za watu binafsi. Hata hata mfuko wa pensheni wa hifadhi ya
jamii unaotoa huduma kwa watu ambao wako katika sekta ya kilimo, sekta ya
uchumi isiyokuwa rasmi na kwa wale ambao wako sekta rasmi na isiyo rasmi
wanaofanya kazi kwa mkataba, na vibarua wengi wao hawajawa wanachama wa mifuko
hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii.
Kwa vijana nguvu kazi wote
wanapunguzwa na kuondoa michango ya pensheni kabla haijakomaa kuwa pensheni
kamili. Ambalo silo lengo kamili la kuanzisha mifumo hii ya hifadhi ya jamii
kulingana na kifungu namba 102 cha ILO cha mwaka 1952.
Cha kushangaza zaidi ni
pale serikali kukubaliana na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitisha
sheria ya kutoa michango ya pensheni kabla hayajaiva na mifuko kukubaliana na
kutangaza rasmi kuwa na fao la kujitoa ambapo kulingana na mafao yanayojulikana
hapa duniani ya hifadhi ya jamii hakuna fao kama hilo la kujitoa ambalo lipo
hapa Tanzania. Kuna baadhi ya sekta zisizo rasmi, na za asili, na mipango ya
bima ya jamii. Vile vile kuna ubaguzi wa jinsia na hifadhi ya jamii ambayo
zaidi mwerekeo wake ni watu wa mjini tu
Serikali kwa miaka kadhaa
imekuwa ikitekeleza mipango ya kuhudumia jamii kwa makundi fulani fulani kwa
ajili ya kutengeneza rasilimali na fursa za kazi. Kuna mipango mingine ya
ustawi wa jamii kwa makundi. Mojawapo ya kinga za jamii ni kama vile TASAF na
baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali yaani NGOs na baadhi ya taasisi za
kimataifa zinazotoa ruzuku na misaada kwa watu maskini. Lakini bado vijana na
wazee wanakosa hifadhi hii ya jamii na kuendelea kukumbwa na maisha hatarishi
kama ya kuvamiwa na majanga kama vile matibabu, kifo, ulemavu, uzee, uzazi,
kuumia kazini, magojwa yatokanyo na kazi, kukosa kazi, na majanga ya asili.
Hifadhi za jamii zilizopo
na shughuli zao bado hazina uhusiano wa aina yeyote na zina idadi ndogo sana za
wanachama, na mafao ya pensheni zao kutokwenda na ukali wa maisha, ingawa
utofauti wa jinsi ya kukokotoa mafao ya pensheni ya muda mrefu na mafao ya muda
mfupi umerekebishwa hivi karibuni. Wakati shughuli hizi za hifadhi ya jamii zimeleta
faida kwa makundi ya watu fulani, lakini ni mara chache sana yamechangia kwenye
mikakati ya kuleta mabadiliko ili kuchangia labda lazima yaunganishwe na sera
za maendeleo. Utekelezaji wa baadhi ya sekta za uchumi hata baadhi ya mifuko ya
hifadhi ya jamii zimekuwa zikifanya vizuri zaidi.
Lakini hizo faida za
ufanisi huo wa kufanya vizuri zaidi mara nyingi umekuwa ukinufaisha watu
wachache mno ukilinganisha na idadi ya watanzania waliopo. Na haufananishwi na
kuongezekwa kwa ustawi. Hivyo ukuaji wa hifadhi ya jamii au uchumi lazima uunge
mkono wa mikakati ya kupunguza umasikini
Ni kwa bahati mbaya ya kuwa
serikali haiwezi kufanya kila kitu kwa ajili ya raia wake. Hivyo na ndio maana
kuna taasisi zisizo za kiserikali, za watu binafsi, za kidini na za hifadhi ya
jamii ambazo zina wajibu wa kushughulikia mambo kama haya kwa niaba ya serikali
kama vile Mashirika ya umma yanayotoa
pensheni yanayoendesha kwa utaratibu wa kanuni za kibima kama vile shirika la
taifa la hifadhi ya jamii NSSF, mfuko wa pensheni wa PSPF, mfuko wa mafao ya
kustaafu wa GEPF, mfuko wa pensheni wa PPF, mfuko wa pensheni wa LAPF, mfuko wa
bima ya afya wa taifa NHIF kwa Tanzania bara na bila kusahau mfuko wa hifadhi
ya jamii wa Zanzibar ZSSF kwa upande wa Tanzania visiwani.
Musabila Nyanda ambaye ni
mfanyakazi wa wizara ya kilimo makao makuu ni mwanachama hai wa mfuko wa
pensheni wa PSPF anasema mwaka jana alipata mkopo kwa ajili ya kukabarabati
makazi yake. “Kwa vile nategemea
kustaafu mwakani niliona nafuu nikianza kujiandaa kustaafu kwa kuomba mkopo wa
nyumba toka PSPF ambapo mimi ni mwanachama wa mfuko huu tangia ulipoanzishwa
mwaka 1999.” Musabila Nyanda anasema.
Anasema tangia alipoomba
mkopo huo wa kukarabati nyumba yake ilichukua wiki tano tu “Baada ya kufungua maombi
yangu ya nyumba baada ya wiki ya tatu nilifika ofisi ya PSPF kuwauliza kama
tayari, niliambiwa baada ya wiki mbili watanitaarifu na kweli baada ya wiki
mbili nilipigiwa simu ya kuwa mkopo wangu upo tayari” anasema Musabila
Anasema mpaka sasa ameweza
kukarabati nyumba yake, na ziada ya pesa ya mkopo iliyobaki anasema ameweza
kununulia shamba na kuanzishia biashara yake ambayo mpaka sasa inaendelea
vizuri.
Mkopo huu umenisaidia
kuanza kuandaa kujipanga vizuri kwa ajili ya kustaafu kwa sababu mwisho wa
mwaka ujao nategemea kustaafu kwa maana hiyo mafao yangu nitakayopata
hayatetereke hata kidogo na wala sitakuwa na msongo wa akili kuhusiana na maisha yangu
baada ya kuataafu. “Nimeanza kufanya mazoezi
ya kustaafu kabla kwa kuanza ujasiriamali na kuandaa makazi yangu ya kudumu”
Nyanda anasema
Mfuko wa PSPF unatoa mikopo
ya nyumba kwa ajili ya makazi kwa wanachama wake pamoja na mikopo ya pensheni
kwa wale waliostaafu kwa masharti nafuu. Na mkopo huo wa nyumba unatolewa kwa
wanachama wake baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 5 tu. Na mkopo wa
nyumba zilizojengwa na mfuko wa pensheni
wa PSPF unaweza kurejeshwa hadi kwa muda wa miaka 25 Lengo la mkopo ni
kumwezesha wanachama kupata nyumba ambazo zimejegwa na mfuko ili kumhakikishia
mwanachama kuwa na uhakika wa makazi yake wakati anapoendelea kufanya kazi na
baada ya kustaafu. “Mkopo
kwa mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya miaka mitano ambapo atatakiwa kulipia kiasi cha shilingi
milioni tano za kitanzania kama malipo ya mwanzo ya nyumba na kiasi kilichobaki
anaweza kurejesha hadi muda wa miaka 25. Mwanachama anaweza kununua nyumba
kupitia akaunti ya mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa
umiliki.
Mfuko
huu wa PSPF ni mfuko pekee unaotoa mkopo wa fedha taslimu kwa mwanachama
aliyebakiza miaka 5 kustaafu kwa lazima kwa ajili ya kujenga, kukarabati na
kununua nyumba ya makazi popote anapotaka hapa Tanzania, ili kuandaa makazi
mazuri mara tu anapostaafu. Na mikopo hii ya pensheni ya kila mwezi huwa
inatolewa bila kutozwa riba ambapo mstaafu au mtegemezi ataweza kukopa hadi
pensheni ya miezi kumi na miwili bila hata kutozwa riba hata kidogo.
Nyanda
anawashauri wanachama wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii kutoondoa mafao yao
kabla ya muda wake ili waje wanufaike na mafao ya muda mrefu na mafao ya muda
mfupi ikiwa ni pamoja na baadhi ya vivutio mbalimbali vinavyotolewa na mifuko
hii ya hifadhi ya jamii nchini pamoja na fursa mbalimbali kama hizi anazozitumia
Nyanda kwa sasa kwa sababu mpaka sasa hana wasiwasi na kustaafu mwakani. “Najisikia
kuwa na faraja kubwa sana kuzitumia fursa hizi za mikopo zenye riba nafuu kwa
wanachama na wastaafu wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii nchini” Nyanda
anasema.
Anawakumbusha wanachama na wastaafu sehemu za kuwekeza mafao yao ya
pensheni kabla ya kupata ushauri wa jinsi ya kuwekeza na badala yake
kutumbukiza mafao yote ndani ya shimo refu
No comments :
Post a Comment