RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKAGUA NA KUWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko
kutoka katika nyumba za watu katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya
ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma
Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari
za mafuriko na kuwafariji wananchi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni
Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji
ya mafuriko wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi
mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na
kuwafariji wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha
mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es
Salaam leo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Buguruni Mnyamani
waloathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia wananchi hao
Rais
Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya
Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko
Buguruni Mnyamani leo.
( Picha na Freddy Maro )
No comments :
Post a Comment