Saturday, July 26, 2014

PPF na MSD waingia mkataba wa mpango wa WEKEZA kwa hiari

Wafanyakazi zaidi ya 400 MSD kuwa wanachama wa PPF kwa mpango wa hiari 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, wakiweka saini mkataba wa “wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014. Chini ya Mkataba huo, zaidi wa wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na PPF, 
 
Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama, mmoja wa wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa Nchini, (MSD), baada ya Mfuko huo kutiliana saini mkataba wa kuanzishwa kwa mpango wa "Wekeza" ambapo zaidi ya wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na mpango huo katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam, Jumatano Julai 23, 2014

Viongozi wa MSD na wenzao wa PPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa MSD ambao wamejiunga rasmi na mpango huo wa "Wekeza"

Mameneja wa PPF

Baadhi ya wafanyakazi wa MSD waliohudhuria hafla hiyo

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, baada ya kusaini mkataba wa mpango wa “Wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, akizungumza wakati wa hafla hiyo

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza kwenye hafla hiyo

Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate Mpuya, (Kulia) na Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko huo, Asumpta Malya, wakiteta jambo

Mkurugenzi wa Operesheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama mmoja kati ya wafanyakazi zaidi ya 400 wa MSD, waliojiunga na mpango huo

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), akimkabidhi cheti cha usajili, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, baada ya Mfuko huo kusaini mkataba na MSD wa mpango wa wekeza, kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD Kerko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), akimkabidhi cheti cha usajili, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, baada ya Mfuko huo kusaini mkataba na MSD wa mpango wa wekeza, kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD Kerko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014.
  
Matukio ya hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akiwahutubia wafanyakazi wake, wakati wa futari iliyoandaliwa na ofisi yake kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 21, 2014

Bwana Erio(Mwenye balaghashia),  na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko huo wakishiriki futari hiyo







No comments :

Post a Comment