Baadhi
ya wazee wastaafu wakihojiwa na waandishi habari hawapo pichani picha na
mitandao
Na Christian Gaya Majira Juni 24, 2014
Kadiri tunavyo kuwa
wazee tunafanya kazi, tunazalisha na kipato chetu kinazidi kuwa kidogo zaidi na
hivyo basi tunahitaji kupata kipato kutoka sehemu nyingine ili kuhakikisha ya
kuwa tunaendeleza maisha yetu. Jamii na serikali mbalimbali za hapa Afrika na
za huku ulaya ikiwemo nchi yetu ya Tanzania wameweza kuwa na vyombo mbalimbali
kwa ajili kuwapa kinga kwa njia ya kuwapa kipato fulani kwa raia wake
wanapofikia hali ya uzeeni kama sehemu ya kinga kwa ajili ya kupunguza
umasikini kwa watu wastaafu na watu wengine waliofikia umri wa uzee ambayo ni
kuanzia miaka sitini kwa mtanzania.
Lakini mipango hii
inatugusa sisi wote kwani haijalishi kwa sasa wewe in tajiri au maskini, halijalishi wewe ni mtoto au mtu mzima au una
umri wa miaka mingapi kwa sasa mipango hii iiliyoiridhiwa inaweza kusaidia
malengo hayo au ikawa ndiyo kizuizi cha kukua kwa maendeleo ya uchumi na
kijamii nchini
Ikumbukwe ya kuwa idadi
ya watu wanaofikia umri wa uzee inavyozidi kuongozeka kila siku, kinga ya
hifadhi ya jamii ya wazee nayo inazidi kuingia kwenye matatizo zaidi. Kwa
sababu sekta isiyo rasmi ya kijamii na mfumo wa hifadhi ya jamii unaotolewa na
familia unazidi kupungua na kuwa dhaifu siku hadi siku. Na mfumo wa hifadhi ya
jamii ulio rasmi kama vile unaotolewa na taasisi hizi zetu za hifadhi ya jamii
za kuchangia na zile zisizo za kuchangia zinakabiriliwa na utumiaji ovyo wa
michango ya wanachama kwa kuwekeza kwa kufuata maangizo ya wanasiasa bila
kutumia vitego vya kitaalamu na kuwa na matumizi makubwa ya michango ya
pensheni za wanachama bila vile vile bila ya kufuata kanuni na utaratibu wa
uwekezaji michango ya pensheni ya wanachama.
Kwa ujumla ni kwamba
mifuko haina utaratibu wa kufuata utawala bora wa jinsi ya kuendesha taasisi
hizi za hifadhi ya jamii, na matokeo yake idadi kubwa ya wazee ambao wamekuwa
wakichangia katika kujenga taifa hili kwa muda mrefu hawana hata kinga ya uzee
yaani kupatiwa mafao ya kustaafu ya kutosheleza mahitaji muhimu ya maisha yao
ya kila siku. Wakati huo huo utaratibu
wa undeshaji wa mifuko ya jamii unaendelea kuwa uleule wa zamani badala kuja na
mikakati ya kisayansi ili kuleta mabadiliko ya kisasa ya jinsi ya kuendesha
mifuko hii ya hifadhi ya jamii. Cha kushangaza ni kuwa hakuna mfuko wa hifadhi
ya jamii unaotoa maelezo halisi ya mwenendo wa hifadhi ya jamii. Leo ukidadisi
juu ya idadi ya wazee wanaopata pensheni kila mwezi ni idadi ndogo sana
ukilinganisha na idadi ya wazee wanaostaafu kila siku.
Hii ina maana ya kuwa
wengi wanaishia kuondoa mafao yao au kwa njia halali au ya udanganyifu na hii
inawezekana kufanywa kwa makusudi au kwa mwoga wa taasisi hizi kwa lengo la
kukwepa kusimamia mafao haya ya uzee. Matokeo yake ni kwamba idadi ya wastaafu
inazidi kupungua kila siku na wakati huo huo umaskini unazidi kuingia kwa kasi kwa wazee.
Kwa mwaka 1990 nusu ya
bilioni ya watu ambao ni kama zaidi ya asilimia tisa (9) ya watu wote
duniani walikuwa zaidi ya umri wa miaka
60. Na inakisiwa ya kuwa kufikia mwaka 2030, idadi hiyo itaongezeka mara tatu
(3) mpaka kufikia bilioni 1.4. na haya mabadiliko ya kuongezeka yatatokea kwa
nchi zinazoendelea ikiwemo nchi yetu Tanzania, ingawa zaidi ya nusu ya ongezeko
hili itatokea nchi za Asia na zaidi ya robo itatokea huko China.
Na ikumbukwe ya kuwa
mahitaji ya bima ya afya yanaongezeka zaidi pale nchi inapozidi kuwa na idadi
kubwa wa wazee, kama unavyojua kuwa matatizo ya ugonjwa kwa umri wa uzee na
teknolojia ya matibabu mara nyingi inafikiriwa kutumika zaidi kwa ajili ya
kupambana na wazee zaidi. Na wakati huo
huo mifuko hii ya hifadhi ya jamii fedha ambazo zinatakiwa kuweka na kuwekeza
pembeni kwa ajili ya wazee watakao
staafu mara nyingi zimelalamikiwa kutumika ovyo kwa kukosa uongozi na utawala
wa bora wa mifuko ya hifadhi ya jamii kama ilivyoelezwa hapa juu. Kwa mfano
inaonesha ya kuwa idadi kubwa ya michango ya pensheni iliwekezwa kwenye hatifungani
na hivyo kupoteza kiwango kikubwa cha fedha za michango kwa mwaka.
Na karibu idadi kubwa
ya michango ya pensheni inayokusanywa inaonesha kutumika kwa ajili ya
kuendeshea gharama za mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Pamoja na hayo
karibu pensheni zote zinazotolewa mara chache sana zinafanyiwa marekebisho
kulingana na mfumuko wa maisha ya kila siku kwa kurekebisha kwa kwa sababu
labda mshahara kuongezeka au kurekebisha kufuatana na mfumuko wa bei ya bidhaa
au huduma mstaafu anazonunua sokoni.
Kwa hiyo ni kinga ndogo
au hakuna kabisa kinga yeyote inayotolewa kwa wazee hawa waliostaafu. Na
serikali inaweka bajeti kubwa sana kwa kuwalipa pensheni kubwa kwa wanasiasa na
baadhi ya viongozi wa ngazi za juu ambao wao hawachangii hata kidogo katika mapato yao ya mishahara minono
wanayopata na hivyo kubebesha mzigo mkubwa kwa serikali kwa kutumia kodi za
wananchi wanazotozwa badala ya kuwaboreshea huduma za kijamii na kiuchumi nchini. Ingawa serikali imepanga kuwalipa
wazee kiasi cha shilingi elfu kumi kwa wazee wote watakaokuwa wanafikia umri wa
miaka 60 na kuendelea, kwa maana hii serikali inahitaji kuliangalia sana jambo
hili kiundani ili kuleta usawa katika kugawana sawa mapato ya taifa bila
ubaguzi wowote na kuibebesha serikali mzigo mkubwa. Kwa sababu unaweza ukakuta
baadaye ukawaambiwa pensheni ya wazee ya shilingi elfu kumi inapunguzwa kwa
sababu serikali haina fedha za kutosha kwa ajili ya wazee ambao kila siku idadi
ya watanzania wengi wanafikisha umri wa kustaafu wa miaka sitini (60)
inaongezeka. Lakini pamoja na hayo mipango ya kuwapatia kiwango hicho kidogo
mpaka leo haijaanza kutekelezwa tangia itangazwe.
Utafiti wa kuwianisha
mapato kwa kuhakikisha ya kuwa mapato ya makusanyo ya taifa kutoka watu wenye
uwezo zaidi na kuyagawanya upya kwa watu wenye pato la chini yaani maskini, na
wakati huo huo lazima ijulikane ya kuwa watu wenye uwezo au matajiri huishi
miaka mingi zaidi kuliko watu maskini
yaani wenye pato la chini kabisa na hivyo hao matajiri au wenye uwezo
wakifikia umri wa kustaafu na kuanza kupata pensheni hupata kwa muda mrefu zaidi
ukilinganisha na masikini
Lakini ikumbukwe kuwa mfumo wa mifuko ya pensheni hapa nchini ina matatizo na changamoto nyingi mno kama vile utaratibu wa kuhamisha michango kutoka mfuko mmoja hadi mfuko mwingine pale mfanya kazi anapopata mwajili mwingine badala yake michango yote ya pensheni za wafanyakazi huishia kuiondoa kabla haijaiva na hivyo kuishia kuiondoa kabla haijaiva na hivyo kuishia kupunguza idadi ya michango ya mwanachama na baadae anapostaafu anaishiwa kuambiwa kuwa michango yake haitoshi kumpatia pensheni ya kila mwezi na kwa upande mwingine ni kwamba kunatofauti kubwa sana kwa upande wa idadi ya mafao yanayotolewa kulingana na idara ya 102 ya 1952 la shirika la kazi duniani ambalo lenyewe limeainisha mafao tisa kama vile fao la pensheni ya uzee,pensheni ya ulemavu ,pensheni ya urithi ambayo ni mafao ya mda mrefu na mda mfupi ni kama vile ;fao la matibabu ,fao la kuumia kazini ,fao la msaada wa mazishi,fao la uzazi, fao la kutokuwa na kazi na la mwisho ni fao la msaada kutunza kupunguza ukali wa utunzaji wa watoto. Na badala yake mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii inaishia kujumuisha pamoja na baadhi ya vivutio kwa wateja wao na kuitwa kama mafao jambo ambalo siyo kulingana na idara namba 102 ya mwaka 1952 ya ILO
Na kumekuwa na tofauti kubwa na hata kwa upande wa fomula za ukokotoaji wa mafao, kwani kila mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii ina fomula yake badala ya kutumia fomula zilizoainishwa na shirika la kazi duniani (ILO)kila mfuko unajitungia fomula zake za ukokotoaji. Ambayo inapelekea hata kuleta tofauti kubwa za pensheni wanazopata wastaafu madhalani unakuta katibu muhitasani anapata pensheni kubwa zaidi kulikomstaafu aliekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni nyingine .wakati huohuo ni asilimia 6 tu ya nguvukazi ndio wanachama wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii.hivyo asilimia karbu 94 ya nguvu kazi hawana kinga ya hifadhi ya jamii.
Ingawa mdhibiti na
msimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii anasema amesha fanyia kazi tayari na
anasubiri maamuzi ya mwisho kutoka katika baraza la mawaziri kuamua utaratibu
wa kuwa kutoka na fomula moja ya kukokotoa mafao kwa mifuko yote hapa nchini
Tanzania bara
Mara nyingi ushirikishwaji wadau katika mifuko hii umekuwa kidogo sana kama siyo hakuna kabisa katika maamuzi ya fedha zao za michango ambalo ni swala la utawala bora wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii.
Hivyo kwa kukosa
utawala bora umepelekea mara nyingi kuleta gharama kubwa za uendeshaji wa
mifuko na hasa kuwekeza bila hata kufuata kanuni za uwekezaji na mara nyingine
bila hata na malengo dhabiti ya
uwekezaji na kuishia kuwekeza kwenye maeneo yasiokuwa na tija hata kidogo. Na
mwisho wa siku matatizo yote haya huishia kwa mchangiaji ambaye ndiye
mwanachama kupatiwa pensheni hafifu na kupelekea kuzidisha janga la umaskini
kila siku
Pensheni ni haki ya kila mtu hasa mwananchi yoyote awe anachangia au asichangie na hii inajulikana wazi na ndiyo maana hata katika idara ya 11 ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na sera ya taifa ya hifadhi ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003 inajieleza wazi na vilevile imeanishwa kwenye katiba wa shirika la kazi duniani ILO idara ya 102 ya mwaka 1952 na kwenye katiba ya kimataifa na haki za kibinaadamu ya mwaka 1948.
Na lengo kubwa la
hifadhi ya jamii ni kuzuia umasikini, kupunguza au kuondoa umasikini, kuifidia
jamii, kugawanya mapato sawasawa kwa wanajamii. Masuala mengi yanayogusa
hifadhi ya jamii ni ya nyeti sana, yanagusa ni kiini muhimu sana cha
wafanyakazi kwenye sekta rasmi na sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini
pamoja na sekta ya bima za jumuiya za waajiri
No comments :
Post a Comment