Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Batilda-Salha Burian akisaini kitabu
cha wageni kwenye banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
kwenye maonyesho ya Kikanda ya Wajasiriamali maarufu Jua
Kali/Nguvukazi, jijini Nairobi juzi. Na Mpigapicha Wetu.
Na Mwandishi wetu, Morogoro
Kwa ufupi
Wakati kampuni imetangaza kupata zabuni ya kusambaza
mkonge tani 500 kwa mwezi nchini China, hivyo kukuza pato lao,
wafanyakazi wanalalamikia wanacholipwa (Sh1,540 za chakula, Sh 4,460)
kwa siku ni kidogo.
Tanzania ni moja ya nchi barani Afrika
inayotegemea kilimo kuinua uchumi wake. Hata hivyo, kutokana na kuwapo
viwanda vichache na kutokuwapo soko la uhakika nchini, watu wengi hawana
ajira na hata waliofanikiwa kuajiriwa au vibarua nao wamekuwa
wakipunguzwa.
Kampuni ya China State Farms Agribusiness (G)
Corporation Tanzania Limited ambayo ipo Rudewa wilayani Kilosa, Mkoa wa
Morogoro, inalima mkonge katika mashamba mawili; moja la Rudewa lenye
ekari 6,351 na Kisangata lenye ekari 7,202.
Kampuni hiyo inauza mkonge nchini na nje ya nchi,
mwaka 2013 uzalishaji ulianza kushuka na kampuni kulazimika kupunguza
wafanyakazi kutoka 740 waliokuwa wameajiriwa kukata mkonge na kubaki
442.
Mwaka huu huenda mambo yakawa mazuri kwani soko la
China linahitaji tani 500 za mkonge kwa mwezi kutoka kwenye kampuni
hiyo jambo ambalo ni neema kwa wafanyakazi na vibarua.
Kampuni hiyo inauza mkonge katika masoko ya China,
Saudi Arabia, Kenya na soko la ndani nchini na mwaka 2013 iliuza tani
2,353 kwa Sh4.8 bilioni, mwaka 2012 tani 2,220 na kupata Sh4.6 bilioni
na iliingiza Sh4 bilioni mwaka 2011 baada ya kuuza tani 1,560.
Uuzaji wa mkonge kwenye masoko ya ndani na nje ya
nchi unapitia kwenye mchakato wa aina mbalimbali kuanzia kukata, kupakia
kwenye matrekta na kukamuliwa kwenye mashine za korona na kutoa
nyuzinyuzi ambazo zinaanikwa.
“Baada ya singa (nyuzinyuzi) kukauka, zinapelekwa
kiwandani ambako zinasafishwa na kuzitenga katika gredi mbalimbali na
kufungwa katika marobota tayari kwa kuuza,” anasema Msimamizi wa Kitengo
cha Uzalishaji wa kampuni hiyo, Mokiwa Kilenja.
Wafanyakazi, vibarua wanasemaje
Msimamizi wa Idara ya Kukata Mkonge kwenye shamba
la Rudewa, Said Mseja anasema kazi hiyo inamsaidia kupata mahitaji
mbalimbali kwa ajili ya familia yake na zaidi anaishauri kampuni hiyo
kusafisha mashamba yake ya mkonge kwa kuwa yana majani mengi na hivyo
kusababisha ukataji kuwa mgumu.
“Mashamba ni machafu, jambo lingine wakataji na
wanaobeba mkonge kupeleka kiwandani wamepunguzwa na kubaki 100 tu kutoka
wafanyakazi 200 kutokana na uzalishaji kuwa mdogo mwaka jana,” anaeleza
Mseja.
Vilevile Mseja anasema vitendea kazi ni vichache,
lakini kubwa zaidi wamekuwa wakikodishwa mabuti kwa ajili ya kufanyia
kazi jambo ambalo Mkurungezi Mtendaji wa kampuni hiyo Guan Shanyuan
anabainisha kuwa wanalazimika kuwakodishia baadhi ya vifaa kwa kuwa
wanauza licha ya awali kupewa bure.
“Tulikuwa tukiwapatia vifaa bure, lakini baadaye
tuligundua walikuwa wanauza, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao,”
anasema Shanyuan.
No comments :
Post a Comment