Mmojawapo wa wafanyakazi wa nyumbani ambao hawana hifadhi ya jamii ya aina yeyote au akiba
ili kulipa bili za matibabu. Ambapo utafiti unaonesha wafanyakazi wengi wa
ndani hawajui haki zao, hivyo hawawezi kudai ulinzi au haki zao kutoka kwa
waajiri wao kama vile kuandikishwa na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii.
Na Christian Gaya majira Januari 28, 2014
Tanzania zikiwemo
Brazil na nchi kadhaa, zimeanza kuwahusisha wafanyakazi wa majumbani katika
sheria za kazi ili kuwapatia kinga au haki za msingi kama vile likizo ya uzazi,
likizo ya ugonjwa na ruzuku ya serikali pindi wanapokuwa hawana kazi.
Hata hivyo, inaweza
kuwa vigumu sana kutekeleza sheria hii katika nchi yetu ambayo wasimamiaji wa
sheria za kazi hawana vitendea kazi au rasilimali za kutosha za kufanyia kazi
zao na mifumo ya taarifa/habari ni duni. Aidha, wafanyakazi wengi wa ndani
hawajui haki zao, hivyo hawawezi kudai ulinzi au haki zao kutoka kwa waajiri
wao kama vile kuandikishwa na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii.
Mapato ya chini na
ukosefu wa ulinzi au uzingatiwaji wa haki unamaanisha kwamba wafanyakazi wa
majumbani wapo katika mazingira magumu na hivyo hatarishi kwa maisha yao.
Endapo itatokea wakaugua au kuumia na hivyo kushindwa kuja kazini, wanaweza
kupoteza mishahara au ujira wao au kufukuzwa kazi. Wanaweza kuwa hawana hifadhi
ya jamii ya aina yeyote au akiba ili kulipa bili za matibabu au kuwafanya
waendelee na maisha mpaka watakapopata kazi mpya. Hali hii inaweza kuonekana
isiyo ya haki kabisa hususani kwa wafanyakazi ambao awali ya yote, chanzo cha
ugonjwa au kuumia ni hiyo kazi yenyewe.
Wamiliki wa nyumba
ambapo wafanyakazi wa majumbani wanafanyia kazi zao wanaweza kufikiri nyumba
zao ni maeneo salama, lakini nyumba hizo hizo zinaweza kuwasilisha matatizo
kadhaa ya kiafya na ki-usalama kwa watu wanaofanya kazi ndani mwake. Utafiti
uliofanywa nchini Salvador na Brazil, kwa mfano, uligundua kwamba wanawake
wanaofanya kazi za majumbani wanakabiliana na viwango vya juu vya kuumia kuliko
wanawake wanaofanya kazi zingine (Santana et al. 2003).
Wafanyakazi wa
majumbani wanatambua kwamba kazi zao zinaweza kuwa hatari kwa afya zao. Utafiti
uliofanywa huko California ulionesha karibu wafanyakazi wawili kati ya watatu
wa majumbani walioshiriki wanachukulia kazi zao kuwa “zenye hatari/hatarishi”
(Smith 2001). Taratibu au sheria za Afya na Usalama katika Maeneo ya Kazi yaani
Occupational safety and health (OSH), ambazo zimelenga katika kuzuia hatari za
kuumia au kupata ugonjwa katika sehemu za kazi, mara nyingi zimeonekana
kuwalinda wafanyakazi rasmi waliopo katika mazingira rasmi ya kazi kama vile
migodini, viwandani, ofisini na madukani ingawa bado kiwango kinachotakiwa
hakijafikiwa.
Kanuni hizi
haziwalindi wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika nyumba binafsi, kitu
ambacho kinamaanisha kwamba japokuwa kazi za nyumbani ni chanzo muhimu cha
ajira, na ingawa kuna hatari nyingi za kiafya na kiusalama katika kazi hizo, na
japokuwa wafanyakazi wa majumbani wapo katika mazingira magumu ya umasikini
endapo wataugua au kuumia, taratibu au sheria za OSH katika nchi yetu hii
haziwazingatii.
Nchini Tanzania
watafiti pia mara nyingi wanatumia njia au mbinu inayoitwa “orodha ya kukagulia
afya” yaani health checklist. Tatizo ni kwamba mara nyingi watu huwa wanasita
kuongelea juu ya miili yao na matatizo ya kiafya wakiwa wanahojiwa na kundi la
watu ambao hawawajui vizuri. Utafiti juu ya Afya na Usalama Katika Maeneo ya
Kazi (OSH) na wafanyakazi wa majumbani unatakiwa kufanyika na mara nyingi
unakuwa na malengo makuu mawili. Lengo la kwanza unakuwa kuelewa matatizo ya
kiafya na kiusalama ambayo wafanyakazi wa majumbani wenyewe wanayapa
kipaumbele. Wafanyakazi wa majumbani wanajua vizuri zaidi juu ya matatizo
wanayokabiliana nayo wao ni wataalamu wa hali ya juu kuhusu mazingira yao ya
kazi, na katika mradi wowote unaojaribu kuelewa mazingira hayo, ni muhimu kwa
kuanza kwa kuzungumza na wafanyakazi wenyewe. Lengo la pili inatakiwa kujua
zaidi kuhusu sheria/taratibu za OSHA nchini Tanzania na kuona ni aina gani ya
mwingiliano wafanyakazi wa majumbani wanao na mamlaka za nchi katika maeneo ya
afya na usalama.
Kwa mfano hapa
nchini, utafiti ulifanywa mwishoni mwa mwaka 2010, na mwishoni mwa mwaka 2009
nchini Brazil. Katika nchi zote mbili, watafiti walitumia mbinu au njia ya
kundi/makundi kwa nia ya kupata muelekeo au muongozo yaani focus group ambapo
makundi ya wafanyakazi walikusanyika pamoja kwa ajili ya mahojiano. Nchini
Brazil watafiti walifanya kazi kupitia Sindoméstico, umoja wa
wafanyakazi wa majumbani. Nchini Tanzania, watafiti walifanya kazi na Chama Cha
Wafanyakazi wa Mahotelini na Majumbani (CHODAWU), umoja ambao pia unaratibu
wafanyakazi wa majumbani. Kwa ujumla wafanyakazi saba wa majumbani walishiriki
katika utafiti nchini Brazil, na 20 walishiriki nchini Tanzania. Wafanyakazi
wote nchini Brazil walikuwa wanawake na nchini Tanzania, 18 kati ya 20 miongoni
mwa washiriki walikuwa wanawake.
Taarifa inasema
nchini Tanzania, walitumia njia kadhaa za kuvutia au kupendeza katika kukusanya
taarifa kutoka kwa wafanyakazi. Njia ya kwanza miongoni mwa mbinu/njia hizo
iliitwa “kadi za hatari” ambazo ni karatasi au kadi zinazong’aa zenye ukubwa
kama nusu karatasi na zenye picha na maneno yenye kuelezea hatari au athari
mbalimbali za kiafya na kiusalama. Kadi hizi zinatawanywa na kisha washiriki
wanaulizwa kama wangependa kuongeza au kuweka kadi hizo katika fungu fulani.
Mara baada ya washiriki kuongeza kadi yoyote ya ziada katika fungu fulani,
wanaulizwa au kutakiwa kuziweka katika kiwango au daraja fulani kutokana na
jinsi wanavyoona lilivyo tatizo linaloonekana au kuoneshwa kwenye kadi. Kiwango
au viwango vya mwisho kwa kadi hizi ni muhimu, lakini pia kilicho muhimu zaidi
ni jinsi ambavyo zoezi hili linawatia moyo washiriki katika mdahalo na
majadiliano yatokanayo na zoezi hili.
Ili kupata ufumbuzi
wa tatizo hili, baadhi ya watafiti walitumia kitu kinachojulikana kama “ramani
ya mwili”, ambapo wafanyakazi wanatakiwa kuchora mfano wa miili yao na kisha
kuonyesha magonjwa yao na majeraha katika mchoro. Umoja wa wakusanya takataka
unaoitwa Kagad Kach Patra Kashtakari Panchayat (KKPKP) huko Pune, India,
wametumia mbinu hii kwa ufanisi sana katika utafiti wao.
Orodha ya kukagulia
afya ni njia nyingine ya kuhamasisha washiriki katika mjadala wa pamoja
kuongelea kuhusu matatizo ya kiafya wanayokumbana nayo kutokana na kazi zao
bila kuongelea sana kuhusu matatizo yao binafsi. Maeneo rasmi ya kazi mara
nyingi huweka orodha ya kukagulia afya, ambazo ni fomu zinazoorodhesha matatizo
ya kawaida ya majeraha na magonjwa ambayo hutokea katika eneo la kazi. Ikitokea
kwamba wafanyakazi wanaugua au kuumia, hutoa ripoti juu ya tukio hilo katika
sehemu zao za kazi na hurekodiwa au kuandikwa katika orodha ya kukagulia afya.
Hii ina maana kwamba
viwango vya ugonjwa na kuumia katika sehemu ya kazi hufuatiliwa kwa makini na
endapo itatokea kwamba watu wengi wanaugua au kuumia katika sehemu fulani ya
kazi, vyama vya wafanyakazi au serikali inaweza kuingilia kati. Wakati wa
uchunguzi katika makundi nchini Tanzania, watafiti walielezea dhana ya orodha
rasmi ya kukagulia afya mahali pa kazi kwa washiriki, ambao baadaye walitakiwa
kutengeneza orodha za kukagulia afya ambazo zitawasilisha matatizo ya kawaida
ya kiafya maalum kwa wafanyakazi wa ndani. Njia hii pia inahimiza majadiliano ya kutosha
katika kundi au makundi kwa ajili ya kutafuta mwelekeo au muongozo. Taarifa za matokeo ya utafiti juu ya afya
na usalama, mazingira mengine ya kazi na mahusiano na mamlaka mbalimbali
kuhusiana na afya na usalama zinasema nchini Brazil, wafanyakazi wa ndani
walisema matusi na udhalilishaji wanaokumbana nao katika sehemu zao za kazi
unawakilisha matatizo yao ya msingi ya kiafya na kiusalama.
Walisema wanahisi
kama wanachukuliwa kama watumwa, ambao wametengenezwa kufanya kazi za
kiudhalilishaji, na mara nyingi wameonyeshwa kutoheshimiwa kama binadamu na
waajiri wao. Kama dondoo ifuatayo inavyoonyesha, matusi na udhalilishaji
umewaacha wakiwa na hisia za kutojithamini kabisa na hisia kwamba kazi
wanayofanya haina maana wala thamani:
“[Matatizo makubwa ni] kuitwa
majina yasiyofaa, kufedheheshwa na kusimama kwa
vipindi au muda mrefu. Niliwahi kufanya kazi katika nyumba fulani
ambapo niliruhusiwa kuketi wakati wa kula tu. Endapo ningekaa chini kupumzika
kungetokea ugomvi au malalamiko, ilikupasa uwe umesimama muda wote, hakuna
ambaye aliweza kukaa katika nyumba yake
“... wanamnyonya msaidizi wao
wa nyumbani kwa kumfanya amhudumie mbwa wao pia, kwa kumuogesha. Sidhani kama
kuhudumia wanyama ni sehemu ya kazi za nyumbani... “ “Inatubidi tufanye vitu
ambavyo hatuna hata fununu ya jinsi ya kuvifanya, ambavyo hatujawahi kujifunza
jinsi ya kuvifanya, jinsi ya kuziba ukuta au jinsi ya kusafisha tanki la maji,
lakini tunalazimishwa kufanya vitu hivi na hii ni aina ya vurugu.“
Katika moja ya
makundi nchini Tanzania, wafanyakazi waliuchukulia unyanyasaji wa kijinsia kama
tatizo muhimu zaidi la kiafya na kiusalama linalowakabili. Mwanamke mmoja
alihusisha kisa cha jinsi alivyotoroka kutoka katika hali kama hiyo:
“Nilikuwa nimeajiriwa na mwajiri fulani katika mkoa wa Iringa kwa
takribani miaka 3...
nilikuwa na tatizo kubwa la unyanyasaji wa kijinsia ambapo baba na mwana walijaribu
kunishinikiza niwe na mahusiano ya kimapenzi nao, lakini mimi nikakataa!
Nilichokifanya, niliamua kumwambia jirani. Jirani akaniambia ni bora
kutoroka; akanisaidia kupata kazi Dar-es-salaam kwa ndugu yake. Ilikuwa ni kitu
cha hatari sana kwangu mimi nilipoamua
kutoroka bila hata ya kuwaambia wazazi
wangu ambao wanaishi Iringa vijijini...sifanyi kazi tena na mwajiri yule. Kitu
kibaya ni kwamba bado wazazi wangu wanafikiri nafanya kazi Iringa, kwa sababu
siwezi kuwasiliana nao.“
Usanisi wa Matokeo
ya Utafiti kutoka Brazil na Tanzania Ukosefu wa vifaa vya kujikinga pia ni
tatizo wakati wafanyakazi wa ndani wanapowahudumia wanafamilia ambao
wanaumwa-hususani kama wanaoumwa wana magonjwa yanayoambukiza kama vile VVU/
UKIMWI na/au TB. Matatizo mengine muhimu ambayo yalitajwa ni pamoja na kubeba
vitu vizito na kulazimishwa kupanda hadi mahali pa juu. Wafanyakazi wa
majumbani wa Tanzania walikusanya pamoja orodha ya kukagulia afya kwa
wafanyakazi wa ndani ambavyo inaonesha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayotokana
na hatari zilizotajwa hapo juu:
Hapa Tanzania
inaonesha wazi kwamba wafanyakazi wengi wa majumbani hawana habari juu ya haki
zao kuhusiana na masuala ya afya na usalama.Tatizo hili lipo kwa sababu
wafanyakazi wengi wa majumbani wanatokea katika mazingira ya kimasikini, mara
nyingi wana elimu kidogo, na wanatengwa kutoka katika makundi ya mengine ya
wafanyakazi. Hii inamaanisha kwamba, kwa pamoja, serikali na mashirika ya
wafanyakazi wa majumbani wanahitaji kufanya jitihada za makusudi kuwaelimisha
wafanyakazi wa majumbani kuhusu haki zao na kuhakikisha haki hizi
zinazingatiwa. inaendelea wiki ijayo.
No comments :
Post a Comment