Thursday, October 10, 2013

Mgimwa aipongeza PPF kutimiza miaka 35 ya mafanikio


 
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Dkt. Makongoro Mahanga (wa tatu kulia), na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mh. Zitto Kabwe wakitazama nembo mpya ya
Mfuko wa Pensheni wa PPF mara baada ya kuzinduliwa mwanzoni mwa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha.

Waziri wa fedha  Dkt. Mgimwa akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya serikali ya Tanzania alianza kwa kuwakaribisha washiriki wote kwenye mkutano wa 23 wa mwaka wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Dkt.Mgimwa aliupongeza Mfuko huo) kwa kutimiza miaka 35 tangu kuanzishwa kwake,ambapo alisema hatua hiyo ni mafanikio makubwa siyo tu kwa kutimiza miaka hiyo, lakini pia kwa kutimiza mafanikio ya utendaji.

Alipongeza mfuko huo kukua mwaka hadi mwaka kama taarifa za Mfuko za kila mwaka zinavyoonyesha kama vile mtaji wa mfuko kuanza na milioni 50 kwa mwaka 1992  mpaka kufikia trilioni 1.09 mwishoni mwaka  2012 ambapo mpaka mwaka kufikia mwisho wa mwaka 2013 mfuko unategemea kuwa na mtaji wa trilioni 1.3.

Mfuko wa Pensheni wa PPF ulianzishwa Julai 1978 kwa sheria Namba 14 ya mwaka 1978 ambayo sasa inafahamika kama “PPF Pensions Fund Act” Sura ya 372 ya sheria za nchi yetu kama ilivyorekebishwa na sheria namba 5 ya mwaka 2012 kwa madhumuni ya kutoa mafao ya uzeeni na mafao mengine kwa wanachama wa Mfuko.  PPF ilianza ikiwa chini ya usimamizi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kama Mfuko wa kwanza wa kuchangia wa Pensheni Tanzania.

Waziri fedha aliyataja mbele ya wanachama, wadau na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania ya kwamba mambo yafuatayo yamethibitisha utendaji wa hali juu ya mfuko wa pensheni wa PPF kama vile:-

Kuweza kutimiza majukumu ya mfuko ya kulipa pensheni na mafao mengine bila kukopa wala kulazimika kuuza rasilimali za mfuko wa pensheni wa PPF, waziri aliendelea kusisitiza ya kuwa hili ni jambo la kutia moyo sana kwani mfuko unadhihirisha wazi kabisa ya kuwa unaendeshwa kisayansi na viongozi na wafanyakazi kazi wa PPF kwa kushirikiana na wanachama na wadau wote wa mfuko kwa ujumla.

Waziri aliupongeza Mfuko wa pensheni wa PPF kwa kuweza kutoa huduma kwa wadau wa ndani ya mfuko na wale wa nje kwa asilimia 80 ukitumia mtandao wa kompyuta hii ikimaanisha ya kuwa asilimia 80 ya mifumo ya TEHAMA itumikayo na Mfuko wa PPF imetengenezwa na wafanyakazi wa ndani.

Alisema jambo hili la kutumia kompyuta ni muhimu siyo tu kwa vile dunia ya sasa ndiyo inakoelekea lakini pia inaitaiwezesha mfuko wa pensheni wa PPF kuendelea kutoa huduma kwa haraka zaidi na pia kwa wanachama na wadau wengine kuweza kupata huduma kama vile taarifa za hesabu  kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu. 

Pamoja na hayo Mgimwa ambaye ni waziri wa fedha vile vile aliipongeza kuanza kutumia mawasiliano mapya kwa PPF kwa njia ya ‘facebook’ ambayo pamoja na mengine aliyazindua nembo mpya ya mfuko wa pensheni wa PPF na tofuti iliyoboreshwa ikiwemo facebook siku hiyo ya ufunguzi  wa mkutano huo wa mwaka wa 23

viongozi wa PPF, na wadau mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa NEMBO mpya ya mfuko wa pensheni wa PPF

Alisema kuwa ushiriki wa  mfuko katika shughuli mbalimbali za uwekezaji ambazo zimeleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Taifa  kwa kushirikiana na Mifuko mingine ya hifadhi na taasisi za fedha kama vile mabenki. 

Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na kile cha Kimataifa cha Sayansi na Ufundi cha Nelson Mandela hapa Arusha, aliipongeza PPF kwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kule Mwanza, utoaji wa mikopo katika sekta za kilimo na viwanda kama vile Kiwanda cha Sukari cha Kagera na kile cha 21st Century pale Morogoro, mikopo ya SACCOS kwa Wanachama wao, ujenzi wa majengo ya hoteli za kitalii Arusha na kule Mwanza alisema ya kuwa ni uthibitisho kutosha wa mchango mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu changa kama Tanzania. 

Na kwamba shughuli hizi za kiuwekezaji siyo tu zimekuwa na manufaa kwenu, bali pia kwa Wanachama kwao,  watanzania kwa ujumla na Serikali, waziri alisisitiza.

Alisema ya kuwa mfuko wa pensheni wa PPF wamewekeza kwa kuzingatia miongozo ya uwekezaji iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Na kwamba kwa kufanya hivyo siyo tu itahakikisha mfuko unapata faida nzuri ya uwekezaji wake lakini pia kwa fedha za wanachama wake kuwa salama.

Na jambo lingine muhimu ambalo waziri wa fedha    aliipongeza PPF ilikuwa juu ya PPF kuweza kubuni na kutoa fao la elimu kwa watoto wa wanachama wake waliofariki wakiwa kazini kwa kipindi cha miaka 10 sasa mfuko umewawezesha watoto hawa kupata elimu na kwa rasilimali watu iliyoelimika kwa siku za usoni kwa taifa. 

Ambapo kwa miaka kumi yote mfululizo fao limekuwa likitolewa kwa watoto tegemezi wa wanachama waliofariki wakiwa kazini mpaka kidato cha nne na kuanzia mwakani 2014 PPF itaendelea kutoa mpaka  kidato cha sita.

Na aliendelea kuupongeza mfuko ya kuwa umekuwa ukipata hati safi za hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa serikali  kila mwaka kwa mfululizo ukizingatia ukubwa na wingi wa shughuli za mfuko huo wa pensheni. Na kwamba mambo yote sita aliyoyataja hapo juu ni ya kupigiwa mfano na kuupongeza sana uongozi wa PPF, wafanyakazi, wanachama na wadau wote kwa ushirikiano wao wa matokeo makubwa ya utendaji

Waziri wa fedha aliupongeza mfuko pia kwa namna ya pekee kwa kufanya mikutano hii ya Wanachama kwa miaka 23 mfululizo sasa. 

Alisema mikutano hii siyo tu inawapa wanachama na wadau fursa ya kukutana watendaji wa  mfuko na kupata taarifa mbalimbali za utendaji za Mfuko wao bali inawawezesha kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha zaidi huduma, mafao na kuhakikisha kuwa Mfuko unakuwa endelevu zaidi na kusisitiza ya kuwa kikubwa zaidi ni kwamba inadumisha misingi ya uwazi na uwajibikaji na kuimarisha utawala bora.

Dkt.Mgimwa  alizungumzia pia juu ya changamoto kubwa kuhusu waajiri kutowasilisha michango kwa wakati muafaka na pia kukwepa kuandikisha baadhi ya wafanyakazi wao kwenye MfuKo.

Kwa upande wa Waajiri, waziri anawakuwakumbusha kuwa suala la kuandikisha wafanyakazi wao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na pia kupeleka michango ni suala la kisheria na siyo la hiyari. 

Na kutofanya hivyo ni kuvunja sheria na aliiagiza PPF isisite kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria waajiri hao. 

Alisisitiza ya kuwa ni vyema waajiri wakakumbuka kuwa kwa kutowaandikisha na kupeleka michango yao kwenye Mifuko, kunawanyima wafanyakazi hao haki yao ya msingi ya kupata pensheni wakati watakapostaafu.

Aliendelea kuwahabarisha wanachama na wadau washiriki ya kuwa taarifa alizokuwa nazo ni kwamba mchakazo wa maswala hayo unaendelea vizuri.

Hivyo aliwaomba wanachama na wadau  wote kuendelee kuwa na subira wakati mamlaka husika zinaendelea na mchakato.

Pamoja na haya yote waziri hakusahau  kuzungumzia juu ya changamoto za utoaji wa huduma ya hifadhi ya Jamii kwenye sekta isiyo rasmi. Alisema mpaka sasa asilimia zaidi ya 90 ya wafanyakazi katika nchi yetu wako katika sekta isiyo rasmi na kwamba bahati mbaya ni wachache sana miongoni mwao wanapata huduma hii.

Lakini alisisitiza na kuwakumbusha PPF kutumia  uzoefu wa miongoni mwa mada zilizokuwa zimewasilishwa  na mtoa mada juu ya utoaji wa huduma hii kwa sekta isiyo rasmi nchini kutoka Kenya kuona ni kwa namna gani watanzania wanaweza kutoa huduma hiyo hapa nchini.

No comments :

Post a Comment