Na Aidan Mhando, Mwananchi
Posted Ijumaa,Septemba13 2013 saa 11:1 AM
Posted Ijumaa,Septemba13 2013 saa 11:1 AM
Kwa ufupi
- Ombaomba hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo walitakiwa kurudi katika makazi yao kuanzia leo ili wasichukuliwe hatua za kisheria.
Dar es Salaam. Ombaomba zaidi
ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada
poa’ usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya
kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano
wa Polisi na askari wa jiji.
Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye
Manispaa ya Kinondoni na Ilala ambapo baadaye walihifadhiwa kwenye
Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) kabla ya
kufikishwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa makosa ya uzurulaji.
Ombaomba hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo walitakiwa kurudi katika makazi yao kuanzia leo ili wasichukuliwe hatua za kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick alipohojiwa alisema,operesheni hiyo,imebaini zaidi ya asilimia 70 wanatoka mikoani .
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kukamatwa kwa ombaomba hao na
kueleza kuwa zoezi hilo ni endelevu.
No comments :
Post a Comment