Mkurugenzi Mkuu wa chombo cha
kudhibiti na kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA) Irene Isaka
Na Christian Gaya majira 30 Julai 2013
Lengo kubwa la hifadhi
ya jamii ni kuzuia umasikini, kupunguza au kuondoa umasikini, kuifidia jamii,
kugawanya mapato sawasawa kwa wanajamii. Masuala mengi yanayogusa hifadhi ya
jamii ni ya nyeti sana, yanagusa ni kiini muhimu sana cha wafanyakazi kwenye
sekta rasmi na sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini pamoja na sekta ya bima
za jumuiya za waajiri
Hifadhi ya jamii ina maana ni aina ya hatua
madhubuti au shughuli zilizobuniwa za kuhakikisha kuwa wananchi wa jamii hiyo
wanapata mahitaji yao ya lazima na ya msingi
na wanapewa kinga ya hifadhi ya kutokana na majanga ili kuwawezesha kuwa
na kiwango cha maisha ya kuishi kulingana na mila na desturi za jamii
Mpaka sasa hapa nchini
kuna mifuko sita ya hifadhi ya jamii ambayo imeanzishwa kwa sheria za bunge
mifuko ambayo ni: Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa pensheni
wa wafanyakaziwa serikali za mitaa(LAPF), Mfuko wa akiba wa wafanyakazi wa
serikali (GEPF), Mfuko wa pensheni wa watumishi wa serikali (PSPF), Mfuko wa
pensheni kwa mashirika ya umma(PPF), Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF).
Mifuko hii ya hifadhi ya jamii ina wajibu wa
Kuandikisha wanachama, Kukusanya michango kutoka kwa wanachama, Kuwekeza
michango ya wanachama, Kuwekeza michango ya wanachama, Kulipa mafao kwa
wanachama yanayoendana na ukali wa maisha au mfumuko wa bei kiuchumi ya wakati
huo. Na kuhakikisha ya kuwa inakuwa na malengo pamoja na mikakati
madhubuti ya kuwaelimisha wanachama, waajiri na
wananchi kwa ujumla ingawa Kumekuweko na ongezeko dogo sana la kuelewa
juu ya mfumo wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, jinsi ya
kujiunga kuwa wanachama, vitega uchumi na shughuli mbalimbali za sekta.
Mapungufu yaliyomo kwenye
mfumo huu wa hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya
hifadhi ya jamii chini ya msimamizi na
mdhibiti wa mifuko hii hifadhi ya jamii yaani SSRA. Na idadi kubwa ya watu
ambao ni wanachama katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale tu ambao
wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi kwa sababu inakisiwa kuwa ni milioni 1.0
hii ni asilimia 6% ya nguvu kazi yote ambayo ni kama milioni 16 ya Watanzania
wote. Hii ina maana yakuwa karibu milioni 15 ya nguvu kazi inashughulika na
sekta isiyo rasmi na wote wako katika hali hatarishi kwa vile hawana kinga
yeyote ya hifadhi ya jamii
.
Mtu yeyote
aliyejiajiri, mkulima, mvuvi, mfanyakazi wa ndani, wafanya biashara wadogo
wanaweza kujiandikisha kwa hiari na kulipa kadri ya uwezo wake na mifuko hii ya
hifadhi ya jamii na akisha anza kuchangia mwanachama wa hiari naye atakuwa na
haki ya kupata mafao yote yatolewayo na mfuko wowote wa hifadhi ya jamii
atakaopendelea kujiunga nao ingawa hakuna mikakati ya makusudi inayoridhisha ya
utekelezaji wa jambo hili inayofanywa na mifuko hii ya hifadhi ya jamii hapa
nchini.
Kwa kawaida mipango ya
mifuko ya hifadhi ya jamii huchangiwa kati ya mwajiri na mfanyakazi kwa kiwango
cha asilimia 20 ya mshahara wa mfanyakazi ikijumuishwa na marupurupu mengine.
Moja kati ya viwango vifuatavyo vinaweza
kutumika kutegemeana na maamuzi ya mwajiri na mwanachama: asilimia 10
kwa mfanyakazi na asilimia 10 kwa mwajiri au asilimia 5 kwa mfanyakazi na
asilimia 15 kwa mwajiri na asilimia 20 yote kuchangiwa na mwajiri
Baadhi ya changamoto
kwa serikali ni kama vile kujaribu kuangalia jinsi ya kufikia watu wengi zaidi
au wote nchini, kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ili kila mtu aishi kwa
heshima na utu. Kulingana na sera za masuala ya nchini Katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ibara ya kama vile sura ya 11 (1) inaainisha wajibu wa
serikali na jamii ulinzi kwa raia wake juu ya majanga ya kijamii kama
vile,magojwa ulemavu na uzee.
Ni wajibu wa mifuko hii ya
hifadhi ya jamii kuhakikisha ya kuwa mwanachama anaelemishwa kama mchangiaji
pamoja na mwajiri wake ili kila mmoja ajue wajibu wake kwenye mfuko hii ya
hifadhi ya jamii. Mifuko hii ya pensheni wa hifadhi ya jamii lazima uweke wazi
juu ya haki za wanachama hasa zile za kumruhusu mwanachama kukata rufaa kwenye
bodi ya sheria au mahakamani atakapoona kwamba pale hajatendelewa haki
inavyotakiwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii. Siyo hivyo mifuko ya
pensheni ya hifadhi ya jamii ina wajibu wa kuweka wazi kwa wanachama mchangiaji
jinsi ya kuwashirikisha kwa vitendo kwenye maamuzi na jinsi ya uendeshwaji wa mifuko.
mwisho
No comments :
Post a Comment