Kwa ufupi
“Bila kutumia fursa hii, ni vigumu kujenga kwa
kukusanya fedha kidogokidogo. Ukikopa benki unapata fursa nzuri ya
kupata nyumba bora huku ukilipa taratibu, kwa ujumla mikopo hii ni
mkombozi wa kupambana na makazi holela kwa kutupatia makazi bora
yaliyopimwa na yenye huduma zote muhimu,” alisema.
Mwanasheria Mkuu wa Kwanza wa Serikali, Jaji
Mark Bomani, amewashauri Watanzania kuchangamkia fursa za mikopo ya
nyumba zinazotolewa na benki hapa nchini ili kupata makazi bora.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani
alisema fursa hiyo ni njia bora na sahihi ya kupata makazi bora kwa
kuwa Watanzania wengi wataweza kununua nyumba katika maeneo yaliyopimwa
na yenye mfumo mzuri kuanzia barabara, umeme na maji.
Jaji Bomani aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa
mradi wa nyumba zilizopo eneo la Goba Kunguru jijini Dar es Salaam,
zilizojengwa na kampuni ya Greystone Holdings.
“Bila kutumia fursa hii, ni vigumu kujenga kwa
kukusanya fedha kidogokidogo. Ukikopa benki unapata fursa nzuri ya
kupata nyumba bora huku ukilipa taratibu, kwa ujumla mikopo hii ni
mkombozi wa kupambana na makazi holela kwa kutupatia makazi bora
yaliyopimwa na yenye huduma zote muhimu,” alisema.
Kwa mujibu wa Jaji Bomani, wananchi wanaweza
kununua nyumba zilizozinduliwa kwenye eneo kwa kukopa fedha katika Benki
Biashara za Kenya (KCB), Commercial Bank of Africa (CBA) na Bank of
Africa (BOA).
“Eneo hili lina barabara, umeme, maji
yaliyochimbwa na bustani nzuri za kupumzikia, kwa ujenzi wetu wa
kudunduliza, ni vigumu kutenga eneo zuri la bustani, hivyo ni muda
mwafaka sasa kwa Watanzania kununua nyumba kama hizi kupitia mikopo ya
nyumba,” alisema.
Nyumba hizo ni zenye vyumba vitatu vya kulala, stoo, jiko na maegesho ya magari.
No comments :
Post a Comment