Wajibu wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii ni
kuhakikisha ya kuwa inawashirikisha wadau wake wote wakuu hasa waajiri,
serikali na bila kusahau wanachama na familia zao ambapo makundi hayo matatu
yanaunda kitu kinachoitwa utatu hawa wote
wanaunda utatu. wananchi lazima mtambue kuwa wawekezaji wa mifuko hii ni
waajiri na wafanyakazi pale wanapojiandikisha na kuwa wanachama wachangiaji kwa
kukatwa asilimia fulani kutoka katika mishahara yao na mwajiri na yeye
kuchangia kiasi hicho hicho au zaidi kwa ajili ya mfanyakazi wake kwa
makubaliano ya kupata huduma mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kutoka
katika kwa hiyo mifuko.
Hivyo uwakilishi wao lazima uwemo ndani ya utawala wa mifuko
hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii mara kwa mara kwa vitendo. Vile vile
inatambulika kuwa hata serikali ina kazi kubwa juu ya mifuko hii ya hifadhi ya
jamii hasa zaidi kwa kuangalia na
kusimamia kiwango cha kinga juu ya majanga wanayokumbana nayo jamii yetu hapa
nchini pamoja na kuangalia mchango wa mifuko hii kwa upande wa uchumi wa nchi
yetu na serikali kama mdhamini mkuu wa
mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii. Serikali kuwa mdhamini hii ina
maana ya kuwa mfuko wowote ukifirisika serikali ndiye atayewajibika kuwalipa
wanachama wa mfuko huo michango na pensheni zao na madeni mengineyo bila
kuteteleka.
Hapa kinachoshindikana ni utekelezaji ingawa utaratibu na
kanuni zote za uhusiano wa utatu uliopo kati ya mwajiri, mfanyakazi na serikali
na jinsi ya kuwashirikisha. Huenda ugumu unaokuja ni jinsi ya kupata taasisi na
au mtu sahihi ambaye anaweza kuwa mwakilishi wa kutosha wa wachangiaji,
wategemezi pamoja na wadau wengine wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Mfuko wa
hifadhi ya jamii unaweza kuwa na wanachama wengi na kukawa na taasisi nyingi
zinazowakilisha waajiri na wafanyakazi wakati baadhi ya wanachama wengine
wakawa hawana mtu yeyote wa kuwakilisha mambo yao. Lakini kwa upande mwingine
mfuko unaweza kuwa na wigo mdogo wa wanachama
na idadi kubwa ya wanachama hao hao wakawa na uelewo mdogo wa dhana ya
hifadhi ya jamii pamoja na kutojua hata utawala wa vitendo wa mfuko wa pensheni
ya hifadhi ya jamii na wakawa hata umoja wao wa wafanyakazi kuwa mdogo kiasi
cha kwamba ukawa hata uwakilishi wao kutokuwa na nguvu yeyote. Hivyo kuna haja
ya kuangalia mgawanyo wa majukumu na kati ya serikali na bodi, mgawanyo wa
majukumu kati ya bodi na wawakilishi na
mwisho mgawayo wa majukumu kati ya bodi na mkurugenzi makuu. Hii mara nyingi
mambo mengi yanakuja kuingiliwa na hali ya kiasi iliyopo nchini. Kwa sababu
unakuta mkurungezi mkuu wa mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii anachanguliwa
na rais wa nchi.
Na kwa upande mwingine wajumbe wa bodi kuchanguliwa wa wizara
mama, mfano mfuko wa pensheni wa mashirika ya umma yaani Parastatal
Pension Fund (PPF) wenyewe uko chini ya wizara ya fedha, Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF)
wizara ya kazi na ajira, Mfuko wa pensheni wa serikali za mitaa yaani Local
Authorities Pensions Fund (LAPF) wizara ya serikali za mitaa, mfuko wa taifa wa
bima ya afya yaani National Health Insurance Fund (NHIF) wizara ya afya. Na
mfuko wa akiba ya wafanyakazi kwa watumishi wa serikali yaani Government
Employees Provident Fund (GEPF) wizara ya fedha . Pamoja na mfuko wa pensheni
wa watumishi wa serikali ya Public Service Pensions Fund (PSPF) ambao nao upo
chini ya wizara ya fedha ingawa kwa sasa yote inasimamiwa na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa
sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA). Mifuko ya hifadhi ya jamii, wanachama,
wafanyakazi, waajiri. Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya
jamii iliundwa kwa sheria Na 8 ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2008 kwa lengo la
kusimamia na kudhibiti sekta ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya wanachama na
kwa taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi rasmi mwaka 2010.
Mamlaka ina jukumu la kusimamia shughuli zote za hifadhi ya
jamii nchini ikiwa ni pamoja na mifuko yote ya hifadhi ya jamii iliyo anzishwa
kwa sheria ya bunge ambayo ni mifuko ya pensheni,mifuko ya akiba .mifuko ya
bima ya afya na mifuko ya hiari na kuhakikisha kwamba mifuko inakuwa endelevu
,inaendeshwa kwa kufuata kanuni na taratibu za kisheria, wanachama wanapata
taarifa za mifuko yao ,mafao yanaboreshwa na serikari inapunguziwa mzigo.
Kwa hiyo wawakilishi wote wa bodi idadi yao kubwa wanatoka
serikali, na mara nyingi katiba za mifuko ya hifadhi ya jamii inaeleza wazi sifa
za hao wajumbe wa bodi au bodi ya wadhamini ambazo hata kidogo hazifuatwi
badala yake kuchaguliwa kwa kujuana na matokeo yake anaishia kumsikiliza
mkurugenzi mkuu bila kuhoji chochote kwa muda wote wa miaka mitatu na mwaka wa
mwisho huenda ndipo anapoweza kuanza kuelewa baadhi za taarifa za mahesabu
lakini mwanzoni anaishia kuitikia kwa sababu ya kutokuwa na upewa wa kutosha
juu ya mambo ya hifadhi ya jamii. Kwa hiyo mzigo wote wa mifuko ya hifadhi ya
jamii unabaki chini ya serikali yenyewe kwa sababu utawala na usimamizi wote wa
mifuko hii upo chini ya usimamizi na uthibiti wa chombo cha serikali hivyo hata
kesho mfuko wowote ukafilisika atayebeba mzigo wa kulipa mafao au pensheni na na madeni itakuwa serikali yenyewe kama
mdhamini wa mifuko yote hapa nchini
No comments :
Post a Comment