Na Fredy Azzah, Mwananchi
Kwa ufupi
- Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda tena kuyafanyia kazi matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia asilimia tisa.
Dar es Salaam. Matokeo ya
kidato cha nne yanayotarajiwa kutangazwa leo, yamezidi kuzua mapya baada
ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni
iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo
likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli
.
.
Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya
matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake
Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani
ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa
wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa,
walijadili matokeo hayo.
“Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule
kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama
2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,”
kilisema.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, katika kikao hicho,
kulikuwa na mvutano kuhusu kanuni ipi itumike ili kuwaokoa wanafunzi hao
alama zao zisishuke.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda
tena kuyafanyia kazi matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa
asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia asilimia tisa.
“Kwa sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake
yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu
kweli,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Ukijaribu kuangalia, Necta wanasimamia kanuni,
lakini wakati mwingine inabidi mtu uangalie hali ilivyo, kwa sasa watu
wanaangalia zaidi mwitikio wa wananchi utakavyokuwa haya matokeo
yakitangazwa badala ya kuangalia vitu vya msingi,” kilisema chanzo
hicho.
No comments :
Post a Comment