NA Christian Gaya Majira 26 March 2013
kwa mujibu wa kifungu cha 30
cha Sheria ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii na sheria za mifuko
kama zilivyorekebishwa, mfanyakazi ambaye hajawahi kujiunga na mfuko wowote wa
pensheni au anayeajiriwa kwa mara ya kwanza anao uhuru wa kuchagua mfuko wowote
kati ya mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii. Hii ina maana mfanyakazi
anapaswa kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu wa pensheni. Kifungu hicho
kinaendelea kusisitiza ya kuwa ni makosa makubwa kwa mfanyakazi mpya kujiunga
au kujiandikisha kwenye mifuko zaidi ya mmoja wa pensheni.
Hiki ni kitu kizuri ili
kuleta ushindani zaidi kwa mifuko ya
pensheni ya hifadhi ya jamii nchini na kuleta uwiano wa wanachama. Na huenda
hii inaweza kusaidia changamoto ya kuongezea idadi kubwa ya wanachama kwenye
mifuko hii ya hifadhi ya jamii hasa kutoka katika sekta isiyokuwa rasmi ambayo kwa muda mrefu imesahaulika na badala
ya kuegamia sheria zilizoanzisha mifuko hii ya pensheni. Kwa sababu mpaka
inakisiwa kuwa idadi ya watanzania wote inakisiwa kuwa
ni milioni 45.
Kati
ya hawa asilimia 70 wako maeneo ya vijijini. Na idadi ya nguvu kazi ya
watanzania inakisiwa kuwa ni milioni 16 ambapo asilimia 5.4 ya nguvu kazi au
asilimia 2.7 ya idadi yote ya watanzania ndiyo iliyojiunga na mfumo kamili wa
lazima wa hifadhi ya jamii. Na asilimia 93 ya nguvu kazi yaani ya watu
wanaojiweza kufanya kazi imejikita kufanya kazi kwenye sekta isiyo kuwa rasmi
kwa sehemu zote za mijini na vijijini. Na asilimia 80 ya hao ambao wamo kwenye
sekta isiyo rasmi wanashughulika na kilimo
Inayokisiwa kuwa ni milioni 1.0 hii ni asilimia 5.4% ya
nguvu kazi yote ambayo ni kama milioni 16 ya Watanzania wote. Hii ina maana
yakuwa karibu milioni 15 ya nguvu kazi inashughulika na sekta isiyo rasmi na
wote wako katika hali hatarishi kwa vile hawana kinga yeyote ya hifadhi ya
jamii
Hifadhi ya jamii ina maana ni aina ya hatua madhubuti au
shughuli zilizobuniwa za kuhakikisha kuwa wananchi wa jamii hiyo wanapata
mahitaji yao ya lazima na ya msingi na
wanapewa kinga ya hifadhi ya kutokana na majanga ili kuwawezesha kuwa na
kiwango cha maisha ya kuishi kulingana na mila na desturi za jamii
Na lengo kubwa la hifadhi ya
jamii ni kuzuia umasikini, kupunguza au kuondoa umasikini, kuifidia jamii,
kugawanya mapato sawasawa kwa wanajamii. Masuala mengi yanayogusa hifadhi ya
jamii ni ya nyeti sana, yanagusa ni kiini muhimu sana cha wafanyakazi kwenye
sekta rasmi na sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini pamoja na sekta ya bima
za jumuiya za waajiri
Mfumo wa hifadhi ya jamii ambayo ni ya lazima kisheria
ambayo wafanyakazi pamoja na mwajiri wanachangia pamoja na kupeleka michango
kwenye chombo cha mfuko wa pensheni (pension fund) au mfuko wa akiba ya
wafanyakazi (provident fund).
Taasisi za hifadhi ya jamii ya
jamii nchini Tanzania zimekuwa zikiwekeza orodha ya fedha kwa faida kwenye
mikopo, nyumba za kupangisha, hatifunganishi, kuweka akiba benki zote hizi
zimechangia maendeleo.
Kumekuweko na ongezeko dogo sana la kuelewa juu ya mfumo
wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, jinsi ya kujiunga kuwa
wanachama, vitega uchumi na shughuli mbalimbali za sekta. Mapungufu yaliyomo kwenye mfumo huu wa
hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya hifadhi ya
jamii. Watu waliomo katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale tu
ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi
Hivyo kama mfanyakazi
utahitaji kujifunza ili kujua na kuzingatia mambo muhimu kabla ya kufanya
maamuzi ya kujisajili na mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii wowote ule.
Najua kila mmoja wetu anaweza kuwa na lengo lake la kutaka kujiunga na mifuko
hii ya pensheni. Na wawekezaji wengi mara nyingi hutumia vigezo vya takwimu au
vigezo vya kifedha, na vigezo vingine au taarifa nyinginezo mbali na fedha.
Hivyo kuna vigezo muhimu hata kama utasikia habari au ripoti kwenye runinga,
magazeti, rafiki, redio n.k. kutoka sehemu tofauti kuhusu uzuri wa mfuko fulani
wa pensheni ya hifadhi ya jamii hakikisha kwanza unaupima kwanza kwa vigezo
vyako
No comments :
Post a Comment