Baadhi
ya nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na baadhi ya mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii
Na christian Gaya Majira 08 Aprili 2013
Jambo la kuangalia
kuhusu mifuko ya pensheni ni kujua bidhaa au huduma zake. Je huduma hiyo
inahitajika na watu wote, chukua mfano wa chumvi. Hivyo jaribu kujiunga na
mfuko wa pensheni ambayo huduma zake zinahitajika na wengi au
wafanyakazi wengi na familia zao, pamoja na wazee, vijana, watoto,
walemavu, wajane, pamoja na watoto yatima. Je huduma zinazotolewa na mfuko wa
pensheni zina mbadala au hazina mbadala. Hiyo huduma ina ina uhakika mkubwa na
wa soko. Ina nguvu kubwa ya ukiritimba ni kiwa na maana ya kuwa na uwezo wa
huduma kuwa na soko kubwa lenye uwezo wa kudai bei kubwa bila kupunguza uhitaji
na matumizi. Hivyo tafuta andika na wekeza kwenye huduma zenye sifa nzuri.
Fanya uchunguzi wa
kutosha au kina kuhusu utendaji wa mifuko hii hasa kwa kufanya utafiti wa
kutambua thamani, soko, kutatua udhaifu, kutoa majibu ya maswali tata, kupata
taarifa zaidi na za uhakika. Kujiunga na mfuko wowote wa hifadhi ya jamii ni
kutafuta sehemu yenye usalama ya kuweza kuwekeza michango ya kila mwezi kwa ajili ya aina mbalimbali ya majanga
yanayoweza kusababishwa na ugonjwa, kuumia ukiwa kazini, kifo, kupata ulemavu, na
kadhalika. Hivyo unahitaji kufanya utafiti wa makini sana kwa kuchunguza
taarifa mbalimbali juu ya mfuko huo wa hifadhi ya jamii unaotaka kujiunga nao
ili taarifa hizo ziweze kukusaidia kutoa maamuzi wa busara wa kukuwezesha
kuzingatia kanuni misingi na vigezo maalumu ambazo vitakusaidia kujibu maswali
mengi. Baadhi ya maswali muhimu yanaweza kuwa kama vile utawezekeza wapi? Na
mfuko upi wa pensheni ya hifadhi ya jamii, na watakata kiasi cha asilimia ngapi
kutoka katika mshahara wangu, na mwajiri wangu yeye atatoa kiasi cha asilimia
ngapi. Hivyo ni juu ya mfanyakazi mwenyewe kama mwekezaji kufanya utatafiti wa
kina ili kujua ubora wa mfuko huo unaotegemea kujiunga nao kabla ya kujisajili.
Unatakiwa usiwe mwepesi wa kufanya maamuzi bila kwanza kuwekeza kwenye utafiti
hasa kama vile kuwaona wataaalamu wanao weza kukusaidia kukupa ushauri mahiri.
Ni muhimu kuangalia
mifuko hii ya pensheni kwa kuangalia uongozi , yaani menejimenti, hali ya
kifedha, thamani ya mfuko wa pensheni kwa sasa, taarifa mbalimbali, matarajio
ya mfuko wa pensheni kwa kipindi
kijacho kama pamoja na thamani ya mfuko
wa pensheni kwa miaka ijayo. Uchambuzi
unahitajika uwe unaolenga zaidi katika kuchambua thamani ya mfuko wa pensheni
kutokana na taarifa halisi zilizopo na siyo taarifa za matarajio ya baadaye. Mchangiaji
wa michango au Mwekezaji makini anatakiwa aweke mkazo katika kufanya makosa
makubwa kwa sababu uchunguzi au utafiti au upembuzi wa mifuko hii ya hifadhi ya
jamii inatakiwa ufanyike kisanyansi kwa kuzingatia uchambuzi wa takwimu na
uchambuzi nyinginezo ingawa vigezo hivi vya takwimu vinaweza kuwa muhimu lakini
mara nyingi huwa havijitesholezi hata kidogo. Hivyo shughuli kubwa katika mambo
ya kujiunga au kujisali na mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii inatakiwa
kufanya utafiti, ingawa unagharimu muda mwingi.
Uamuzi wa kuwa mwanachama wa mfuko wa pensheni
ya hifadhi ya jamii unatakiwa utokana na takwimu na taarifa nyinginezo makini
zinazotakiwa zifanywe na mfanyakazi mwenyewe na siyo kufuata mkumbo wa watu
wengi wanasemaje. Kwa kufanya hivyo tumeona mara nyingi wafanyakazi wengi hukosea
kwa sababu alifuata mazungumzo ya watu wengi juu ya mfuko fulani wa pensheni
hivyo anatakiwa kufanya utafiti na uamuzi wake ufuate utafiti na takwimu siyo uzushi
au habari motomoto ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wowote. unahitaji wewe kama
mfanyakazi kuhakikisha ya kuwa unafanya utafiti au uchunguzi wa kina na kuchambua ripoti za kila mwaka za mifuko
ya hifadhi ya jamii huku ukuzingatia yale yanayotendeka katika sekta tofauti
nchini na kwingineko
Unahitaji kujua usalama
wa michango yako unayochangia kila mwezi. Lazima ujue hiyo michango yako
huwekezwa mahali ambapo uwezekano wa kupata hasara ni mdogo sana, na kuchunguza
kama huwekezwa sehemu ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata faida. Hii
ijulikane na itambulike ya kuwa kiupambele katika ufuatiliaji wake kwenye
michango yako au fedha yako unayochangia kwanza inatakiwa kuwa na usalama wake
na siyo faida. Kipa umbele hapa kwanza ni inatakiwa kuwa michango yako na siyo
faida unayotakiwa kutarajia. Faida inatakiwa kushika nafasi ya tatu na siyo
nafasi ya kwanza au ya pili
Unatakiwa kulikumbuka
hili jambo sana ukitaki ufanikiwe kutokana na mifuko hii ya pensheni ya hifadhi
ya jamii hakikisha unafanya utafiti au uchunguzi kuhakikisha ya kuwa mfuko
unafuata utaratibu wa kisayansi wa uwekezaji wa michango yako kwa kufuata kanuni
za kulinda usalama wa fedha zako unazotegemea kuchangia na uwekezajji uwe ule wa
kuleta faida na kuwa na uwezo wa kitega uchumi kubadili kuwa fedha taslim na
siyo vinginevyo, na mfuko ambao unajitoa kuchangia masuala ya kijamii inayoizunguka
na kuwa na uwezo mkubwa wa kutawanya uwekezezaji wa michango yako bila kufuata misukumo
ya wanasiasa
katika nyanja za hifadhi za jamii.
No comments :
Post a Comment