Kumruhusu mtu
kuchukua michango yake kabla ya haikomaa au kufikia muda wake wa pensheni kuiva
hii inaweza kuleta hali hatarishi kwa mwanachama mchangiaji. Kama
mwanachama mchangiaji aliyewekewa bima anaweza kuruhusiwa kuchukua michango
yake ya pensheni ya uzee inaweza kuleta mgongano wa hasi zaidi hasa pale atakapoanza kuchagua kiwango cha
kiasi gani cha pensheni yake atapata.
Kwa mfano sera
ya hifadhi ya jamii Tanzania
ya mwaka 2002 inataja rasmi kuwa mwanachama ataruhusiwa kupata mafao yake ya
pensheni ya asilimia 25 kama mkupuo ambao
hauna kodi kabla hajafikia umri wa miaka 55 ya hiyari au 60 ya lazima kustaafu.
Kutoa michango yote sio jambo nzuri, kwa sababu michango ikisha tolewa baada ya
hapo hufanyiwa nini? Kama inawekezwa kwenye vitega uchumi kama
vile hatifungani, hisa, vipande na uwekezaji mwingine ni bora zaidi kuliko kwa
ajili ya mahitaji ya leo tu.
Hapa inaonyesha
ya kuwa wafanyakazi wengi wanapendelea kuondoa michango yao kwa mkupuo bila ya hata kuelemishwa juu ya matokeo ya pensheni yake ya mwisho
yaani ya kustaafu. Hii tabia itawaweka watu wengi baada ya kustaafu kwenye hali
au mazingira hatarishi hasa watakapo kuwa wanapata pensheni kidogo kuliko
walivyokuwa wakitegemea kupokea baada ya kustaafu na pale muda wao wa kuishi
utakapokuwa mkubwa zaidi kuliko pensheni waliyopata. Na kiutaratibu zaidi
inatakiwa mchangiaji asisitoe michango yake yote ya pensheni. Inatakiwa kama
atatoa theluthi ya michango yake ya pensheni basi theluthi mbili zibaki kwa
ajili ya pale atakapokuwa hana uwezo tena kupata pato lake kwa
njia ya kujiajiri au kuajiriwa tena.
Kwa sababu ya
hali hii hatarishi, kuchukua michango kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kwa
hiyari yaani miaka 55 au lazima baada ya kufikisha miaka 60 kwa kweli imefikia
muda msimamizi na mdhibiti wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii yaani Social
Security Regulatory Authority (SSRA) au kwa kila mfuko wa pensheni ya hifadhi
ya jamii kuwa na mikakati ya makusudi ya kuandaa programu za kuelemisha na
kufundisha na kutoa ushauri kwa wananchi au mwanachama pamoja na familia zao
juu ya matokeo au madhara ya kutoa michango yao ya pensheni kwenye mifuko ya
hifadhi ya jamii kabla haijafikia muda wake.
SSRA inatakiwa kuhakikisha kuwa inaadaa programu iliyo kamili kwa ajili
ya kutoa elimu kwa watu na wakati wowote inapohitajika iweze kupatikana. Lakini
hata mifuko yote ya pensheni ya hifadhi ya jamii inatakiwa kutoa elimu ya juu
Na hii lazima ifahamike wazi ya kwamba karibu mifuko yote ya pensheni
inayoendeshwa kwa utaratibu wa bima kama vile Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), shirika la
pensheni kwa ajili ya mashirika ya umma (PPF), Mfuko wa Pensheni wa hifadhi ya
jamii kwa ajili ya Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Bima wa Taifa yaani
(NHIF), mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali za mitaa yaani (LAPF)
Michango ya
wanachama wao yote huingizwa kwenye chungu au mfuko mmoja bila kujali ukubwa au
udogo wa michango ya wanachama na huwekezwa kwenye mfuko mmoja. Kwa maana hii
inakuwa vigumu kwa mfuko kama hii kutoa
michango kwa wanachama kabla ya wakati wake. Kwa vile michango yote huingizwa
kwenye akaunti moja tu. Ila pale mwanachama anapopatwa na janga lolote
litalomfanya kupunguza pato lake
kama vile kuumia akiwa
kazini, kustaafu, kujifungua yaani uzazi, ugonjwa pale anapougua pamoja na
familia yake gharama zote za matibabu zinachotwa kwenye akaunti hiyo hiyo.
Kuchukua
michango ya pensheni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kama
NSSF, LAPF, PSPF, LAPF, NHIF, AU PPF ambayo michango wanachama huwekwa kwenye
mfuko mmoja bila kujali umechangia kiasi
ngapi kunaweza kuharibu kabisa thamani ya mifuko hii na hata kupelekea
baadaye kutokuwa endelevu. Na hii inaweza hata kuleta madhara makubwa hata kwa
wanachama wengine wa mifuko hii ambao wataendelea kuchangia. Kwa vile hakuna akaunti ya mwanachama mmoja
mmoja hivyo kunafanya uchukuaji wa michango ya pensheni mapema kuwa vigumu
zaidi. Lakini kwenye mifuko ya akiba ya wafanyakazi ya taifa kama
ilivyokuwa NPF yaani National Provident Fund
kabla haujabadilishwa kuwa mfumo kamili wa hifadhi ya jamii yaani NSSF pamoja na
Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi wa Serikali (GEPF) ambao wenyewe mpaka sasa kila
mwanachama ana akaunti yake ya michango ya pensheni.
itaendelea
wiki ijayo
No comments :
Post a Comment