Thursday, January 31, 2013

Nyumba za NHC na NSSF Kigamboni, Dar Es Salaam





20120511-212943.jpg
NHC ina mpango wa kujenga nyumba zipatazo 200 na NSSF ina mpango wa kujenga nyumba 300 katika awamu kwa kwanza. Nyumba hizi ni za aina tofauti na zina vyumba kati ya 2-4.
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko toka kwa wananchi kuwa nyumba za bei nafuu (affordable houses) bado si rahisi kwa mwananchi wa kipato cha kati na chini. Bei ya nyumba mpya za NHC hivi karibuni zimekuwa ni zaidi ya TSh 100 millioni kila moja. Bei hii inalalamikiwa kuwa ni kubwa sana kwa mlalahoi.
Katika mradi huu wa Kigamboni, NHC ina mpango wa kuuza nyumba zake kati ya TSh 30-40 millioni kutegemea na ukubwa. Sikuweza kupata bei za nyumba za NSSF.
Pamoja na miradi hii mizuri itakayopendezesha Jimbo la Kigamboni, nyumba hizi zinaweza kununuliwa kwa matajiri wachache kutokana na bei kuwa kubwa. Kuna umuhimu wa kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini na kati kupata mikopo ya muda mrefu itakayowawezesha kununua nyumba hizi.
Kwa watanzania walio nje ya nchi, hii ni fursa nzuri ya kununua nyumba, itumieni.









20120511-213203.jpg

No comments :

Post a Comment