Tuesday, January 29, 2013

Fahamu changamoto zinazowakabili wazee nchini Tanzania



Na Christian Gaya: Majira 29 Januari 2013

Changamoto kubwa ya nchi yetu ya Tanzania ni kudidimia kwa mfumo wetu wa hifadhi ya jamii usio kuwa rasmi hasa kwa njia ya kutoa fedha taslimu na kujikimu au kusaidia kwa pande zote za familia zaidi ya moja na kama chanzo cha jumuiya. Na mwongezeko zaidi wa changamoto ni kutokana na mabadiliko ya muundo wa familia na kudidimia kwa mitandao ya kusaidiana kijamii.

Tangia enzi za zamani hifadhi ya jamii isiyo rasmi ilinajulikana kuwa ndiyo inayofaa kutoka vizazi kimoja hadi kingine kuwa ndiyo chombo au mtandao maalum kwa kutoa michango mikubwa wa kusaidia wazee na kwa wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi. Na kutokana kwa kuongezeka kwa miji na madhara ya mlipuko wa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS) mtandao huu muhimu wa kusaidiana umekuwa unaendelea kubomoka na kuporomoka zaidi hasa kwa upande wa baadhi ya makundi ya kijamii hasa yale yaliyoguswa na madhara ya mlipuko wa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS). Dhima na wajibu wa jamii umekuwa kinyume kabisa na inavyotakiwa iwajibike kwa wazee, watoto, wamama, vilema na wale ambao wanaishi kwenye mazingira hatarishi.

Kwa upande mwingine utafiti unaonyesha ya kuwa wazee yaani akina babu na bibi ndio wanatunza watoto yatima na kutoa hata faraja kwa wajane, ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila siku. Na takwimu vil;e vile zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 (hamsini) ya watoto yatima hapa Tanzania wanaishi na babu au bibi zao. Kwa upande mwingine ni kwamba kutokea na kuongezeka zaidi kwa virusi vya ukimwi (VVU/AIDS) kumesababisha kutokea haraka kwa kundi la hili la wazee wanaoishi peke yao ambalo hawatambuliwi na jamii wala jumuiya na hata na serikali yao, na bila kunufaika na mwangalizi yeyote. Utafiti uliofanywa kutoka katika nchi sita za Kiafrika unaonyesha kuwa idadi ya asilimia zaidi ya 4 (nne) ya wazee wanasumbuliwa na magonjwa sugu ya moyo na kisukari hasa pale wanapofikisha umri wa miaka zaidi ya sitini ukilinganisha na wale ambao wako chini ya umri wa miaka sitini.

Utawala na menejimenti wa magonjwa ya sugu na ya muda mrefu na yale mengine ya ulemavu yanatakiwa kuwa na idadi kubwa ya rasilimali watu yaani wataalam na fedha kutoka serikalini, jumuia mbalimbali, na hata kwenye familia. Pamoja na hayo bado serikali kama ya Tanzania, inatumia kiwango kidogo sana cha kipato kwa kichwa cha mtu kwa matumizi ya afya ukiachilia mbali mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hayagusi kabisa makundi haya yanayoishi kwenye mazingira hatarishi ukilinganisha na nchi zilizoendelea.  

Kwa mfano halisi ni kwamba Tanzania haina mpango wa kutoa huduma ya jamii kwa wote au mpango rasmi wa kuwatunza na kuwajali wazee, kwa kweli bado hawa wazee wanategemea mfumo usio rasmi wa hifadhi ya jamii unaotegemea zaidi muundo wa familia na wala siyo serikali. Kwa hiyo gharama hasa ya matibabu mara nyingi anaachiwa mwananchi ambaye hana uwezo wa kubeba mzigo bila msaada wowote kutoka serikalini au jumuia yeyote au asasi.    

Utafiti kutoka nchi kumi na tano za Kiafrika ikiwemo Tanzania unaonyesha idadi kubwa ya watu wa kipato cha chini wanakimbilia au wanaishia kukopa au kuuza rasilimali zao ili kuweza kwenda pamoja na gharama za matibabu. Hali hii imepelekea familia nyingi kuingia kwenye janga la umasikini zaidi na afya zao kuwa mbaya zaidi na zaidi 

Licha ya mapadiliko haya ya demografia muhimu ya takwimu ya kima cha uzazi, uzee, vifo, maradhi yanaonyesha hali halisi ya jamii yetu, demografia ya uzee haionekani hata kidogo kuzungumziwa kwenye midaharo na mihadhara ya sera mbalimbali. Kutoonekana kwa mazingira hatarisha ya wazee kwenye makaratasi ya sera muhimu za nchi inaletwa na msukumu wa kutoonekano kwao hata kwenye mipango ya maendeleo ya taifa. Wakati malengo ya maendeleo ya milinea yaani millinium development goals (MDGs) inatoa malengo maalumu ya watoto, vijana na akina mama, hawakumbushii wala kuzungumzia ya kwamba nao wazee ni kundi muhimu.

Matokeo yake hili kundi la wazee halinufaiki na mipango hii maalum ya misaada ya maendeleo. Kukosekana kwa kutotambuliwa hili kundi la wazee hata kwenye ajenda za MDGs ajenda ambayo ni mipango iliyopewa kipa umbele na mipango ya maendeleo ya kimataifa umechangia kwa kudidimiza zaidi hali ya kundi muhimu la wazee ambao ndio wachangiaji wakubwa wa uchumi wa taifa hili la Tanzania.

No comments :

Post a Comment