Tuesday, December 11, 2012

Sera na mikakati ya serikali katika kuboresha mifumo ya hifadhi ya jamii



Kila binadamu anazingirwa na hali za hatari na majanga ambayo hayatabiriki yanaendena na kipato kama ndiyo njia ya kukidhi mahitaji yake. Kama hatarishi za kijamii na za kiuchumi pamoja na vitu ambavyo havitabiriki katika maisha ya binadamu yanalazimisha kuunda na kuhitaji chombo kama hifadhi ya jamii. Mizizi ya hifadhi ya jamii na asili yake inatokana mahitaji ya mshikamano na kuchangia kwa pamoja na jamii katika kupambana na hali hatarishi zinazomkumba binadamu. Ifahamike ya kuwa hakuna mtu mwenyewe peke yake anaweza kujihakikishia hifadhi ya jamii peke yake

Mfumo wa hifadhi ya jamii iliyo rasmi hapa Tanzania na nchi zingine za zinazoendelea za hapa Afrika ni matokeo ya kutawaliwa na wakoloni. Wakati wa enzi za ukoloni hifadhi ya jamii iliyo rasmi ilipelekwa kwa watu wachache waliokuwa katika ajira za kikoloni. Idadi kubwa ya watu walikuwa hawana hifadhi ya jamii na wala hawakuingizwa kwenye mfumo huu wa hifadhi ya jamii.

Idadi kubwa ya watanzania walitegemea mfumo wa hifadhi ya jamii usiokuwa siyo rasmi kwa ajili ya kinga ya hifadhi ya jamii ambayo mpaka sasa inaendelea kutoa huduma chini ya familia au kiukoo.  Baada ya uhuru, serikali ya Tanzania ilitoa mfululizo wa sera na mikakati mingine ya kuondoa hali iliyowekwa enzi za wakoloni
Baadhi ya mikakati ilijumuuisha ilikuwa ni kwa kila mtanzania kupata elimu na matibabu bure, kutoa huduma za ustawi kijamii kwa makundi yanaishi hali kwenye hali hatarishi kama vile wazee, watu wenye ulemavu na watoto, na kama vile uanzishwaji wa mifuko ya lazima kisheria ya hifadhi ya jamii





Baadhi ya wamama na watoto wao wakisubiri kupewa huduma mbalimbali katika kituo cha afya
Pamoja na hayo, huduma zote zinazofadhiliwa na mapato ya kodi za wananchi zimeonyesha kuwa siyo endelefu kama ilivyoshuhudiwa na uanzishwaji wa uchangiaji wa gharama za huduma kwenye sekta mbalimbali kama vile elimu na afya.

Hifadhi ya jamii ina maana ni aina ya hatua madhubuti au shughuli zilizobuniwa za kuhakikisha kuwa wananchi wa jamii hiyo wanapata mahitaji yao ya lazima na ya msingi  na wanapewa kinga ya hifadhi ya kutokana na majanga ili kuwawezesha kuwa na kiwango cha maisha ya kuishi kulingana na mila na desturi za jamii.

Dhana au wazo la hifadhi ya jamii limekuwa likibadilika mara kwa mara kutokana na mila na desturi mpaka kuingia kwenye mambo ya kisasa. Baada ya jamii kuwa na maendeleo ya viwanda baada ya mapinduzi ya viwanda ya karne ya 19 watu wengi walitegemea kazi ya kuajiriwa ili kupata mahitaji yao ya muhimu ya kila siku na ikawa ndiyo chanzo cha kuachana na kutotegemea kutoka hifadhi ya jamii ya asili

hasi ya mapinduzi ya viwanda na matokeo ya mijini mambo haya yaliwavutia watunga sera kuhararisha mfumo wa hifadhi ya jamii kuwa sekta rasmi ambayo ilisaidia kutatua matatizo na mambo ya kijamii jamii yaliyojitokeza.

Hifadhi ya jamii inaelezwa maana yake kwa undani zaidi na shirika la kazi duniani (ILO) kama chombo cha kinga ambacho jamii hutoa kwa watu wake wanaomzunguka kwa kutumia vyombo vya umma mbalimbali dhidi ya majanga ya kiuchumi na kijamii ambayo yangeweza kusababishwa na kusimamishwa au kupungua kwa mapato ya kutosha yanayosababishwa kutokana na ugonjwa, uzazi, kuumia kazini, kukosa kazi, ulemavu, uzee, kifo, na kutoa huduma ya msaada wa matibabu kwa wale wenye watoto



Serikali kwa kusaidiana na taasisi zisizo za kiserikali zinatakiwa kuwajibika kwa kuwasaidia wazee kwa kutoa matibabu bure na pensheni ya kima cha chini kila mwezi kwa ajili ya kujikimu.
Mfumo wa hifadhi ya jamii wa ILO unazingatia na kusimamia juu ya mihimiri mitatu anasisiza kutumia vyanzo vya fedha kwa ajili kutoa kinga bora kwa wananchi. Nguzo hii inahitaji kutatua mahitaji muhimu ya makundi mbalimbali ndani jamii kwa ajili kipato na kiwango hatarishi. Mfumo huu unajumuisha yafuatayo

Hii inahusika kwa ajili ya kutoa huduma kama vile afya ya msingi, elimu ya msingi, maji, usalama wa chakula na huduma zingine kwa misingi ya kujaribia kama kweli ni muhitaji. Hizi huduma zinafadhiliwa na serikali na baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali (NGOs).

Muhimiri wa pili kwa kawaida ni wa lazima na unaitwa Tier Two- Mandatory Schemes. Unatakiwa kuchangiwa na mwajiri na mwajiriwa kwa pamoja wakati wa mwajiriwa anaendelea kufanya kwa ajili ya mafao ya muda mfupi na ya muda mfupi

Muhimiri wa tatu ni wa hiyari au wa nyongeza au ziada yaani (Tier Three - Voluntary or Supplementary Schemes). Mifuko ambayo iko chini ya muhimiri huu inajumuisha mifuko ya akiba, ushirika, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa, mifuko ya pensheni inayoendeshwa na waajiri makazini, mifuko ya pensheni watu binafsi: kama vile inayosimamiwa na waajiri, taasisi za kitaalamu, taasisi zote za kijamii, pamoja na watendaji wa taasisi za watu binafsi.

No comments :

Post a Comment