Majira Jumanne Desemba 25,2012
Hifadhi ya jamii ni chombo cha usimamizi na udhibiti wa
kuwakinga raia dhidi ya majanga ya kijamii. Huu mfumo umekuwepo hapa nchini
Tanzania umedumu hata kabla ya ukoloni Ambapo
maelezo mengi ya sera za hifadhi ya jamii zilikuwa zikiundwa na sheria
mbalimbali zilipitishwa juu ya hifadhi za jamii kwa ajili ya kuwakinga jamii
dhidi ya majanga mbalimbali kama vile kuumia ukiwa kazini, uzee na kupoteza
kazi iliyokuwa inakupa mapato ya kukuwezesha kuishi.
Baada ya uhuru sheria nyingi ziliundwa na zingine
zilirekebishwa upwa. Hizi zikiwa pamoja na sheria namba 57 ya 1962 ya severance
allowance; Mfuko wa taifa wa akiba ya wafanyakazi yaani National Provident Fund
NPF) sheria namba 36 ya mwaka 1964
iliyorekebishwa chini ya sheria Namba 2 ya mwaka 1975 ya kuwa shirika la
umma ambayo baadaye ilibadilishwa kuwa mfuko kamili wa hifadhi ya jamii yaani
National Social Security Fund (NSSF) sheria namba 28 ya mwaka 1997 unaoendeshwa
kwa utaratibu wa sheria za pensheni za bima; Pensheni za mashirika ya umma
Parastatal Pensions Fund (PPF) ya kifungu cha sheria namba 14 cha mwaka 1978;
Hizi zikiwa kama vile Master and Native Ordinance Cap 78 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha sheria namba 371 cha mwaka 1942, mfuko wa akiba kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali kifungu cha sheria namba 51yaani Provident Fund (Government Employees) Ordinance Cap 51, mfuko wa akiba ya wafanyakazi wa serikali za mitaa kifungu cha sheria namba 53 yaani Provident Fund (Local Authorities) Ordinance Cap. 53, na sheria ya malipo ya fidia ya mfanyakazi kifungu cha sheria namba 262 yaani Workmen’s Compensation Ordinance Cap 262.
Na sheria zingine zilizoudwa ni kama vile pensheni kwa
ajili ya watumishi wa umma sheria namba 2 ya mwaka 1999 yaani Public Service
Pension Fund (PSPF) iliyoibadili ile sheria ya Pensheni, Sura ya 371 ya mwaka
1954.; Mfuko wa bima ya afya wa taifa wa sheria namba 8 ya mwaka 1999
yaani National Health Insurance Fund
(NHIF), Mfuko wa pensheni kwa ajili watumishi wa serikali za mitaa (LAPF) chini
ya kifungu cha sheria namba 9 ya mwaka 2006 na
mfuko wa akiba ya wafanyakazi wa serikali yaani Government Employees
Provident (Fund GEPF) yaani utaratibu wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa na
Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa wafanyakazi wa serikali wasio kuwa
chini ya mpango wa pensheni ulioibadili ile sheria ya Pensheni ya mwaka 1942
Kwa sasa kuna mifuko mikubwa mitano ya pensheni ya
hifadhi ya jamii ambayo inatoa kinga ya hifadhi ya jamii kwa watanzania. Hiyo
mifuko ni kama vile mfuko wa pensheni wa mashirika ya umma yaani Parastatal
Pension Fund (PPF) ulioundwa kwa ajili ya kutoa huduma ya pensheni ya hifadhi
ya jamiii kwa wafanyakazi wote wa mashirika ya umma na wa sekta ya watu binafsi
na sekta ilisiyokuwa rasmi.
Mfuko wa pensheni wa serikali za mitaa yaani Local
Authorities Pensions Fund (LAPF) mfuko wa taifa wa bima ya afya yaani National
Health Insurance Fund (NHIF) unaotoa huduma ya bima ya afya kwa watumishi wote
wa serikali. Na mfuko wa akiba ya wafanyakazi kwa watumishi wa serikali yaani
Government Employees Provident Fund (GEPF)
Jumla ya idadi ya wanachama wa mifuko hii ya pensheni ya
hifadhi ya jamii kwa Tanzania ni watu 967,573 na imegawanywa kama ifuatavyo
NSSF ni 466,000, PSPF 254,559, PPF ni
144,014, na kwa LAPF 71,000 na GEPF ni 32,000. Hii inawakilisha kama asilimia
85 ya watu wote waliajiriwa kwenye sekta iliyokuwa rasmi
Juhudi za serikali katika kutoa huduma ya kinga ya
hifadhi ya jamii imeleta mafanikio makubwa ya maendeleo hapa nchini. Lakini kwa
sababu sera ya hifadhi ya jamii ya kudhibiti na kusimamia bado haijaanza
kutekelezwa inavyotakiwa tangia ianzishwe, udhaifu kwenye ngazi za utekelezaji,
muundo, na udhaifu wa sera zilizoridhiwa na mfumo wa hifadhi ya jamii kutoka
kwa wakoloni bado zinaendelea mpaka leo. Ingawa mdhibiti na msimamizi wa mifuko
hii ya hifadhi ya jamii yaani SSRA tangia imeanzishwa chini ya kifungu cha
sheria namba 8 cha mwaka 2008 ndio inaendelea kujipanga vizuri katika
utekelezaji wa usimamizi na udhibiti wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii
Taasisi za hifadhi ya jamii ya
jamii nchini Tanzania zimekuwa zikiwekeza orodha ya fedha kwa faida kwenye
mikopo, nyumba za kupangisha, hatifunganishi, kuweka akiba benki zote hizi
zimechangia maendeleo ya kiuchumi nay a kijamii.
Kumekuweko na ongezeko kidogo sana la kuelewa juu ya
mfumo wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, jinsi ya kujiunga
kuwa wanachama, vitega uchumi na shughuli mbalimbali za sekta. Sekta ya hifadhi ya jamii isiyo kuwa rasmi hasa kwa
makundi ya kusaidiana yamekuwa yakijipanga vizuri zaidi kwa sasa ukilinganisha
na hapo siku za nyuma.
Mapungufu yaliyomo kwenye mfumo
huu wa hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya hifadhi
ya jamii yakisimamiwa na mdhitibi na msimamizi wa hifadhi ya jamii. Idadi kubwa
ya watu
waliomo katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale tu ambao wameajiriwa
kwenye sekta iliyo rasmi, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu
kutoka katika sekta isiyokuwa kuwa rasmi inazidi kupungua kila siku kuwa
wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii badala ya kuongezeka
Hata hivyo inaonyesha kuwa
idadi kubwa ya mafao yanayotolewa na mifuko hii ya hifadhi ya jamii nchini
Tanzania yako chini ya kiwango cha shirika la kazi la dunia (ILO) yaani kwa
idadi ya mafao, ubora wa mafao, na kutokwenda na ukali wa maisha ya kila siku.
Mpaka sasa kuna chombo cha kudhibiti na kusimamia mashirika haya ya hifadhi ya
jamii ingawa hajaanza kuleta mabadiliko. Hivyo mpaka sasa haya mashirika ya
hifadhi ya jamii kila moja ina wizara yake inayoisimamia na kuwa utaratibu na
kanuni tofauti za uendeshaji wa mifuko hii. Matokeo yake ni kwamba kiwango cha
michango, mfumo wa mafao, na sifa za kupata mafao na hata mipako na vipa umbele
vinatofautiana kabisa kwa kila mfuko.
Mpaka sasa hakuna utaratibu ulioanzishwa wa kuruhusu haki
za mafao ya mwanachama kuhamishwa kutoka mfuko mmoja hadi mwingine. Matokeo
yake wafanyakazi wamekuwa wakipoteza baadhi ya haki zao za mafao wakati
wakihama kutoka sehemu moja ya mwajiri hadi mwajiri mwingine. Pia hii
imechangia sana kuongezeka kwa tabia ya kuondoa michango ya pensheni kabla
haijakomaa kiwango cha kuwa tayari kama mafao ya kustaafu.
Baadhi ya mifuko ya hifadhi ya
jamii wanachama wanakuwa hawana haki ya mafao yao ila wanachukulia kama
marupurupu. Kwa kawaida wanachama wanapoteza baadhi ya mafao yao kama wanaacha
kazi kabla hawajatimiza miaka yao ya kustaafu. Na mazingira mengine haki za
mafao ya mwanachama zinaaamuliwa na mwajiri kutegemeana na jinsi ya kuacha kazi
haya yote ni baadhi ya changamoto za mdhibiti na msimamizi wa mifuko hii ya
hifadhi ya jamii kuifanyia kazi. Mpaka sasa kuna baadhi ya
wafanyakazi na watumishi wa serikali wanaopata mafao au pensheni ya hifadhi ya
jamii yote kutokana na kodi za mapato ya wananchi ambapo hii ni mzigo mkubwa
kwa serikali hii ikiwa ni pamoja na pensheni ya viongozi wa juu serikali kama
vile rais, waziri mkuu yaani specified government leaders pension scheme,
pamoja pensheni za wanasiasa kama vile
wabunge yaani political leaders pension scheme.
Kumekuwa hakuna soko huru la hifadhi ya jamii ambalo
linaweza kuruhusu hata taasisi za watu binafsi au sekta ya watu binafsi
kuendesha mifuko ya hifadhi ya jamii kwa muda mrefu ingawa kwa sasa mdhibiti na
msimamizi wa mifuko hii ametoa uhuru wafanyakazi wapya kuchagua mfuko wa
hifadhi ya jamii anaoutaka pamoja na waajiri wapya kujiunga na mfuko wowote ule
kulingana na kifungu namba 30 cha sheria cha mwaka 2008. Miongozo ya uwekezaji
wa rasilimali za mifuko hii ya hifadhi ya jamii imeshaanza kutolewa tayari na
mdhibiti na msimamizi wa hifadhi.
Christian
Gaya ni Mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni. Kwa Maelezo Zaidi.
0655131341
No comments :
Post a Comment