Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres mjini Tunis,Tunisia, Agosti 27, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Rais wa Tunisia Kais Saied alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres kuhudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8), mjini Tunis,Tunisia, Agosti 27, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Tunisia, Mhe. Kais Saied alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais des Congres kuhudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8), mjini Tunis,Tunisia, Agosti 27, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo.NA OWM, TUNIS
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemshukuru Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kwa misaada ambayo nchi yake inaipatia Tanzania ili kuleta unafuu kwenye maisha ya wananchi wake.



















