President Samia Suluhu Hassan receiving a Special Audit Report from the Controller and Auditor General (CAG), Charles Kichere.Pages
Thursday, July 1, 2021
Special audit report at BOT reveals irregularities at Tanroads and TPA Report and TPA
President Samia Suluhu Hassan receiving a Special Audit Report from the Controller and Auditor General (CAG), Charles Kichere.WIZARA YA KILIMO YAENDESHA KONGAMANO KUHUSU MIFUMO YA CHAKULA

Mwakilishi wa Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Sera na Mipango
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Mbaraka Stambuli akifungua kongamano la
kujadili mifumo ya chakula kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini leo mjini
Njombe. 
Kinara wa Mifumo ya Chakula
(National Food System Champion) na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Neema
Lugangira akizungumza kwenye kongamano la mifumo Nyanda za Juu Kusini
leo mjini Njombe ambapo ametoa wito kwa wadau kuangalia mabadiliko ya
tamaduni ili kuwa na lishe bora nchini. 
Mwakilishi wa mratibu wa
Mifumo ya Chakula toka Wizara ya Kilimo Bi. Magret Natai akizungumzia
lengo la kongamano hilo ambapo amesema Tanzania inautoshelevu wa chakula
wa asilimia 126 lakini bado kuna tatizo la udumavu hivyo kuhitaji
mjadala wa kukuza uelewa juu ya lishe bora. 

Mwakilishi wa kikundi cha
Wakulima wa Parachichi Ruvuma Bw. Beno Mgaya akizungumzia umuhimu wa
matunda kwenye kuboresha mifumo ya chakula nchini. 

Picha ya pamoja ya wajumbe toka mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma,Mbeya na Songwe wanaoshiriki kongamano la kujadili mifumo ya chakula linaloratibiwa na Wizara ya Kilimo leo mjini Njombe kwa lengo la kujadili changamoto za mifumo ya chakula na lishe.
(Habari na Picha Wizara ya Kilimo)
*************************
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau inaendesha makongamano kuhusu mifumo ya
BALOZI SOKOINE AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA (PEACE CORPS)

Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa
Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes
katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine Ripoti ya Mwaka ya Shirika hilo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kumalizika kwa maongezi yao.
**************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea
MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO CHA USHIRIKIANO NGAZI YA MAKATIBU WAKUU BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS (SMZ)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akifungua kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 1, 2021 Jijini Dodoma, kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Shughuli za Serikali kwa pande zote mbili.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Idarous Thabiti Faini akifafanua jambo wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika tarehe 01 Julai, 2021 Dodoma.

Mkurugenzi wa Uratibu Sherehe za Kitaifa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bi. Riziki Daniel akichangia jambo kuhusu masuala ya uratibu wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ).

Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Raymond Kaseko akiwasilisha taarifa kuhusu Uratibu wa Shughuli za Serikali Bungeni wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika Dodoma.

Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Vonyvaco
Luvanda akiwasilisha kuhusu Muundo wa Majukumu ya Ofisi hiyo wakati wa
kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri
Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ).
Kaimu Murugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Issa M. Khamis akiwasilisha Muundo na Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) wakati wa kikao hicho.

Baadhi ya majumbe wakifuatilia kikao kazi hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akifafanua jambo kuhusu masuala ya kuratibu Serikali kuhamia Dodoma wakati wa kikao hicho.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda (katikati), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Idarous Thabiti Faini (kushoto kwake), Naibu Katibu Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kaspar Mmuya (wa pili kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu (Wa kwanza kushoto) pamoja na Afisa Utumishi Idara na Shughuli za SMZ Dar es Salaam Bw. Heri Khamis Makame (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki katika kikao hicho.
(PICHA ZOT NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
DK.HUSSEIN ALI MYINYI AMEKUTANA NA UONGOZI WA (ZIPA NA TIC)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisisitiza
jambo wakati alipokutana na kwa mazungumzo na Uongozi wa Mamlaka ya
kukuza Uwekezaji (ZIPA) pamoja na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) leo walipofika Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu]
01/07/2021. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi (kulia) leo amekutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji (ZIPA) pamoja na Uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 01/07/2021.
MANJU DUOX YAJIGAMBA KWA UBORA WA BIDHAA BORA MAONESHO YA SABASABA

Na Khadija Seif Michuzi Tv
TAASISI ya The warrior Women yawakaribisha wajasiriamali na wapenzi wa bidhaa zao katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam.
RAIS SAMIA APOKEA TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM WA MATUMIZI YA FEDHA NA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea
Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa
kufanyika mwezi Agost,2022, kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.
Albina Chuwa, leo Julai 01,2021 Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum inayohusu matumizi ya Fedha zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kati ya mwezi Januari na March mwaka huu, kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Charles Kichere Jijini Dodoma leo Julai 01,2021.
(Picha na Ikulu)
