Sunday, July 14, 2019

BoT YASITISHA AJIRA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIB CORPORATE BANK BW. FRANK NYABUNDEGE


    Bw. Frank Nyabundege
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesimamisha ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Bw. Frank Nyabundege kuanzia Julai 13, 2019 kutokana na
ufanisi mbovu wa benki.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano na Itifaki ya BoT leo Julai 14, 2019 imesema uamuzi huu umechukuliwa baada ya BoT kutoridhishwa na utendaji wa benki hiyo kama inavyopasa.
Taarifa hiyo imefafanua, kuwa uamuzi huo wa BoT umechukuliwa chini ya Kifungu namba 33 (1) na 33 (2) (f) vya Sheria ya Usimamizi wa Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Aidha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), chini ya kifungu cha 33 (2) (b) cha Sheria za Mabenki na Taasisi za Fedha, imeamua kumteua Bw. Fred Luvanda kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki kusimamia shughuli za kiutendaji za kila siku za benki hiyo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank.
Taarifa kamili ya BoT inapatikana hapo chini.

No comments :

Post a Comment