Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa
Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba
Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa
vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa
kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi.
Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.
.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta Sabasaba Moshingi akiongea na wana-saccos wa Manispaa ya
Kigoma-Ujiji, kabla ya kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/=kama
mkopo ili kuinua mitaji yao. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Issa Machibya
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa
Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama
wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania,
Timotheo Mwakifulefule.
Mmoja wa vijana ambaye
anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya
wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa
na serikali akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU
kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda
kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati
walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu
Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na
Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya askari wakijiandaa
kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na
Mipango Posta jijini Dar es salaam.
Wanafunzi hao wakifurumushwa na
polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila kibali kwenda kumuona
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Wanafunzi hao wakitoka mbio baada ya kuamriwa na polisi kuondoka eneo hilo na kutawanyika.
Askari polisi wakizunguka maeneo mbalimbali kuangalia hali ya usalama.
Polisi wakiwazuia wanafunzi hao na kuwaamuru kutawanyika kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
Mmoja wa polisi akiwaamuru wanafunzi hao kutawanyika eneo hilo.
Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Dar es Salaam.
Chama cha Watu Wenye Ualbino
Tanzania (TAS) wameiomba Serikali kuwasaidia kumtafuta Bw. Said Abdalah
Ismail (47) mkazi wa Kijiji cha Mbezi Mlungwana Wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani.
Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti
wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya
Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania
Girl Guide Association.
Wanachama wa Girl Guide
wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza katika kusherekea World
Thinking Day ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
Mama Salma Kikwete akiingia
katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide
kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu na kulia ni Mama
Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa Girl Guide
Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo
PICHA NA YUSUPH BADI
………………………………………………………………………………………………………………….
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano
yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video
iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw
na kusambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja
kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Kenya.
Video hii imeibua majadiliano
katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao
wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko
Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa
Mkoa wa Tanga katika kikao maalum kilichoangaliwa kwa ajili yake
kilichofanyika Ikulu ndogo mjini Tanga jana jioni Februari 28, 2016.
(Picha na OMR)
Wamawake wakiwa wametandika
khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari
29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea
mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali
ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake
hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini
hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Wamawake wakiwa wametandika
khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari
29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea
mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali
ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake
hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini
hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza
nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majliwa
akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa
ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili
kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa
kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari
29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja
wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari
29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili
ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza
umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa
Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika
ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na
Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na
mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua
rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika
hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo
endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo
Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na
Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi
Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika
hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo
endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo
Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti
kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki
Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika
hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo
endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo
Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith
Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili
kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya
viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha
hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya
Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili
kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya
viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha
hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya
Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.(Picha na OMR)
Makamu wa Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya
kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye
mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati
Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Picha na Mafoto
Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi
atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan
Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati
wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati
maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa
Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar . Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
zawadi, mshindi wa pili wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi
atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan
Tukufu, Ibrahim Omary, aliyepata pointi 90 kwa upande wa Tajweed, wakati
wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati
maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran
nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. Picha na Mafoto Blog
Baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal,
wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
Baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal,
wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea
zawadi kutoka kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar, wakati
wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha
Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu hayo
yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb
28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya
Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Al-had Mussa Salum. Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya
kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye
mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu. Picha na Mafoto Blog
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi, kufunga mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa
Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze
kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja
wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………
-
- Kwa
kuzingatia matakwa ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Kukuza Huduma za
Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 pamoja na Kanuni zake kupitia Gazeti la
Serikali 232 la tarehe 11Julai 2014, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu inakaribisha maombi ya kufanya shughuli za
Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira kwa kipindi cha mwaka 2016
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Bibi. Zawadi Msalla( katika) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu wanachi kutoa maoni juu ya Maboresho ya Sera ya Michezo
leo jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw.
Alex Makoye Nkenyenge na kushoto ni Afisa Uchumi Mwandamizi wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Richard Kundi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bw. Alex Makoye Nkenyenge akizungumza na waandishi wa Habari
|
Maelfu ya wakazi wa Moshi na wanariadha mbalimbali wakifuatilia mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushirika Mjini Moshi |
|
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano
ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo yaliyofanyika jana
kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Waziri
wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Nape mnauye ( katikati
mwenye kofia) akisubiri kufungua mbio za Tigo Kili half Marathon 2016,
mkoani Kilimanjaro, kulia kwake Meneja masoko Olivier prentout atika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi . |
|
Wanariadha wa Tigo Kili half Marathon wakisubiri kuanza mbio katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakikimbia mbio za Tigo half Marathon katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Meneja chapa Tigo, William Mpinga akimalizia mbio za kilometa 21 katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Wafanyakazi wa Tigo wakiwa kwenye water point kwa kutoa huduma kwa wakimbiaji katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Mzee mwenye Umri wa miaka 70 akiungana na wanariadha wenzake katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon katika mashindano hayo
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Wanariadha mbalimbali wakikimbia katika katika
mashindano ya Tigo Kili Half Marathon mashindano hayo yaliyofanyika
jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi
|
|
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez nae akionyesha ushirikiano mzuri kabisa na wananchi kwa wa kuungana nao katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akipata huduma ya kwanza wakati akikimbia na
kumalizia kilomita 42 za kili marathon katika mashindano yaliyofanyika
katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana |
|
|
Meneja mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akimaliza mbio za kilomita 42 za kili marathon katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana |
|
.Meneja
mkuu wa Tigo , Diego Gutierrez akipongezwa na mkiambiaji wenzie Mara
baada ya kumaliza mbio za Kilimanjaro marathon za kilomita 42 katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana |
|
Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Nape mnauye akimkabidhi akimkabidhi hundi ya sh Milion 2 Bernard Matheka (mkenya miaka 27) baada ya kuibuka mshindi kwa upande wa wanaume katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa kukimbia kilometa 21 na kutumia saa 1.14.55 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi
Baadhi ya washiriki waliopata bahati ya kuzawadiwa na Tigo kwenye mbio za Kili Marathon katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi
|
Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya
Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa
Septemba 2015.
Meneja
wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin,
(katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya
Go4school, Henning Nathow.
Katika
kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi
jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na
Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada
wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia
msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa
lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule
ambao wengi wao
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha
baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani).
Mbio
hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school
Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini
Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda
na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia
mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin
alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa
kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa
kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.
Alisema
kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya
kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama
hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia
hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika
kufanikisha mbio hizo.
Mwanzilishi
wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili
kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu
bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio
hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio
mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi
kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International
Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,”
Afisa
Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO
Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule
18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi
Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza
kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi
wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa
ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini
hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan
Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa
Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze
kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja
wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa ma Mwanaidi Mussa na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya
Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia
shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma
za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo leo
Februari 28, 2016
Chipukizi wa Umoija wa Vijana wa
CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum oleo
Februari 28,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana
wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa
ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani
humo leo Februari 28,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa
Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais
yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa
Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha
na OMR)
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na
wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za
Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8
walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka
nchini Kenya.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye
riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
Mshindi
wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama
ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisoma risala
mara baada ya kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo
aliwapongeza wahiriki wote, wadhamini na kuwataka Watanzania kutumia
mbio hizo kama fursa ya kuutangaza utalii uliopo nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.
Kigwangalla akitoa hutuba fupi wakati wa tukio hilo la kambi maalum ya
matibabu ya bure kwa wananchi wote iliyoandaliwa na Care Foundation kwa
kushirikiana na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mh.
Mussa Hazan Zungu.
………………………………………………………………………………………………………………………………….
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla amehimiza Jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara
kwa mara katika hali ya kubaini matatizo yanayowakabili ilikuchukua
hatua ikiwemo kupata tiba mapema
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo mapema leo Februari 28.2016, jijini Dar
es Salaam, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kambi maalum ya kupima
afya bure kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Ilala kwa
kuandaliwa na Care Foundation na wadau wengine wa afya ikiwemo Hospitali
ya Ebrahim Haji Chartable Health Centre ambao wanasimamia kutoa huduma
za matibabu kwa kushirikiana na taasisi zingine.
Akitoa
hutuba yake fupi, kwa wananchi mbalimbali walifika katika tukio hilo la
kupatiwa matibabu hayo ya bure, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla amesema
Jamii wanatakiwa kuwa na maisha yenye afya hivyo zoezi la kupima afya
mara kwa mara ni bora zaidi kaika kuimalisha afya ya mwili.
“Wananchi
wapo na wakati mwingi wakifanya shughuli zingine na hata muda kupima
afya inakuwa ngumu. Kukinga ni bora Zaidi kuliko tiba. Zoezi hili
litasaidia sana wananchi wengi na tunaomba muendelee na maeneo yote ya
nchi yetu.” Ameeleza Dk.Kigwangalla.
Aidha,
Dk. Kigwangalla amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hazan Zungu
kwa kuwezesha kuandaa zoezi hilo kwa kushirikiana na wadau hao kwani ni
mfano bora wa kuigwa na wabunge wengine pindi wapatapo nafasi ya
kutumikia jamii iliyowachagua.
Pia
katika zoezi hilo, Mbune wa jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla walipata wasaha wa kupima afya zao pamoja na
kutembelea maeneo ya kutolea huduma na kushuhudia namna huduma
zinavyotolewa kwa wananchi.
Kambi
hiyo ya matibabu, inatoa matibabu hayo bure kwa wananchi wote wanaofika
hapo ambapo pia mbali na matibabu wanatoa huduma ya dawa huku wakitoa
pia mawani kwa watu wenye matatizo ya macho. Watu mbalimbali
wamekaribishwa kupatiwa matibabu hayo ambayo pia yanatolewa na madaktari
bingwa wa magonjwa husika.
Tukio likiendelea
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwa katika meza ya kupima afya ya
mwili ikiwemo magonjwa yasio ambukiza kama vile Magonjwa ya moyo,
sukari, shinikizo la damu na mengine mengi katika zoezi linaliendelea
katika viwanja vya Bustani ya jiji iliyopo mkabara na Ukumbi wa
Karimjee.
Naibu Waziri wa Afya. Dk.Kigwangalla akiwa katika vipumo hivyo..
Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa Hazani Zungu, akipima afya katika zoezi hilo..
Dk.
Efrahim Mika Zaky wa Msimbazi Eyes Vision Center, (kushoto) akimpima
macho mmoja wa wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo linaloendelea
leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Bustani ya jiji, mkabara na
Ukumbi wa Karimjee.
Uchunguzi wa macho ukiendelea..
Dk. Efrahim Mika Zaky wa masuala ya macho, akimpima macho Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa zoezi hilo..
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa katika kupima macho kwenye kambi
maalum ya kutoa huduma za matibabu ya bure yaliyoandaliwa na Care
Foundation na wadau wengine katika viwanja vya Bustani ya Jiji, Posta
Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika moja ya sehemu ya kutolea dawa na
miwani kwa watu watakaobainika kuwa na matatizo katika macho..
Naibu
Waziri akipokea ua maalum kama ishara ya kukaribishwa katika ufunguzi
huo wa kambi maalum ya matibabu ya bure yaliyoandaliwa na CARE
Foundation na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mussa
Hazzan Zungu.(Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog/Mo tv