Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwasili Makao Makuu ya Shirika
la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam huku akilakiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu wakati waziri
huyo akiwa katika ziara yake ya kujifunza na kusikiliza Changamoto na
mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na shirika hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiuliza jambo kwa mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu wakati alipofanya
ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisaini kitabu cha
wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia
Mchechu wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli
zinazofanywa na shirika hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwa katika kikao na wakuu wa
vitengo mbalimbali wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua
shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa
habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC , kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu .
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC Upanga.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari hawapo pichani katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC
Upanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa na
waandishi wa habari wakati Naibu Waziri Angelina Mabula alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea shirika hilo
leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Muungano Saguya
katikati na kulia ni Yahya Charahani Maafisa kutoka shirika hilo la NHC.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada
kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika
mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar
es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku
Kuu ya Mwaka Mpya 2016.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto
na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi
katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha
jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
Sehemu ya makazi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando akifafanua jambo kwa
Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam(Hawapo Pichani).
Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa
Umma na Utafiti Rehani Athumani akiongea na Waandishi wa Habari
(Hawapo pichani) kuhusu maboresho katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Waandishi wa Habari wakifatilia
taarifa iliyokuwa ikitolewa na Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) Leo Jijini Dar es salaam
Picha na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
unategemea kuboresha baadhi ya huduma zao ifikapo 2016 ili kuongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma hizo kwa wananchi.
Akiyasema hayo leo Jijini Dar es salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Michael Mhando amezitaja baadhi ya huduma ambazo
wana mpango wa kuziboresha kwa mwaka 2016 zikiwemo za kuongeza huduma
ya matibabu ya moyo kwa kutumia bima ya NHIF,kutoa mikopo ya
dawa,kurekebisha mfumo wa ulipaji wa baadhi ya huduma pia kubadili
gharama za huduma ambazo zinalipwa kwa watoa huduma ili kuendana na hali
halisi ya mfumuko wa bei.
‘’mimi binafsi nimefurahishwa na agizo la
Mheshimiwa Rais kutengeneza maduka ya dawa kila Hospitali ya Mkoa na
nitakua tayari kushirikiana nao kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya
kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote ili kuboresha huduma za afya
kwa wananchi’’alisema Mhando.
Naye Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na
Utafiti Rehani Athumani amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili
zikiwemo za kukosekana kwa dawa katika hospitali husika pamoja na tabia
ya baadhi ya wanachama kugushi baadhi ya nyaraka wakati wa usajili.
Aidha,Bw. Rehani Athumani ametaja hatua
itakayochukuliwa ili kudhibiti ubora wa huduma zitolewazo na mfuko huo
kuwa ni kufanya ukaguzi wa kushtukiza ujulikanao kwa jina la kitaalamu
kama ‘Medical surveillance’ katika vituo vya matibabu ili kuona ubora wa
huduma wanazotoa kwa wananchi.
Katika kutoa huduma bora za afya kwa
wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utahakikisha kuwa hatua kali za
kisheria zitachukuliwa kwa watoa huduma ambao wataongeza bei za huduma
kwa wanachama wa mfuko huo na maboresho hayo hayataathiri kiwango cha
michango kinachotolewa na wanachama.
Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Mjengwablog
Ndugu zangu,
Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma
salamu za Mwaka Mpya kwa wajumbe wangu wa Mjengwablog, marafiki zangu
kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.
Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo.
Naandika salamu hizi nikiwa hapa Iringa, na nikiwa na mambo mawili ya kuwaeleza;
Mosi, napenda kuwahakikishia kuwa Mjengwablog/KwanzaJamii itaingia mwaka mpya wa 2016 na kasi zaidi ya mwaka jana. Tutazidisha ubunifu katika kuwaletea huduma mpya na bora zaidi.
Mosi, napenda kuwahakikishia kuwa Mjengwablog/KwanzaJamii itaingia mwaka mpya wa 2016 na kasi zaidi ya mwaka jana. Tutazidisha ubunifu katika kuwaletea huduma mpya na bora zaidi.
Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa
blogu ya kwanza hapa Tanzania kuja na ubunifu wa kuweka kurasa za mbele
za magazeti mwaka 2007. Mwaka huu tumekuwa blogu ya kwanza Tanzania kwa
kuwa wa kwanza kila alfajiri kuwaletea habari za magazetini zikiwa na
uchambuzi wa habari ku 3 ikiwamo uchambuzi wa katuni bora ya siku.
Mwakani tumedhamiria kuunganisha
huduma hizo na radio blogging ikiwa na maana ya kufanya chambuzi kwa
njia ya radio ya mtandaoni na kuposti ( KwanzaJamii Radio). Mengine
mapya ya kiubunifu yako jikoni, yatakuja kwa mwaka ujao, 2016.
Jambo la pili nililotaka kulisema
linahusu hali ya mtanziko wa kisiasa Zanzibar. Ni majuzi tu nilikuwa
Zanzibar kwa takribani juma moja. Nilitembea Zanzibar mjini na vijijini.
Hakika, sijawahi kupanda boti na
kuviacha visiwa vya Zanzibar nikiwa na shaka ya kitakachotokea nyuma
baadae. Safari hii niliondoka Zanzibar nikijisikia hivyo. Zanzibar
sikuikuta hali njema ya upepo wa kisiasa. Nakumbuka nikiwa kitongoji
kimoja pale Jambiani nilioongea na wenyeji walioonyesha shaka kwenye
mazungumzo. yao wakati wakiongea nami.
Pale Jambiani niliiona chuki
baina ya wenyeji iliyotokana na tofauti za kiitikadi. Chuki
iliyoonyeshwa hata kwenye maandishi ya kutani na kwenye milango ya
nyumba. Ni chuki iliyoonyeshwa hata kwenye mijadala ya mitandaoni ambayo
binafsi niliianzisha kwa madhumuni ya kuamsha fikra na kubadilishana
maarifa na uzoefu.
Niliyoiona si Zanzibar
niliyoifahamu. Bado naamini, Zanzibar imejaa watu wakarimu na wenye
upendo. Suluhu ya Zanzibar itapatikana na Wazanzibar wenyewe na kwa njia
ya mazungumzo hadi kufikia muafaka.
Na walio kwenye meza ya
mazungumzo wasitangulize maslahi binafsi. Kwenye kujadiliana ili kutatua
mgogoro pande husika ziwe tayari kupata na kupoteza. Si vema pia kwenda
kwenye meza ya mazungumzo ukihitaji jambo moja tu, kwamba kama
ukilikosa ndio mwisho wa dunia.
Na duniani hapa mengine
yaliyofutwa, na kama ni kisheria na yakachapwa hata kwenye gazeti la
serikali, basi, si rahisi yakarejeshwa kwa wino ule ule. Ni vema
ikatangulizwa hekima na busara. Ni vema na ni busara yakawekwa mazingira
ya, hatma ya yote, kuwa pande zinazokinzana zote zikaibuka washindi.
Na hakuna namna yeyote ile ya
kuvifanya visiwa vikawa tulivu bila ya uwepo wa makubaliano ya Serikali
ya Umoja wa Kitaifa ambapo viongozi wakuu wa pande zote mbili wafanye
kazi ya ziada ya kuwahimiza wananchi wao kuchimba makuburi marefu ya
kuzizika chuki zao baina ya wao kwa wao. Chuki zilizojengeka kwenye
misingi ya ubaguzi. Na sote tunajua dhambi ya ubaguzi, ni kama dhambi ya
mwanadamu kuonja nyama ya mwanadamu mwenzake, hawezi kuacha.
Ni iwekwe wazi, kuwa suala la
Muungano wetu halipaswi kuwa mjadala tena kama uwepo au usiwepo, bali ni
kwa namna gani tutauimarisha.
Maana, daima utabaki kuwa ukweli, kuwa jambo la Zanzibar ni letu Bara, na kinyume chake.
Maana, daima utabaki kuwa ukweli, kuwa jambo la Zanzibar ni letu Bara, na kinyume chake.
Na tuwe tayari kupambana hadi
risasi ya mwisho, na nguvu zote hasi, za ndani na nje ya mipaka yetu,
zinazotaka kututenganisha kwa misingi ya Uzanzibar, Upemba, Ubara na
hata udini.
Ni imani yangu, kama ilivyotokea huko nyuma, kuwa Zanzibar imeweza kuvuka mitihani migumu na ikasimama tena.
Naziona ishara za tumaini jipya
la Zanzibar linalokuja. Kwamba viongozi wakuu wa CCM na CUF Zanzibar
watazishinda nguvu hasi na zinazochagizwa na wahafidhina wa pande zote
mbili, hivyo, kupata formula mpya ya kuvivusha visiwa vya Zanzibar na
Pemba kutoka kwenye mtanzuko wa kisiasa uliopo sasa.
Mungu Ibariki Tanzania na Heri Ya Mwaka Mpya.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YAKE.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo
alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es
salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za
Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es
salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi
ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto)
kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe.
Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uratibu wa
Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto
akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya
mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo
mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo
alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es
salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na
baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara
ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Serikali imepiga marufuku
matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au
kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa
wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS)
ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia
ya Mtandao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na
Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa
ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA
Serikalini.
“Sasa kuna watumishi 7000
wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima
iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali
kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa
Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye
mawasiliano binafsi.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa
uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa
matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao
mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia
Barua Pepe za Serikali.
Mhe. Kairuki amewataka watendaji
wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili
kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa
na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.
“Katika hili ninatoa siku 60
muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale
watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa” Ameeleza Mhe. Angella.
Aidha, ametoa wito kwa watendaji
wa Wakala hiyo kuweka mpango wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa
kitaaluma watumishi waliopo kazini kwa kujenga utaratibu wa
kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na
utendaji wa Wakala hiyo.
Mhe. Kairuki amewataka kuwa
wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana
ya Serikali mtandao ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya
fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa
kupitia matumizi ya TEHAMA.
Akizungumzia kuhusu ununuzi wa
vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili
kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika
kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa
bei ya kawaida.
“katika hili Serikali itachukua
hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise
mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya
ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na
manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha”
Amesema Serikali itaendelea
kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata
huduma hizo mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi
wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov) kuwa wabunifu katika kutengeneza
programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata
huduma.
Aidha, katika hatua nyingine
ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na
majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na
kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo
ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma
zote ziweze kupatikana katika eneo moja na kuondoa urudufu wa mifumo
iliyopo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya
utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto
mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata
ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.
Amesema kuwa Wakala hiyo
inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi
kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la
huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.
Aidha amesema kuwa Wakala ya
Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya
matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali
vinazingatiwa.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI ASISITIZA UTENDAJI KAZI WENYE TIJA
Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Watumishi wa Jeshi la
Magereza(hawapo pichani) kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na
kuukaribisha Mwaka mpya 2016. Baraza hilo limefanyika Desemba 31, 2015
katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Askari wa vyeo mbalimbali wa
Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
wakati akitoa hotuba yake kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na
kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakiwa timamu kumpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akiwasili tayari kwa
kulihutubia Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa
2016.
Maafisa ngazi ya juu wa Jeshi la
Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi aliyoitoa Kamishna Jenerali
wa Magereza, John Casmir Minja(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
…………………………………………………………………………………………………
Na Lucas Mboje, Dar es Salaam
WATUMISHI wa Jeshi la Magereza
wametakiwa kuzingatia utendaji kazi wenye tija mahala pa kazi na kuacha
kufanya kazi kwa mazoea(Business as usual).
Rai hiyo imetolewa na Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye
Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016 katika
Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini, Dar es Salaam.
Jenerali Minja amewaagiza
Watumishi wote wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa wanawajibika kwenye maeneo
yao ya kazi ili kufikia ufanisi uliotarajiwa pamoja na kutumia vizuri
rasilimali za Ofisi kwa manufaa yaliyokusudiwa.
“Utekelezaji wenu wa kazi za kila
siku lazima uwe na tija na uendane sambamba na kasi ya Serikali ya
Awamu ya Tano ili kufikia ufanisi unaotarajiwa”. Alisema Jenerali Minja.
Aidha Jenerali Minja amezungumzia
baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa Mwaka 2015 ambayo ni pamoja na
kukamilika kwa Sera ya Taifa ya Magereza ambayo italiwezesha Jeshi hilo
kutekeleza mpango wake wa Maboresho ya maeneo mbalimbali, kusainiwa kwa
Mkataba na Kampuni ya Poly Teknology ya China itakayojenga nyumba 9,500
za Makazi ya Maafisa na Askari, kusainiwa kwa Mkataba wa Magari 9,05 na
Kampuni ya Ashok Leyland ambapo magari hayo yanatarajiwa kupokelea
mapema mwakani.
Mafanikio mengine ni pamoja na
Usajili wa kudumu wa Chuo cha Urekebishaji ambapo Chuo hicho kitatoa
elimu stahiki ya Urekebishaji itakayotambulika ndani na nje ya Nchi,
Jeshi la Magereza limepeleka Maafisa wake kwenye shughuli za Ulinzi wa
Amani kwenye nchi mbalimbali zenye migogoro, Jeshi limeingia ubia na
Wawekezaji mbalimbali katika miradi ya Kilimo, uchimbaji madini ya
chokaa, ujenzi wa maduka makubwa(shopping Malls) katika Mikoa ya
Morogoro na Kilimanjaro ambapo miradi hiyo itakuwa na manufaa makubwa
kwa Jeshi.
Vilevile Jeshi limefanikiwa
kuandaa Maandiko mbalimbali ikiwemo andiko la kujitosheleza kwa chakula
na miradi minane ambayo miradi hiyo ikiwezeshwa inaweza kuongeza thamani
za mali zinazozalishwa na Jeshi hilo.
Aidha Jenerali Minja alieleza
changamoto mbalimbali ambazo Jeshi hilo linakabilianazo ambazo ni ufinyu
wa bajeti, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri, ukosefu wa zana za
kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kuathiri Uzalishaji, tatizo la
miundombinu ya magereza na msongamano magerezani hali inayopelekea kwa
kiasi fulani kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
John Minja ametoa Salaam za kheri ya Mwaka mpya 2016 kwa Watumishi wote
wa Jeshi hilo na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na
Taratibu zinazotawala uendeshaji wa Jeshi la Magereza.
TAARIFA MUHIMU KWA UMMA KUTOKA UTUMISHI
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
inawatahadharisha wateja na wananchi wote kujihadhari na watu wanaotumia
jina la ofisi kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa
kujitambulisha kuwa ni watumishi wa ofisi hii. Imebainika miongoni mwa
wanaotapeli anatumia jina la James Josephat na kujifanya ni mtumishi wa
masijala. Namba ya simu inayotumika kutapeli ni namba 0657 888 277.
Ofisi haina mtumishi mwenye jina hilo, na huduma za ofisi hazitolewi kwa
ada ya aina yoyote. Ofisi inawatahadharisha wadau na wananchi
kuzingatia taratibu zilizopo na kuelewa huduma hazitolewi kwa malipo ya
aina yoyote. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Kny: Katibu
Mkuu-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
POLISI ARUSHA YASHTUKIA “DILI”
Askari wa Jeshi la Polisi wa wilaya ya Arusha na
vikosi vingine wakiwa wanamsikiliza Afisa Masoko wa URA SACCOS toka
makao makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe alipokuwa anatoa elimu hiyo
katika ukumbi wa bwalo la Polisi uliopo jijini hapa. (Picha na Rashid
Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mmoja wa wanachama cha Ura
saccos CPL Ezekiel akiuliza swali lililokuwa linamtatiza kwa muda mferu
ambalo baadae lilijibiwa vizuri na Afisa Masoko huyo toka makao makuu
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi
Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko akitoa ufafanuzi
kwa askari waliohudhuria kikao hicho juu ya Ura Saccos kulia kwake ni
Mkaguzi wa Polisi shabani Jumbe ambaye pia ni Afisa Masoko wa chama
hicho. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Baadhi ya askari wakiwa wanajaza fomu za Ura
Saccos kwa ajili ya kujiunga na chama hicho mara baada ya kupata elimu
iliyoeleweka toka kwa Afisa Masoko toka Makao makuu Mkaguzi wa Polisi
Shabani Jumbe. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
………………………………………………………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ikiwa tunauaga mwaka 2015 na
kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 masaa machache yajao baadhi ya askari wa
Jeshi la Polisi Mkoani hapa wanaonekana kufurahia baada ya wengi wao
kupata elimu ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Ura Saccos
iliyokuwa inatolewa na Afisa Masoko na uelimishaji wa Chama hicho toka
Makao Makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe.
Elimu hiyo iliyotolewa na Afisa
Masoko huyo, iliwafanya askari zaidi ya 100 wabadilishe mawazo ya
kujitoa kwenye Chama hicho na badala yake walichukua fomu za kujiunga na
Chama hicho kwa ambao hawakuwa wanachama na kwa wale ambao walikuwa
wanachama waliamua kuongeza kiwango cha makato kwa asilimia 50 hadi 90
huku wengine wakiendelea kupiga simu kwa msimamizi wa Ura Saccos mkoa wa
Arusha PC Said wakitaka fomu za kujiunga na Chama hicho.
Awali akitoa elimu hiyo katika
wilaya za Arumeru, Monduli, Longido na Arusha mjini, Afisa Masoko huyo
alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni ufinyu wa elimu kwa wanachama na
wasio wanachama na kufafanua kwamba wameamua kutoka ofisini na kuwafuata
mikoani kwa lengo la kuwaelimisha ili waone umuhimu wake.
Alisema wanachama wengi
walikuwa hawajui sababu zinazosababisha kupata mikopo midogo ndani ya
Chama hicho kwamba zinatokana na kiasi cha Akiba wanazoweka kwa mwaka
kuwa ni kidogo huku akisema wengi wao wanaweka elfu kumi kwa mwezi.
“Sasa mfano utakuta mwanachama
anaweka Tsh. 10,000/= Kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja anajikuta ana Tsh
120,000/= alafu baada ya miaka mitatu anaomba mkopo hivi unafikiri
utapata kiasi gani”? Alihoji Afisa Masoko huyo Shabani Jumbe ambaye pia
ni Mkaguzi wa Polisi.
Alisema Chama hicho kwa sasa
kimeweka utaratibu wa kumwekea Mwanachama 3% kwa kila laki tano ambayo
atakuwa ameweka akiba ndani ya chama hicho ambayo inaitwa riba juu ya
Akiba.
Akitoa ufafanuzi juu ya
utaratibu wa Mwanachama kutoa Akiba yake ndani ya siku 90 na si chini ya
hapo alisema hii inatokana na idadi ya wanachama wanaochukua mikopo
kuwa kubwa lakini pia inatoa fursa ya kukusanya madeni toka kwa
wanachama wengine waliokopa.
“Wanachama wengi wanashindwa
kutofautisha kati ya Akiba na Amana ambapo kwenye Amana mwanachama
anaweza kutoa fedha yake wakati wowote na haina notisi ya siku 90 lakini
kwenye Akiba utaratibu wetu ni siku 90 lakini pia karibu askari 21,000
kwa mwezi wanachangia Tsh 10,000 hali ambayo inakwamisha uwezo wa chama
kukua na kusababisha kushindwa kutoa mikopo mikubwa kwa wanachama”.
Alisema Afisa Masoko huyo.
Alisema mbali na kuweka akiba
kwenye chama hicho lakini pia wanachama wanatakiwa wawe wananunua hisa
zaidi ya zile za msingi ambazo ni 20 lakini tu zisizidi 20% ya hisa zote
za chama hicho ili kuondokana na hali ya uchangiaji tu bali pia wawe
wamiliki wa sehemu ya chama na mwisho wa mwaka kupata gawio.
Alisema uwepo wa Chama hicho
ambacho kwa sasa kina wanachama wanaokadiriwa 34,000 kimesaidia kuweka
usimamizi wa nidhamu ya fedha Kwani ni watu wachache wenye uthubutu wa
kuwa na utamaduni wa kuweka Akiba kila mwezi na kuongeza kwamba mpaka
sasa toka mwaka 2007 kimetoa mikopo kwa wanachama wake kiasi cha Tsh.
82.3 bilioni.
Naye Mkuu wa kituo kikuu cha
Polisi cha Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko ambaye
kitaaluma ni Mhasibu aliwataka askari kuongeza viwango vya akiba zao
hali ambayo itawasaidia kupata mikopo mikubwa na pia kunufaika na riba
ya aslimia tatu ya kila mwezi kwa watakaoweka kuanzia Tsh. 500,000/=.
Alisema awali askari walikuwa
na wasiwasi juu ya Chama hicho lakini baada ya elimu walielewa hivyo
aliwataka wachangamkie fursa hiyo ya kupata mikopo yenye riba nafuu.
Kwa upande wao baadhi ya askari
waliopata elimu hiyo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa huu walisema
wameweza kubadilishwa mawazo yao ya kutaka kujitoa kwenye chama hicho na
hivyo wameamua kuongeza akiba hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wao
siku za usoni.
“Nashukuru sana kwa Inpekta
Shabani Jumbe kutoa elimu hii binafsi nimeifurahia na kuongeza ufahamu
kwa upande wangu hali iliyonipa hamasa ya kuchukua fomu na kuongeza
akiba yangu toka 10% hadi 50% kwa mwezi”. Alisema Asia Matauka ambaye ni
Mkaguzi wa Polisi na kushauri kwamba wajenge matawi katika mikoa yote.
“Baada ya kupata elimu
nimegundua kwamba Chama hiki cha ushirika ni chama muhimu sana kwa
askari na mimi nimeamua kuongeza akiba yangu toka elfu 10 hadi elfu 80
kwa mwezi” .Alisema D/C Anzelim toka wilaya ya longido.
TAHADHARI YA JESHI LA POLISI KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA
Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015
na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, wananchi hutumia muda huo kwenda
katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya
starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia
fursa hiyo kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.
Jeshi la Polisi nchini,
limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya
uhalifu vitakavyojitokeza hususani katika kipindi hiki cha kuelekea
mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo
yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine
yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa
tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za
haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu
katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi
endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.
Pia, Jeshi la Polisi
linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa
makini na kuzingatia sheria za usalama barabar
ani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
ani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Vilevile, wananchi kuacha tabia
ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote
atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA FEDHA (JFC) WAFANYIKA LEO OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (mbele),
akitafakari jambo wakati wa kikao cha kujadili changamoto na utekelezaji
wa majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) jijini Dar es Salaam leo,
kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Abdulrahaman Jumbe. (Picha na
OMR)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (katikati),
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC)
katika Mkutano wa kujadili changamoto na utekelezaji wa majukumu ya
Tume hiyo. (Picha na OMR)
Benki ya maendeleo ya kilimo kuanzisha ofisi za kanda
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara
wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal
(Kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Benki,
Bibi Neema Christina John (aliyevaa miwani) wakati wa uhakiki wa fomu
zilizojazwa na moja kati ya vikundi vilivyofanikiwa kupata mkopo kutoka
Benki hiyo.
Mwanasheria mwandamizi wa TADB,
Bibi Salome Masenga (Kulia) akimuelekeza mmoja wa wanakikundi waliopata
mikopo kutoka Benki hiyo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto)
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Kasunga (Kulia).
Picha ya pamoja
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Iringa
Benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) imesema hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa
imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima nchi
kote.
Mikakati hiyo iliwekwa bayana na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila
wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na
wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa,
wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Bibi Kurwijila alisema kuwa TADB
inalenga kutelekeza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza
changamoto zinazowakabili wakulima nchi kote.
Aliongeza kuwa kwa sasa Benki inalenga kusambaa nchi nzima kwa kuanzisha Ofisi za Kikanda ndani ya miaka mitano ijayo.
“Tunalenga kuwafikia wakulima
wote nchini kadri siku zinavyoendelea kwenda na kutegemea mtaji
unavyoongezeka ama upatikanaji wa fedha toka vyanzo mbali mbali ili
kuweza kuwawezesha kumudu shughuli zao za kilimo,” alisema.
Aliongeza kuwa Benki inaleenga
kuwajengea uwezo na kuanzisha Programu Maalumu ya Vijana wajihusishao na
shughuli za Kilimo cha kibiashara na kushirikiana na wadau wengine
kuhuisha shughuli za umwagiliaji na miradi ya kisasa ya umwagiliaji.
Malengo mengine ni kutafuta fedha
toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha
Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye
mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na
Minne (14) ya Mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia
kuwaunganisha Wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kwamba Benki
yake imedhamiria kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo
nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo
cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na
kupunguza umaskini nchini.
Bw. Samkyi alisema TABD
imejizatiti kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mapinduzi ya kilimo kwa
kuongeza tija na upatikanaji wa mikopo ya riba nafuu maalum kwa sekta ya
kilimo, kama njia ya kuleta Mapinduzi yenye tija kwa wakulima nchini.
“Benki imejipanga kutoa mikopo
yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Wakulima wadogo
wadogo, wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa
fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani katika tasnia za kilimo,
mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bw. Samkyi.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba
kwa kuanzia walengwa wakuu wa TADB ni wakulima wadogo wadogo, hatahivyo,
hata wale wakulima wa kati na wakubwa watahudumiwa.
Bw. Samkyi imejidhatiti katika
kufanya tathmini ya kina katika mnyororo mzima wa thamani ili kutambua
mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza
thamani na ushindani kwenye masoko.
“Sera ya TADB ni kutathmini
mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji
utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani
kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza
umaskini,” aliongeza.
Katika hafla hiyo, jumla ya
vikundi nane (8) vyenye jumla ya wakulima wadogo wadogo 857, vilimiza
vigezo na kupewa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.
Kwa mujibu wa Bw. Samkyi kabla ya
kutoa mikopo hiyo, benki iliwatembelea na kutoa elimu kwa wakulima
jinsi ya kuimarisha vikundi vyao, ambapo jumla ya vikundi 89 vyenye
jumla ya wanakikundi 21,526 vilifikiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mama
Amina Masenza amewaasa Wakulima wote nchini kutumia vizuri mikopo
wanayopewa ili kuweza kutimiza malengo yao binafsi na ya Serikali katika
kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni
endelevu nchini Tanzania.
Mama Masenza alisema kuwa
wakulima wakitumia mikopo waliyopewa kwa malengo husika watafika mbali
na kuweza kuchagiza mikakati ya Benki hiyo katika kusaidia Mapinduzi ya
Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kilimo kibiashara ili
kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
“Naamini, wakati Benki ya
Maendeleo ya Kilimo itapoanza kufanya tathmini ya mikopo hii iweze kuona
matunda ya uwekezaji wake hasa kwa nyie ambao mmeweza kubahatika kupata
fursa ya awali kabili kunufaika na huduma za TADB,” aliwasihi.
Mama Masenza aliwaomba wakulima
hao kuwa Mfano Bora na wanaojitambua vilivyo, hasa nia ya kutoka katika
kiwango fulani cha maisha kwenda katika hatua nyingine za juu zaidi
kimaisha kwa kuongeza kipato na ubora wa kimaisha kwa ujumla kupitia
huduma za TADB.
“Nawasihi kutotumia pesa hizi
kinyume na malengo yaliyokusudiwa, kwani kwa kufanya hivyo, siyo tuu
tunaiua Benki yetu bali pia tunajimaliza wenyewe kiuchumi. Wito wangu
kwenu ni kujipanga kwa dhati ili kuweza kutimiza malengo makuu ya mikopo
hii ambayo ni kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini
kwa kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia
maendeleo ya kilimo nchini,” aliongeza.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini
Lindi. Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu
ya Serikali, katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa
maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua endelevu
Droo ya nne ya promosheni ya “Jaza Mafuta na Ushinde” ya GAPCO yafanyika jijini Dar es Salaam
Meneja
Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe
kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya
“Jaza Mafuta na Ushinde” inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za
mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa
michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa
Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.
Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde afanya ziara makao makuu ya Tigo leo
Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo katika makao makuu ya Tigo kijtonyama jijini Dar es laam |
JK,WAZIRI LWENGE WAKAGUA MITAMBO YA MAJI WAMI,CHALINZE
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne,
Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge
wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika
Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.
Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji
Wakiwa katika picha ya pamoja
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne,
Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto
kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami,
katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.
RAIS MAGUFULI ATANGAZA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu
Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
wakisikiliza kwa makini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya
Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya
Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishuhudia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Mara baada ya kumkabidhi orodha ya Makatibu
na Manaibu Katibu Wakuu aliwateua leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha
zote na IKULU
………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na
manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi – Ombeni Sefue
- Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
- Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
- Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu – Elimu)
- Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)
- Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu – Sera)
- Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu – Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu – Uvuvi)
- Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu – Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu – Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu – Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)
- Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)
- Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)
- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu – Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu – Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)
- Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)
- Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu – Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu – Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)
Mhe. Kairuki aendelea na ziara katika taasisi zilizo chini ya ofisi yake kuhimiza uwajibikaji
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na
watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (wa pili kulia)
akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto)
akimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala
alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitazama nyaraka
inayoandaliwa kutunzwa katika nakala laini (soft copy) alipoitembelea
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitazama
moja ya kifaa cha kutunzia kumbukumbu alipoitembelea Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.
WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA MAOFISA BIASHARA MANISPAA DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa
ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa
ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa
Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu
katika utoaji wa leseni za biashara.
Kutokana na hali
hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu
Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa
kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa
dhidi yao.
Agizo hili limetolewa na Mhe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi
kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya
rushwa.
Katika uchunguzi ambao umefanyika
katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na
maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za
msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.
Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha
wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni
ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
Mhe. Simbachawene ametoa agizo
kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na
kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais – TAMISEMI
30 Desemba, 2015
Watakaofanya fujo mkesha wa mwaka mpya kukiona
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Jeshi la Polisi
Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya
fujo wakati wa mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa
watakaokaidi amri hiyo.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa
matairi ya gari, upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zaweza
kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
“ Ni baraka
zaidi kusherekea sherehe kama hizi kifamilia na sio vizuri kuingia mwaka
mpya ukiwa mahabusu, huo ni mkosi” Alisema Kamishna Kova.
Kamishna
Suleiman Kova aliongeza kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni
pamoja na Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya
ulinzi shirikishi pamoja na kutumia ndege za Polisi kufanya doria ili
kuhakikisha kuwa wanailinda amani na kudhibiti aina yoyote ya uhalifu
utakaojitokeza.
Aidha Kamishna
Kova amesisitiza kuwa vituo vyote vya polisi vitakuwa wazi masaa 24 ili
kuwawezesha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapopata matatizo au
wanapoona dalili zozote za uvunjifu wa amani pia amehakikisha kuwa fukwe
zote za bahari na maeneo yote yenye mikusanyiko yatalindwa.
Katika
kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka wa 2015 Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es salaam limetoa rai kwa wananchi kushirikiana na Jeshi
hilo katika kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa haraka pindi waonapo dalili
za uvunjifu wa amani.
WAZIRI WA AFYA ,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)
Waziri wa Afya, maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la
kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD
Prof.Idris Mtulia
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi
wa maghala hayo ,kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto
ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya
serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo
Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa
Waziri
Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi
ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya
Afya)
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya
Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali
linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri huyo ameeleza hayo baada
ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu
wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji
mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali na hilo, waziri huyo wa
Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na
serikali kwaajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa
hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema,
huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika hatua nyingine ameishauri
Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa
moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati
wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo
zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza
kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa
inazofikisha.
Waziri huyo ambaye alifuatana na
Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya
kuhifadhia dawa ya Makao Makuu, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na
kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine
ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye
vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na
kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa
hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha
kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli
alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani
mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia