Msajili wa Hazina, Bw. Athumani
Mbuttuka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini
Dodoma baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB
Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani
Mbuttuka (kulia), akisikiliza jambo baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa
Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), jijini Dodoma.
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani
Mbuttuka, wa tatu kushoto na Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw.
Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi
baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate,
katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
SERIKALI
imziunganisha benki za TPB Bank Plc pamoja na TIB Corporate ili
kuimarisha
utendajikazi wa benki hizo na kuhimiri ushindani wa
kibiashara kwenye sekta ya fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Athuman Mbutuka alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari.
Aidha Mbutuka
amesema kuwa Kufuatia uamuzi huo leo Juni Mosi mwaka huu, benki ya TPB
itachukua mali na madeni ya benki ya TIB huku serikali ikisisitiza
kulinda maslahi ya wafanyakazi wote kwenye benki hizo.
Mbutuka
amesisitiza kuwa maslahi ya wenye amana na wateja wote yatalindwa kwa
mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa benki na taasisi za
fedha.
“Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mashirika
na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu
yanayofanana kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za
uendeshaji,” ameeleza Mbutuka.
Mbutuka ameongeza
kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa
ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na kitaswira ili benki iweze kuhimili
ushindani kwenye sekta ya fedha nchini
Mbutuka
amehitimisha kwa kuwatoa hofu wateja wa benki wa TPB na TIB wataendelea
kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa
vinginevyo na huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote kutokana na
mabadiliko hayo.
No comments :
Post a Comment