Helikopta hiyo ikiwa chini baada ya kuanguka
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RUBANI wa helikopta ya Doria ya Mamlaka ya
Wanyamapori Nchini, (TANAPA), Roger Gower raia wa Uingereza ameuawa baada ya
kupigwa risasi akiwa angani na watu wanaosadikiwa kuwa majangili kwenye pori la
akiba maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu majira ya jioni Januari 30,
2016.
Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan
Shana ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema, askari mmoja wa wanyamapori
aliyekuwemo ndani ya helikopta hiyo amejeruhiwa.
“Helikopta hiyo haikudunguliwa, bali risasi
ilimpata Rubani na hivyo akauawa na helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.”
Alifafanua Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Simiyu, Jonathan
“Tutawasaka pori kwa pori, pango kwa pango,
kijiji kwa kijiji hadi tuwatie mbaroni wahalifu hao. Tumeleta FFU wenye silaha
za nkutosha, ili kutekeleza amri ya kamanda IGP, Kamanda DCI na RPC, ndio maana
tuko hapa na silaha nzito.” Alisema Mkuu huyo wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, walifika eneo la
tukio na kushngazwa na tukio hilo ambapo waziri alisema, sasa wahalifu hawa
wamefikia kiwango cha juu cha uhalifu hadi kuhujumu teknolojia ya kuhifadhi
mazingira, kwa kuwashambulia watendaji wetu, Waziri alisema kwa huzuni na
kuongeza
Serikali haitavumilia uhalifu huo na kuahidi
kuwasaka popote walipo.
Hili ni tukio la kwanza kwa majangili kutungua
kushambulia helikiopta ikiwa angani na kusababisha kifo.
Waziri Profesa Maghembe, akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
Waziri akionyeshwa sehemu risasi ilipopenya kwenye helikopta hiyo
Askari na maafisa wa serikali wakionyeshana sehemu helikopta hiyo ilipopigwa risasi na kuanguka baada ya rubani kuuawa