Pages

Monday, June 1, 2020

SERIKALI YAIMARISHA UTENDAJI WA BENKI ILI KUHIMIRI USHINDANI WA KIBIASHARA


Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka (kulia), akisikiliza jambo baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma.
Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, wa tatu kushoto na   Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi baada ya  kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
SERIKALI imziunganisha benki za TPB Bank Plc pamoja na TIB Corporate ili kuimarisha
utendajikazi wa benki hizo na kuhimiri ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Athuman Mbutuka alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari.
Aidha Mbutuka amesema kuwa Kufuatia uamuzi huo leo Juni Mosi mwaka huu, benki ya TPB itachukua mali na madeni ya benki ya TIB huku serikali ikisisitiza kulinda maslahi ya wafanyakazi wote kwenye benki hizo.
Mbutuka amesisitiza kuwa maslahi ya wenye amana na wateja wote yatalindwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa benki na taasisi za fedha.
“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji,” ameeleza Mbutuka.
Mbutuka ameongeza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la  kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na kitaswira ili benki iweze kuhimili ushindani kwenye sekta ya fedha nchini
 Mbutuka amehitimisha kwa kuwatoa hofu wateja wa benki wa TPB na TIB wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo na huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote kutokana na mabadiliko hayo.

No comments:

Post a Comment