Tuesday, March 3, 2020

MADAKTARI BINGWA WAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA VITUO VYA AFYA MANISPAA YA UBUNGO

 Daktari Bingwa akitoa huduma kwa wananchi katika Kituo cha Afya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam ikiwa  ni kusogeza huduma za afya za kibigwa kwa wananchi na kupunguza  mrundikano  katika hospitali na pamoja na hospitali za Rufaa.
 Huduma mbalimbali zikiendelea katika Kituo cha Afya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakisubiri huduma za Kibingwa  katika Kituo cha Afya Mbezi Luis wakati Madaktari Bingwa walipofika katika hicho.Manispaa ya Ubungo imeanza kutoa huduma za kitabibu katika vituo vya Afya vilivyopo katika Manispaa hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa Ubungo Beatrice Dominic amesema yoezi hilo limeanza leo katika kituo cha Afya Mbezi Louis na litakuwa la wiki tatu. 
Amesema katika Wiki ya pili huduma zitahamia kituo cha Afya Kimara na wiki ya tatu litamalizia katika kituo cha Afya Makurumla. Dominic amesema huduma za kibingwa zitakuwa zikitolewa bure katika wiki zote tatu. 
Aidha amesema Madaktari bingwa watakaokuwa wakitoa huduma katika vituo hivyo ni madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto, madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na wataalam wa upasuaji.
Amesema lengo ya kupeleka Madaktari Bingwa ni kusogeza huduma za kibingwa kwa  wananchi wote waliopo Manispaa ya Ubungo pamoja kutaka  wananchi hao kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata huduma hii kutoka kwa madaktari hawa bingwa.

No comments :

Post a Comment