Tuesday, March 3, 2020

BENKI KUU KUJA NA TOLEO JIPYA LA SHERIA YA USIMAMIZI WA MADUKA YA FEDHA ZA KIGENI (BUREAU DE CHANGE BAADAYE MWAKA HUU


Meneja wa Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, akiwasilisha mada kuhusu "Usimamizi wa sekta ya fedha na maduka ya kuendesha fedha za kigeni" kwenye semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha.

Semina ikiendelea.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Meneja wa Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, akiwasilisha mada kuhusu "Usimamizi wa sekta ya fedha na maduka ya kuendesha fedha za kigeni" kwenye semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja, akizungumza wakati wa semina hiyo Machi 3, 2020.

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha

SHERIA ya usimamizi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ya mwaka 1992 itafanyiwa mapitio baadaye mwaka huu na patakuwa na toleo jipya ili kuendana na wakati, Meneja wa Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, amesema.
 Bw. Tarimo amesema toleo la mwaka 2019 kuna mabadiliko kadhaa yalifanyika na mojawapo ni kumeondolewa madaraja (Classes) ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Alisema wakati kwenye kanuni za mwaka 2017 kulikuwa na  leseni daraja A na daraja B, ambapo leseni daraja A waliruhusiwa kufanya miamala ya kubadilisha fedha za kigeni papo kwa hapo (Spot purchase ans sells of foreign currency) tu, na leseni daraja B, waliruhusiwa kufanya miamala ya papo kwa hapo na kufanya Money Transfer.

Hata hivyo Bw. Tarimo amesema kwenye kanuni za mwaka 2019 leseni za madaraja haya ziliondolewa  na imebaki daraja moja tu na hii ilitokana na operesheni ya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni mwaka 2019 mbapo BoT ilibaini kuwepo kwa udanganyifu ambapo mwenye leseni ya daraja A alitoa huduma zote mbili za kufanya miamala ya papo kwa hapo (Spot purchase and sells of foreign currency) na kufanya Money Transfer kinyume na sheria.

Akifafanua zaidi amesema leseni ya daraja A ilimtaka mmiliki wa Bureau de change awe na mtaji wa kima cha chini kabisa kiasi cha shilingi milioni 300 na daraja B bilioni 1, kwa kanuni mpya ikaamuliwa kuwepo na leseni moja tu ambayo itamlazimu mtu anayetaka kuanzisha biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kuwa shilingi bilioni 1 na itaruhusu kufanya huduma zote mbili, yaani kuuza na kununua fedha za kigeni lakini pia kusafirisha fedha za kigeni yaani Money Transfer.

No comments :

Post a Comment