Daktari
Bingwa akitoa huduma kwa wananchi katika Kituo cha Afya Mbezi Luis
jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusogeza huduma za afya za kibigwa kwa
wananchi na kupunguza mrundikano katika hospitali na pamoja na
hospitali za Rufaa.
Huduma mbalimbali zikiendelea katika Kituo cha Afya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakisubiri huduma za Kibingwa katika Kituo cha Afya Mbezi Luis wakati Madaktari Bingwa walipofika katika hicho.Manispaa
ya Ubungo imeanza kutoa huduma za kitabibu katika vituo vya Afya
vilivyopo katika Manispaa hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa Ubungo
Beatrice Dominic amesema yoezi hilo limeanza leo katika kituo cha Afya
Mbezi Louis na litakuwa la wiki tatu.
Amesema
katika Wiki ya pili huduma zitahamia kituo cha Afya Kimara na wiki ya
tatu litamalizia katika kituo cha Afya Makurumla. Dominic amesema huduma
za kibingwa zitakuwa zikitolewa bure katika wiki zote tatu.
Aidha amesema Madaktari bingwa watakaokuwa wakitoa huduma katika vituo hivyo ni madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto, madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na wataalam wa upasuaji.
Amesema lengo ya kupeleka Madaktari Bingwa ni kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi wote waliopo Manispaa ya Ubungo pamoja kutaka wananchi hao kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata huduma hii kutoka kwa madaktari hawa bingwa.

No comments:
Post a Comment