Tuesday, June 2, 2020

RC.MAKONDA AMEPOKEA VIFAA TIBA NA UJENZI KUTOKA MGULANI JKT



*****************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amesema wanaendelea na ujenzi wa ofisi za Walimu na kuboresha huduma za afya kwa kutoa vifaa na wahudumu wa kutosha katika
hospitali ambazo zimejengwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amezungumza hayo wakati wa kupokea vifaa tiba na ujenzi vilivyo tolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania Mgulani JKT.
Pia RC Makonda amesema anaishikuru Mamlaka ya Bandari kwa kumvisha nguo wiki mbili zilizopita alitoa ahadi ya mashine mbili za Utrasound na anazikabidhi Wilaya hiyo ili hospitali ianze kufanya kazi kwa haraka.
Vilevile Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini TPA Eng Augustine Witonde wanaendelea kutoa msaada ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais wametoa mashine mbili za Utrasound kubwa na ndogo pia milango ya alminium 37na madirisha 27,milango ya magril 8 na madirisha 53 vyote hivyo vimetengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Hatahivyo Eng Witonde amesema vifaa vyote hivyo vinagharimu Milioni 60 na kuwataka wananchi waendelee kutumia Bandari yao na rasilimali zake.
Sanjari na hayo Mkuu w Wilaya ya Temeke Mh Felix Lyaviva amesema TPA hawapo mbali na Wilaya yake kwakuwa mwaka jana walitoa mashuka na round Table kwaajili ya kujifungulia Leo wameamua kukabidhi vifaa hivi naomba tuvipokee kwa mikono miwili

No comments :

Post a Comment